Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Wanabodi.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)..

Kimejikita zaidi kwenye vurugu na watanzania sasa wameamini maneno ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Slaa..

Akiapa kwa uchungu kwamba watahakikisha nchi haitawaliki.

Hata kwenye majimbo ya uchaguzi ambayo Chadema imeshinda aidha ubunge au udiwani, wabunge na madiwani hao walioshinda kwa tiketi ya Chadema..

Hawafanya lolote chanya la kuwaletea wananchi maendeleo badala yake wanaendesha mivutano isiyoisha wakipinga hata yasiopingika..

Wabunge wa majimbo ya Kawe (Halima Mdee), Ubungo (John Mnyika). (Tundu Lissu) Singida, (Lema) Arusha (Wenje) Mwanza..

Hawakai majimboni mwao wala hawana mpango wowote na wapiga kura wao, badala yake wamejikita kuteleza mikakati ya Chadema makao makuu wanazunguka nchi nzima kuhamasisha watanzania wasigane na serikali ili hatimaye nchi isitawalike..

Huko Mbeya nako moto umewaka lakini kwa staili ile ile ya watu kusigana na serikali pasipo sababu za msingi..

Mbunge wa Mbeya mjini anaitwa kwa jina la sifa Mr. Sugu, amepewa sifa nyingine ziada inayozidi cheo cha ubunge, anaitwa Rais wa mkoa wa Mbeya, je, huu sio uhaini?

Upinzani wa Godbless Lema, na Tundu Lissu, Dr Slaa, Freeman Mbowe, haufai na unadhirisha wazi kwamba wahusika hawakupitia darasa la urai..

Uko wapi uzalendo wa Watanzania wenzetu!

mnisamehe wanajamvi, nilijua mtu ndo kapost huu uchafu kumbe kuku wa kuliwa?????naondoka
 
Hatakuwa rais wa kwanza kutomaliza muda wake! elewa kuwa rais huyu hatuheshimu, haiwezekani akubali mipango sisi tuibiwe, kama ana-compromise na wezi anaonyesha hawezi kusimamia sheria, asilazimishe kuendelea kuongoza!
Hivi wewe hukuwaona kina chapombe walivyo kuwa wanachekelea kuonana na Raisi Hizo picha za ikulu lazima colgate wazitumie kwenye matangazo yao ya biashara.

Mlimkataa kuwa sio rais, na wengine wakamzarau lakini mwisho wake mkarudi kujipendekeza.
 
Wanabodi.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)..

Kimejikita zaidi kwenye vurugu na watanzania sasa wameamini maneno ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Slaa..

Akiapa kwa uchungu kwamba watahakikisha nchi haitawaliki.

Hata kwenye majimbo ya uchaguzi ambayo Chadema imeshinda aidha ubunge au udiwani, wabunge na madiwani hao walioshinda kwa tiketi ya Chadema..

Hawafanya lolote chanya la kuwaletea wananchi maendeleo badala yake wanaendesha mivutano isiyoisha wakipinga hata yasiopingika..

Wabunge wa majimbo ya Kawe (Halima Mdee), Ubungo (John Mnyika). (Tundu Lissu) Singida, (Lema) Arusha (Wenje) Mwanza..

Hawakai majimboni mwao wala hawana mpango wowote na wapiga kura wao, badala yake wamejikita kuteleza mikakati ya Chadema makao makuu wanazunguka nchi nzima kuhamasisha watanzania wasigane na serikali ili hatimaye nchi isitawalike..

Huko Mbeya nako moto umewaka lakini kwa staili ile ile ya watu kusigana na serikali pasipo sababu za msingi..

Mbunge wa Mbeya mjini anaitwa kwa jina la sifa Mr. Sugu, amepewa sifa nyingine ziada inayozidi cheo cha ubunge, anaitwa Rais wa mkoa wa Mbeya, je, huu sio uhaini?

Upinzani wa Godbless Lema, na Tundu Lissu, Dr Slaa, Freeman Mbowe, haufai na unadhirisha wazi kwamba wahusika hawakupitia darasa la urai..

Uko wapi uzalendo wa Watanzania wenzetu!

OK. Kwa hiyo CHADEMA ndiyo wamesababisha CCM ishindwe kuleta maendeleo kwa watanzania for the last 50 years. Unless uwe unaumwa ndiyo unaweza kufikiri hivyo. Elewa wanachi wanajua kuliko wewe na CCM yako, jinsi CHADEMA inavyowasaidia watanzania, kwa kuibana CCM na serikali yake fisadi.
 
