Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!



Ni wazi Rais hajavunja sheria ila kwa ujanja ujanja hataki kujaza nafasi hiyo ama anavuta subira hadi ampate mtu wake muafaka kwake (yes man) au ana hofu ya kumpata mtu mwenye msimamo asiyeyumbishwa hovyo.

Mh. Tundu Antiphas Lissu anaona mbali na ndio maana Prof. Kabudi alikwepa kujibu hoja zake na kuishia kuzungukazunguka kwa majigambo.

Nadhani hapa tunamdhania sana Prof. Ibrahim; kwamba kwa namna fulani si mtu mwadilifu na kuwa hawezi kutekeleza wajibu wake kwa sababu ana hofu ya kupoteza hiyo nafasi kwa msingi wa hii 'security of tenure'. Kudhania huku msingi wake ni nini?
 
hajaapishwa manake bado hajawa Rais kwa hiyo rais anayeondoka madarakani atateua Jaji Mkuu mwingine?

Na hapo unadhani haitokuwepo hoja ya kwanini wasisubiri Rais ajaye kumteua Jaji Mkuu hasa kama ikitokea Rais ajaye ni wa chama toafauti na cha Rais wa sasa? Si umeona hivi majuzi Wamarekani walivyochezeana baada ya kutokea nafasi ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Marekani? Tena wao walimkatalia Obama kuteua jajii mwingine ndani ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi!
 
Hoja ni kwamba jaji mkuu akiwa kaimu basi anaweza kupindisha sheria na kujaribu kujipendekeza ili apate ujaji mkuu.

Na akiwa Jaji Mkuu hawezi? mbona hii haina mantiki kabisa. Yaani, mnahofia kaimu kujipendekeza kuliko mtu mwenyewe hasa? Chukulia kwa mfano akiteuliwa mtu mwingine kushika Ujaji Mkuu hatojipendekeza kwa atakayemteua
 
mkuu leo umenishangaza kidogo, unaongelea nadharia tu na si hali halisi, hata siku moja huwezi kumfananisha dereva wa gari na dereva deiwaka aliyepewa kupiga route wakati mwenye gari yake anapata lunch.
Mfano wako unafurahisha akili lakini hauna mantiki...
 
Nimesikiliza kwa makini kile kinachoitwa "darasa" la Prof. Kabudi jana Bungeni kuhusiana na suala la Kaimu Jaji Mkuu na hasa hoja nzima ya kukaimiwa kwa nafasi ya Jaji Mkuu. Inasikitisha kwanza kwamba kuna watu wanasifia kuwa ametoa "darasa" na kwamba watu walikuwa wanamsikiliza kama wanafunzi katika Shule ya Msingi Mtakuja!

Je, ni kweli kile alichokisema watu walikuwa hawakijui? Ni kweli wabunge na wanasheria walioko Bungeni walikuwa hawajui yale yaliyokuwa yanasemwa?

Kuna hoja ya kuuliza swali; kwamba - kwanini Rais amemteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu kwa muda wote huu. Swali ambalo halipaswi kuulizwa na tulilikataa wakati ule ni kuhusu mamlaka ya Rais kumteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu. Hili liko ndani ya mamlaka ya Rais (Presidential prerogative). Lakini pia swali hili kwa ukubwa wake halipaswi kuulizwa isipokuwa kisiasa (political question) ili watu kupata hoja za kisiasa au ujiko wa kisiasa. Kwamba, mtu anataka kuonesha kuwa Magufuli amekosa mtu wa kuwa jaji mkuu, au kwamba Magufuli ana tatizo na mahakama n.k. Hili si jambo sahihi; wabunge kama wanaona Rais anatumia muda mrefu kujaza nafasi ya jaji mkuu wana uwezo wa kubadilisha sharia na hata Katiba chini ya Ibara ya 100 ya Katiba yetu.

