David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Ila Kijana ana confo za kutosha nilikuta anamalizia mahojiano yake na Mlimani TV
 
Si vizuri kuropoka ropoka anadhani huku ankoenda ndio kuna amani. Angalia hata CCM wanavyotafunana wenyewe kwa wenyewe. Yeye alitakiwa kutulia kuomba msamaha ili aanze upya. Hata katika dini ukikiuka taratibu zake unatengwa, kinsingi unakuwa umejitenga mwenyewe na Mungu. Kumbuka kila taasisi ina maadili yake. Kusaini hundi Mwenyekiti is not an issue.
 
Kafulila Kaflila Kafulila!!! Ni kweli naipenda CHADEMA? Kwa nini unaiterekeza hasa wakati umegundua ina viongozi wenye CHUKI wanapohojiwa khsu ukweli? Kafulila naondoka CHADEMA ili uende chama gani? Kafulila unaamini hatua uliochukua inajenga CHADEMA?? Kafulila hko uendako unaenda kukua au kufa kisiasa??Kafulila hivi unafahamu vizuri CHADEMA inamaanisha nini kwa watanzania makini hasa vijana??Kafulila ume-retreat au ume-surrender??Why Kafulila??Heri ipi na kwa nani unaitaka Kafulila??Kilichoanzishwa na Mungu, wanadamu hawawezi kukishinda.
 
nimesikiliza mahojiano ya kafulila mlimani tv...kwa kifupi ni kijana ambaye hata kwa mpangilio wa hoja zake ..anaaonyesha bado anahitaji malezi ya kisiasa....nadhani haukuwa wakati muafaka kwake kuhama ....nitamshauri tu asifanye kosa kwenda CCM ..kwani hatapata cheo anachotarajia.....ni vema akaenda chama kidogo kama NCCR ambacho kule kigoma kinajulikana ..ili aendelee kujijenga kisiasa..au la afikirie upya msimamo wake na kubakia CHADEMA.

Nadhani tubadilike kifikra ...kuhama vyama kwa tofauti ya kimtazamo kumepitwa na wakati ...internal power strugle kwenye association yeyote ni jambo la kawaida......na unatakiwa upiganie mabadiliko ndani ....kabla ya kutaka umaarufu nje..ya kundi au chama chako...that is normal political evolution....

ndio maana unaona hata rebels wa CCM wanapigana wakiwa ndani....ninafurahisha hata muheshimiwa zitto ..anakubaliana na dhana ya kupigania mabadiliko ndani ....kwa ndani...hiyo ndiyo siasa...historia haiwapi nafasi nzuri sana rebels wanao ditch boat...kwani angalia looosers kama kina kabourou,hiza tambwe na wengine...zaidi ya kupata pesa ya kununua mkate kurudi nao nyumbani jioni...they lack a really constituets as of now......ndani hawaaminiki ..na nje hawaaminiki....

na si vema mwanasiasa kujijengea legacy ya kutoaminika.....bora uwe na msimamo hadi mwisho....
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo kinaelekea kuzimu kwa hatua zote ambazo kimekua kikipitia hadi sasa! walianza kwa kuhitilafiana na Dr warid, Marehemu chacha wangwe, kina Mzirai na hatimaye Kafulila.
Uwezekano wa Chadema kuelekea kuzimu ni mkubwa sana kwa kuwa historia ya mparaganyiko wa vyama vya siasa ni mparaganyiko pale swala la fedha linapoguswa! Wangwe alilalamikia matumizi ya ruzuku, kina Mzirai matumizi ya ruzuku, Kafulila matumizi ya Ruzuku aagh! kwa sisi wa mikoani hasa Tabora mjini ni aibu kweli kweli hasa unapozungumzia ofisi za Chadema, wanatumia kipande cha Gogo la mnazi lililolazwa chini huku Mwenyekiti wa Chadema na katibu wake wa Mkoa wakifanya biashara ya kukodisha baiskeli 2 (mbili) kama mradi wao waotegemea wakati vigogo wao wakiishi kwa neema huku wakiitaka ubunge na Urais Aibu!
 

Hapa nina tatizo moja na Kafulila
ktk huo mstari wa mwisho anamaanisha nini? alimwaga damu ya nani? maana nielewavyo mimi unaposema kumwaga damu maana yake ni kuua.Ama ana maana gani?
 
Tusubiri next move kama sio CUF basi ni kulekule kwa "Mwenda tezi na omo, marejeo ngamani'. Its only a matter of time!.
 
Huyu Kafulila kwangu mimi naona kafulia kweli kweli.

Katika maelezo yake hakuna mahali ambapo kuna nguvu ya Hoja ya kumfanya atimue toka CHADEMA. Unaposoma katikati ya mistari inaonekana kuwa Kafulila amekuwa anatumia na nguvu kutoka nje ili kuivuruga CHADEMA.

Kama kweli yeye alikuwa upande wa Zitto Kabwe wakati wa Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA na alimfanyia kampeni Zitto ili amwangushe Mwenyekiti Freeman Mbowe basi matokeo ndiyo haya.

Tatizo la vyama vyetu vingi vya Siasa ni kuwa kila mtu anataka kuwa maarufu ndani ya Chama. Zitto Kabwe ameanza kujiona kuwa ni bora na ni maarufu kuliko hata waasisi wa CHADEMA. Hilo ni kosa la wazi. Ni utovu wa nidhamu kama siyo kukosa adabu kupingana na wazazi wako kwa kile wanachokiona ni bora kwa familia.

Zitto Kabwe anataka ku-gain popularity kupitia CHADEMA. Ndiyo maana ana thubutu kujaribu kupingana na Wakuu wake ndani ya Chama.Hilo ni kosa.

Zitto anatakiwa kusoma alama za nyakati na kuangalia nyuma kule chama kilikotoka. Wazee wa CHADEMA kina Edwin Mtei na Bob Makani waliwapisha kina Freeman Mbowe na kina Slaa kwa ustaarabu kabisa bila matatizo.

Kwamba wazee hawa waliamua kung'atuka kuwapisha vijana! Zitto alitakiwa ajifunze kutokea hapo.Yeye ana haraka gani ya kuchukua chama? Kwa nini asisubiri wakti kina Mbowe watakaposema hawataki tena Uenyekiti wa Chama? Mbona hata CCM wana ustaarabu wa kuachiana kiti cha Mwenyekiti kwa ustaarabu?

Kwangu mimi naona kuwa CHADEMA imeshaanza kuhujumiwa na CCM. Siwezi kushangaa kusikia kuwa mtu kama Kafulila ni mamaluki wa CCM aliyepandikizwa ndani ya CHADEMA. Bado nafuatilia nyendo za Mhe. Zitto Kabwe kuona kama na yeye ameshaanza kutumiwa na mafisadi kuivuruga CHADEMA.

TUKUMBUKE KUWA CHADEMA NDIYO WALIOSABABISHA kuyumba kwa serikali ya Kikwete kwa kutaja yael majina 11 ya mafisadi(List of shame). Mwanzo CCM walianza kwa kupinga kabisa kuwa madai ya CHADEMA hayakuwa kweli lakini baada ya ushahidi kuanza kuibuliwa na CHADEMA, CCM wakabadili mwelekeo. Wakakubaliana na CHADEMA kwa shingo upande kitu ambacho kimewagharimu sana CCM.

Jambi hili halijaifurahisha CCM hata kidogo kwa hiyo inafanya kila mbinu kupenya ndani ya ngome ya CHADEMA ili kuisambaratisha kabla ya uchaguzi wa 2010. Huo ndiyo ukweli.
 
. Nitaikumbuka sana chadema kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni. ​



unazidi kuniweka mbali na siasa. Haya mambo ya kuropoka ropoka kwenye vyombo vya habari haya?
 
yaani pasipo madaraka watu hawawezi kukaa upinzani?

Na hicho ndo kinachowasababisha watu wanashindwa kuendelea kukaa katika vyama vya upinzani.Mtu akishapata kaumaarufu kidogo basi alishajiona yeye ndo chama huku akijivimbisha kichwa kwamba anaweza kwenda kokote na akawa mtu katika watu.wengi wa walio upinzani hawana uvumilivu hasa wale wenye damu ya ccm.
 
nimesoma vizuri andiko lake David kafulila kwa vyombo vya habari iliyowekwa humu kwenye Jf, nimestushwa na kauli yake ya kusema kuwa amemwaga damu chadema, hivi kivipi jamani.mi ninavyojua nchi yetu haijamwaga damu yoyote eti kwaajili ya ukombozi, atuambie vizuri anahusika katika mauaji na anataka kuuambia nini uma kuwa chadema kimeshamwaga damu kwenye movement zake? au ni huku kutapatapa.......

kama ni kutapatap kweli umeanguka kabisa my broo.
 
Sasa swali hili si-ungeuliza kwenye thread yenye hilo andiko kwa vyombo vya habari, kulikuwa na umuhimu gani kuanzisha thread mpya..?MNI
 
halafu wewe MOD unaefuta post,narudia tena kusema mzimu wa wangwe unaikomesha CHADEMA.
 
KAFU-LILA.............jina linajieleza,hopefully alikuwepo ka papet
 
Kijana kafulia....Mtu yeyote unapopata mitihani kama hii ndio kwanza unazidisha mapambano ndani ya chama chako. Kuondoka kama mwanachama sio solution hata kidogo.
Na anaposema alimwaga damu hii inatisha! tunahitaji maelezo zaidi...
 
Baada ya habari zake kuandikwa sana nilichukua hatua za kumtafuta huyu Kafulila ni mtu wa namna gani, na nilipata majibu yafuatayo;
1. huyu jamaa ni mtu anapenda sana kujiona anauwezo kumbe hana ,na hili ni kwa mujibu wa watu waliokuwa nae kwenye maeneo mbalimbali na haswa alipokuwa na vijana imara wa CUF kwenye vikao vya TCD.
2.Nimeambiwa kuwa alikuwa anasoma UDSM kozi ya BBA Evening programme ila alidisco.
3.Nimeambiwa aliwahi kuanguka kutoka gorofa ya kumi hotel moja kariakoo ,sikumbuki jina nililotajiwa .

Nilipofika hapo nikaona sina haja ya kumjua zaidi kwani ni mtu ambaye hata shule ilimshinda ,tena evening class kudisco , na ukichanganya na kuanguka kutoka gorofani basi unapata jibu kuwa inawezekana amechanganyikiwa.

Kama taarifa nilizopewa na jamaa wanaomfahamu ni sahihi basi sintaendelea kumjadili wala kumfuatilia kwani nimeshaweka maoni yangu-kifupi nampuuza tuu.

Nilimfuatilia kwani nilitaka kumshawishi ajiunge na chama dume , ila hafai.
 
Unajua kikwetu KAFULILA ni mtu ALIYEFULIA, kwa mtazamo wangu kama kweli Kafulila alikuwa na dhamira ya kweli ya kujenga upinzani ulio na nguvu asingeongea mambo yote hayo baada ya kujitoa. Hii inaonyesha alikwenda chedema kutafuta madaraka au kama mamluki. Siamini kama amekwenda kukuza chama ndo maana aliponyang'anywa uongozi akaona hakuna tena faida zaidi ya kutoa lawama.
Kama kweli alikuwa anaitakia mema chadema angekaa na kupambana humohumo au kukaa kimya ili akina mbowe wadhihilishe kwamba wao ndo tahira lakini kwa picha ilivyo sasa Kafulila si mtu wa kuaminika. kwanza hafai hata kuwa baba kwani atakuwa anatoa siri za mkewe na nyumbani kwake.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…