Dark days 17/03/20

Dark days 17/03/20

Anaejua tafsiri ya hii plz
1756218099410.png
 
State ni wahuni wale wale.

Nyerere na wenzake wanastahili lawama, walipokumbali mfumo wa vyama vingi,
Walipaswa kuweka misingi mingine ya chama kisikae madarakani muda wote kimoja,

Wangefanya japo vyama viwili vyenye sera tofauti kupishana madarakani kila baada ya muda fulani,

Hii ikitokea chama fulani kimewekwa kando kiweze kujiafakari wapi kimekosea,

Wao wakaishia tu kuwa na utaratibu wa kiti cha urais mtu akae mihula miwili,
Na eti Nchi hii bila chama cha CCM madhubuti itayumba,

Waliangalia ubinafsi si maslahi mapana ya taifa ya muda mrefu.

Mwl hayupo madarakani, katiba ameiona akitokea rais kichaa anaweza kuitumia vibaya akaonekana ni mungu mtu, wakati Mwl ushawishi kwenye chama bado anao je kitu gani kilimzuia kutengenezwa katiba mpya mwaka ule wa kukubali vyama vingi?
Akaishia kutuma mashushushu waanzishe vyama vya upinzani nchi kwa nje ionekane ina vyama vya upinzani kumbe hamna lolote,
Akina Augustine Lyatoga Mrema, Seif Sharif Hamad, Hamad Rashid, Juma Duni, Mabele Nyaucho Marandu na wengine wengi.
...
 
Kabla ya Uchaguzi boss alitaka amuweke mrithi wake kwenye kampuni yake, mrithi anayemtaka yeye. Ila kutokana na upinzani mkubwa ndani ya kampuni maamuzi magumu ilibidi yafanyike

Baada ya Uchaguzi kuna mtu alipata uongozi accidentally. Hakuwa chaguo la boss, alipewa sababu ya kuua kambi!

Big boss anayemaliza muda alifanya maamuzi hayo akiamini ataweza kum-control kwakuwa file lake analo na anamjua na amempa ili kunusuru mkatiko mkali kwenye kampuni.

Alijua ataleta umoja ndani ya kampuni. Mambo yalibadilika baada ya new boss kupewa kijiti na kukabidhiwa ofisi!

Alichofanya ni kutengeneza timu yake na kuondoa timu yote ya mtoa kijiti! Akaenda mbele zaidi kupitia files na kuanza kutindua maslahi ya mtoa kijiti kwenye kampuni!

Mbaya zaidi, akamfukuza mwenye kijiti, au the old boss kwenye kampuni anayoamini ni ya kwake na bila yeye haiendi!

The New Boss alipewa notification na maelekezo kuhusu mambo kadhaa mara kadhaa, ila aliskika akijibu, yeye ndio mwenye kijiti na hakuna wa kumpangia! Hataki maelekezo na kwanza haelekezeki!

Alijibu hivyo hadharani bila woga wala hofu! Kwakuwa alimjua adui ni nani! Alianza mpaka kutangaza kuwa kampuni ile sasa ni yake na chini yake inafanya makubwa sana, na wale wa zamani walikuwa wanaifilisi!

Haikuwa habari njema saaaana kwa mwenye kijiti kabla ya uchaguzi na backup system yake! Discussion zilifanywa mara kadhaaa kumjadili new big boss in town kumbe the new boss alikuwa anawarecord all the time!

Alichokifanya ni kuvujisha badhi ya convos za washirika wa adui mkuu kum-notify ironically kuwa anajua wanachomjadili na anajua hawampendi! Na amejipanga au ameji-sacrifise yupo tayari kwa lolote!

Shida ikaanza, after a discover kuwa deal za the old big boss zinazimwa na zinachukuliwa kwa nguvu na stakeholders wapya chini ya maelekezo ya the new big boss na stakeholders wa zamani wanatupwa nje ya ukuta!

Ikatisha zaidi baada ya boss mpya kutaka kuwa CEO wa milele! Na akapanga watu wa kuhakikisha hilo linakamilika!

The old boss akakaa chini, akafikiria akaona kama huyu 4 years tu kanifanya hivi je 20 years to come?

Muda ukaenda, the old boss played dead! But came up with a plan, involving the closest friend and the system in the company kama tunavyojua, the old the wine...... the fine it becomes!

The new Big boss kajichanganya during campaings za kuusaka u-CEO tena, akapigwa tukio, after Uchaguzi wa pili wa kampuni only three months akatema ndoano!

Msaidizi wake akaitwa chemba, maelekezo akapewa achukue kijiti, afanye reform mambo kwabu yanapaswa kurudi kama zamani!

Msaidizi kuangalia hali ilivyo, akaanza kurudisha the old structure kwenye kampuni! The only difference ni yeye ndio CEO but behind the scene there is another CEO!!

Let see will the new boss stick to the plan? or...


Itaendelea.......


Guess the company!??

Muendelezo Soma Dark days 17/03/20.…...

Angalizo: Story hii haihusiani na chochote Dark days 17/03/20...
Huyu mwandishi aliandika mambo ambayo yanaonekana kuwa ni ya kweli.
 
Back
Top Bottom