DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

DCI Manumba: Mwakyembe hajalishwa sumu!

Nadhani huu ndio ikweli wenyewe!. Kibarua sasa kimebaki kwa Mhe. Mwakyembe mwenyewe ku disclose anaumwa nini!.

Get well soon Mwalimu Mwakiyembe na achana na michezo michafu, rudi darasani ukaiendeleze fani ya kufinyanga wakombozi wa mahakamani.

pasco...i cant concur with you more.

nilishasema mahala pengine kuwa mwakyembe ninayemfahamu mimi kama taarifa ya kidaktari ya huko uhindini (ambayo tayari alikuwa anaijua hata kabla hajarejea) ingekuwa imeonyesha poisoning, jamaa angepiga kelele hadi picha kupelekwa cnn hata voa!

this guy is sick... ni unafiki na ubinafsi ndivyo vinavyom-drive kutaka kutafuta mchawi!
kama uchawi duniani upo basi amerogwa na watanzania wote ambao walichukizwa na kitendo chake cha kuikalia taarifa kamili ya richmond.......honestly I have no sympathy to this guy ambaye thanks to him bado vichwa vya nazi vimeendelea kukaa pale magogoni hadi leo!!
 
Jason bourne!


Uko wapi Kamanda wetu?
Hapa mawazo yako ni very impornant sana Kamanda!

Tunasubiria mistari yako tafadhali!
 
sasa mheshimiwa mwakyembe amepewa rungu; atoe vithibitisho vya daktari ili kuwaumbua polisi. Hilo tu vinginevyo maneno ya kwamba amelishwa sumu yatakuwa ni maneno ya kutunga. Hata hivyo sijawahi kumsikia Mwakyembe akisema amelishwa sumu!
 
Mkuu Pasco, nikukumbushe kuwa kuna mtu aliwahi kueneza tuhuma kuhusu wewe nadhani unakumbuka. Yeye alisema pasco ..... kwa kutumia vigezo na hisia.

Wewe ulikuja hapa jamii forum na kutoa maelezo ya kujitosheleza kuwa huna hulka ilitosemwa, ukaenda mbali na kutoa ushahidi wa wewe kuanzia makutopora, chuo kikuu n.k. Hukusema tu 'Sina tabia hiyo' bali ulienda mbali ku-prove beyond doubt.
Serikali imesema 'hakuna sumu' , je inatosha kukanusha madai mazito kama hayo ya maisha ya raia kiongozi?

Pili, kumbu kumbu zinaonyesha kuwa Dr Mwakyembe ameshawahi kufikisha madai ya ajali, na yale mazito sana ya kuuawa kule Morogoro. Serikali haijashughulikia madai hayo. Hii inaondoa kabisa hoja ya kuwa 'hajaripoti polisi' kwasababu hata angeripoti bado hakuna utashi wa kushughulikia kwasababu madai yake yanawagusa watu wazito waliomo na waliostaafu na waliojiuzulu.

Kama madai ya Sitta ni uongo serikali inawajibu wa kumshataki. Haijafanya hivyo na haitafanya hivyo kwa kujua kuwa Sitta anaweza kutoa ushahidi utakaoleta utata. Ndiyo maana PM na kila mkubwa wa serikali anaogopa kuzungumzia tuhuma hizo.

Huwezi kujua mazingira yanayomlazimisha Mwakyembe kukaa kimya. Unakumbuka Said Kubenea alipotoka India alitaka kuitisha mkutano na wanahabari! unajua nini kilitokea hadi leo hajazungumzia suala hilo? Walikamatwa vibaka ili kumzuia 'technically' asizungumzie suala hilo.

Kama madai ni kuisumbua Polisi, iweje polisi hiyo hiyo isisumbuke wakati wa utata wa ajali na tuhuma za mauaji Morogoro?
Kwanini serikali ichague mambo ya kushughulikia yanayomsibu Mwakyembe na si maisha yake as whole!
Hadi tutakapopata ukweli wa jaribio la kumuua kule Morogoro hatutakuwa na imani na taarifa yoyote hasa kutoka Polisi kuhusiana na Mwakyembe! Nitty gritty

Na mwisho, endapo serikali imethibitisha kuwa sio sumu, ilitakiwa iende mbali zaidi. 'Sio sumu' ni kauli inayoweza kutolewa na mtu yoyote. Haya ni madai mazito sana na tayari yapo vichwani mwa watu, huwezi kuyafuta kwa neno moja bila kukata kiu kwa maelezo yanayoeleweka.

Wewe hukusema 'mimi siyo..' ulienda mbali zaidi. Hapo mkuu huoni kuna upungufu kwa serikali hasa tukizingatia unyeti wa suala lenyewe
Mkuu Nguruvi3 kwenye hili la sumu, mwisho wa uwezo wa serikali kusema sio sumu ndio hapo. Serikali haipaswi kusema ilichunguza nini na ni kwa vigezo gani waliend up kuhitimisha sio sumu, japo pia nina doubt na uwezo wa kiteknolojia kufanya uchunguzi wa sumu kama polonium!.

Maadam kauli rasmi ya serikali ni " Hakulishwa Sumu", this is only one side of the coin, the other side of the coin ni kile ambacho Mwakyembe anachoumwa!. Nashauri subirini mjue anaumwa nini!.

Ile hoja kuwa alishalalamika huko nyuma bali polisi hawakufanya chochote its still valid, polisi walipaswa wauambie umma wa Watanzania why ili wengi wenu msio mwelewe vizuri Mwakyembe what he is really is!.

Kuusema ukweli sisi waandishi wa Tanzania ni wavivu na sio wachokonozi!. Waandishi wanaoripoti issues za polisi, kazi yao ni kumeza tuu kila wanacholishwakwenye zile daily press co. zao badala kuuliza serious issues.

Kuna zile tuhuma za waziri kijana, polisi kimya!. Tuhuma za Mwakiyembe kutishiwa kuuwawa, polisi kimya, Tuhuma za kumbambikia ntoto wa kigogo 'mzigo', polisi kimya!, sasa hizi tuhuma za sumu si angalau wamejibu!, si wangeweza kukaa kimya na wasiulizwe chochote kama kawaida yao!.
 
Heeeeeee..... this is joking with DEATH.....so anaumwa niniiii......mtu kazeeswaa ghafla kawa like 85 yrs old, .....????????????!!!!!?????????? No answer here...
hivi Dr. Mwakyembe si anaongea? Kwani hata yeye hajui ugonjwa wake? Aseme..
 
Maskini Mwakyembe...

Unafiki wake ndio umemponza. Kama angemaliza kabisa ile ishu ya Richmond kwa kuleta hata ule ushahidi aliosema kama ungewasilishwa pangechimbika, yote haya yasingemkuta. MWakyembe kigeu geu, Lowassa kigeu geu, Pinda kigeu geu, Manumba kigeu geu

Umemsahau Sitta, nae kigeugeu na mnafiki mkubwa! Mwakyembe unafiki na kujikomba baada ya kupewa kau-naibu waziri ndivyo vinavyomuuwa!!

Huyu Manumba...si ndiye alieshiriki kumtilia madawa ya kulevya mtoto wa Mengi?! Tanzania bwana, huyu jamaa ni Jambazi kabisa lakini eti bado yuko madarakani!
 
nani anajua dR ATARUDI? |May be statement ya dci inafahamika yeye dr hatakaa areact! I mean kalishwa amelishwa inategemea mwenye maumivu anaonaje afya yake na hisia za watz juu ya afya yake.
Lakini Dr Kasema kuwa anakwenda Appolo atakapo rudi ndio ataweka wazi,so tusubiri na subira huvuta kheri
 
Kama polisi kazi yao ni kuchunguza tuhuma na sio maradhi sasa wizara ya Afya walifuata nini?
Yaani to you DCI suala la Mwakyembe bado liko ktk level ya Tuhuma kwa iyo kama angekufa iyo status ya tuhuma bado ingesound?
Sipati picha mahela yaliyotumika kuhakikisha iyo statement inatoka!
 
Nakubaliana na Manumba, sumu hata ya panya saa hizi angekuwa ameshakufa.
 
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:

"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".

Alipoulizwa na waandishi wa habari:

Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?


DCI alijibu kwamba:

"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli
."


Mkuu mchambuzi ingekuwa vizuri kama ungeeleza zaidi kuhusu habari hii. Ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa hizo kauli mbili ni kama hazijatolewa na DCI, ya kwanza inasema hakuna ushahidi kuwa amelishwa sumu, ya pili inasema jeshi halikuchunguza maradhi. Tuhuma ni kuwa Mwakyembe kalishwa sumu, so implied meaning ni kuwa anasema hajalishwa ila amejilisha, au anasema kuwa Mwakyembe hana tatizo la sumu. So Wizara ya afya inachunguza vipi shutuma? Ukiangalia hizi kauli unaona wazi kabisa mtu anayezisema hawezi kuwa DCI wa Tanzania.

