Wastaafu kuwakabili Slaa, Lipumba Igunga; Mangula aongezewa RC Masishanga, ma- DC wastaafu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,781
Mwandishi Wetu Raia Mwema | 21 Sep 2011 | Toleo na 204


  • Mangula aongezewa RC Masishanga, ma- DC wastaafu
  • CHADEMA, CUF sasa waonekana watagawa kura za ushindi

Imejitokeza hali ya kugawa kura za Upinzani katika uchaguzi mdogo wa Igunga, kati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), huku hali ya mambo ikiwa si shwari ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Raia Mwema ikielezwa kuwa mikakati ya hujuma imeshamiri ndani ya chama hicho.

Taarifa za ndani ya CCM zinabainisha kuwa mikakati hiyo inafadhiliwa na mmoja wa wanasiasa ndani ya chama hicho ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu na aliyepata kuwa mbunge. Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa kwa sasa kuna kambi ya chama kwa upande mmoja, na kambi ya mwanasiasa huyo kwa upande mwingine.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa kuwapo kwa katibu mkuu mstaafu wa CCM, Philip Mangula, kumesaidia kuanza kuvuruga mikakati ya hujuma ambayo inatajwa kuwa ilianza kushindwa kudhibitiwa na Katibu Mkuu wa sasa, Wilson Mukama.


Mbali na Mangula, kiongozi mwingine mstaafu wa CCM ambaye amekwisha kufika na kufanya kampeni Igunga ni rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye wakati yeye akiwa Mwenyekiti, Mangula alikuwa Katibu Mkuu, na wao ndio waliokabidhi mikoba ya chama hicho kwa Mwenyekiti Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Yusuf Makamba.


"Tangu amefika Mangula, hali kidogo imeanza kuleta matumaini ndani ya chama. Kambi ya chama na ile ya huyu jamaa zimeanza kuelekeza imani kwa Mangula kwa sababu yeye hayumo kwenye kundi lolote ndani ya siasa za chama kwa sasa...si unajua huyu mzee alistaafu na kwenda kulima kijijini kwake Njombe?," kilieleza chanzo chetu cha habari ndani ya CCM, Igunga.


Mangula anatajwa kubadili masuala mbalimbali yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho akitajwa kulenga kuboresha zaidi kasi ya kampeni za chama hicho.


Mangula abomoa mkakati

Inaelezwa kuwa Mangula amebomoa mkakati wa awali wa kampeni uliokuwa umesukwa na timu ya kampeni kabla ya kuwasili kwake huko. Awali, inaelezwa kuwa vituo vya uratibu wa kampeni ya CCM vilikuwa katika ngazi ya tarafa, lakini Mangula amebadili na kuviweka katika ngazi ya kata.

"Ametueleza kuwa kwenye tarafa si mahali muafaka kwa sababu unakuwa mbali na watu, kwa hiyo tumesogea sasa tuko kwenye kata. Mashambulizi ni katika kata. Nguvu kubwa sasa inabaki kwenye kata," kinaeleza chanzo chetu cha habari.


Mbali na uamuzi huo, inaelezwa kuwa nidhamu imeanza kurejea kati ya makundi yaliyokuwa yakihasimiana, kwa sababu Mangula anatajwa kuwa na uwezo wa kumkaripia yeyote katika makundi hayo.


"Kuna watu mwanzo walionekana hawakosei mbele ya Katibu Mkuu Mukama, lakini Mangula amekuwa mkweli, anakosoa na kumkaripia yeyote anapokosea. Kuna watu walikuwa wanawasilisha ripoti za hovyo na Mukama alikuwa akizikubali, lakini wengine wenye ripoti zenye ukweli walipuuzwa si kwa kigezo cha ubora wa ripoti zao bali masuala mengine binafsi.


"Kwa hiyo, Mzee Mangula ameleta nidhamu. Kuna watu wamekuwa wakirudishwa na ripoti zao za ubabaishaji....inawezekana walikuwa wanatumika kufanya hujuma. Huyu Mangula amekuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua ripoti, na kama umefanya ubabaishaji au kupachika uongo atakung'amua."


