Zitto Kabwe amefeli sana kwenye siasa tangia arubuniwe kuisambaratisha CHADEMA amekwenda ACT hana tena mvuto ameamua kustaafu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Msaliti hana maisha marefu kwenye siasa. Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo waliandaa njama yakuivuruga CHADEMA , wakakamatwa na kufukuzwa. Akaenda kuanzisha chama chake kwa lengo lakuisambaratisha chadema . Amepambana awezavyo ameshindwa imemlazimu aamue kung'atuka chama kisife mikononi mwake.

Lakini alikuwa anakubalika sana kwenye jamii, leo hakuna mtu anayefuatilia siasa zake. Ameungana rasmi na akina Cheyo na Lipumba.

Waliomtuma kuivuruga chadema bado wanamfadhili au walishatumbuliwa ? Alifaidika nini na huo usaliti?
 
Huyu anautaka uwenyekiti tu ,mda mwalimu mzuri
 
KILA ATAKAYEJARIBU KUIUA CHADEMA ATAKUFA YEYE CHADEMA ni mpango wa MUNGU

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Msaliti hana maisha marefu kwenye siasa. Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo waliandaa njama yakuivuruga CHADEMA , wakakamatwa na kufukuzwa. Akaenda kuanzisha chama chake kwa lengo lakuisambaratisha chadema . Amepambana awezavyo ameshindwa imemlazimu aamue kung'atuka chama kisife mikononi mwake.

Lakini alikuwa anakubalika sana kwenye jamii, leo hakuna mtu anayefuatilia siasa zake. Ameungana rasmi na akina Cheyo na Lipumba.

Waliomtuma kuivuruga chadema bado wanamfadhili au walishatumbuliwa ? Alifaidika nini na huo usaliti?
Kama amefeli ebu niambie leo hii Chadema Ina wabunge wangapi?
 
Mbowe anashutumiwa kwa kuhodhi madaraka na kutostaafu, anatakiwa astaafu.

Zitto anashutumiwa kwa kustaafu.

Lawama haziishi. Ukistaafu, usipostaafu, lawama tu.
Shutuma huwa zina maana kwa wanaozitengeneza. Ukiangalia CCM woote wanataka Mbowe ajiuzulu kwasababu wameshindwa kuimaliza CHADEMA. Huyu Zitto, Wapinzani woote hawamtaki kwa sababu wanaamini anatumiwa na ccm.
Yote nanaweza kuwa kweli lakini pia sijui kama yakitokea watapata wanachotaka.
 
Mbowe mbona kama kashatulizwa na hana makali yoyote.

Mimi napenda logical consistency tu.

Kama kuhodhi madaraka muda mrefu ni kitu kibaya, basi tusimlaumu Zitto kujiuzulu. In fact Zitto anatakiwa awe mfano wa kuigwa hapo.

Kama kujiuzulu katika mapambano ni kitu kibaya, basi tusimtake Mbowe ajiuzulu katikati ya mapambano.

Kwa sasa hivi, kwa uchambuzi uliouandika, inaonekana karata ya kujiuzulu inatumika kisiasa tu kwa interests za watu, na inakosa uzito wa hoja kubwa za kifalsafa.

It's just games to win at politics, not deep rooted governance issues. There is a big difference.
 
Msaliti hana maisha marefu kwenye siasa. Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo waliandaa njama yakuivuruga CHADEMA , wakakamatwa na kufukuzwa. Akaenda kuanzisha chama chake kwa lengo lakuisambaratisha chadema . Amepambana awezavyo ameshindwa imemlazimu aamue kung'atuka chama kisife mikononi mwake.

Lakini alikuwa anakubalika sana kwenye jamii, leo hakuna mtu anayefuatilia siasa zake. Ameungana rasmi na akina Cheyo na Lipumba.

Waliomtuma kuivuruga chadema bado wanamfadhili au walishatumbuliwa ? Alifaidika nini na huo usaliti?
The toilet paper theory...! Well preserved and adorable before used...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe mbona kama kashatulizwa na hana makali yoyote.

Mimi napenda logical consistency tu.

Kama kuhodhi madaraka muda mrefu ni kitu kibaya, basi tusimlaumu Zitto kujiuzulu. In fact Zitto anatakiwa awe mfano wa kuigwa hapo.

Kama kujiuzulu katika mapambano ni kitu kibaya, basi tusimtake Mbowe ajiuzulu katikati ya mapambano.

Kwa sasa hivi, kwa uchambuzi uliouandika, inaonekana karata ya kujiuzulu inatumika kisiasa tu kwa interests za watu, na inakosa uzito wa hoja kubwa za kifalsafa.

It's just games to win at politics, not deep rooted governance issues. There is a big difference.
Inawezekana ni kweli Mbowe hana makali, lakini CCM wana propaganda kwamba Mbowe ni mwenzao, hili linafanywa ili akose ushawishi kwenye kambi yake ya Upinzani, ambako kawasumbua CCM kwa muda mrefu sana. Inaonekana wameanza kufanikiwa kwasababu wanachama wengi wa chama chake wameanza kuamini hilo, sijui kama ni kweli au ndizo propaganda zenyewe. CCM wamefanya kila aina ya ufedhuli kuisambaratisha CHADEMA, lakini Mbowe imekuwa ni kisiki kigumu kwao kwa muda mrefu tena sana.

Mbowe anajua kujenga hoja, mbowe nana jua ku recruit vijana na kuwajenga ndani ya chama chake. Mbowe amekabidhiwa chama kichanga amekifanya kiwe kikomavu. haya yote CCM wanayafahamu. Miongo yote CCM wamecheza rafu kwa Chadema, kuweka mapandikizi, na hata kuwa nunua viongozi ndani ya chadema yote hiyo ni kutaka kuimaliza CHADEMA lakini Mbowe bado ana recruit vijana na wana kubalika. Patrobas Katambi, Dr.Vincent Mashinji, Mwita Waitara, Dr.Slaa na wengine wengi, ccm walifanya na kuuaminisha umma kwamba wanaikimbia kwasababu zoote zilizosemwa lakini Mbowe bado ana recruit na wanakubalika na wanaendelea kuisumbua CCM.

Hivyo hata hili naamini liko mule mule kwenye kumchafua Mbowe ili kuuaminisha umma kwamba hafai kuwa kiongozi, na mbinafsi. Lakini kumbuka hivi vyama bado vichanga sana visipopata viongozi wazuri wenye kujali Maslahi yao havifiki mbali. Na yoote hayao yana ratibiwa na CCM.

Walijaribu kumrubuni Maalim Seif wakashindwa, waka mtumia Hamad Rashid na kumsaidia kuanzisha chma cha ADC, wakashindwa, wakamtumia Prof.Lipumba aliyejiuzulu mwenyewe na kuutangazia umma, lakini kupitia ofisi ya msajili wakafanikiwa kuisambaratisha CUF.

NCCR unafahamu ilivyokuwa imara, CCM wakaigawa mara mbili, Wakaimaliza. Mrema na TLP alikuwa Imara, wakammaliza.

Juzi hapa umesikia NCCR tena, wanaimaliza kupitia SELASINI, wanamfukuza Mwabukusi.
Wao CCM ndio wanataka Mbowe ajiuzulu, wanafahamu hapo watakuwa wamefanikiwa kuimaliza CHADEMA. Wanadai kazeeka. Unajua Philip Mangula kakaa muda gani ccm kama katibu mkuu, Muangalie Abdulaman Kinana ni kijana?

Sasa Mbowe akiondoka unadhani Chadema itahimili vishindo vya CCM? CCM wanataka wenye bei, lengo lao ni kutaka kutawala milele.

Wameiba chaguzi, kuikatisha chadema tamaa wanakuta Mbowe hatetereki, wamemchukulia viongozi yupo tu, wameharibu ngome upande wa kina mama kulazimisha kuwapa ubunge kina Halima na wenzake 18, na kujaribu kutaka kuiua chadema wamekuta ukuta, na wamepigania kesi kwa mahakamani na kwa msajili bado ccm wameshindwa lakini hawataki kuwaachia kina Halima. Yoote analengwa Mbowe.

Wana mchonganisha na Lisu wanamkuta katulia sasa wameona kujiuzulu ndiyo karata yao.

Anyway kila myu anaona anavyoona lakini naamini CCM wana mbinu chafu sana. Tutaona kama watafanikiwa kwenye hili.

Utasikia sio mzalendo, lakini wanadai wamesha mlambisha asali, na eti yuko ccm.
 
Inawezekana ni kweli Mbowe hana makali, lakini CCM wana propaganda kwamba Mbowe ni mwenzao, hili linafanywa ili akose ushawishi kwenye kambi yake ya Upinzani, ambako kawasumbua CCM kwa muda mrefu sana. Inaonekana wameanza kufanikiwa kwasababu wanachama wengi wa chama chake wameanza kuamini hilo, sijui kama ni kweli au mlambisha asali, na eti yuko ccm.
Mbowe kamkaribisha Samia achangie ujenzi wa kanisa la KKKT Machame, Samia kachangia sh milioni 150.

Mbowe mwenyewe anawasaidia CCM kueneza hizo habari kwamba amenunuliwa na Samia.

Mbowe alitakiwa kuelewa Separation of Religion and State, na kukemea tabia ya rais kutumia pesa zisizojulikana chanzo chake ovyo ovyo, badala yake Mbowe ndiye amekuwa enabler kamualika Samia.

Kama Mbowe hajanunuliwa, anawasaidia wanaosema kanunuliwa kutengeneza mazingira ya kuonekana kanunuliwa.
 
Naelewa unachosema, lakini kumbuka Mbowe naye alialikwa kutumia umaarufu wake kuchangisha fedha kujenga kanisa. Kwa muktadha huo isingewezekan yeye achangishe halafu asiseme nani katoa kiasi gani. Samia Suluhu ni rais lakini ni mtanzania kama wengine.

Wengi walichangia lakini kwasababu ya umaalumu wake na kwakuwa wanatoka kambi mbili hasimu, mchango wa SSH ulionekana zaidi, na hasa pale ambapo Mbowe ndiye aliyeutangaza.

Kwanza ni mujiriwa kwa nafasi yake kwa sababu analipwa mshahara. hivyo sielewi kwanini kuchangia kwake iwe Tatizo.

Pia kumbuka hii ni Tanzania lolote linaweza kuwa sahihi, pesa zimetoka wapi hata mimi sielewi ila nimejibu kwa mtizamo wangu siyo fact.

Anyway nisionekane namtetea lakini najiribu kuona mbali jinsi CCM wanavyoshambulia na kuwafanya watu waone wanvyotaka waone.
 
Back
Top Bottom