David Silinde: Nilivutiwa sana na aina ya siasa za Dkt. Slaa na Zitto Kabwe ndipo nikajiunga CHADEMA

..huyu alichanga karata zake vibaya.

..angejisalimisha kwa ccm mapema.

..vilevile alitakiwa awe mwehu-mwehu na ajilipue kama wenzake wakina Waitara na Mollel.

..huo upole unamponza.
Siasa ni sayansi

Huu ndio wakati muafaka na barua yake ya kujiunga CCM aliileta kitambo yeye na Mnyika!
 
Achague chama ambacho kinaendekeza usaliti.
Mbunge wa Momba mh David Silinde yuko mubashara Star tv katika kipindi cha medani za siasa akizungumzia sintofahamu ya uanachama wake ndani ya Chadema.

Up dates;

Silinde amesema yeye siyo mwanaharakati hata Mbowe analijua hilo na kwamba yeye na Zitto ni marafiki lakini baadhi ya viongozi hawalipendi hili.

Silinde anahoji Halima Mdee amekuwa na urafiki na Ester Bulaya tangu mwaka 2010 wakati huo Bulaya akiwa CCM na wamekuwa wakiishi nyumba moja wakati wote huo wawapo bungeni lakini hakuna aliyehoji. Kwahiyo Silinde anasema mambo ya kuchaguliana marafiki yamepitwa na wakati na kwamba yeye ana marafiki wengi CCM kama ambavyo wabunge wengi tu wa Chadema wana marafiki wengi.

Silinde anasema kwa sasa yeye ni mtu huru na wiki mbili zijazo atatoa msimamo wake kwamba anakwenda wapi.
Anasisitiza kuwa Mbowe ni kama mfalme pale Chadema na hataki kupingwa kwa lolote na ukijaribu kumpinga utaitwa ni msaliti.

Silinde anasema wabunge wa kuchaguliwa wanakatwa 10% ya mshahara wao kuchangia ujenzi wa chama na wabunge wa viti maalumu wanachangia 30% ya mishahara yao.

Silinde anasisitiza kuwa atagombea tena ubunge mwezi October kupitia chama atakachohamia!

Silinde amemalizia kwa kuishauri Chadema ijitahidi kuiheshimu katiba yake maana Mbowe anakanyaga katiba ya chama sasa kwa tabia hii wakiingia Ikulu Mbowe na genge lake wataisigina katiba kabisa. Fikiria alivyolazimisha wabunge kwenda karantini wakati hawajacontact na mgonjwa yoyote wa Corona sasa huu kama siyo udikteta ni nini?

Maendeleo hayana vyama!
 
Mi nacheka ikiwekwa thread ya Silinde kuongea, BAVICHA wanavyoamshwa hata kama wamelala kuja kupinga bila kuelewa wanachopinga!
 
Bwashee usikariri mifano ya zamani toa ya hivi karibuni ya akina Mwita Waitara na Dr Mollel!
Sisi makada wazoefu tunaumia sana.

Kitakachofuata ni kuroga na kuwawekea sumu panya buku wote.

Haiwezekani tujenge chama wageni waje,tuambiwe sisi tumejaza sebule. Tutawapunguza wenyewe.

Sent using iphone pro max
 
Silinde hajui karantini ilikuwa ni kwa ajili ya kucheki afya zao?

Hajui karantini ni ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya?

Wamekaririshwa kumshambulia Mbowe wote wanaimbishwa wimbo wa dikteta kama kasuku, nao wanaitikia tu, sijui hata kama wanajua maana ya dikteta.

Analakamika kukatwa mshahara kuchangia chama, leo ndio amejua hilo ni tatizo? siku zote alikuwa wapi kulisemea hilo? au sababu alikuwa bado hajatongozwa na CCM/NCCR!

Anazungumzia kuchaguliwa marafiki, hii sababu ya kitoto sijui kaitoa wapi, yaani hajui mpaka leo kilichomfanya akaondolewa CDM? au anataka kuwadanganya wajinga!.

Kama hawezi kukubaliana na mawazo ya wenzake anaamua kupita njia zake bora akatafute panapomfaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati walikuwa wanazurura mtaani?hivi kwanini Mbowe atoze ushuru wabunge CHADEMA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kituko cha Mwaka,unajilockdown na kujiunlock mwenyewe,halafu unarudi mazingira yaleyale
 
Kituko cha Mwaka,unajilockdown na kujiunlock mwenyewe,halafu unarudi mazingira yaleyale
Kosa liko wapi acha ujinga, hao ambao wako lockdown baada ya lockdown si wanarudi mazingira Yale Yale, Kama ulikua huendi kazin baada ya lockdown unarudi kazini dunia kote ndo hivyo wanafanya ama kweli ujinga ni mzigo
 
Back
Top Bottom