We ni kati ya zile maiti ambazo kenyata alidai nyerere anaziongoza(kwa sababu limelala jamani tusiliamshe tutalala sisi)
 
Hakuna kitu nisichopenda hapa duniani kama 'unafiki & propaganda' huyu bwana mdogo mleta thread hii ni mnafiki, sioni issue ya kujadiliana naye hapa ktk jamvi.
 
bila CHADEMA tusingejua mengi.CDM ni Chama makini kinachopigania ukombozi wa watanzania aote bila kujali ni magamba au ccm B!
 
Wanabodi.

Pamoja na CHADEMA kufanya ziara katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na kutangaza kauli mbiu ya M4C Watanzania wanahoji kwa nini CHADEMA hawasemi wana mipango gani yenye tija kwa taifa letu na watawakomboa vipi kama wanavyojinadi kuwa wao ni wakombozi?

Moja ya kauli ya viongozi wa CHADEMA ni ile hakuna kulala mpaka kieleweke pamoja na ile tunataka kuwakomboa Watanzania, hawaelezi mambo yanayohusu maendeleo ya taifa lao.

Watanzania wanataka CHADEMA wangekuwa wanawaeleza Watanzania ni kipi watafanya wao ambacho CCM kimeshidwa kuwafanyia, waseme ni barabara zipi ambazo watazijenga na waeleze vyanzo Vya fedha watakazotumia kujenga barabara hizo.

Kwenye mikutano ya CHADEMA huwezi kusikia wanaelezea Watanzania kuwa watawajengea hospital au watafanyaje katika kuboresha elimu hiki ndio kipindi cha kuwafafanulia Watanzania juu ya utekelezaji wa sera yao waliyosema wakati wa kampeni 2010 kuwa CHADEMA watatoa elimu bure chekechea hadi chuo kikuu kwa fedha kutoka wapi na kwa uchumi upi wa nchi.

Wananchi wanasema wanaofika kwenye mikutano ya CHADEMA wanachokisikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMAa kauli mbiu zao 'Mpaka kielekewe hakuna kulala' 'Ukombozi unakaribia' Wao wana pesa siye tu Mungu'

Nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.
 
Wewe mtu wa ajabu sana.

Umewahi kusoma manifesto ya Chadema?
Umewahi kuwasikia viongozi wa Chadema wakizungumzia vision yao ya Tanzania? Kwa kuanza tu, uwekezaji utawalenga zaidi

Watanzania badala ya sera za Kikwete za kuwaleta wageni eti Watanzania anaowaita "watu wa pembezoni" nao watanufaika. Kwa Chadema Watanzania hawatakuwa watu wa pembezoni.

Chadema itapangua mikataba mibovu ya madini ili akina Sinclair wasiendelee kutuibia madini yetu na kuwafaidisha wachache kukiwa pamoja na familia ya Kikwete ambayo wanae wanaishi kimjinimjini.

Chadema imeshasema kuwa serikali yake itakuwa na baraza dogo la mawaziri jambo litakalopunguza matumizi yaliyokithiri katika serikali ya Kikwete. Sasa wewe unataka wakuambie watajenga barabara gani na hizo hela zitatoka wapi? Kwani Kikwete kazitoa wapi?CCM imeshindwa kuwaletea Watanzania wote maisha bora. CHADEMA itaweza kwa kupangua priorities zilizopotoka za CCM.
 
Acha kukurupuka ritz CHADEMA sera zake zinaeleweka kwa wananchi

1.Kuhusu katiba mpya ni sera ya CHADEMA kwa hiyo CCM mnatekeleza sera ya CHADEMA.

2.Mpaka sasa sera za CHADEMA ndiyo zinaongoza nchi isipokuwa CCM imeshindwa kuzitekeleza kwa sababu hawana uwezo wa kuziishi

Ninachokiona wewe umepoteza network nadhani bado unatafuta posho.
 
hii ya kukomesha ufisadi na kuwaseka ndani mafisadi wote wewe peke yako ndo hujaisikia eti?poleeeeeni sana magamba.....
 
Jamani mimi sioni tatizo. kweli hawa CDM kwa upande wanafanya vizuri lakini si mara zote.
Hili la kueleza mipango mikakati nikweli lazima kwenye mikutano yao waeleze.

Mimi ningeshauri kama kweli ni wakombozi wachukue japo kijiji kimoja tu hapa tanzania kiwe cha mfano.
Watoe maendeleo tuone. Kunawabinge wapo wa chadema je wamefanya nn kwenye majimbo yao?

