DC aendelea na kuifanyia CCM kampeni Igunga

DSC_6309.jpg

haha haha hawa dawa yao kuondoa hicho kiti ili wapasuke vizazi!!
 

Hii Fuso si ya mjomba wake na RA ambayo alipewa na RA! yaani pamoja na jamaa kuwa nanga kwamba chama chao kinaendeshwa kwa siasa uchwara bado wameenda kuomba kusaidiwa usafiri na kumpigia magoti aje kwenye sherehe za ufunguzi wa kampeni, kweli kazi ipo. Watz wezangu naomba mnisaidie kwani napata taabu kweli kweli ,chama hasa chama cha siasa kinawezaje kuwa na siasa uchwara kisiwe na viongozi au uongozi uchwara? Inakua vipi basi wote tunakaa kimya na kukukubali kuongozwa na viongozi uchwara chini ya siasa uchwara za ccm?
 
Mkuu nadhani unazungumzia katiba ya saccos ya mtaani kwenu na si katiba ya nchi! Katiba ya nchi inawakataza watendaji wote wa serikali kujishughulisha na shughuli za vyama vya siasa. Nadhani ni heri hao wavivu kufikiri kuliko wewe unayefikiri kwa kutumia masaburi!
Filipo mkuu fanya research katika hili kuliko kuishia kulaumu.
Mimi naona Mzee wa Rula ndiyo ufanye utafiti au hujaelewa anacho kiongelea Filipo...DC anajishughulisha na kampeni za chama tawala kinyume na katiba hazungumzii kuwa mwanachama msome hapo kwenye nyekundu....au na wewe una malalamikio ya DC kuvuliwa ushugi....hahahahaha
 
Tangu sakata la kukamatwa kwa DC wa Igunga akihalifu sheria chama ca CCM kimekuwa kikifanya propaganda chafu sana,ya UDINI hapa Igunga mjini,jana wilayani Uyui Dc huyu alitoa laki moja hadharani na kulia machozi,huku akiwahamasisha waislama kuandamana kuipinga chadema et alivuliwa HIJAB.Huu ni mkakati mchafu wa ccm,na ni uwendawazimu,kimsingi chadema hatukumkamata huyu DC kwa dini yake,au rangi ya chama chake.tulimkamata kwa kuwa alihalifu sheria,na nguvu iliyotumika kumkamata inakubalika kisheria.
Dc huyu anaendela kuifanyia ccm kampeni,na usiku wa jana alikuwa n a wakinamama(wanawake)kwenye jengo la serikali anakoishi,anatumia kodi za wananchi kuifanyia ccm kampeni.

Nitawashangaa waislamu watakao unga mkono upuuzi huu,sijui kuna uhusiano gani kati ya uvunjaji wa sheria na uislamu...muulizeni huyu DC kawai kukanyaga msikitini kama sio unafiki,lakini pia uislamu unaruhusu watu kuchakachua haki? Hakuna dini ambayo inahimiza kudai haki tena hata kwa nguvu pale mnapohisi inaminywa na wahuni wachache...Kwa wale wana-historia wanaweza kukumbuka source ya vita vya Jihad ni nini? Tuache kuficha ushenzi na uovu wetu katika dini,hii si sawa hata kidogo...
 
Hatushangai mama huyu kufanya hayo. Aliletwa Igunga kwa ajili ìyo kwani Dc aliyemtangulia aliondolewa kwa sababu aliitii katiba; hakuwa akishabikia chama chochote!
 
Kimsingi hali ya ccm hapa Igunga ni mahututi,hata baada ya kuleta lundo la viongozi bado umma wa Igunga umeonyesha dhahiri kuwa wapo tayari kwa mabadiliko
pamoja na vitisho kutoka kwa kundi haramu la green guard,ambalo Nape ameliruhusu kushambulia watu bado wanaIgunga wapo tayari kwa ukombozi.

Mkuu, hamasisha wana Igunga wenzako kikamilifu ili kuhakikisha kwamba hilo Lundo la viongozi na hao green guards wanaondoka Igunga Kwa aibu( ikiwezekana usiku) kabla matokeo hayajatangazwa. Hii ni nafasi muhimu kwa Wana Igunga kuliweka Taifa katika mwelekeo unaofaa.
 
Hatushangai mama huyu kufanya hayo. Aliletwa Igunga kwa ajili ìyo kwani Dc aliyemtangulia aliondolewa kwa sababu aliitii katiba; hakuwa akishabikia chama chochote!
Hili nilikuwa silikumbuki.....kweli mama yuko kikazi zaidi
 
Acha kubwabwaja kama kuku wa mayai wewe. Hao wameacha kazi kwa muda ili wapate nafasi ya kufanya kampeni zao lakini sheria ya nchi haimkatazi mtumishi wa serikali kujihusisha na siasa. Mfano mdogo huu utakusaidia kuondokana na utapiamlo wa mawazo; mawaziri wote ni watumishi wa serikali na wakati huo huo ni wanachama wa CCM. Tumia akili yako ikuzoee masaburi wewe.


I can now bet with anybody on how ur mind is empty! I'm not a teacher but I can help u to get rid of ignorance which you've been fed by Tambwe Hiza and Makamba Sr!
Mtumishi yeyote wa serikali haruhusiwi kufanya kazi kwa ushabiki wa chama chochote cha siasa. Wala haijalishi kama ni mwanachama wa chama fulani au la. Rc, ras, dc, ded hata makatibu wa wizara pa1 na katibu kata wote hawaruhusiwi sio tu kukifanyia chama kampeni bali hata kukishabikia na kuonesha upendeleo. Ni makosha kisheria na mshindi katika huo uchaguzi anakuwa sio halali kisheria. Kwahiyo hata huyo dalali wenu anaweza kupokwa ushindi na mahakama kama ikithibitika mahakamani.
Ndio maana nakusisitiza kutumia ubongo maana hujui unachoandika hapa!
 
Ni vyombo vya ulinzi na usalama tu ndiyo hawaruhusuriwi kuwa wanachama wa chama chochote, lakini wengine hawafungwi na katiba. Ndiyo maana katibu mkuu wa CCM wa sasa alikuwa katibu mkuu wa wizara gani sijui lakini akachaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama. Kama angekuwa haruhusiwi basi ingebidi ajiunge na chama ndiyo achaguliwe.


Ibara sipo specific ni ibara ya ngapi lakini hilo nalijua vizuri kuwz ni vyombo vya ulinzi na usalama tu


Filipo mkuu fanya research katika hili kuliko kuishia kulaumu.

Mkuu naomba ukaisome tena upya katiba ya nchi ili ujiridhishe na kuwa na uhakika wa watu wanaozuiliwa kujihusisha na siasa huku wakiwa watumishi wa umma.

Kitu kingine ambacho naona hujakielewa ni mantiki ya hoja ya Filipo; Kwamba hata kama kuna watumishi wa umma wasiozuiliwa kuwa wananchama wa chama cha siasa, watumishi hao hawaruhusiwi kutumia ofisi za umma kwa ajili ya shughuli za kisiasa. Anachodaiwa kufanya madame dc ni shughuli za kisiasa kukisaidia chama chake cha magamba.

Kama wangekuwa wanaruhusiwa kisheria na kikatiba wasingekuwa wanafanya kampeni kwa kificho, wangefanya hadharani lakini kwakuwa wanafahamu kwamba hawaruhusiwi ndio maana utaona toka walivyokamatwa isakamaliwa amekuwa akieleza kwamba alikuwa na mkutano wa ndani na watendaji wa vijiji, na hapa tena tumeambiwa alifanya vikao na akina mama wa magamba usiku kwenye jengo analotumia.

Tujaribu kutofautisha mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa na kutumia nafasi yake ya utumishi wa umma kukisaidia chama anachokiunga mkono. Na ndio maana kafumu na kashindye wamechukua likizo ili wajishughulishe na mambo ya siasa.
 
Kamateni tena makamanda, hao wanapewa pesa wakaandamane wanawakilisha matumbo yao kwa kujivika uislam, waislam tumetulia tunaangalia namna ya kuleta ustawi bora kwa taifa letu.
Kwa mtindo huo, hata suala la mabadiliko ya katiba litageuzwa kuwa la kidini! Itakuwa ni masikitiko makubwa na huzuni pale waislamu watakaporubuniwa na vibaka wa ccm kwa masilahi yao binafsi kwamba suala la mabadiliko ya katiba ni kwa ajili ya masilahi ya Wakristo au Chadema! Huko ndiko tunakoelekea! Bado tuna safari ndefu lakini tutafika tu!
 
I can now bet with anybody on how ur mind is empty! I'm not a teacher but I can help u to get rid of ignorance which you've been fed by Tambwe Hiza and Makamba Sr!
Mtumishi yeyote wa serikali haruhusiwi kufanya kazi kwa ushabiki wa chama chochote cha siasa. Wala haijalishi kama ni mwanachama wa chama fulani au la. Rc, ras, dc, ded hata makatibu wa wizara pa1 na katibu kata wote hawaruhusiwi sio tu kukifanyia chama kampeni bali hata kukishabikia na kuonesha upendeleo. Ni makosha kisheria na mshindi katika huo uchaguzi anakuwa sio halali kisheria. Kwahiyo hata huyo dalali wenu anaweza kupokwa ushindi na mahakama kama ikithibitika mahakamani.
Ndio maana nakusisitiza kutumia ubongo maana hujui unachoandika hapa!

Mkuu usipoteze nguvu zako bure kumuelimisha huyo kijakazi wa Nape. Hawezi kukuelewa anatumikia 55,000 per day.

Kama sio mambo ya multiple Ids asingekuwa anaendelea kuchangia hapa JF. Siku ile dc aliponaswa isakamaliwa akiwafanyia kampeni magamba, jamaa alilipuka hapa kwamba chadema wamemvua nguo, hadi suruali amefanya kuazima. Picha zilipotua hapa na kuonyesha kwamba dc ni mwanamke jamaa alipotea jukwaani ghafla hadi leo haonekani. Baada ya kutoonekana ndio ameibuka huyu philanderer akiwa na ujumbe ule ule!!
 
Dc ni mhalifu,na anataka kuficha uhalifu wake kupitia dini,eg anasema amevuliwa hijabu,ndugu zangu mkiangalia picha wakati DC anashikwa hakuwa amevaa hijabu,alivaa gauni fupi,na la mikono mifupi kinyume na sheria za dini ya kiislam,juu amevaa mtandio, haiwezekani kabisa kuvaa gauni la mikono mifupi,na fupi linaloishia magotini kisha kusema ni hijabu
Lakini alirekodiwa akisema mtandio wake,
 
Katiba ya nchi haimkatazi mkuu wa wilaya kushabikia na hata kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa. Tatizo wengi wenu magwanda ni wavivu wa kusoma.

" Na pia katiba ya nchi inamtaka mkuu wa wilaya kukipigia kampeni chama tawala wakati wa uchaguzi".
 
Back
Top Bottom