johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 82,754
- 139,559
Mbunge wa Momba mh David Silinde yuko mubashara Star tv katika kipindi cha medani za siasa akizungumzia sintofahamu ya uanachama wake ndani ya Chadema.
Up dates;
Silinde amesema yeye siyo mwanaharakati hata Mbowe analijua hilo na kwamba yeye na Zitto ni marafiki lakini baadhi ya viongozi hawalipendi hili.
Silinde anahoji Halima Mdee amekuwa na urafiki na Ester Bulaya tangu mwaka 2010 wakati huo Bulaya akiwa CCM na wamekuwa wakiishi nyumba moja wakati wote huo wawapo bungeni lakini hakuna aliyehoji. Kwahiyo Silinde anasema mambo ya kuchaguliana marafiki yamepitwa na wakati na kwamba yeye ana marafiki wengi CCM kama ambavyo wabunge wengi tu wa Chadema wana marafiki wengi.
Silinde anasema kwa sasa yeye ni mtu huru na wiki mbili zijazo atatoa msimamo wake kwamba anakwenda wapi.
Anasisitiza kuwa Mbowe ni kama mfalme pale Chadema na hataki kupingwa kwa lolote na ukijaribu kumpinga utaitwa ni msaliti.
Silinde anasema wabunge wa kuchaguliwa wanakatwa 10% ya mshahara wao kuchangia ujenzi wa chama na wabunge wa viti maalumu wanachangia 30% ya mishahara yao.
Silinde anasisitiza kuwa atagombea tena ubunge mwezi October kupitia chama atakachohamia!
Silinde amemalizia kwa kuishauri Chadema ijitahidi kuiheshimu katiba yake maana Mbowe anakanyaga katiba ya chama sasa kwa tabia hii wakiingia Ikulu Mbowe na genge lake wataisigina katiba kabisa. Fikiria alivyolazimisha wabunge kwenda karantini wakati hawajacontact na mgonjwa yoyote wa Corona sasa huu kama siyo udikteta ni nini?
Maendeleo hayana vyama!