David Kafulila ahamia CHADEMA akitokea NCCR Mageuzi

David Kafulila ahamia CHADEMA akitokea NCCR Mageuzi

Ndani ya ukawa kuna vyama vitainuka na vingine vitakufa au kumalizwa nguvu na vyama vilivyokuwa n nguvu zaidi c hivyo tu hata nje ya ukawa kuna vyama vitakufa eg act wazalendo
 
Lizabon njoo useme chochote huku
Ngoja nimsemee bila ridhaa yake lizaboni ni hivi wanaume wa Kigoma wanajiamini sana hata kama hawana kazi hawawezi mfuata mke hata awe ana pesa vipi awe mbunge viti maalum au LA kisa tu ndie analisha watabaki waliko au hata wakitaka kuhama chama wataenda chochote kila siyo cha mke.Wanaume wa Kigoma ni kweli au sio kweli?
 
Kafulila ahama NCCR, ahamia Chadema
Dar es Saam. Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, amekihama chama hicho huku akieleza kuwa anajiandaa kuhamia Chadema.

Kafulila alithibitisha taarifa hizo na kusema tayari ameshawasilisha barua ya kujivua uanachama wa NCCR na kujiunga Chadema leo.

“Nimewashukuru kwa kuwa pamoja katika kujenga chama na nafasi ya uenezi waliyonipa mara zote. Nimeweka wazi kuwa natarajia kujiunga na Chadema. Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.” alisema

View attachment 446944

SOURCE: Mwananchi

Kabla ya NCCR, Kafulila alikuwa mwanachama wa CHADEMA. Habari. zaidi soma=>David Kafulila ahamia NCCR Mageuzi akitokea CHADEMA
Cc:mcubic
 
Mpango wa chadema kuua NCCR,CUF unaenda kwa kasi sana.Kama NCCR ni ukawa kwanini ahamie Chadema ambao ni washirika katika ukawa?
Kuliko hata walivyotarajia.

Hii ndio ile nunua moja upate mbili bure.
 
Maamuzi ya Kafulila yametoa picha tatu.

1) Hoja ya Prof. Lipumba ya kuishutumu CHADEMA kuua vyama ndani ya UKAWA imeanza kusimama kwa sababu hata Kafulila amesema, ‘’Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.”

2) Ndani ya UKAWA hakuna umoja na mshikamano kama inavyoonekana kwa nje.

3) Tusiwaamini sana wanasiasa wetu.
Kwani Lumuuuuuumba yy ni mpinzani ????
 
Tuimalishe chama cha chadema ili wale majangili tuwafukuze kwa pamoja na kwa kishindo.
 
Seif na Wapemba wenzie nao wanamalizia Mazungumzo ya Mwisho Mwisho na Mzee kule Mikocheni kwa Mwenye Chama kabla hawajamsusia CUF Prof baada ya kuona Prof ni Kota pin ya Baiskeli haichomolewi kwa Mazungumzo !

Hahahahaaaa nimecheka sana. Eti Kota pin ya baiskeli. You have made my day.
 
Kaenda kwa mkewe, sioni kama ita muimarisha yeye kisiasa bali ita msaidia mkewe zaidi.

Halafu kama wote NCCR na CDM ni UKAWA kuna haja gani ya Kafulila kuhama!? Au ndio umoja wa mashaka wenyewe!!
kaka umeionaje sababu yake ya kuhama? we need to be one
 
hii thread ingekuwa amehamia ccm ungesikie mara njaa mbaya, mara usaliti mbaya lakini kwa kuwa ataenda chama pendwa atapongezwa
 
Akili za shisha hizi, mbona Juma duni Haji karudi Cuf? Mpendazoebna nusu mkia ccm? Je Afande sele? Wapi Habib Mchange?
Akilo za panzi hizi, sisiemu kuna umoja ipo na ishu ya Duni ina maana haukukua toka mwanzo tageti na lengo lilikuwa ni nini??
 
Rekebisho kidogo, David Kafulila hajahamia Chadema, bali amerejea Chadema, NCCR Mageuzi ndio alihamia na sasa amerejea nyumbani, ataisaidia sana Chadema kuziba pengo la ZZK kama ata team up na JJ. Mnyika. Kafulila is good so does JJMNYIKA na wengine wachache. Pengo la ZZK ndani ya Chadema halijazibwa so does pengo la Dr.Slaa, na Bavicha ya sasa haina big impact so does Bawacha.

Mimi kama ningekuwa mshauri wa Chadema ningemshauri Mbowe his time it's time up. Ameifanyia Chadema mengi na makubwa but amefikia optimum take. Kama night solution, it is a saturated solution, it can take no more than it can.

Chama makini kinatakiwa kuanza jana kujipanga kwa kesho, kwa uchaguzi wa 2020 hata yule jamaa yangu atakuwa ni spent force unless Chadema imeridhika kuendelea kuwa msindikizaji tuu na sio mshindani.

Hongera sana Kafulila, welcome back home kwako ulikotoka na kugeuka mwana mpotevu aliyerejea nyumbani kwa baba take.

Paskali
ushauri mzur ila kuna nukta zako sijui km chadema watazukubali
 
Kafulila ahama NCCR, ahamia Chadema
Dar es Saam. Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, amekihama chama hicho huku akieleza kuwa anajiandaa kuhamia Chadema.

Kafulila alithibitisha taarifa hizo na kusema tayari ameshawasilisha barua ya kujivua uanachama wa NCCR na kujiunga Chadema leo.

“Nimewashukuru kwa kuwa pamoja katika kujenga chama na nafasi ya uenezi waliyonipa mara zote. Nimeweka wazi kuwa natarajia kujiunga na Chadema. Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.” alisema

View attachment 446944

SOURCE: Mwananchi

Kabla ya NCCR, Kafulila alikuwa mwanachama wa CHADEMA. Habari. zaidi soma=>David Kafulila ahamia NCCR Mageuzi akitokea CHADEMA
Ulipotezwa na nyepesi
 
Back
Top Bottom