David Kafulila ahamia CHADEMA akitokea NCCR Mageuzi

Kafulila ahama NCCR, ahamia Chadema
Dar es Saam. Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, amekihama chama hicho huku akieleza kuwa anajiandaa kuhamia Chadema.

Kafulila alithibitisha taarifa hizo na kusema tayari ameshawasilisha barua ya kujivua uanachama wa NCCR na kujiunga Chadema leo.

“Nimewashukuru kwa kuwa pamoja katika kujenga chama na nafasi ya uenezi waliyonipa mara zote. Nimeweka wazi kuwa natarajia kujiunga na Chadema. Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.” alisema

View attachment 446944

SOURCE: Mwananchi

AYAAA MAMA TANZANIA KACHWA PEKE YAKE ????
 
Kila la kheri Mh Kafulila.

Haya ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa ndani wa CHADEMA?
 
Mbatia itambidi kuhamia CDM kama anataka kujiimarisha kisiasa
Sema waangalie jinsi gani ya kuunganisha nguvu na kuwa Chama kimoja. Chadema na NCCR.
KUHUSU Cuf wanaweza kuwa na huo ushirika hadi pale itakapoonekana inafaa kuungana
 
"Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari" ---> Hakika hii ndio kauli bora kabisa kwa mwaka 2016 karibu chama cha watanzania D. Kafulila.
 
Maamuzi ya Kafulila yametoa picha tatu.

1) Hoja ya Prof. Lipumba ya kuishutumu CHADEMA kuua vyama ndani ya UKAWA imeanza kusimama kwa sababu hata Kafulila amesema, ‘’Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.”

2) Ndani ya UKAWA hakuna umoja na mshikamano kama inavyoonekana kwa nje.

3) Tusiwaamini sana wanasiasa wetu.
 
ilitegemewa nccr imeshakufa tayari....hakuna wakutegemea tokea wavurugane wenyewe kwa wenyewe......mhe.mbatia hawezi okoa jahazi kwa sasa,kupanga ni kuchagua vunja chama jenga chama,wakubaliane tu kukiua nccr ongeza nguvu upande mwingine wa upinzani.....
 
Mpango wa chadema kuua NCCR,CUF unaenda kwa kasi sana.Kama NCCR ni ukawa kwanini ahamie Chadema ambao ni washirika katika ukawa?
huu umoja nilishtukia sio chadema waliposimamisha mgombea segerea wakati wanajua kuna julius mtatiro wa cuf yule mama wa cdm kazigawanya kura za ukawa akasababisha ccm ikashinda halafu yy akapewa kiti maalum iliniuma sana ile kitu.
 
Sisimizi kilichokutoa chadema kimeondoka?Mbowe yule yule bado ni mwenyekiti na Mbowe alishindwa kufanya kazi na wewe
Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA
Kafulila ni mpenda mdaraka na ukubwa utawezana na ulipo tupo?

Kafulila atishia: Nikishindwa kesi nitahamia chama kingine
NCCR yamfukuza uanachama Kafulila na wenzake!

Kafulila ana dharau kwa wapiga kura hata kwa waliompandisha chati ya kisiasa kwa kumpa mabomu ya kurusha bungeni
Zitto: Wakati mama yangu anaumwa, mimi nilimpatia Kafulila makabrasha ya ESCROW akapambana
VIDEO: Kafulila azomewa na kushushwa jukwaani, Kigoma

Kafulila ni bingwa wa migogoro chama chochote anachokwenda lazima kiwake
Kafulila akamatwa 'uchawi' NCCR-Mageuzi; MBUNGE wa Kasulu M.Machali yuko tayari kujiuzulu
 
Haka kajamaa ni kichwa sana..nimependa alivyotoa sababu ya nzuri kabisa tena yenye mashiko na inaweza kuimarisha zaidi UKAWA.
"Nimeona kuwa kuna mahitaji ya watu wenye nia ya mabadiliko kuwa katika chama kimoja ili kufupisha safari.
Hata mimi nilijiuliza kama wewe ila hiyo sababu imemaliza swali langu
Sawa wafanye utaratibu formaly wakiue NCCR waungane wote CDM ila wasichukuane mmoja mmoja tuu
 
Back
Top Bottom