Mimi sipendi kuongea ongea tu nataka vitendo kama unasema wewe una MUNGU nani hapa Duniani asie na MUNGU. acheni bwana kutetea ubovu hawa chadema hata ukiwapa nchi wataboronga sana tena zaidi ya CCM. Tambua kua CCM nichama kilichokomaa. Chadema bado wachanga.
 
kila wanachofanya chadema ndicho ccm wanaiga.
huu si wakati wa kampeni ni wakati wa ccm kutekeleza waliyoahidi wananchi na chadema kwa sasa ni wakili wa wananchi.
kama unataka kujua cdm kitasema nini wakati wa kampeni subiri.
 
wanabodi.

Pamoja na chadema kufanya ziara katika baadhi ya mikoa ya tanzania na kutangaza kauli mbiu ya m4c watanzania wanahoji kwa nini chadema hawasemi wana mipango gani yenye tija kwa taifa letu na watawakomboa vipi kama wanavyojinadi kuwa wao ni wakombozi?

Moja ya kauli ya viongozi wa chadema ni ile hakuna kulala mpaka kieleweke pamoja na ile tunataka kuwakomboa watanzania, hawaelezi mambo yanayohusu maendeleo ya taifa lao.

Watanzania wanataka chadema wangekuwa wanawaeleza watanzania ni kipi watafanya wao ambacho ccm kimeshidwa kuwafanyia, waseme ni barabara zipi ambazo watazijenga na waeleze vyanzo vya fedha watakazotumia kujenga barabara hizo.

Kwenye mikutano ya chadema huwezi kusikia wanaelezea watanzania kuwa watawajengea hospital au watafanyaje katika kuboresha elimu hiki ndio kipindi cha kuwafafanulia watanzania juu ya utekelezaji wa sera yao waliyosema wakati wa kampeni 2010 kuwa chadema watatoa elimu bure chekechea hadi chuo kikuu kwa fedha kutoka wapi na kwa uchumi upi wa nchi.

Wananchi wanasema wanaofika kwenye mikutano ya chadema wanachokisikia kutoka kwa viongozi wa chademaa kauli mbiu zao 'mpaka kielekewe hakuna kulala' 'ukombozi unakaribia' wao wana pesa siye tu mungu'

nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.

itatuchukua muda mrefu sana kuweza kupata uhuru wa fikra!na kuepukana na mawazo mgando!
 
kuiondoa ccm madarakani ni mpango namba 1 katika maendeleo ya taifa hili. kila mtanzania mwenye akili timamu analijuwa hilo.

kwa hadhi yako, hukupaswa kuweka huu uzi mkuu wangu.
Mkuu, hapo nilipo bold...huyu anahadhi gani? naomba jibu mkuu
 
Wanabodi.

Pamoja na CHADEMA kufanya ziara katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na kutangaza kauli mbiu ya M4C Watanzania wanahoji kwa nini CHADEMA hawasemi wana mipango gani yenye tija kwa taifa letu na watawakomboa vipi kama wanavyojinadi kuwa wao ni wakombozi?

Moja ya kauli ya viongozi wa CHADEMA ni ile hakuna kulala mpaka kieleweke pamoja na ile tunataka kuwakomboa Watanzania, hawaelezi mambo yanayohusu maendeleo ya taifa lao.

Watanzania wanataka CHADEMA wangekuwa wanawaeleza Watanzania ni kipi watafanya wao ambacho CCM kimeshidwa kuwafanyia, waseme ni barabara zipi ambazo watazijenga na waeleze vyanzo Vya fedha watakazotumia kujenga barabara hizo.

Kwenye mikutano ya CHADEMA huwezi kusikia wanaelezea Watanzania kuwa watawajengea hospital au watafanyaje katika kuboresha elimu hiki ndio kipindi cha kuwafafanulia Watanzania juu ya utekelezaji wa sera yao waliyosema wakati wa kampeni 2010 kuwa CHADEMA watatoa elimu bure chekechea hadi chuo kikuu kwa fedha kutoka wapi na kwa uchumi upi wa nchi.

Wananchi wanasema wanaofika kwenye mikutano ya CHADEMA wanachokisikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMAa kauli mbiu zao 'Mpaka kielekewe hakuna kulala' 'Ukombozi unakaribia' Wao wana pesa siye tu Mungu'

Nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.

Sasa mkuu hukuelewa nn kile ambacho CDM tumehaidi kwa wananchi?
Be a guy.
 
Back
Top Bottom