Kama wanataka nafasi ya Jaji Mkuu isikaimiwe indefinitely (kama hoja ya Lissu ilivyoashiria) namna pekee ni kubadilisha Katiba au sheria ili kuweka kikomo kama ilivyo katika baadhi ya nafasi za utumishi wa umma ambapo sheria inasema mtu atakaimu nafasi kwa muda fulani na baada ya hapo basi mtu wa kudumu ateuliwe au aliyekaimu athibitishwe. Wao wabunge (watunga sheria na wanaoweza kufanya mabadiliko ya Katiba) wanaweza kuweka kikomo labda kwa ajili ya mustakabali)

Kama kwa mfano Rais angejaza cheo cha Ujaji siku moja tu baada ya Jaji Othman kustaafu wapo ambao labda wangeweza kuja na hoja ya kwanini amejaza nafasi haraka bila kuonesha tafakari sana au klutumia muda kufanya utafiti wa kutosha! Lakini pia kuna swali ambalo inabidi liulizwe kwa wale wanaolalamikia - kwa Rais kuweka Kaimu Jaji Mkuu ni shughuli gani ya Mahakama Kuu ambayo haiwezi kufanyika sasa hivi kwa vile kuna kaimu Jaji Mkuu au ni kitu gani hakifanyiki katika mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambacho kinapaswa kufanywa na jaji mkuu peke yake. Hili ndilo linaweza kuwa hoja ya kwanini inahitajika Jaji Mkuu na siyo Kaimu Jaji Mkuu?

Lakini kung'ang'ania kitu ambacho wote wanajua hakipo - kwamba Rais hajavunja sheria wala Katiba, na kuwa hakuna kikomo cha muda kilichowekwa kwa hoja ya kuwa ni mazoea mapya haitoshi kuwa hoja.

Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la. Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Urais wakati Rais hayupo kwa mujibu wa sharia ana madara yote ambayo ameruhusiwa kuwa nayo kwa mujibu wa Katiba. Na hili ni kweli kwa mtu mwingine yeyote ambaye Rais anaweza kumpa nafasi ya kukaimu jambo lolote kwa niaba yake. Mtu yeyote professional hajali sana kama atamfurahisha mtu au la atafanya kwa mujibu wa madaraka aliyopewa. Mtu ambaye atajali kuwa akifanya jambo Fulani atamuudhi aliyemteua au chombo cha juu hafasi kushika nafasi hiyo.

Somo ambalo Kabudi angepaswa kulitoa na labda wengi wanalihitaji kulielewa ni hili la Presidential prerogatives..

Hata Mimi Nilimsikiliza Naweza Kujumlisha Kuwa huyu Bwana hana Lole ni Mojawapo ya Wasomi, Malaya wakisiasa wasio na Msimamo ni aina ya Mwakyembe, Muhongo na sasa Huyu Kabudi, Bado wana ile kasumba ya Nguruwe wa Shamba la Wanyama waliodhania ni Wajuaji kuliko wanyama wengine kwa Kuwa tu walijifunza Kutembea kwa Miguu Miwili wakiambatana na Wanadamu huku wakiwabeza sana Wanyama Wengine kwani hawakupewa Fursa ya Kuwa Karibu na Binadamu. Kabudi ameuza Kichwa na Naomba siku yoyote Mahali Popote nipate Mdahalo naye. Na nione ni Jinsi gani Professor wa sheria atatetea Kumweka Jambazi Kuwa Mkuu wa Mkoa au Kuteua Kaimu Judge indefinitely ili Umkalie Kichwani!
 
Hoja ya lissu mbona iko wazi kabisa...hajasema kuwa rais amekosea..anachosema lissu ni kuwa sheria zetu/katiba hazijaweka limit ya kuwa na acting chief Justice

Kitu ambacho kinaweza kuwa na madhara...hivi hebu chukulia kwa mfano rais aendelee kuwa na kaimu jaji hadi mwaka 2020.....hili jambo lin athari katika utendaji wa jaji

Kwa bahati mbaya Watu wengi huwa hamumuelewi Lisu kwa kipindi hicho anaongea...mnakuja kumuelewa baada ya miezi kadhaa au miaka kadhaa kupita
Hivi Lisu ni mtaa gani vile ?
 
Inategemea umemsikiliza vipi and how you interpreted his egotist argument.

Though for the most part information provided was not necessary given the setting and not to ignore the annoying self proclaim of his legal virtuous. Nevertheless the speech was informative on legal rituals and eye opening to most of us, more like a follow up to his previous argument about tying anthropology to legal education to enhance perception.

At the end of the day you can tell he is just a legal scholar not a politician its obvious from his arguments there are huge limitations outside the legal world no wonder wakataka katiba itoe ruzuku za mbolea.
 
