Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Wanabodi.

Pamoja na CHADEMA kufanya ziara katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na kutangaza kauli mbiu ya M4C Watanzania wanahoji kwa nini CHADEMA hawasemi wana mipango gani yenye tija kwa taifa letu na watawakomboa vipi kama wanavyojinadi kuwa wao ni wakombozi?

Moja ya kauli ya viongozi wa CHADEMA ni ile hakuna kulala mpaka kieleweke pamoja na ile tunataka kuwakomboa Watanzania, hawaelezi mambo yanayohusu maendeleo ya taifa lao.

Watanzania wanataka CHADEMA wangekuwa wanawaeleza Watanzania ni kipi watafanya wao ambacho CCM kimeshidwa kuwafanyia, waseme ni barabara zipi ambazo watazijenga na waeleze vyanzo Vya fedha watakazotumia kujenga barabara hizo.

Kwenye mikutano ya CHADEMA huwezi kusikia wanaelezea Watanzania kuwa watawajengea hospital au watafanyaje katika kuboresha elimu hiki ndio kipindi cha kuwafafanulia Watanzania juu ya utekelezaji wa sera yao waliyosema wakati wa kampeni 2010 kuwa CHADEMA watatoa elimu bure chekechea hadi chuo kikuu kwa fedha kutoka wapi na kwa uchumi upi wa nchi.

Wananchi wanasema wanaofika kwenye mikutano ya CHADEMA wanachokisikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMAa kauli mbiu zao 'Mpaka kielekewe hakuna kulala' 'Ukombozi unakaribia' Wao wana pesa siye tu Mungu'

Nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.
Hata kama akili hazifanyi kazi... masikio na macho navyo havifanyi kazi????
 
Dawa ya mjinga ni kum-ignore tu! upo ndani ya box ndio maana una fikra duni kama za mzoga wa bundi!

Siku zote mtu akiwa mtupu anaweza kununuliwa au kununua nguo, lakini mtu anapokuwa uchi kiakili hakuna cha kumsaidia zaidi ya kumuombea kwa mungu.
 
Siku zote mtu akiwa mtupu anaweza kununuliwa au kununua nguo, lakini mtu anapokuwa uchi kiakili hakuna cha kumsaidia zaidi ya kumuombea kwa mungu.
Naive, dry as dust!
 
Ritz amewashika pabaya, huu ukweli ulio wazi kabisa na ndio maana mnabaki kurusha matusi. Tanzania sio gari la kufanya test drive. Jamaa wanataka wapewe nchi wakati hata mkoa wameshidwa kuuendesha.

Chadema itaendeshaje mkoa wakati haitawali? Ccm sio tu imeshindwa kuleta maendeleo bali pia ni kikwazo kwa maendeleo. The first thing first ni kuiondoa ccm.
 
Watanzania kwa nini tunatolewa nje ya mambo ya msingi ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania imefikia wapi au mimi sielewi maana yake?Kinachoelezwa leo ni siasa za ukabila, udini, ukanda na sio tumefikia hatua ya ngapi tuone mwanga wa maisha bora kwa kila mtanzania.Mtanzania anashindwa kuhoji kwa nini leo mafuta ya taa yamekuwa bei sawa na petroli hii inamaana kwamba yule aliyeko kijijini anauwezo wa kuendesha gari kwa maana ya kulihudumia kwa mafuta sababu petroli ni sawa na mafuta ya taa.
Mtanzania wa kawaida anaona ni bora leo kuliko kesho kwa sababu leo imepita kwa kudra za mwenyezi Mungu!Watanzania tupime mambo kwa kina kwa nini kila siku tunaambiwa tutafanya hiki na kile ingali siku zinasonga mbele kwa nini wasifanye leo?
 
sijaona hiyo mipango wala plan mpaka sasa!, Ritz may be you should ask again
 
Ritz ana ugonjwa wa uvivu wa kufikiri na kutafuta mambo. Angefanya haya mawili asingeandika aliyoandika
 
Jasusi.
Mpango wa Nyerere wa kipindi kile tofauti na sera za Chadema mkuu, unachotaka kufanya wewe ni kumsemea Slaa, ebu tuambie mbinu gani watatumia Chadema mpaka mfuko wa Saruji Wananchi tununue Sh5000.

Tuwaambie mbinu tutakayotumia ili muibadilishe iwe sera ya CCM? Mlipolalia ndipo sisi tulipoamkia.
 
Wanabodi.

Pamoja na CHADEMA kufanya ziara katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na kutangaza kauli mbiu ya M4C Watanzania wanahoji kwa nini CHADEMA hawasemi wana mipango gani yenye tija kwa taifa letu na watawakomboa vipi kama wanavyojinadi kuwa wao ni wakombozi?

Moja ya kauli ya viongozi wa CHADEMA ni ile hakuna kulala mpaka kieleweke pamoja na ile tunataka kuwakomboa Watanzania, hawaelezi mambo yanayohusu maendeleo ya taifa lao.

Watanzania wanataka CHADEMA wangekuwa wanawaeleza Watanzania ni kipi watafanya wao ambacho CCM kimeshidwa kuwafanyia, waseme ni barabara zipi ambazo watazijenga na waeleze vyanzo Vya fedha watakazotumia kujenga barabara hizo.

Kwenye mikutano ya CHADEMA huwezi kusikia wanaelezea Watanzania kuwa watawajengea hospital au watafanyaje katika kuboresha elimu hiki ndio kipindi cha kuwafafanulia Watanzania juu ya utekelezaji wa sera yao waliyosema wakati wa kampeni 2010 kuwa CHADEMA watatoa elimu bure chekechea hadi chuo kikuu kwa fedha kutoka wapi na kwa uchumi upi wa nchi.

Wananchi wanasema wanaofika kwenye mikutano ya CHADEMA wanachokisikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMAa kauli mbiu zao 'Mpaka kielekewe hakuna kulala' 'Ukombozi unakaribia' Wao wana pesa siye tu Mungu'

Nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.

Kazi kwelikweli...Ina maana majibu yote na discussions zilizokuwa zikiendelea ndani humu hazijaweza kusafisha mindset ya kimagamba gamba fulani, vipi ukizeeka zaidi na pengine ubongo ukakosa maji na electrolytes za kutosha kuruhusu good flow of brain elictrical signals?
Kwa udogo na distribution of power within CDM ukiwa na serious debators utakuwa na wakati mgumu kuthibitisha usemayo kuhusu kampuni ya biashara na familia ya damu moja(km donge ni mbowe- mbowe si damu ya mtei ndio maana akaoa kwao, na mbowe hatoki jamii zinazosema binamu nyama ya Hamu+Kikwete na Riz kuanzia kampeni walionyesha kuwa ilikuwa issue ya familia, sijui na uongozi utasemaje).Ingawa vinchi km vyetu vinavyoweza ONGOZWA NA SERIKALI ZENYE WATU DUNI KIFIKRA KM WA CCM bado asubuhi inafika na pakiwa na survivors wa kutosha, kuongoza Google ni kugumu kuliko.

By the way inaudhi km consistency na sense of responsibility havina thamani ktk wasomi wetu, kwani ndipo wanapopoteza patriotism wakidhnai wanazidi kuwa patriotic.

MWISHO KULALAMIKIA CDM KM CHAMA UPINZANI NI KM UNAKUBALI CCM IMESHINDWA NA UNAIONA KM CDM WANACHELEWA ASSUME CONTROL.
 
Jamani mimi sioni tatizo. kweli hawa CDM kwa upande wanafanya vizuri lakini si mara zote.
Hili la kueleza mipango mikakati nikweli lazima kwenye mikutano yao waeleze.

Mimi ningeshauri kama kweli ni wakombozi wachukue japo kijiji kimoja tu hapa tanzania kiwe cha mfano.
Watoe maendeleo tuone. Kunawabinge wapo wa chadema je wamefanya nn kwenye majimbo yao?

Mimi sipendi kuongea ongea tu nataka vitendo kama unasema wewe una MUNGU nani hapa Duniani asie na MUNGU. acheni bwana kutetea ubovu hawa chadema hata ukiwapa nchi wataboronga sana tena zaidi ya CCM. Tambua kua CCM nichama kilichokomaa. Chadema bado wachanga.

Mawazo mfu kabisa eti wachukue kijiji kimoja walete maendeleo,,
Hivi unadhani chini ya uongozi huu wa CCM hilo linawezeka? Si ndo CCM watapata kisingizio cha kuhalalisha hoja žao kwamba CDM ni chama kikanda. Lengo la cha CDM ni ukombozi kiuchumi,kisisa, na kijamii nchi nzima wala sio kijiji. Na kwanza usitufundishe kazi.
 
Nchi haiwezi kuongozwa mithiri ya kampuni ya biashara au familia ya watu wa damu moja.

Shabash!!!! Hebu twambie msanii Kikwete na Serikali yake ya magamba anaendesha nchi yetu mithili ya nini mpaka inasababisha nchi kurudi nyuma kimaendeleo!?

Kutokana na umasikini uliokithiri wananchi wengi wamekua wakiishi katika nyumba zisizo bora kwa kukosa fedha za kulipa kodi.
 
Tuwaambie mbinu tutakayotumia ili muibadilishe iwe sera ya CCM? Mlipolalia ndipo sisi tulipoamkia.

Ahsante mkuu kwa kumweleza huyu mchumia tumbo wa magamba ukweli. Si unaona nape anavyojitapa sasa hivi, eti katiba mpya ilikuwa sera ya magamba wakati 2010 hawakuwahi hata kulitamka hilo neno kabla ya uchaguzi na kwenye mikutano yao ya kampeni.
 
Hii nchi ya CCM na itabaki kuwa ya CCM, nyie mko kuturahisishia kupata hela za wazungu tu.
Matokeo ya uchaguzi wa 2015 yanajulikana,sasa wala usisumbuke kupanga mstari kupiga kura

very low thinking!! Time will tell, we know your plans especially now, we will do something better that you never expected.
 
Ahsante mkuu kwa kumweleza huyu mchumia tumbo wa magamba ukweli. Si unaona nape anavyojitapa sasa hivi, eti katiba mpya ilikuwa sera ya magamba wakati 2010 hawakuwahi hata kulitamka hilo neno kabla ya uchaguzi na kwenye mikutano yao ya kampeni.

Jibu hoja Watanzania wanaitaji kujua Chadema mna mipango gani ya maendeleo ya kwa taifa letu.
 
Shabash!!!! Hebu twambie msanii Kikwete na Serikali yake ya magamba anaendesha nchi yetu mithili ya nini mpaka inasababisha nchi kurudi nyuma kimaendeleo!?

Kutokana na umasikini uliokithiri wananchi wengi wamekua wakiishi katika nyumba zisizo bora kwa kukosa fedha za kulipa kodi.

Tatizo kubwa la Pro-Chadema pamoja na viongozi wao wanakuwa wakosoaji kwa CCM lakini wao kama Chadema hawasemi watawasaidiaje Watanzania zaidi ya kusema wanataka kuwakomboa Watanzania.
 
Tatizo kubwa la Pro-Chadema pamoja na viongozi wao wanakuwa wakosoaji kwa CCM lakini wao kama Chadema hawasemi watawasaidiaje Watanzania zaidi ya kusema wanataka kuwakomboa Watanzania.

Tangu lini Chama kinatakiwa kutangaza sera zake miaka miwili na nusu kabla ya uchaguzi!? Mmeishiwa sera mnataka kuiga kila kitu toka kwa CDM...Kweli magamba iko ICU!

Back
Top Bottom