"CUF ni CCM- B". - Kampeni ya CHADEMA Igunga na uchaguzi mkuu 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"CUF ni CCM- B". - Kampeni ya CHADEMA Igunga na uchaguzi mkuu 2015

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Zawadi Ngoda, Nov 6, 2011.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Igunga alitumia dakika 20 katika moja ya kampeni zake nilizohudhuria kueleza kuwa CUF ni CCM-B. Kwa muda wote huo nilikuwa nasubiri kusikia jinsi atavyotatua matatizo ya wanaigunga (maji, kilimo, elimu n.k) pale akichaguliwa kuwa mbunge. Kwa bahati mbaya uvumilivu wangu ulikwisha baada ya dakika 20, kwani alikuwa ameganda kwenye topic moja "CUF ni CCM-B". Ukweli niliondoka kimya kimya, sijui kama baadae alizungumzia matatizo yanayowakabili wananchi wa Igunga na ufumbuzi wake. sidhani!

  Alipokuja Tindu Lisu (mbunge-CHADEMA) Katika kampeni hizo nilikuwa na hamu sana ya kumsikiliza kwani nimemsoma katika magazeti tu. Huyu alitumia dakika 30 kueleza kuwa CUF ni CCM-B. Ilipofikia dakika ya 30 niliondoka kistaarabu bila kumwabia yeyote yule hata rafiki yangu niliyekuja naye pale.

  Katika uchaguzi mkuu 2015, eti hiyo ndio 'KARATA DUME' wanayoitegemea kuieleza Tanzania nzima. Inawezekanaje kuingia IKULU kwa kuwaeleza wananchi milioni 30 kuwa CUF ni CCM- B.

  Wananchi wanataka kujua ni jinsi gani CHADEMA MNA dawa ya kuondoa matatizo yao yanayowakabili kila siku? Umasikini, elimu, matibabu, miundo mbinu, kilimo duni njaa n.k

  Kwa mtindo wa kampeni hizo ninahakikisha kuwa Tanzania hatuna vyama vya upinzani, na hasa CHADEMA ndio bure kabisa. Najuta kwenda kwenye kampeni zao, huwezi kujifunza lolote lile.
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Usichague chama wewe chagua "mgombea" kwa uwezo wake..

  Mimi nimeshaacha mambo ya chama naangalia "uwezo wa mgombea" period

  Vyama vyote na kelele tu
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  huyo mtu anakuwa mgombea binafsi au??
  unajichanganya changanya tu!!
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Wewe mwenyewe umetaja CFF ni CCM-B mara ngapi hapo juu???

  Hebu tukumbushe CUF walipata kura ngapi kule Igunga.
   
 5. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni mpya, nafikiri sasa hivi nianze kampeni ya kuwaelewesha watanzania kuchagua mtu na sio chama. Lakini kuna wanaoamini kuwa ukiwa umezungukwa katika CHAMA na akina Chako changu na changu ni changu, hata ukiwa mzuri namna gani hutaweza kuongoza nchi vizuri.

  Kwa hiyo naomba unishawishi ni vipi unaweza kuondoa ufisadi ikiwa wewe ni mgombea wa CCM? Nauliza hivi kwa nimekutana na watu wsemao kuwa hata ukiwa kiongozi mzuri maadam umechaguliwa kwa tiketi ya CCM huwezi kuondoa rushwa. Nawe wasema vinginevy, hebu nipashe.
   
 6. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Sizungumzii CUF, NAzungumzia CHADEMA NA KAMPENI ZAKE. Shauku yangu si kura ngapi walipata CHADEMA, bali ni ufinyu wa kampeni zao.
   
 7. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Bado tu mnaweweseka na Igunga? Kazi iliyokuwepo kule mnaitambua, ukichanganya na damu mliyoimwaga kumpa kafumu msalaba wa ubunge itachukua mda kuacha kuweweseka.
   
 8. madatta

  madatta Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  swala si nini CDM/CUF itawafanyia nini. Ahadi na porojo za uchaguzi CCM imeshaahidi ahadi nyingi ambazo hata hazitatekelezwa. jK anaahadi ngapi?
  Basi elewa watu wameshachoka na ahadi wanaangalia mtu na chama haitaji uende chuo kikuu kulitambua hilo.
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na wewe unaweza kutukumbusha magamba walipata kura ngapi????hebu acheni upinzani wa kijinga ndani ya upinzani,haiwezekani watu wooooote wasiokua magamba wakawa chadema na kama ambavyo ilivyo ni ngumu kwa watu wote wasiokuwa magamba kuwa cuf,huo ndio ukweli na hiyo ndio demokrasia duniani kote iko hivyo!sasa nini cha kufanya hapa ili kuwazidi magamba ujanja wao,vyama vyote vya upinzani viungane,cuf na chadema waliwahi kuonyesha mfano wa kuungana na kusimamisha mgombea mmoja wa urais na pia kuachiana majimbo,lakini sijui wameingiwa na wazimu gani sijui eti ndio wamekuwa wapinzani ndani ya upinzani!!!sidhani kama kweli wote wana nia thabiti ya kuwaondoa magamba madarakani...hali hii iko kwa viongozi mpaka kwenu nyie humu ndani mnaojifanya wakereketwa uchwara wa chadema na vyama vingine vya upinzani,mnashambuliana wenyewe kwa wenyewe!!!
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,566
  Likes Received: 4,687
  Trophy Points: 280
  Kwani uongo kuwa CUF ni CCM B?
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  CUF kuwa CCM B ina changia vipi ktk matatizo ya wananchi.
   
 12. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa yaliyokukuta, achana na mikutano yao, hawana sera zaidi ni taarabu tu i.e majungu.
   
 13. W

  Welu JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Mtoa mada acha uongo. Propaganda za kijinga unamhadithia nani? Hivi watu ZAIDI ya 23000 waliopigia kura CDM unadhani waliichagua kwa ajili gani? Kwa taarifa yako muda wa kudanganya watu haupo tena. Lengo lazima magamba wang'oke 2015. Ebu tazama ulivyojichanganya kwenye post yako "baada ya dak 20 niliondoka. Je ulimsikieje Lissu dak 30 wakati ulikuwa hupo?" Ndio nyie mliokuwa mkidanganya watu kuwa "mkichagua upinzani wataleta vita".
   
 14. Officer2009

  Officer2009 JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kwa kuwa uwezo wako wa kufikiri ni mdogo, acha nikusaidie kureason ni kwa nini zilitumiwa dkk 20 kuiponda CUF. CUF ilikuwa ikijinadi kuwa yenyewe pia ni chama pinzani. Katika mazingira kama Tz, maendeleo ya watu yamezuiwa na mfumo mbovu pamoja na sera zisozotekelezwa za CCM. Hatua ya kwanza ya kutatua kero ya wananchi ni kuwafungua macho kwa kuwaeleza mabaya na maovu ya ccm. Sasa kwa kuwa lengo ni kuleta maendeleo kwa kuindoa ccm madarakani, ni vizuri na sahihi kuilezea uma ni jinsi gani na kivipi cuf ni ccm b. Upo? Tumia akili kufikiri, usitumie masaburi!
   
 15. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mleta mdaa nazani umekuja kishabiki kwanini nakwambia ivi?ebu tujuze aadi ambazo cuf walizitoa igunga zaidi ya kuiponda cdm kwamba imekuja kugawa kura za upinzani.pia ivi unajua sababu zilizosababisha cuf kuitwa ccmb?na je ulishawai kujiuliza ni kwanini chama kinapokubalika kwa wakati fulani apa tanzania huweza kuundiwa zengwe ili kiweze kudhoofishwa?
   
 16. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Wazo la leo: kuing'oa ccm CDM inabidi isimame peke yake na kisiungane na chama chochote cha upinzani. Vyama vingine ni CCM B, CCM C, CCM........J. Msilogwe mkadanganywa hata kwa lugha gani kuungana. Hata hivyo kuna ushirika gani kati ya sera za CDM na vyama vingine? Kila chama kina sera yake. Mkitaka kuungana, ili muungano uonekane wa dhati inabidi kila chama kukana sera zake na kuanza sera mpya. Je hii inawezekana? CDM songa mbele ushindi ni dhahiri 2015. Isipokuwa anzeni kuandaa watu kuanzia sasa.
   
 17. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ccm ndo sana inafurahi kuona upinzani kutofautiana ukweli tofauti hizi za kupeana majina ya ccm b hazina faida
   
Loading...