Na akiwa Jaji Mkuu hawezi? mbona hii haina mantiki kabisa. Yaani, mnahofia kaimu kujipendekeza kuliko mtu mwenyewe hasa? Chukulia kwa mfano akiteuliwa mtu mwingine kushika Ujaji Mkuu hatojipendekeza kwa atakayemteua

Its human nature babu, it runs in our DNA. Tunatofautiana tu extent, ila wote greed inaathiri sana rational thinking,, only that kwa different extent.
Ktk post za nyuma kuna mtu ametoa mifano ya watu (wanasiasa) ambao walisema na kupinga kile ambacho baada ya wao kupokea teuzi za raisi wamegeuka na kukupigia chapuo! Unadhani ni coincidence? Its written all over their DNA,, kwa lugha nyepesi ni kwamba "everyone has a price, all you have to do is make them tic".

Lakini la msingi kabisa kwenye bandiko lako la leo, naona umeegemea sana kwenye nadharia ,, kana kwamba hakuna room for logic na rational thinking. Kusema kwamba inawezekanaje kaimu jaji akajipendekeza ili kumfurahisha bosi amteue ikibidi ,, kana kwamba hili haliko wazi mzee!! Mbona hili linafanyika kila mahali, hata tu ma housegirl hujipendekeza kumteka baba mwenye nyumba! lakini pia, katika zile scenario ambazo inapaswa kuteuliwa (ama kukaimishwa) kaimu jaji, hakuna hata moja ambayo ni relevant kwa situation tulionayo sasa,, pamoja kwamba rais hakuvunja sheria, just because the law doesnt state length ya term ya kukaimu. Kujikita kwenye sababu na tafsiri ya namna hii pekee ni matusi kwa taaluma ya sheria!!

Mwisho, kuna hoja nyingi za msingi ambazo zimetolewa na wachangiaji mbalimbali ktk post za nyuma , ingekuwa vyema ungezijibu maana naona unaruka na kuchagua zile "nyepesi nyepesi tu", which is very uncharacteristic of you..

What happened to reason??
 
Naomba izingatiwe kuwa msisitizo mweusi na wa italiki ni wa kwangu kwa ajili ya kuweka msisitizo.

Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwenye issue ya kukaimu, sorry you've missed the point.

Sheria yoyote inapotungwa na Bunge inanakuwa na madhumuni fulani. Lengo la kifungu cha mamlaka ya rais kuteua Kaimu Jaji kilidhamiria Kaimu Jaji Mkuu atateuliwa pale tuu Jaji Mkuu yupo lakini yuko nje ya nchi, ama ana maradhi yaliyopelekea kushindwa kutimiza majukumu yake, hivyo anateuliwa Kaimu as a temporary measures, Jaji Mkuu akirudi au akipona anaendelea na majukumu yake.-

Kwanza kabisa, siyo kweli - kama mtu akisoma Katiba - kwamba lengo la kifungu cha kumpa Rais kuteua Kaimu Jaji "kilidhamiria" kuwa atateuliwa pale tu "jaji mkuu yupo" lakini kwa namna fulani anashindwa kutekeleza majukumu yake. Huku ni kudhania (assumption) ambayo haina msingi.

Katiba imesema kuwa endapo mambo matatu yakitokea basi Rais anaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu. Mambo hayo kwa mujibu wa Ibara ya 118:4 ni kuwa Rais anaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu endapo mambo yafuatayo yatatokea: a. Kiti kitakuwa wazi (na hapa ina kuwa implied kwa sababu mbalimbali ikiwemo, kifo, kujiuzulu, kustaafu n.k), b. Jaji Mkuu hayupo Tanzania (sehemu ya hoja yako) na tatu Jaji mkuu atashindwa kutekeleza majukumu yakekwa sababu yeyote ile (na implication hapa ni vitu kama ugonjwa, katekwa n.k) basi Katiba inasema " Rais ataona kuwa kwa muda wa
tukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua Kaimu Jaji Mkuu, basi Rais anaweza kumteua Kaimu Jaji Mkuu kutoka miongoni mwa Majaji wa Rufani."


Hivyo, SI KWELI na haina msingi wowote katika Katiba kuwa lengo la Ibara ya 118:4 lilikuwa ni pale tu Jaji anapokuwa yupo lakini hawezi kufanya kazi yake. Hili ni la kujitungia tu halina msingi katika Katiba na ukilifikiria halina mantiki ya kiutendaji. Hivyo, linaanguka lenyewe.

Lakini Jaji Mkuu anapomaliza muda wake wa utumishi wa umma, 6 months before notification hutumwa na rais kupelekewa majina matatu to choose from.

Hili pia ndugu yangu Nguruvi kalisema hapo juu; lakini wewe na yeye wote hamsemi je sheria au utaratibu huo unamtaka Rais ateue mtu muda gani tangu apewe majina hayo matatu? Kama kuna mtu anaamini RAis amechelewa kinyume cha sheria tangu apate majina hayo matatu wapo wanasheria makini tu wafungue kesi mahakamani iamuliwe! Lakini sijaona hata mmoja anayedai kuwa Rais amevunja sheria.


Huu Uteuzi wa Prof. Juma kama Kaimu Jaji Mkuu wakati nafasi ya Jaji Mkuu iko wazi permanently is not right!.

This is very absurd; Inawezekana vipi kiti cha Jaji Mkuu kiwe wazi permanently halafu unataka kijazwe. Au neno "permanently" halina maana tena? Kama kitajazwa hakiko permanently vacant! It is only because it is temporarly vacant ndio maana watu wanataka kijazwe. I don't like self contradictions.

It is as if Dr.Juma is not trusted hivyo yuko under probation kama atafiti ndipo ateuliwe na asipofiti anateuliwa mtu mwingine!. Hii ni very demoralising na Dr.Juma hawezi kuwa na confidence ya ku exercise all his powers kwa sababu kuna vitu Kaimu Jaji hawezi kufanya ikiwemo kukaimu nafasi ya Urais!.

Then, watu wanaoona hivyo wanatakiwa wamtake yeye ajiuzulu siyo wamlazimishe Rais ajaze nafasi. Rais halazimishwi kupokea ushauri wa yeyote kwa mujibu wa Katiba kama sivyo itakuwa ni chaos na hatokuwa huru kivile. Rais akimteua mtu mwingine kesho au akimthibitisha si watu wengine wanaweza kulalamika kuwa Rais kashinikizwa au kalazimika na hivyo itatolewa hoja nyingine kabisa.

Ukaimu huu sio sawa na ule Ukaimu wa mtu kukaimu nafasi fulani temporary mwenyewe akirudi unapisha. Huku ni kukaimu wakati nafasi haina mwenyewe!.
Mbona hii si nafasi ya kwanza ambayo inakaimiwa wakati mtu anasubiriwa kuteuliwa.

Kingine ambacho Mwanakijiji hakijui, hajui kuwa kaimu hata kaimu rais, hawezi kusaini amri yeyote ambaye inapaswa kusainiwa na rais ikiwemo kusaini sheria, kutangaza hali ya hatari, kuteua wala Kaimu rais haruhusiwi kusaini Presidential Preventative Detention Order!.

Enzi za Nyerere kuna siku Ali Hassan Mwinyi alikaimu na akasaini hati ya kizuizini, aliyetiwa kizuizini alishitaki Mahakama Kuu, amri ile ikapigwa chini kwa sababu Kaimu rais ni kaimu na sio rais, ukaimu unaishia kwenye kutoa maagizo na sio kusaini jambo lolote linalohitaji saini ya rais!.

Una assume mambo mengi sana. Kwanini unafikiria sijui tofauti ya kukaimu mbalimbali; si ndio maana ya swali langu hapa? Suala la nafasi ya jaji hakuna mtu anayesema Rais amevunja Katiba; na kama hajavunja sasa shida iko wapi? Ni kweli kawaida au taratibu ni kama sheria lakini neno "kama" ina nguvu yake; kawaida si sheria! Ukitaka iwe sheria ifanye sheria.


Mfano Bunge likitaka kufanya impeachment process Kaimu Jaji Mkuu hawezi kwa sababu aliielezwa kwenye sheria ni Jaji Mkuu.[/quote]

Hili linaweza kuwa kweli; kama ni matakwa ya sheria basi atakuwepo Jaji Mkuu. Sasa hivi hakuna impeachment process yeyote iliyoanzishwa au kitu chochote ambacho kinahitaji Jaji Mkuu ambacho hakijafanyika na sijajuzwa nimeulizwa kwenye original post. labda wewe uniambie ni kitu gani ambacho kinahitaji Jaji Mkuu ambacho hakifanyiki na kinaleta shida kwenye mhimili wa mahakama sasa hivi?

Taratibu ni kama sheria. Kama hutajawahi kuwa na Kaimu Jaji Mkuu muda wote huu, why now?!.

Paskali

This is another silly argument; kama kitu hakijawahi kufanyika ambacho kinaweza kufanyika na sasa kikafanyika haina maana ni makosa kufanyika! Labda hatujawahi kuwa na Rais aliyechukua uamuzi wa muda mrefu kama huu lakini haina maana anayechukua sasa anafanya makosa. Swali labda watu wajiulize ni kwanini amechukua muda mrefu (siyo amechelewa); na kwa vile hatuna namna ya kuhoji kisomi matokeo yake tunatengeneza vitu kwenye vichwa vyetu, tunavivarisha kengele na mapembe halafu tunaanza kuvikimbia wenyewe. Hivi kuna ugumu gani kwa mbunge kuuliza swali jepesi tu na kusikilizia jibu lake badala ya kutoa tuhuma zilizopikika kichwani mwa mtu?

Mheshimiwa Spika naomba kumuuliza mheshimiwa Waziri wa Katiba - ni lini Serikali inatarajia au inapanga kuhakikisha nafasi ya Jaji Mkuu inajazwa ama kwa kumthibitisha anayekaimu au kumteua mwingine?

Hili lingehitaji majibu bila lecture ya legal history and anthropology! Ila kwa vile mtu anataka maksi za kisiasa matokeo yake tunashindwa kupata majibu ya maana na baadaye watu wanaanza kutunga stori zao wenyewe na kuziamini.
 
Mwisho, kuna hoja nyingi za msingi ambazo zimetolewa na wachangiaji mbalimbali ktk post za nyuma , ingekuwa vyema ungezijibu maana naona unaruka na kuchagua zile "nyepesi nyepesi tu", which is very uncharacteristic of you..

What happened to reason??


Sijaona hoja nzito ambayo inahitaji kutumia mikono yangu yote miwili. Zinazohitaji majibu zinajibiwa kwa kadiri ninakuwa na muda wa kutulia kujibu. Hoja hujibiwa kwa hoja!
 
Umetoa hoja ambayo unajua kabisa wabunge wa CCM hawawezi kukubali jambo hilo hata kama lina faida,Wabunge wa CCM wapo kulinda chama sio maslahi ya nchi.

Jamani, haya ndio matokeo ya demokrasia! Ukitaka wasiwe na nguvu hiyo unakuwa na wabunge wengi! Sasa kama wana wabunge wengi na wanatumia wingi wao kwa ajili ya maslahi yaona Rais au chama chao; ndio demokrasia uzuri na ubaya wake. Na tusipoangalia tutaendelea kuwa wkenye hali hii hadi tuamue kujenga upinzani wa kweli ambao unaweza kushinda angalau kuwa na Bunge! Hili huwezi kuwalalamikia CCM wasipounga mkono.
 
Hii mada ina upande mwingine wa shilingi. Management ya watumishi (Jaji Mkuu ni mtumishi wa umma) ni fani ya kitaalamu yenye kanuni na taratibu zake. Mtumishi anapaswa kutimiza wajibu wake katika mazingira yatakayofanya utendaji wake uwe bora to the maximum ili kutimiza kikamilifu malengo ya nafasi yake. Mtumishi hawezi kamwe kutimisa azima hii katika mazingira ya kukaimu nafasi aliyo nayo. Hii ni kanuni na hili halina ubishi. Kuna tofauti kubwa sana kiutendaji kati ya afisa anayekaimu cheo na aliyethibitishwa kwenye hicho cheo. Hii bila shaka ilikuwa ndio concern ya Tundu Lissu kama mdau wa mfumo wa utoaji haki nchini.

Labda kitu kinachohitaji tafakuri pana hapa na ambacho kitalazimu kuingia kwenye viatu vya Rais Magufuli ili kuwa katika nafasi ya ku-hypothesize: je, ni kwa nini rais hakuteua Jaji Mkuu kamili na badala yake akateua kaimu? Hapa haitarajiwi hoja nyepesi na ya kisiasa kama, "rais alifanya hivyo kwa sababu ana mamlaka hayo"! Presidential prerogative just for the sake it?

Hapa naona watu wanajaribu kutetea watendaji wazembe wazembe; sasa kiapo anachokula ni cha nini kama hana mpango wa kutumika kwa kadiri ya uwezo wake wote? Yaani, mnataka kusema mtu atakuwa mzembe au hatofanya kazi sana kwa sababu anaweza asipate nafasi hiyo rasmi? Hizi ni fikra gani hizi. Inawezekana watu wamo humku ambao wakipewa nafasi ya kukaimu basi hawatendi kwa kadiri ya uwezo wao wote na kwamba wasipopewa nafasi ya kushika permanently hawatoumia sana na kuona wamerukwa! Hii ni dalili ya kutetea uzembe. Ukiteuliwa kushika wadhifa fulani iwe kwa muda au rasmi ni lazima utende kazi kwa uaminifu na weledi wako wote maana hilo ni jukumu lako.
 