CCM na kampeni za kuvizia

Inaelezwa kuwa mgawanyo wa majukumu ya kampeni sasa umebadilika. Wakati wengine wakifanya kampeni za jukwaani, makada wengine wa chama hicho watakuwa wakifanya siasa za kufuata makundi ya watu, kama wazee, wanawake na vijana.

Taarifa za ndani ya CCM zinaeleza kuwa Mangula ndiye mwenye jukumu la kukabiliana na makundi ya wazee na anatarajiwa kuongezewa nguvu na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro sasa mstaafu, Stephen Masishanga, anayetajwa kuwa na heshima kubwa kwa watu wa kabila la Wasukuma, wilayani Igunga.


Katika orodha hiyo, wamo pia baadhi ya wakuu wa wilaya wastaafu wa Igunga, wanaotajwa kuwa na nguvu ya ushawishi wilayani humo, ambao pia jukumu lao litakuwa ni kampeni za chini kwa chini na si za jukwaani.


Miongoni mwao ni pamoja na aliyepata kuwa DC wa Igunga, Andrew Masanje, ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM, na DC mwingine wa zamani wa Igunga, Deogratius Mtambalike.


Viongozi hao wanatajwa kama wanaokubalika na wazee wa Igunga, kwa sababu wakati wa uongozi wao kama wakuu wa wilaya walikuwa karibu mno na jamii hiyo ya wana-Igunga.


Taarifa zaidi zinaeleza kuwa tayari Mangula amefanikiwa kubadili misimamo ya baadhi ya koo za kikabila, ukiwamo ule wa Wataturu, wanaotajwa kuwa awali walishawashiwa na wakajiunga na CHADEMA.


Taarifa zinaeleza kuwa ujio wa Mangula Igunga ni kama umeanika udhaifu wa Mukama. Sasa Mukama anazungumzwa na wana-CCM wanaoshiriki kampeni za Igunga kama kiongozi aliyekuwa hayapi uzito unaostahili masuala mazito yaliyokuwa yakijitokeza wakati wa kampeni.


"Wengi hawakuridhishwa na Mukama, wanasema alikuwa anachukulia mambo kirahisi mno, hakuwa makini. Alikuwa akipuuza taarifa nyingine nyeti.


Mikakati ya hujuma ndani ya CCM

Hata hivyo, inaelezwa kuwa ingawa CCM imekuwa na timu maalumu ya kampeni ya wanachama wake kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwamo Dar es Salaam, wapo baadhi ya wanachama, hasa vijana, wenye makazi Dar es Salaam na maeneo mengine nje ya Igunga, ambao wako Igunga kwa ufadhili maalumu.

Inadaiwa kuwa baadhi yao ni vijana ambao kuwapo kwao mjini Igunga, hakuna uhusiano wa moja kwa moja na chama na badala yake wamekuwa wakigharimiwa nje ya chama.


Inaelezwa kuwa kundi hilo linafadhiliwa liendelee kuwapo hapo kwa ajili ya kuratibu mikakati ya hujuma, ambayo ni pamoja na kushambulia au kuzomea baadhi ya viongozi wa chama hicho wasio na maslahi nao.


Hata hivyo, mipango hiyo imekuwa ikifanyika kwa siri kubwa, ingawa taarifa za ndani ya CCM zinaeleza kuwa wahusika wamekwisha kubainika na tayari wamekwisha kumhujumu mmoja wa viongozi wa kampeni hizo, kwa kumtengenezea tukio la kumdhalilisha, akidaiwa ‘kutembea' na mke wa mwanachama mwenzake.


Mgawo wa kura CUF, CHADEMA

Chama cha Wananchi (CUF) ambacho katika Uchaguzi Mkuu uliopita kilishinda nafasi ya pili kwa kupata kura 11,000 za ubunge, kwa mgombea wake, Leopard Mahona, kimekuwa kikikituhumu CHADEMA, kukihujumu kwa kulenga kugawa kura za upinzani.