Jeshi letu la Polisi au CID ina maabara na wanasayansi wanaoweza kuchunguza sumu za radiation? hapa Tanzania sumu ya panya yenyewe kuchunguza ni vigumu. Kuna Toxologists wangapi wanaoweza kufanya kazi na tukaamini kuwa wanafanya kazi kweli na tukapewa majibu kweli? au ndio yale yale ya kesi ya nyani kwa ngedere.
 
Mkuu Ngongo, the disclosure rights lies with the patient. Hivyo hilo ni jukumu la Mwakyembe mwenyewe!.
Pasco, sasa hicho ndio kiingereza gani? Ingependeza kama ungeweka hivi 'the disclosure rights lie with the patient'
 
Pasco kwenye huo mfano wa kichapo cha mume, umeielezea hii issue kwa ufasaha. Well said. Nadhani that is how it is, manake Mwakyembe hajalalamika what do u expect!
 
Tumuombee jamani apone, kisha tutajua mengi yaliyojificha kwa sasa ni mapema mno kusema kama alivyosema manumba, sasa akirudi mwenyewe na kusema kinaachomsibu akina manumba wataficha wapi nyuso zao? Nakuombea kwa Mungu upone haraka ili uendelee na majukumu ya kulijenga Taifa.

Mwakyembe hatutendei haki watanzania. Akifa bila kusema yaliyomo kwenye ripoti yake na bila kusema nani alimpa sumu, hakuna atakeyemwamini Sitta akitueleza baada ya kufa. He better do it now before it is late.
 
Manumba anasemaa hajalishwa sumu, anepinga alete ushahidi, kama hamna ushahidi its a closed topic.
 
Kwani mlitegemea jibu lingine tofauti na hilo kutoka kwa hawa corrupt police? Hapo hakuna uchunguzi uliofanyika ni usanii tu! Kumbukeni kwamba hawakuwa tayari kufanya uchunguzi hata baada ya Dr Mwakyembe kuwataarifu kutishiwa maisha yake, sasa mnategemea watasema ni kweli alilishwa sumu? Police ni taasisi isiyoaminika tena hapo Tanzania kwasababu wanafanya kazi za siasa badala ya taaluma yao!!
 
Aliyewekewa sumu ni Mwakyembe hajaripoti polisi kuhusu kuwekewa sumu. Aliyepayuka hadharani kuhusu jinai ya sumu ni jirani (Sitta). Polisi wamechukua maelezo ya Sitta na kufanya uchunguzi, wakakuta hakuna jinai ya sumu!. Mwakyembe mwenyewe wala familia yake hawajalalamikia sumu!. Kama ambavyo mkeo hajalalamikia polisi kuhusu kichapo alichokula!.

Mwakiyembe anaumwa, hajalalamikia kupewa sumu. Jirani ndio anae eneza uvumi wa simu ili kuwanyooshea kidole mahasimu wake wa kisiasa!. Sasa kwa vile issue ilikuwa ni kupewa sumu, imethibitika sio sumu!. Mwambieni jirani sasa na atoe uthibitisho, ila its high time Dr. akirudi toka matibabu ya India awaambie Watanzania ukweli wa anachoumwa!.

Mkuu Pasco,

Mtu akiwekewa sumu hawezi kujua kabla hajaambiwa na wataalam wa tiba. Unaweza kuwekewa sumu na usijue kwamba umewekewa sumu ila utaona unaanza kuugua na vipimo vya hospitali ndio ambavyo vinaweza kuthibitisha kwamba huyu mtu aliwekewa sumu na wanaweza ku-identify hata aina ya sumu aliyowekewa kama wana utaalam wa kutosha na vifaa vinavyoweza kugundua.
Litvinenko-aliwekewa Polonium-210, hakujua mpaka alipoenda hospitali na baadaye kuanza ku-trace alipita wapi na wapi na watu gani aliokutana nao. Kama unakumbuka vyema kwenye hilo sakata sehemu zote ambazo alipita siku hiyo ziliwekwa under investigation na kuzuwia watu wasiende. Sasa Mwakyembe ange-ripoti vipi bila kuwa na uhakika wa kulishwa/kuwekewa sumu?

Zama za Mkapa, Mh. John Pombe Magufuli aliwahi kuwekewa sumu na hakujua sumu hiyo aliipata wapi, alipelekwa haraka sana Ujerumani kwenda kutibiwa na baada ya hapo Mh. Pombe alipewa ulinzi na Jeshi la Polisi, walimpa bila kuomba. Maelezo ya Polisi yalikuwa kwamba mtu akishakumbwa na msukosuko kama huo huwezi kujua mtu aliyemfanyia hayo alikuwa na nia gani. Sikumbuki ulinzi huo ulidumu kwa muda gani.

Kwa kufuatilia mtiririko wa matukio ambayo Mwakyembe aliya-report, la kuhusu ajali kule Iringa na kutaka kuuawa Morogoro, kama jeshi la polisi linafanya kazi inavyotakiwa basi lingeweza kuanza kufuatilia nyendo zake hata bila kutangaza na hiyo ingewapatia jibu.

Tatizo la Jeshi la Polisi, linafanya kazi kwa maslahi ya kundi fulani la watu. Kibaya zaidi ni kwamba kwenye tuhuma za Mwakyembe, polisi na gari la polisi walikuwa ni wahusika/watuhumiwa. Sasa unapokuta kwamba Jeshi la Polisi linatuhumiwa, polisi inapoteza sifa ya kufanya uchunguzi ambao unaweza kutoa majibu sahihi. "Dili" kama hizo za kutumia magari ya polisi na polisi wenyewe kufanya jinai, mara nyingi huwa zina baraka za wakubwa wa Jeshi hilo, refer, case ya Zombe na askari wake.

Kwa hiyo Mwakyembe asingeweza kujua kabla hajaenda India kutibiwa. Muhimu ni kile ulichokisema kwamba as long as Manumba amesema Mwakyembe hajalishwa sumu, basi Mwakyembe akirejea kutoka India aje aseme kwamba report ya madaktari inasema nini.
 
Wanabodi, tuacheni conspiracy theories, vuteni subira kwanza mkijue anachoumwa ndipo mziendeleze hizi conspiracy theories zenu!.

Serikali makini itamshughulikia Sitta haraka iwezekanavyo, scrap him his ninisterial positions na kumpandisha kizimbani kwa kosa la "uchochezi"!.
Tugawie basi na sisi ulichopewa na mamvi!!!unavyomtetea, asipokuwa rais mara moja the hague anakostahili
 
Mwakyembe hatutendei haki watanzania. Akifa bila kusema yaliyomo kwenye ripoti yake na bila kusema nani alimpa sumu, hakuna atakeyemwamini Sitta akitueleza baada ya kufa. He better do it now before it is late.

Sitta ni mwongo sana, ndio kilichomponza akauokosa ufalme wa bunge. Mwakyembe nae ni mnafik, sakata lote alilojidai la Richmond, mbona mitambo ipo na amekaa kimya? yote ilikuwa ni hasira za kuzidiwa kibiashara, alijuwa na project ya kuleta yeye mita,mitambo ya umeme kupitia kampuni yake ya umeme wa upepo hewa, ni uoga tu uliomfanya atunge uongo.

Halafu isitoshe huyo jamaa, ana matatizo ya kichwa kama mnabisha mwambieni aseme ukweli katibiwa nini India.
 
haya aliwekewa sumu kwenye kitambaa (handcachief) akajifuta usoni ndio ikasambaa
sasa hakuinywa huyo Manumba anasemaje na hapo? mtu ngozi imeharibika kwa ajili ya kusema ukweli tuu?
 
haya aliwekewa sumu kwenye kitambaa (handcachief) akajifuta usoni ndio ikasambaa
sasa hakuinywa huyo Manumba anasemaje na hapo? mtu ngozi imeharibika kwa ajili ya kusema ukweli tuu?

Na hiyo henkachifu aliwekewa na mkewe? vitu vingine hebu pima wewe.

Yule ana kansa na yale yanayomnyoa manyoya ya mwilini ni madawa ya kansa. Asijidai, sumu. Yule alivyo, angekuwa kawekewa sumu dunia nzima ingeshajuwa ni sumu ipi na wapi alipowekewa, eti henkachifu.

Hiyo henkachifu mtu aiibe mfukoni kwake, aweke sumu, na huyo mtu ni mzima bado?

Ujinga huo.
 
Back
Top Bottom