..sasa akija kuteua Jaji Mkuu tofauti na huyu aliyekaimu miezi 5+ si itakuwa ubaya jamani?

Kwanini iwe ubaya? kwani alimteua kwa masharti kuwa "nitakuthibitisha baadaye"? Kama yeye Jaji Ibrahim anaona kuwa anacheleweshwa kuthibitishwa au anaona Jaji Mkuu mpya anacheleweshwa basi anachotakiwa kufanywa ni kuomba Rais amteue Jaji mwingine kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu. Very simple.
 
Alichofanya Kabudhi ni kutetea position ambayo ipo na wala siyo kwamba amefanya jambo lenye akili za ajabu.

Mtu yeyote akipewa position akaitetee, akapewa siku mbili tati za kujiandaa, anaweza kutetea hata jambo la hovyo kabisa. Watu wanatetea kwa umakini hata the holocaust - sembuse hili!

Hii dhana kwa wazungu wanaliita apologism. Mara nyingi linaendana na arrogance of power.
 
Nadhani hapa tunamdhania sana Prof. Ibrahim; kwamba kwa namna fulani si mtu mwadilifu na kuwa hawezi kutekeleza wajibu wake kwa sababu ana hofu ya kupoteza hiyo nafasi kwa msingi wa hii 'security of tenure'. Kudhania huku msingi wake ni nini?
Prof Ibrahim hana tatizo katika mjadala huu kabisa. Yeye ni mteuliwa
Prof kateuliwa na Rais baada ya kupewa majina. Kumteua Prof ni prerogative ya Rais , hakuna tatizo katika hilo na anatumia vigezo gani ni privilege ambayo kama prerogative haina tatizo

Ni makosa makubwa kwa yoyote kumtuhumu Prof iwe kwa uteuzi au uwezo wake
Ni makosa kudhania au kutilia shaka uadilifu wa Prof Ibrahim kuhusu uwezo wa majukumu yake

Msingi wa wa dhana yoyote inayoonyesha Prof kukwazwa inajengwa na 'Teuzi'
Nafasi ya kukaimu ina makusudi talaa linatokea lisilotarajiwa na mhimili lazima usimame

Prof Kabudi anaposimama na kutupa historia ya Nyerere bila kutueleza nini kinatokea leo
Kwamba jibu la kwanini kuna kukaimu kwa muda mrefu ni 'Nyerere alifanya hivyo pia'

''That was too low!'' Prof Kabudi alitakiwa asimame na kujibu hoja ya Lissu kwanini kuna kukaimu kwa muda mrefu. Tungepewa jibu rahisi kama la Nyerere! hakuna

Tena Lissu alisema kuna mambo mawili. Prof Ibrahim athibitishwe au achaguliwe mwingine

Hilo linatuacha na hoja kuwa, Prof amewekwa njia panda kwa kazi ya 'probation'

Uteuzi wa Jaji mkuu unapowekewa probation lipo tatizo!
Mhimili wa sheria unapoteza nguvu kwasababu Jaji mkuu ni alama ya mhimili

Kazi ya kwanza ya Bunge ni kumpata Spika, si kumpata kaimu Spika
Kazi ya kwanza ya Serikali ni kumpata Rais si Kaimu Rais
Teuzi ya kwanza ya Rais ni Mwanasheria mkuu si kaimu mwanasheria mkuu

Leo tuna Kaimu Jaji mkuu ambaye akiwa na Rais na Spika, yeye yupo katika 'probation'

Swali ambalo Prof Kabudi na MM wanaweza kutusaidia ni moja, kuna sababu gani za nafasi ya Jaji mkuu kwa mwaka 2017 kukiwa na wastaafu, wazoefu, vijana n.k. katika fani ya sheria kuwekewa kaimu Jaji katika mtindo wa 'probabtion'

Kabudi hakuwa na majibu, alizunguka zunguka na hakika 'darsa' alilosimama ilikuwa aibu

Labda MM anajibu, so far hatujaona katika aliyoandika
 
Hii ndio post yako yangu bora kabisa Mkuu!
 
Back
Top Bottom