Kwa mujibu wa CUF, CHADEMA ilipaswa kuiunga mkono kwa kuwa tayari CUF ina mtaji wa kura 11,000 za mwaka jana. Hata hivyo, CHADEMA kwa upande wake imekuwa ikiishambulia CUF kwa kudai ni CCM-B, na hivyo ina utata kuwapo katika kambi ya upinzani.


Mvutano kama huo umewahi kujitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana katika uchaguzi wa ubunge, Jimbo la Tarime, ambako mgombea wa CCM, Nyambari Chacha Nyangwine alishinda dhidi ya mgombea wa CHADEMA, Mwita Mwikabe na yule wa CUF, Charles Mwera.


CHADEMA yajizatiti kuweka mtandao

Kwa upande mwingine, taarifa kutoka ndani ya CHADEMA zinaeleza kuwa chama hicho kimejipanga ngazi ya kata ambako kila kata kumewekwa timu maalumu.

Timu hiyo katika kila kata inatajwa kuhusisha mbunge, vijana wanne kutoka vyuo vikuu na ofisa mmoja kutoka makao makuu ya chama hicho, ambao ndio wamekuwa waratibu wa ujio wa mgombea ubunge wao, Joseph Kashindye, kila anapofika huko kwa ajili ya mikutano ya hadhara.


Hata hivyo, pamoja na mkakati huo bado inaelezwa kuwa CUF imekuwa na nguvu kubwa katika baadhi ya maeneo kuliko CHADEMA ambayo pia katika baadhi ya maeneo imefanikiwa kuyadhibiti na ikitarajiwa yanaweza kuendelea kubaki kuwa ngome yake hadi wakati wa upigaji kura, Oktoba 2, mwaka huu.


Uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, unafanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Aziz, kujiuzulu baada ya kutakiwa "ajivue gamba" ndani ya chama hicho kwa kujiuzulu nyadhifa zake za kisiasa, naye akajivua zote hadi ubunge.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,189
Vijana wapiga kura wapya ambao ndio wengi zaidi Igunga kamwe hawana Time na Wanasiasi ZILIPENDWA type kama hao ambao baada ya kutelekezwa na Kikwete leo hii wanalazimishwa kwa nguvu kwenda kukinadi Chama Cha Magamba Igunga.

Hata na hawa wazee wenyewe hivi sasa wanalazimika kunadi bidhaa ambayo hata wao wenyewe hawaiamini hata tone sasa nani aje akaamini maneno yao juu ya urembo wa CCM leo hii?????????????
 

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,740
742
Jk alitupa dhahabu akaokota magalasha sasa anakumbuka kumbe ile ilikuwa dhahabu, mzee Mangula na Mashishanga Jk aliwatupa eti coz hawakumuunga mkono, si wakati wote utaungwa mkono na kila mtu, angekuwa alikuwa na akili ya kujua haya Jk hakika angekuwa amejenga ccm imara sasa anakumbuka blanket wakati kumekucha pole Mkweere
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,189
SALA ZA CCM MBALIMBAALI ZILIZOPIGA KAMBI VIJIJI VYA IGUNGA KUTETEA
'MDUDU UFISADI' KWA NGUVU YA DOLA, HALI NA MALI NA MATOKEO TARAJIWA MARA BAADA YA KUMPATA MRITHI WA ROSTAMU


Kwa kweli wadaduji mbali mbali wa mambo ya kisiasa nchini pengine watapata ka-muda kuchimbua zaidi undani wa punje la wazo kwamba uchaguzi Igunga inayo kila dalili ya kuwa a
'MONUMENTAL ANTI-CLIMAX' (kikatisha Burudani cha kihistoria) kwa chama Tawala na mahasimu wa jadi ndani mwake.


CCM Kikwete-NdiaMukama-Nnaye

Moja, wala si siri tena kwamba hivi sasa CCM Kikwete-NdiaMukma-Nnaye, CCM dhaifu-chokambaya-na sura halisi ya watetezi wa UFISADI nchini, itakua na hali ngumu haijapata kutokea n hali hiyo itakua mbaya zaidi endapo CHADEMA wangeweza kukubali na kukiruhusu CCM kishinde Igunga - bahati tu zuri kwa CCM hiyo hapo juu ni kwamba CHADEMA kitawasaidia kuchukua kiti hicho na kusaidia kuwaondolea masimango kwa wana-CCM wenzao waliowaengua kwenye jukwaa kuu la siasa kutokana na ugonjwa CHOYO MOYONI na kitoto kujihisi kidume cha mji kuliko baba yake.

Kikundi hiki mpaka sasa kimelika mno na kutu na kutapaka choo cha UFISADI mwili mzima. Ni nani anayeweza kubisha kwamba CCM hii isioona mbali ilienda tu Igunga kutimiza ratiba kwa kuwa Mzee Kiravu na Tendwa wasingeweza kuruhusu vinginevyo???

Kwa kifupi, hii ni CCM-Mikono-kichwani baada ya mtoto kupata hekima za 'Mtoto-akililia Wembe'. Hii ni CCM kijani mpauko ambayo haifahamiki saaana kote kwa wakulima hata akina Mgaya nchini; lakini ni CCM iliyojaa ukwasi wa rasilmali kedede lakibi isiopendeka hata kwa dawa wala kuonyesha dalili za kujua wanakodhamiria kulipeleka taifa.

CCM hii ni ile ilikwenda Igunga ikiwa ni Vuguvugu-Moto-na- Baridi-barafu kwa wakati mmoja kuhusu swala nyeti kwa wengi wa wapiga kura walazwahoi nchini - UFISADI na vita kuiteketeza nchini ili wananchi tupate japo ahueni.

Kwa hapa vinara wake ni akina Zungu wa Ilala, Masaburi wa Musoma, Mzee Ruksa, Mzee waa Usingizi, Mzee Msekwa, Anna Abdalla, Meghji, Kamanda Ngunguli Mahita, Ridhiwani Kikwete, Vita Kawawa, Hussein Mwinyi, Tambwe Hiza akiwa ni mfungaji wa kutegemewa sana hadi pale aliponyeshwa lango baada ya msajili wake Mzee Yussufu kutundishwa daluga kwa kwa kuchezea mdomo sana kinyume na taratibu za siasa tunazotaka vija.

CCM Rostamu-Aziza-Chenge-Lowassa

Pili, hii CCM hapa wengi huwaita CCM-Mapacha-Watatu. Lakini kwangu nitawata CCM Rangi-Tatu-Mbagala. Hii CCM ni le iliokwenda kwenye kampeni Igunga ikiwa imejaa uvundo wa minoti ya kukwapuliwa kwa walipakodi, ikawa inahemea mashine baadaya kinara wake Azizi kugeuziwa moshi wa moto uliokokwa na wananchi kwa kunyunyizia pilipili katika kila pembe ya taifa hili.

CCM ni ile isiyotazamana uso kwa uso na Nape Nnauye pamoja na bosi wake Ndiamukama LAKINI huku wakigongeana dole-gumba-juu na Mzee wa kaya kiaina na kutabasamu kusikoisha juu ya CINEMA inayoendelea hadi sasa chamani kwao.

Ni nani asiyejua kwamba hizo ishara mbili mpaka sasa zimewaacha Mi-kada kibao CCM vichwa chini na kuishiwa nguvu kabisa hata ya kuwawezesha kutekeleza ile ilani tanzu ya CCM ya 'BISHANA MPAKA KUFA PINDI UKUTANAPO NA ADUI MPINZANI' nchini?????

Kwa kifupi, ni kwa sababu jimbo la Igunga ilikua ilishikiliwa mateka kifedha na 'Mtuhumiwa-Mbarikiwa-wa-Chama' Rostamu Aziz hadi kunapoitishwa uchaguzi huu mdogo.

Hii ndio maana chukizo la Watanzania tuliowengi na kusababisha kupigwa chini kule ghafla limegeuka dhahabu na Jiwe la Pembeni kwa Wana-CCM 'Watakatifu-Wakingavifua kwa Ufisadi nchini.

Jambo hili hapa ni zaidi ya 'Simulizi za Kusisimua' kwa vizazi vijavyo kuhusu swala zima la 'Taifa letu: Utawala wake na Sura Mia za Watawala Vipindi Kadhaa baada Mapumziko ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere'.

Kwa msingi huo, ushindi wowote wa CCM kwa jimbo la Igunga na lingine lolote la aina hiyo (Monduli) ni sharti litegemee tabasamu usoni mwao hawa Mbagala-Rangi-Tatu kutoa ufunguo wa fedha ili rafu za Makame 2010 ziweze kujirudia kwa kishindo.

Tofauti na hapo ushindi wa CCM hata kwa kukodisha Mizee yetu Mistaafu ni kupoteza tu wakati wakati kundi hili likiendelea kukazia nati mara mbili zaidi ya Kundi la Mzee Mkapa wanavyotafuta pa kutokea kuokoa jahazi lililokwisha zamishwa robo-tatu chini ya bahari.

Kwa kweli CCM hii ni dola kamili bila uhalali (a Political Power-base without legitimate authority yet are the real rulers by design) mbele ya macho ya wapiga kura wa nchi hii zaidi tu ya kufikia walikofikia kwa miujiza ya Mashua Donari 30.

Hatima ya CCM hii iko mashakani kila dakika zinavyosogea, machoni mwao CCM-Originals and Hardcore Party Conservatives, bila kujali kwamba chama kitnufaika au kupoteza nini kutokana na wao.

Ni kwa sababu hii ndio maana CCM Mbagaala-Rangi-Tatu hivi sasa imechukua CCM Mpauko nayo mateka na kuanza kutumia kiti cha Igunga na viti vingine vinavyofanania kuwa ni sehemu kamili ya wao kuwatafuta CCM Conservatives masikio KUTUPILIA MBALI KITANGA 'VUA MAGAMBA', kama walivyokwishaafiki CCM mpauko, ili ndio waweze kuleta Miujiza-Makame-2010 CCM kuzoa viti vingi vya ubunge si kwa itiko la wapiga kura bali ni kwa kupitia mtelezo tarakimu wa vikokotozi telezi kwa msaada wa baadhi ya 'Vijana wa Makumbusho' kama ilivyowahi kudaiwa huko nyuma kidogo.

Je, dua hizi huenda zikalazimika kuitikiwa huko CCM kwa gharama yoyote ile na ni akina nani hao ambao wangependa kushuhudia gharama hizo kama vile kugeuzwa KANU ya kule Kenya na wapiga kura????

Washika bendera wa CCM hii ni pamoja na akina Makongoro Mahanga, Nazir Karamagi, Mgeja, Gamanywa, January Makamba, 'Wasomi' wetu Prof Majimarefu na Lusinde, Masipika wote wa sasa bungeni, Bendera, Kimbau wa Mafia, Lamek Airo, Ngeleja, Nahodha wa Zenji, Nchimbi na Rijali Mwigulu Nchema, kwa uchache tu!!


CCM-Mka
pa-Filipo-na-Mashishanga


Tatu, hii ni CCM-kipindi mpito. CCM hii inazo sura za CCM Nyerere ilioaminika sana na kuwa na upendo mkuu kwa raia wake na wakati huo huo inayo CCM chat 'Wachacharika wa enzi zao Abdalla Kigoda, Jeuri Masilingi, Mashishanga, Mangula, Limbu, Prof Sarungi, Ole Sendeka, Kilango Malecela, Samueli Malecela, Mzee Joseph Rwegasira, Sir George Kahama, Salim Ahmed Salim, Mzee Sinde Warioba ...; hapa ni CCM mchanganyiko maalu kati ya Pure Nyerereists na Political Orphans wa serikali za awamu mbalimbali.

Kwa wale wanaoendelea kutazama na kutathmini vihoja na matukio ya CCM Igunga bila shaka watakubali kwamba kuna sura ambazo hakuna hata Mtanzania aliyefikiria kujitokeza kwao ulingoni.

Hii ni sawa na kusema kwa CCM wamejikuta 'RESERVE COMBATANTS' wakiwa kwenye mbuga za vita vya siasa za kisasa Igunga huku wengi wao wakiwa wamesahau budi zao ukutani majumbani kwao na hata wengine kuonekana kusahau kabisa hata mbinu rahisi tu za kivita kisiasa wangali huko Igunga.

Kwa jicho la jirani saaana, ni ruksa kabisa mtu atakaye waita hawa generation ya akina Mangula na Mashishanga, kujitupa kwao uwanja wa siasa Igunga huku jua likiwa tayari limewazamia, kuwa CCM's LAST SUICIDE CAMPAIGN MACHINE ama kwa urahisi zaidi kuwaita 'CCM ZILIPENDWA' aambao uwepo wao kule Igunga wala hakujatokana naa kuunga kwao ama CCM Mpauko au CCM Mbaga Rangi-Tatu wala kuwa na uwezo wowote wa kuweza kuhimili siasa za vijana wa kileo (Doti Kom Politics) bali tu lao ni kule kupiga moyo konde na kujiapishaa kwamba CHADEMA watugaragaze tu uwanjani kuliko kuwaachia kila kitu kana kwamba sisi sote ndani ya CCM hatupo.

This is very desparate indeed of the people's once darling political party - a home for the society's grays, come rain come sunshine!!!!!!!! Mpaka hapa bado tunasema tathmini za CCM mbali mbali, ming'ato za 'maadui' wasiopatanika hata kwa shekhe wala askofu wa ndani kwa ndani yaa chama na ndoa za kuvungiana Igunga bado inaendelea ...

CHADEMA CURBS; Makamanda Lema, Zitto, Mr II, Owenya, Abwao, Mnyika, BAVICHA, Wana-Igunga wa Vyuo Vikuu mbali mbali nchini pamoja na 'Think Tank' wote wa Chama CDM People's Power, chukueni hizo na zaidi mwendo mchaka mchaka CCM Zilipendwa ulimi nje hata kabla ya ngwe ya lala salama kuwadia Igunga -- tupo pamoja???????
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,189
CCM sampuli mbalimbali kule Igunga ni sawa na mchanganyiko wa maji na petroli, hata angeletwa mkemia mkuu hawezi kufanya Dr Mwakyembe kufanya kazi na Lowassa Igunga wala Mungai kwa Tambwe Hizza.

Hakika ni hatari tupu lakini salama.
 

The Stig

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,117
1,101
Katika mataifa yalioendelea, ukishastaafu siasa, unawaachia kizazi kilichokuridhi. Unakubali kuwa ulishapewa chance na umefanya uliyoweza kufanya - ni wakati wa kupumzika, taifa ni zaidi ya wewe mwenyewe.

Hakuna watu waliitetemesha dunia kama Margareth Thatcher, George Bush, Dick Cheney au hata akina Nelson Mandela. Lakini leo hautwasikia wakisema chochote. Wamewaachia kizazi kipya.

Hapa TZ siyo kwamba tu hawanyamazi, la hasha. Hapa WANAPIGA KAMPENI kabisa!!!!
 

mwaJ

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
4,074
2,942
Mh! Magamba yatawafufua wote waliosahaulika! Yanajitahidi kuchekecha walao wachache wasio na kashfa nyingi wakasaidie kuokoa jahazi!
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,189
Hapo kwenye RED, kwa hali ya kawaida huko nyuma mambo yakiwa magumu sana watu walikua na kawaida ya kukimbilia kwa WAZEE WA HESHIMA kwenda kutafuta majibu ya maswali magumu, LAKINI sasa kwa hili la CCM ZILIPENDWA kujimwaga wenyewe Igunga baada ya kutambua upepo wa mabadiliko haina simile tena sasa kukitokea hali ya 'Maswali Magumu' kitaifa sasa Tanzania tutawakimbilia akina nani???????

Ni nani atakayewaokoa hawa wazee wetu wa CCM na hatari ya ugonjwa wa 'MAPIGO YA MOYO KUPANDA MAPIGO YA MOYO KUSHUKA' kwa jinsi matokeo ya Igunga yanavyotarajiwa kutua kibindoni mwao CDM People's Power?????????

Wasije wakasema ya kwamba hawakutahadhaarishwa vya kutosha kuhusu azma za vijana nchini kukipa kisogo CCM na kukinyanyua CDM tangu Igunga leo hadi Ikulu hapo 2015??????????

Katika mataifa yalioendelea, ukishastaafu siasa, unawaachia kizazi kilichokuridhi. Unakubali kuwa ulishapewa chance na umefanya uliyoweza kufanya - ni wakati wa kupumzika, taifa ni zaidi ya wewe mwenyewe.

Hakuna watu waliitetemesha dunia kama Margareth Thatcher, George Bush, Dick Cheney au hata akina Nelson Mandela. Lakini leo hautwasikia wakisema chochote. Wamewaachia kizazi kipya.

Hapa TZ siyo kwamba tu hawanyamazi, la hasha. Hapa WANAPIGA KAMPENI kabisa!!!!
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
mliokuwa hamuamini kuwa CCM imeishiwa nafikiri kwa mtaji huu sasa mtahamini sasa.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,189
MADAI YA WATAZAMAJI WA UCHAGUZI EU KUHUSU UCHAGUZI WA TANZANIA:
CCM NI ILE ILE NA MBINU ZILE ZILE SAWA NA MWANGA ASiYE nA UWEZO WA KUBADILISHA TABIA YAKE KWA SIKU MOJA TU


Mzee Katapila ni miongoni mwao wale CCM Conservatives wachache waliobakia ndani ya chama hicho ambao, kama kawaida ya ile CCM ya enzi za Mwalimu Nyerere na umiliki wa Wakulima na Wafanyakazi, kwake yeye anaamini hawa CCM Mbagala Rangi Tatu wote ni watu wa kufukuzwa milele kutoka kwenye chama bila hata kufunika maneno na utamu wowote wa sukari kwa nje.

Naye pia kama Jeshi lingine la 'Wastaafu wa Kisiasa' ndani ya chama hiki, CCM Kijani Mpauko badala ya kile kilichozoeleka kama CCM Kijani ya Mgomba, endapo ataonekana kule Igunga kwa kipindi chchote kile cha kampeni basi ni wazi ujue kwamba kaamua tu kujitoa mhanga bila kujali reputation yake kwa mtaji wa yale yatakayotokea kwenye sanduku la kura Igunga.

Haya yote ninayoyanyumbua hapa, ifahamike kwa mtu na au kikukundi, kwamba DUNIA NZIMA iko Igunga wiki 7 tangu kabla kampeni hazijaanza rasmi hapa. Yale ya mwaka jana Kuchakachua kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita hivi sasa ymewekwa kwenye kimuliko kikali mno kutaka kujiridhisha kama madai yale yalikua ni ya kweli kiasi gani vile.

Hii inamaana kwamba licha ya CCM na vurugu za Watumishi wa Umma kama vile Ma-DC na RCs kuamua kujiingiza kwenye siasa kukipigia chapuo CCM kwa masikitiko ya vile vyama vingine vya ushindani, Chama Cha Mapinduzi ndicho kikundi kimojawapo nchini ambacho kinaingia kwenye chaguzi hizi kwa woga mkubwa toka kwa wananchi wake na washikdau wa kimataifa kwa ujumla wao.

Hakika mpaka sasa kitendo cha CCM kuingiza tena UDINI kwenye kampeni zake Igunga, Rushwa ya pishi la ubwabwa, ugawaji fedha na mahindi ya msaada hasa kwa wakati huu wa kampeni, na matmizi ya VYOMBO VYA DOLA kwa faida yake kwenye uchaguzi huu mpaka sasa ni tope zito ambalo sijui watalibanduaje wenzetu hawa.

Karibu kila kilichoripotiwa na Watazamaji wa EU hivi sasa ni maradufu zaidi Igunga - mbona ni sikitiko kuuu kwa CCM hivi!!!!!!!!!!!!!!!

Jamani Tingatinga bado kufika Igunga?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom