Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Tangu lini Chama kinatakiwa kutangaza sera zake miaka miwili na nusu kabla ya uchaguzi!? Mmeishiwa sera mnataka kuiga kila kitu toka kwa CDM...Kweli magamba iko ICU!

Hivi Mwananchi wa kawaida ambaye ndio mpiga kura kumwambia hakuna kulala mpaka kieleweke, au nataka kumkumboa hivi ndio kumsaidia?
 
Mawazo mfu kabisa eti wachukue kijiji kimoja walete maendeleo,,
Hivi unadhani chini ya uongozi huu wa CCM hilo linawezeka? Si ndo CCM watapata kisingizio cha kuhalalisha hoja žao kwamba CDM ni chama kikanda. Lengo la cha CDM ni ukombozi kiuchumi,kisisa, na kijamii nchi nzima wala sio kijiji. Na kwanza usitufundishe kazi.

Wewe unakasirika pasipo mpango. kwani nyie CDM ni kitu gani kwani. Mimi siwezi kuletewa maendeleo na chama.
Do some not just talking talking.
Mnalalamika lalamika tu.
Kila wakati kulalamika ili wananchi wawa hurumie. Acheni hizo.
Tayari watu wameshapandikiziwa chuki ndani ya mioyo yao. No way CCM bado ni chama chenye uwezo kuliko CDM
Hata kama ukatae. The Truth shall set you free.
 
Wewe mtu wa ajabu sana.

Umewahi kusoma manifesto ya Chadema?
Umewahi kuwasikia viongozi wa Chadema wakizungumzia vision yao ya Tanzania? Kwa kuanza tu, uwekezaji utawalenga zaidi

Watanzania badala ya sera za Kikwete za kuwaleta wageni eti Watanzania anaowaita "watu wa pembezoni" nao watanufaika. Kwa Chadema Watanzania hawatakuwa watu wa pembezoni.

Chadema itapangua mikataba mibovu ya madini ili akina Sinclair wasiendelee kutuibia madini yetu na kuwafaidisha wachache kukiwa pamoja na familia ya Kikwete ambayo wanae wanaishi kimjinimjini.

Chadema imeshasema kuwa serikali yake itakuwa na baraza dogo la mawaziri jambo litakalopunguza matumizi yaliyokithiri katika serikali ya Kikwete. Sasa wewe unataka wakuambie watajenga barabara gani na hizo hela zitatoka wapi? Kwani Kikwete kazitoa wapi?CCM imeshindwa kuwaletea Watanzania wote maisha bora. CHADEMA itaweza kwa kupangua priorities zilizopotoka za CCM.

Hili siyo jibu mkuu ritz analolitaka...kua makini kidogo sema CDM inaona tatizo liko a, b, c, d kwa hiyo CDM itakuja na sera a,b,c,d kuimarisha uchumi, kuongeza ajira, kupanua pato la taifa..kwa mfano sera mahsusi ya kilimo CDM ikoje? sera ya Viwanda je? Elimu mtaboresha shule zetu au mtafumua kabisa mfumo uliopo wa elimu? serikali ndogo nakubaliana nayo na nguvu kupelekwa kwa wananchi kupitia majimbo, lakini sasa hii itawekwa vipi haswa na utenganisho wa nguvu za hawa viongozi wa majimbo na hawa wa kitaifa itakuaje? ili kupambana na ufisadi mmeshasema mtawafungulia kesi baadhi ya watu kama Mkapa, lakini hamjaeleza mtafanyaje kuuzima kabisa huu mfumo wa kifisadi kwa sababu mafisadi hawaishi bila ya mfumo wanaoujenga...na mengine kama hayo

Kumbuka kura za kuichoka CCM mtazipata, lakini kura nyingi zinataka kujua haya kwa undani kuonyesha umakini wa CDM vinginevyo watu wengi makini pamoja na kua wanaona kasoro CCM, lakini bado hawajashawishiwa kupiga kura CDM. Na chama chochote cha upinzani kinahitaji tabaka hililenye umakini ili kushika dola.
 
Tuwaambie mbinu tutakayotumia ili muibadilishe iwe sera ya CCM? Mlipolalia ndipo sisi tulipoamkia.

Tunataka kujua sera mahsusi itakuaje CCM waibe sera mahsusi ya chama kingine? ikiwa mahsusi ina maana itakua ya kwao na CCM wakiichukua au kuiba vipanda vipande si wananchi wataona..mbona unataka kuleta ujanja na umjini mjini kujibu maswali na hoja za msingi.

Kuna tofauti ya kufanya mkutano wa kujenga chama na mkutano wa kampeni......kama wakifanya kampeni kipindi hiki watakuwa wanakiuka utaratibu na kanuni za msajili wa vyama vya siasa.
Kazi yao kubwa sasa ni kueleza serikali ifanye nini kwa wananchi na kuikosoa serikali hiyo. Ccm wanataka kuwaforce chadema ili wawashtaki kwa msajili wa vyama.
Jaribu kufuatilia hata hotuba za labour party ya uingereza kwa sasa.
By the way...jaribu kusoma mapendekezo ya bajeti ya upinzani na kuwa mfuatiliaji wa hoja zao bungeni au hata kwenye account zao katika mitandao ya kijamii.
Kueleza utafanya nini sio kufanya....ndicho wanachofanya ccm kila mwaka.
 
Mkuu mharakati.

Nashukuru sana kwa ufafanuzi wako murua..Chadema wanatakiwa watufahamishe Wananchi mipango yao kwenye mikutano yao watawasaidiaje vijana, watawasaidiaje wakulima, watawasaidiaje wafanyabiashara, watawasaidiaje wawekezaji, watafanyaje kuhusu mikataba ya madini, na mbinu watakazotumia kuinua uchumi wetu.

Mwananchi wa kawaida utapomwambia people's power, hakuna kulala mpaka kieleweke, wao wana pesa sisi tuna mungu, tunataka kuwakomboa, sidhani kama hizi ndio sera za kuwavutia watu.

Itakumbukwa Chadema imekuwa ni chama cha matamko toka Bavicha wachaguane mpaka leo wameishatoa matamko yaidi ya 10 lakini hakuna hata tamko mmoja ambalo wamelezea mipango ya Chadema kimaendeleo kuwasadia vijana zaidi ya maandamano.
 
Last edited by a moderator:

Kama hawana sera mahsusi kwa ajili ya maendeleo yetu basi hawa CDM siyo mbadala wa CCM.

wanachofanya wenyewe ni kupigia kelele mambo Obvious tunayoyaona wote na kuyafanya mitaji ya kuingia ikulu bila ya kua wawazi na mikakati yao maalum ya kuendeleza taifa hili.

unaposema serikali ndogo na kuondoa ufisadi ina maana unataka kuokoa pato lilolopo linalopotoa kwa ufujaji huu, lakini haujasema kama unataka kuliongeza hili pato kupitia a, b, c...z. na hapa nina mashaka na hawa watu na mikakati yao ya dhati ya kuipeleka Tz pale inapostahili.

CDM imekua kama wanaharakati wa kisiasa kwa sana badala ya chama makini kinachotarajiwa kushika dola siku moja(kwa sababu wanaharakati ni watu wa kukosoa sera na mienendo mibovu ya serikali bila ya kusema wao wana mikakati gani kwa kua hawana malengo ya kushika dola).

hizi kauli mbiu za kila siku ni upumbazaji wa wananchi na kuwafanya wawe na fikra finyu kuhusu nini CDM inaweza kurekebisha haswa..vague political slogans ni ubabaishaji ili utakapoingia usishikwe shati kua haujatimiza yale uliyosema. hizi tunaita mass politics na Tanzania ya sasa hatutaki tena siasa siasa hizi tunahitaji watekelezaji, Mbowe et el wanaonekana wamenogewa na siasa na wataongoza kisiasa nchi maskini isiyohitaji siasa katika kipindi hiki.
 
Acha kukurupuka ritz CHADEMA sera zake zinaeleweka kwa wananchi

1.Kuhusu katiba mpya ni sera ya CHADEMA kwa hiyo CCM mnatekeleza sera ya CHADEMA.

2.Mpaka sasa sera za CHADEMA ndiyo zinaongoza nchi isipokuwa CCM imeshindwa kuzitekeleza kwa sababu hawana uwezo wa kuziishi

Ninachokiona wewe umepoteza network nadhani bado unatafuta posho.

evoddy. katiba mpya ni sera au pendekezo? unajua maana ya sera au policy wewe au ushabiki tu? na hili ni tatizo la wanaCDM wengi-USHABIKI

1. sera/policy ni mahsusi/exclusive na ina malengo ya moja kwa moja yaani, katiba siyo mahsusi/inclusive na haina malengo ya moja kwa moja kwani inalenga jamii nzima na siyo sehemu fulani ya jamii au sekta fulani.

2. Sera inapimika kama imefeli au imefanikiwa katika malengo yake na hivyo kupitiwa mara kwa mara na kurekebishwa, katiba utaipimaje imefanikiwa katika hili au lile? ndiyo maana kubadilisha katiba ni kazi kubwa kuliko sera hata ikiwa kubwa kiasi gani haitaji bunge kubadilisha sera ila katiba inaligusa bunge.

3.sera kama katiba ni elekezi, sera kama katiba ni msimamizi, lakini sera inaishi ndani ya katiba wakati katiba iko juu na inajitegemea.

Nafikiri umepata kidogo mantiki yangu, katiba mpya popote pale siyo sera ya chama husika cha siasa bali ni madai au mapendekezo yao ya kuboresha sheria za nchi ili iongozwe vizuri na kwa ufanisi.
 
Tuwaambie mbinu tutakayotumia ili muibadilishe iwe sera ya CCM? Mlipolalia ndipo sisi tulipoamkia.

Jasusi,

Watanzania wanaitaji kujua mna mipango gani ya maendeleo sio CCM...Jibu ni jepesi semeni ni barabara zipi ambazo serikali ya CCM imeshindwa kuzijenga, na Chadema watazijenga wakichukuwa nchi, semeni mna mipango gani ya kujenga vyuo vikuu, huwezi kujenga nchi kwa kauli mbiu na maandamano mkuu bila sera.
 
Hivi Mwananchi wa kawaida ambaye ndio mpiga kura kumwambia hakuna kulala mpaka kieleweke, au nataka kumkumboa hivi ndio kumsaidia?

Mwananchi wa kawaida atazifahamu sera za CDM wakati muafaka utakapowadia, CDM haiwezi kutangaza sera zake miaka miwili na nusu kabla ya uchaguzi ili waigizaji wa magamba wazikwapue na kuzifanya ni zao. Mmeshindwa kupigia debe sera zenu ambazo ni mufilisi sasa eti mnaishinikiza CDM itangaze sera zao!!!! Ama kweli mfa maji haishi kutapatatapa.

Pipoooooz Powaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Alutta Continua! Continua!

😛eace:😛eace:😛eace:

Maandiko yako ya mwisho kabisa kwenye post yako ndio sera ya Chadema.
 
Maandiko yako ya mwisho kabisa kwenye post yako ndio sera ya Chadema.

Watanzania wanayaona bomba kabisa halali mtu mpaka kieleweke ili nchi ikombolewe toka mikononi mwa mafisadi wa magamba.
 
Hivi kuwambia Watanzania tunataka kuwakomboa lakini hamsemi mtawakomboa vipi wakuu ebu tupeni michango yenu nngu007 Mungi Kimbunga Mkandara
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuwambia Watanzania tunataka kuwakomboa lakini hamsemi mtawakomboa vipi wakuu ebu tupeni michango yenu nngu007 Mungi Kimbunga Mkandara

Mzee wa Jamhuri ya Nauru Mkuu ritz hoja yako ni mzigo mzito sana. Hakika CDM wanapita mikoani lakini hawasemi watawafanyia nini Watanzania pindi wakiingia ikuku. Tanzania na dunia kwa ujumla inakabiliwa na kuporomoka kwa uchumi nchi tajiri zina matatizo makubwa ya kiuchumi maisha ni magumu kila mahala. CDM hawasemi wataikomboa kivipi nchi kutokana na tatizo la uchumi wa kidunia. Wakombozi wote duniani hujinasibu kwa wananchi wanaotaka kuwakomboa kwa kuwaambia watawafanyia nini.

Nadhani CDM hawasemi mbele ya wananchi kinagaubaga watafanya nini kwa kuogopa wasije wakaulizwa kwamba mlikuwa mnasema hivi mbona haiwi? CDM kama vyama vyote vya kiasiasa wanatumia matatizo yaliyopo yawe ya CCM ama ya kidunia kuwahadaa wananchi ila tatizo wao hawasemi watafanya nini kutatua matatizo. Tuambieni tuwe na matumaini badala ya kama alivyosema Ritz ni kauli za mpaka kieleweke; kikishaeleweka ndio basi?!
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuwambia Watanzania tunataka kuwakomboa lakini hamsemi mtawakomboa vipi wakuu ebu tupeni michango yenu nngu007 Mungi Kimbunga Mkandara

Mzee wa Jamhuri ya Nauru Mkuu ritz hoja yako ni mzigo mzito sana. Hakika CDM wanapita mikoani lakini hawasemi watawafanyia nini Watanzania pindi wakiingia ikuku. Tanzania na dunia kwa ujumla inakabiliwa na kuporomoka kwa uchumi nchi tajiri zina matatizo makubwa ya kiuchumi maisha ni magumu kila mahala. CDM hawasemi wataikomboa kivipi nchi kutokana na tatizo la uchumi wa kidunia. Wakombozi wote duniani hujinasibu kwa wananchi wanaotaka kuwakomboa kwa kuwaambia watawafanyia nini.

Nadhani CDM hawasemi mbele ya wananchi kinagaubaga watafanya nini kwa kuogopa wasije wakaulizwa kwamba mlikuwa mnasema hivi mbona haiwi? CDM kama vyama vyote vya kiasiasa wanatumia matatizo yaliyopo yawe ya CCM ama ya kidunia kuwahadaa wananchi ila tatizo wao hawasemi watafanya nini kutatua matatizo. Tuambieni tuwe na matumaini badala ya kama alivyosema Ritz ni kauli za mpaka kieleweke; kikishaeleweka ndio basi?!
 
Last edited by a moderator:
Tangu lini Chama kinatakiwa kutangaza sera zake miaka miwili na nusu kabla ya uchaguzi!? Mmeishiwa sera mnataka kuiga kila kitu toka kwa CDM...Kweli magamba iko ICU!

Mkuu BAK yaani hata wewe huwezi kutofautisha kati ya sera na ilani ya uchaguzi? Tangia lini sera za chama zikawa siri? Sera zinakuwepo na zinatakiwa zitangazwe na Chama muda wote ili ziingie mifupani mwa wanachama na wanachama tarajiwa. Ilani inaelezea jinsi ya kutekeleza sera ndio maana huwa inatangazwa wakati wa uchaguzi. Hapo wanasiasa ndipo husema kwamba tupeni dola ili tutekeleze sera zetu kwa kufanua yafuatayo. Mkuu sera siyo siri hata kidogo.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK

Kuna nyingine bado zinapikwa jikoni mkuu hizi zitazidi kuwavuta Watanzania kwa CDM na magamba kamwe hawawezi kuziiga maana wameshashindwa kuzitekeleza na zikiwa tayari tu zitatangazwa rasmi. Wanachoweza kufanya magamba ni kuziponda tu lakini zitakuwa na umaarufu mkubwa miongoni mwa Watanzania wengi.
 
BAK hii si kweli mkuu. Yaani chama cha siasa kinaficha sera zake kweli? Inabidi tujifinze kufahamu tofauti ya sera na ilani za uchaguzi.
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuwambia Watanzania tunataka kuwakomboa lakini hamsemi mtawakomboa vipi wakuu ebu tupeni michango yenu nngu007 Mungi Kimbunga Mkandara

​Ritz, Kimbunga

1.Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
10. Kubana matuzi Ikula (Yuko tayari kula mihogo
)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom