Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Tundu lisu amekutana na gwiji. Hata mmutee vipi anapwaya alikuwa anapewa kiki na wasiojua sheria. Sasa kaja mwenyewe. Ila nilikuwa nasikia siku nyingi sana kuwa tundu lieu hajui sheria Bali ni mwanaharakati tu Wa sheria na mpayukaji pasipo kujua lolote ndo mana kabudi kasema mwanasheria yeyote anapaswa kuwa na busara siyo kila kitu kinatatuliwa na sheria bali jamii nabethics sake.
Lakini kila siku anawabwaga mahakamani.
 
Hoja ya lissu mbona iko wazi kabisa...hajasema kuwa rais amekosea..anachosema lissu ni kuwa sheria zetu/katiba hazijaweka limit ya kuwa na acting chief Justice

Kitu ambacho kinaweza kuwa na madhara...hivi hebu chukulia kwa mfano rais aendelee kuwa na kaimu jaji hadi mwaka 2020.....hili jambo lin athari katika utendaji wa jaji

Kwa bahati mbaya Watu wengi huwa hamumuelewi Lisu kwa kipindi hicho anaongea...mnakuja kumuelewa baada ya miezi kadhaa au miaka kadhaa kupita

Kweli mkuu
 
Hili pia ndugu yangu Nguruvi kalisema hapo juu; lakini wewe na yeye wote hamsemi je sheria au utaratibu huo unamtaka Rais ateue mtu muda gani tangu apewe majina hayo matatu? Kama kuna mtu anaamini RAis amechelewa kinyume cha sheria tangu apate majina hayo matatu wapo wanasheria makini tu wafungue kesi mahakamani iamuliwe! Lakini sijaona hata mmoja anayedai kuwa Rais amevunja sheria
MM, kwanza, binafsi nimejadili hakuna sheria aliyovunja Rais kwa kuteua kaimu Jaji mkuu.

Pili, nimekubaliana nawe uhusu prerogative aliyo nayo Rais.

Kutoweka muda ni katika preorogative hizo kwa maana asifanye kazi hiyo under duress.

Katika kuhakikisha hilo Paskali kasema Jaji mkuu alitoa notisi ya miezi 6. yaani nusu mwaka.

Tatu, Rais anavyombo vyote vya kumwezesha kufanya kazi zake haraka na kwa ukamilifu.

Nne, Rais ana prerogative ya kumsamehe mtu aliyehukumiwa kunyongwa n.k.

Hata hivyo, kama Rais atamsamehe mtu huyo kwasababu zenye shaka, hiyo preorgative inapoteza nguvu zake na kitu kinachofuata ni 'abuse of power'

Rais alimteua mkuu wa majeshi baada ya aliyekuwepo kustaafu. Hakukuwa na kaimu kwasababu ya umuhimu wa nafasi hiyo katika Taifa. Umuhimu huo ndio ule wa mhimili wa sheria katika mihimili 3

Prerogative aliyopewa ni ya kuteua kaimu Jaji mkuu, inapotokea uteuzi huo ukaleta shaka kutokana na muda na sababu ambazo hazieleweki, prerogative inapoteza maana yake

Tunaweza kuwa na Kaimu Jaji mkuu-2020, hakuna sheria iliyovunjwa, imetumika prerogative.

Machoni mwa umma hiyo itakuwa dereliction of duties inayotokana na abuse of power iliyojengwa katika msingi wa 'prerogative'

Kwamba Rais ana full power, ana prerogative, ana privilege zote halafu anatenda kwa matakwa na si kwa public interest, hiyo haiwezi kuwa prerogative mbele ya umma, ni abuse of power
 
Na akiwa Jaji Mkuu hawezi? mbona hii haina mantiki kabisa. Yaani, mnahofia kaimu kujipendekeza kuliko mtu mwenyewe hasa? Chukulia kwa mfano akiteuliwa mtu mwingine kushika Ujaji Mkuu hatojipendekeza kwa atakayemteua
MM kuna point hapa una miss. Mchakato wa kumuondoa CAG ni mzito ndiyo maana siku zote unaona kuna kujiamini

Kumuondoa Jaji mkuu (CJ) kuna mchakato mzito na si jambo rahisi
Kumuondoa Kaimu CJ ni suala la kusema amefanya vetting na Mzee Mwanakijiji sasa ndiye CJ, simple

Kwa maana hiyo, nafasi ya Kukaimu CJ haina tofauti na kiongozi yoyote wa serikali, au CCM

Ndiyo maana kuna wasemayo kuna 'Mhimili uliojichimbia zaidi kwenda chini'
Katika mazingira hayo uteuzi wa kaimu CJ ni mwendelezo tu , lakini pia ni humiliation kubwa kwa judicial system nchini

Vinginevyo tueleze kuna sababu gani zinazopelekea nafasi hiyo kukaimiwa kwa muda mrefu kiasi hicho? Sioni tatizo kama tutaajiri Jaji kutoka Malawi, Vanuata au Trinidad and Tobago kama hatuna qualified people.

Lakini pia hatuwezi kukwepa ukweli kuwa nafasi hiyo kuwekewa 'probation' au 'apprentice' si jambo zuri
 
Inategemea, kwangu mimi lilikuwa ni muhimu kwani nimejifunza mengi ambayo sikuyafahamu, siyo tu kuhusu mambo ya uteuzi wa Jaji bali kwa mfano sikujua kwamba Raisi wa AK hachaguliwi na Wananchi kama wetu bali huchaguliwa na Bunge, na kwamba Chama kiko juu ya raisi wa AK na kinaweza kumuondoa madarakani kama Mbeki alivyoondolewa, hivyo nimejua tofauti ya Raisi wa AK na wetu na zipi limitations za mifumo yote miwili n.k.

Hivyo leo hii siwezi kuanza kumlinganisha Raisi wa JMTZ na Raisi wa AK kwa mfano kwani najua ni vyeo viwili vinavyofanana lkn ni tofauti!
Pole.
 
Tundu lisu amekutana na gwiji. Hata mmutee vipi anapwaya alikuwa anapewa kiki na wasiojua sheria. Sasa kaja mwenyewe. Ila nilikuwa nasikia siku nyingi sana kuwa tundu lieu hajui sheria Bali ni mwanaharakati tu Wa sheria na mpayukaji pasipo kujua lolote ndo mana kabudi kasema mwanasheria yeyote anapaswa kuwa na busara siyo kila kitu kinatatuliwa na sheria bali jamii nabethics sake.
Dk migiro, Dk Harrison, werema na masaju ni kwel hawajui sheria? Mana umesema mwenyewe kaja, INA mana waliomtangulia hawakua bora kama yeye.
 
Mnyika na Salum Mwalim walikaimu nafasi ya ukatibu mkuu muda mrefu ndani ya Chadema, kinyume na katiba. Lisu akuliona ilo upofu ndani ya Chadema (Sababu ya Tumbo)... Siasa za Tundu Lisu ni za tumbo Lake, ni sawa na Mario, anaelelewa na mwanamke, anaishi nae ila aoni kasoro zozote, ila anakosoa maisha ya Mario wenzake
 
Huna akili ya kumwelewa Lissu. Na hiyo 'ansard' unayotaka watu wakasome haipo duniani.

Na Lissu hakuingia bungeni mara ya kwanza 2011
We upo dunia gani Lissu ameingia bungeni uchaguzi wa 2010, kikao cha pili ndio akakurupuka na maneno roporopo hayo.
Tatizo mna mahaba na mtu kupitiliza, wahenga hawakukosea "Ukipenda, chongo huona kengeza"
 
How? litakuwa na madhara gani? Na kama sheria au Katiba haijaweka kikomo hilo ni tatizo la nani hasa? Kwanini LIssu asije na hoja ya dharura ya kutaka mabadiliko ya sheria au kushawishi wabunge angalau 2/3 yao wafanye mabadiliko ya Katiba?
How? litakuwa na madhara gani? Na kama sheria au Katiba haijaweka kikomo hilo ni tatizo la nani hasa? Kwanini LIssu asije na hoja ya dharura ya kutaka mabadiliko ya sheria au kushawishi wabunge angalau 2/3 yao wafanye mabadiliko ya Katiba?

Bunge lipi unaloongelea la kufanyia marekebisho ya katiba yatakayoletwa na Upinzani? Hili la tulia Wa tz au
 
Kwa kweli hakukuwa na darasa lolote. Binafsi sijaona jambo jipya ambalo Prof Kabudi alilisema ambalo hao "wanafunzi" wake walikuwa hawalijui. Kama alikuwa amekusudia kujibu hoja za Mh Lissu, pia sikusikia hoja zikijibiwa zaidi ya mipasho na majigambo tu. Ukishaona mtu ana demand aheshimiwe (kwa umri wake?), ujue tayari lipo tatizo. Ukweli na hoja zinapaswa kusimama zenyewe bila kuangalia anayezitoa.
Kama hukuona darasa lolote jua kabisa kilichofundishwa kiko juu ya upeo wa akili yako. sawa na kumfundisha advanced mathematics mtoto wa chekechea hawezi kuamini unamfundisha. Ila Lissu alielewa na ndio maana halitulia.

Pia sio kosa kuwafundisha watu wanaojua lakini wanajifanya kutojua ili kupata kiki kutoka kwa wananchi wasio jua. Ukimsikia Tundu alitamka wazi kabisa rais amevunja katiba. Kama hakuwa na maana hiyo basi inabidi apelekwe shule ya kuongea ili asiendelee kuongea vitu asivyomaanisha.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Sijasikiliza hayo ya bungeni na sidhani kama bado nina interest ya siasa za bunge hivi sasa ambazo kwangu naona ni kama zimekosa mvuto!!

Tuje kwenye hiyo hja ya kwamba, kukaimu kwa muda mrefu hakuwezi kumfanya Kaimu Jaji kushindwa kufanya kazi zake sawa sawa!!!

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Rais hana mamlaka ya kumtumbua Jaji wa Mahakama Kuu kirahisi rahisi tu!

Inapotokea sababu ambazo rais anaona Jaji huyu hafai tena kuwa jaji, hata kama ni suala la ukosefu wa maadili, bado Rais anatakiwa kwanza kuunda Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume, na miongoni mwao angalau nusu wanatakiwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu kutoka nchi za Jumuiya ya Madola!

Tume hii itachunguza tuhuma dhidi ya Jaji kuona kama ni kweli au hapana!

NOTE: Nitapitia katiba ili nione kifungu hicho kinasemaje kwa yakini!!

Kutokana na kifungu hicho cha Katiba, Jaji Mkuu na in fact, Jaji yeyote wa Mahakama Kuu hawezi kuwa na hofu ya kutekeleza wajibu wake kwa kuhofia mamlaka ya uteuzi kwa sababu, anafahamu, hawezi kuondolewa hovyo hovyo au hata kwa makosa ya kubambikiwa!!!

Kaimu Jaji Mkuu kwa nafasi yake hiyo sio Jaji wa kawaida na wala sio Jaji Mkuu ambao wanaweza kulindwa na kifungu hicho hapo juu! Kwahiyo, Rais anaweza kumtoa muda wowote bila maswali kwa sababu, atakachomvua sio Ujaji wala Ujaji Mkuu bali Ukaimu Jaji Mkuu ambao sidhani kama Katiba inatoa ulinzi niliotaja hapo juu!!!

Hoja ndiyo hiyo hapo juuu!!

Na kwa staili hiyo, unaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu kama ilivyo sasa; na ukiona anazingua unamtoa unamweka mwingine nae anakuwa Kaimu Jaji Mkuu!! Sasa hofu isije kwamba, kwa kuhofia kutokuwa na ulinzi wa katiba, basi huenda wengine wanaweza kufanya mambo kwa kuyaridhisha mamlaka ya uteuzi!!
Hili lako ndilo darasa haswa! La Paramagamba katika hoja hii halikuwa darasa, bali Profesa alidhihirisha namna wasomi wetu wanavyojivua usomi pale wanapopata ulaji, na kumshangilia Palamagamba ni kukubali kuliweka rehani taifa letu! Jaji Mkuu kukaimu kipindi kirefu tafsiri yake ni kuiondolea mamlaka Mahakama! Akina Mwanakijiji nao kwa kujitoa akili wanaanza kufananisha kitendo cha nafasi ya Jaji Mkuu kukaimiwa ni sawa tu na Makamu wa Rais kukaimu urais!
 
MM, kwanza, binafsi nimejadili hakuna sheria aliyovunja Rais kwa kuteua kaimu Jaji mkuu.

Pili, nimekubaliana nawe uhusu prerogative aliyo nayo Rais.

Kutoweka muda ni katika preorogative hizo kwa maana asifanye kazi hiyo under duress.

Sasa hoja nzima inasimama na kuanguka na hiyo. Kama Rais hajavunja Katiba na kwamba prerogative yake inampa uhuru wa kutofanya kitu under duress; huoni kinachofanyika hapa ni kile ambacho kinataka kutengeneza duress kwa Rais? na hivyo kuvunja dhana ya prerogative ya Rais. Nini kitawazuia watu wakati mwingine tena kumshinikiza Rais kinyume na sheria au Katiba kufanya jambo fulani ili ionekane amelifanya wanavyotaka watu hao?


Katika kuhakikisha hilo Paskali kasema Jaji mkuu alitoa notisi ya miezi 6. yaani nusu mwaka.

Nguruvi, sikuijibu hoja hiyo ya muda kwa sababu sijaona mahali popote ambapo panathibitisha kuwa Jaji Mkuu alitoa notisi miezi sita na alituma majina wakati huo. Sijui unajuaje kama Jaji Mkuu alitoa naotisi hiyo kama Paskali anavyodai. Ni jambo moja kudai ni jingine kabisa kuthibitisha ili tuzungumzie kitu chenye uhakika.

Tatu, Rais anavyombo vyote vya kumwezesha kufanya kazi zake haraka na kwa ukamilifu.
Unajuaje kwamba vyombo hivyo hivi sasa havifanyi kazi kwa haraka? Sote tunakumbuka jinsi alivyochukua muda kuunda baraza la mawaziri, na hata kuteua watu wengine. Kwanini tusimpe uhuru ule ule linapokuja suala la Jaji Mkuu? Binafsi nina mpa benefit of the doubt kwamba vyombo vyake vya kumsaidia katika uteuzi vinafanya kazi kwa jinsi ambavyo alitarajia. Sijui kwanini wenzetu hamtaki hili liwe hivyo kwamba ni lazima angekuwa ameshajaza nafasi hiyo miezi kadhaa nyuma ili isionekane muda umepita. Binafsi hata ukipita mwaka sitashtuka sana zaidi ya kuenddelea kuamini kuwa anaelewa umuhimu wa kuwa na Jaji Mkuu na uamuzi wake wa kumfanya mtu akaimu labda una jambo kubwa zaidi kuliko ambavyo tunadhania.


Nne, Rais ana prerogative ya kumsamehe mtu aliyehukumiwa kunyongwa n.k.

Hata hivyo, kama Rais atamsamehe mtu huyo kwasababu zenye shaka, hiyo preorgative inapoteza nguvu zake na kitu kinachofuata ni 'abuse of power'

Madaraka na prerogative ya Rais kumsamehe mtu ni absolute. Hivyo hata akiabuse - God forbid - bado itakuwa ni absolute. Hakuna mahali pa kudai au kuweza kuonesha kuwa ameabuse. Ndio maana Marais wengi wanapokaribia wanasamehe watu wakati mwingine hata kiushkaji kwa sababu hakuna wa kuweza kuwahoji. Kumbuka ya Clinton na hata Obama na Bush.

Rais alimteua mkuu wa majeshi baada ya aliyekuwepo kustaafu. Hakukuwa na kaimu kwasababu ya umuhimu wa nafasi hiyo katika Taifa. Umuhimu huo ndio ule wa mhimili wa sheria katika mihimili 3
Ni kwa kiasi gani sheria na kattiba inamruhusu kumteua Kaimu Mkuu wa Majeshi? Masuala ya majeshi yanaongozwa kwa taratibu zake. lakini pia Jeshi siyo Mhimili mwingine; yeye ndio Amiri Jeshi Mkuu hivyo suala la kumteua mtu mwingine labda si gumu kivile kwani kama unavyojua alimuongezea Mwamunyange mwaka mmoja - ni kama alitumia mwaka mzima kumfikiria mtu anayemtaka kumteua kushika nafasi hiyo. Inawezekana hili pia linaendelea kwenye Mahakama? Hapana sina majibu ni speculation tu.

Prerogative aliyopewa ni ya kuteua kaimu Jaji mkuu, inapotokea uteuzi huo ukaleta shaka kutokana na muda na sababu ambazo hazieleweki, prerogative inapoteza maana yake

Hii shaka anayo nani? Na msingi wake ni nini. Binafsi sijaona shaka yoyote ile na ndio maana nilisema kama Prof. Ibrahim ndio mwenye shaka ana njia ya kushughulikia suala hilo. Hawa wengine hawajaonesha standing yao ni nini kwamba Rais hajampata Jaji Mkuu mpya. Msingi wa shaka hii uko kisiasa zaidi kuliko kisheria au Kikatiba. Hakuna tatizo lolote la Kikatiba hivi sasa. Ama lipo ambapo binafsi sijalielewa, nitashukuru ukinionesha. NI tatizo gani la Kikatiba au la Kisheria ambalo lipo kwa Prof. Ibrahim kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu akisubiri Jaji Mkuu mpya kupatikana? Suala la muda siyo suala la kisheria au kikatiba; suala la 'shaka' ni la kufikirika kwaa kweli kwa sababu hiyo shaka imekaa kisiasa zaidi.

Tunaweza kuwa na Kaimu Jaji mkuu-2020, hakuna sheria iliyovunjwa, imetumika prerogative.
Inawezekana kabisa na hakutakuwa na sheria kuvunjwa au tatizo la msingi. Japo, inawezekana isionekane vizuri kwa baadhi ya watu. Lakini ndiyo sheria iko hivyo. Wabunge wakiona ni tatizo kubwa kabisa wanahitaji kukuza balls zao na kutunga sheria au kufix sheria ili tatizo hili lisiendelee kuwepo. So far, wabunge wengi hawajaona kuwa ni tatizo na halijawa tatizo kubwa hivyo. Walikuwa na umoja zaidi wa kumfuatilia Makonda na "kejeli yake" na kina Mbowe na Mdee kuliko suala la Jaji Mkuu. Go figure.

Machoni mwa umma hiyo itakuwa dereliction of duties inayotokana na abuse of power iliyojengwa katika msingi wa 'prerogative'
It is only an abuse of power if power is abused; if its not then its not abuse of power. Kama Rais hajavunja sheria au katiba hakuna abuse of power. Abuse of power is a legal concept not a political sentiment or statement.

Kwamba Rais ana full power, ana prerogative, ana privilege zote halafu anatenda kwa matakwa na si kwa public interest, hiyo haiwezi kuwa prerogative mbele ya umma, ni abuse of power

Not necessarily; unajuaje hafanyi kwa maslahi ya umma? kama asingemkaimisha mtu kabisa na akaacha nafasi hiyo then tungekuwa na hoja nzito sana ambayo hata MIMI ningesimama kudai awepo kaimu kama hajapata mtu wa kujaza nafasi hiyo. Lakini kwa vile mtu yupo na kazi zinafanyika then hoja nzima inaanguka bila kusukumwa.
 
Bunge lipi unaloongelea la kufanyia marekebisho ya katiba yatakayoletwa na Upinzani? Hili la tulia Wa tz au
Si limechaguliwa na wananchi; ndio hilo hilo. Kama huoni lina uwezo next election chagua watu wengi ambao unafikiri wataweza kufanya kile uanchokitaka. Hatuwezi kulalamikia Bunge wakati wabunge 10 tu kati ya wabunge zaidi ya 350 wanateuliwa na Rais; wengine wote wanapigiwa kura somehow; with the exception of ex-officio member.
 
Naomba izingatiwe kuwa msisitizo mweusi na wa italiki ni wa kwangu kwa ajili ya kuweka msisitizo.

Kwanza kabisa, siyo kweli - kama mtu akisoma Katiba - kwamba lengo la kifungu cha kumpa Rais kuteua Kaimu Jaji "kilidhamiria" kuwa atateuliwa pale tu "jaji mkuu yupo" lakini kwa namna fulani anashindwa kutekeleza majukumu yake. Huku ni kudhania (assumption) ambayo haina msingi.

Katiba imesema kuwa endapo mambo matatu yakitokea basi Rais anaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu. Mambo hayo kwa mujibu wa Ibara ya 118:4 ni kuwa Rais anaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu endapo mambo yafuatayo yatatokea: a. Kiti kitakuwa wazi (na hapa ina kuwa implied kwa sababu mbalimbali ikiwemo, kifo, kujiuzulu, kustaafu n.k), b. Jaji Mkuu hayupo Tanzania (sehemu ya hoja yako) na tatu Jaji mkuu atashindwa kutekeleza majukumu yakekwa sababu yeyote ile (na implication hapa ni vitu kama ugonjwa, katekwa n.k) basi Katiba inasema " Rais ataona kuwa kwa muda wa
tukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua Kaimu Jaji Mkuu, basi Rais anaweza kumteua Kaimu Jaji Mkuu kutoka miongoni mwa Majaji wa Rufani."


Hivyo, SI KWELI na haina msingi wowote katika Katiba kuwa lengo la Ibara ya 118:4 lilikuwa ni pale tu Jaji anapokuwa yupo lakini hawezi kufanya kazi yake. Hili ni la kujitungia tu halina msingi katika Katiba na ukilifikiria halina mantiki ya kiutendaji. Hivyo, linaanguka lenyewe.
Mkuu Mzee Mwqnakijiji, with due respect tangu mwanzo nilikuambia you've missed the point, na hapa sasa bado you've missed the point again and you will miss it again and again kwa sababu ameisha amini hicho unachojua ndicho kumbe sicho!.

Hizo scenarios zote tatu za kutokuwepo kwa jaji mkuu ni sawa kama ulivyoeleza ila usichojua wewe na sio hujui bali hutaki kujua kuwa uteuzi wa kaimu jaji mkuu hufanyika nafasi hiyo ikiwa wazi kwa sababu nyingine zozote na sio wakati jaji mkuu amemaliza muda wake!.

Kuna sheria kibao zimewekwa kwa nia njema lakini zinakuwa applied wrongly na wakuu wa serikali yetu.

Mfano kwenye uteuzi wa mawaziri katiba inasema mtu kuteuliwa waziri lazima awe mbunge, tumeshuhudia mtu atateuliwa ubunge na kuwa mbunge mteule kisha anateuliwa waziri na kuingia ofisini kabla hajaapishwa kuwa mbunge kamili.
Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

Hivyo matumizi ya kukaimu kwenye issue ya Jaji Mkuu ni makosa kwa sababu Tume ya Majaji ilikwisha peleka majina matatu, miongoni mwa majina hayo, mmoja wao ateuliwe kuwa Jaji Mkuu. Kitendo cha rais Magufuli kuteua Kaimu Jaji Mkuu ni dharau kubwa kwa Tume ya Majaji.

Kama jina la Prof. Ibrahim Juma lipo miongoni mwa majina matatu hayo, then anachofanya rais Magufuli ni dharau kubwa kwa mhimili wa mahakama. Mahakama ni mhimili wa dola, mhimili ni egemeo, kama yalivyo mafiga matatu yote yanatakiwa kuwa sawa ili chungu kisimame, figa moja likiwa tenge chungu kitakuwa tenge. Kwa nini mhimili huu ukaimiwe? .

Unless kupitia vetting, majina yote matatu yaliyopendekezwa na tume ya majaji yalikataliwa, hivyo rais Magufuli akamteua Kaimu ili kushikilia kwa muda wakati Tume ikitafuta majina mengine!.

Hili pia ndugu yangu Nguruvi kalisema hapo juu; lakini wewe na yeye wote hamsemi je sheria au utaratibu huo unamtaka Rais ateue mtu muda gani tangu apewe majina hayo matatu? Kama kuna mtu anaamini RAis amechelewa kinyume cha sheria tangu apate majina hayo matatu wapo wanasheria makini tu wafungue kesi mahakamani iamuliwe! Lakini sijaona hata mmoja anayedai

Ni kweli sheria haikuweka muda, sio kila kitu sheria imeweka muda, vitu vingine ni application tuu ya logic na common sense ambavyo very unfortunately havipo. Jaji Mkuu amestaafu, amestaafu ghafla kabla ya muda wake, then ingekuwa right kuteua Kaimu wakati tunatafuta Jaji Mkuu, this was not the case!. Do we need kuweka time frame?!

This is very absurd; Inawezekana vipi kiti cha Jaji Mkuu kiwe wazi permanently halafu unataka kijazwe. Au neno "permanently" halina maana tena? Kama kitajazwa hakiko permanently vacant! It is only because it is temporarly vacant ndio maana watu wanataka kijazwe. I don't like self contradictions.
Sometimes tumia context ya nilichomaanisha na sio kutumia syntax ya neno permanently!. Nimekueleza Kaimu Jaji Mkuu anapaswa kuteuliwa wakati nafasi ya Jaji Mkuu inapokuwa wazi temporarily safari au ugonjwa na akirudi au akipona anaendelea. Au Kaimu Jaji Mkuu atateuliwa kikitokea kifo, hili ni tukio la ghafla hivyo hakuna maandalizi yoyote ya kumpata Jaji Mkuu ndipo mtu anateuliwa kukaimu kutoa muda wa kumtafuta Jaji Mkuu. Hivyo hapa Kaimu ni kama kiraka tuu.

Situation iliyopo ya Jaji Mkuu kustaafu kwa umri hivyo maandalizi yote yamekamilika ya replacement. Kustaafu kwa umri ni permanent na sio temporary hadi ku warrant Kaimu!. Hapa Jaji Mkuu has left the office permanently, angekuwa amesafiri then ingekuwa temporarily!. Why uweke Kaimu kwa nafasi wazi ya Mkuu wa chombo cha dola?.
Then, watu wanaoona hivyo wanatakiwa wamtake yeye ajiuzulu siyo wamlazimishe Rais ajaze nafasi. Rais halazimishwi kupokea ushauri wa yeyote kwa mujibu wa Katiba kama sivyo itakuwa ni chaos na hatokuwa huru kivile. Rais akimteua mtu mwingine kesho au akimthibitisha si watu wengine wanaweza kulalamika kuwa Rais kashinikizwa au kalazimika na hivyo itatolewa hoja nyingine kabisa.

Mbona hii si nafasi ya kwanza ambayo inakaimiwa wakati mtu anasubiriwa kuteuliwa.
Yote usemayo kuhusu rais ni kweli, kitendo tuu cha kuteuliwa kuwa Kaimu ni Heshima tosha, hakuna anayemlazimisha rais kutimiza wajibu wake lakini hakijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu nafasi ya mhimili mmoja wa dola kukaimiwa kwa kipindi kirefu hivi huku nafasi ikiwa wazi permanently!.

Kitendo cha kumkaimisha Prof. Juma ni kama kutuambia kuwa hatoshi ndio maana yuko under probation!. Tunamlazimisha rais Magufuli amthibitishe na ikitokea akamteua mtu mwingine (probably kwa kumtafuta Msukuma popote), then Dr.Juma aage tuu na kujipumzikia kwa amani.

Una assume mambo mengi sana. Kwanini unafikiria sijui tofauti ya kukaimu mbalimbali; si ndio maana ya swali langu hapa? Suala la nafasi ya jaji hakuna mtu anayesema Rais amevunja Katiba; na kama hajavunja sasa shida iko wapi? Ni kweli kawaida au taratibu ni kama sheria lakini neno "kama" ina nguvu yake; kawaida si sheria! Ukitaka iwe sheria ifanye sheria.

Mfano Bunge likitaka kufanya impeachment process Kaimu Jaji Mkuu hawezi kwa sababu aliielezwa kwenye sheria ni Jaji Mkuu.

Sio naasume, bali huu ndio ukweli wenyewe ndio maana kwako kukaimu ni kukaimu tuu, hujui tofauti ya nafasi wazi temporarily kunakohitaji Kaimu na nafasi wazi permeability kunako hitaji replacement!.

Kwa kumalizia Magufuli ni rais wetu ila vingi anafanya ndivyo sivyo, wahusika wa kumshauri kwa karibu ndio hawa wanamuogopa. Huku kwenye social media kwa kwa manguli critical kama Mzee Mwanakijiji ndio hawa sasa wanamuabudia hadi kumuita ni Alfa na Omega, unategemea nini?.

Siku ile ulipomuita Magufuli alfa na omega nilikubishia nikakueleza Magufuli is only a human being kama mimi na wewe ila ni rais wetu

Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba!

Nikasema anaweza kuwa anafanya makosa ila sio makosa yake, kwa sababu ana washauri, anaweza kuwa anashauriwa vibaya, hivyo kila analotenda ndivyo sivyo, wa kulaumiwa sio yeye bali ni waliomshauri, au wasaidizi wake wanaoona ndivyo sivyo na wananyamaza badala ya kumshauri kufanya ndivyo.

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa chini na mchanga kusafirishwa?

AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa Nguvu ya Kisheria

Paskali
 
Kama hukuona darasa lolote jua kabisa kilichofundishwa kiko juu ya upeo wa akili yako. sawa na kumfundisha advanced mathematics mtoto wa chekechea hawezi kuamini unamfundisha.
Hakuna jipya alilosema wala hakujibu hoja. Sasa kama kutokuona jipya ni upeo wa chini, hapo sina namna nzuri ya kukusaidia.

Hivi kusema Rais wa SA hachaguliwi kama ilivyo wa Tz ni kitu kipya kwako? Au kusema UK hawana written constitution nayo ni jambo jipya? Mambo hayo yanajibu hoja za Lissu? Hapana ubishi kuwa Prof Kabudi yupo vizuri sana, lakini hilo haliondoi ukweli kuwa hakuna jambo jipya alilosema pale bungeni. Lakini nakubaliana na wewe, kuwa kuona "darasa" inategemea sana na upeo wa mtu.
 
Kwa kweli hakukuwa na darasa lolote. Binafsi sijaona jambo jipya ambalo Prof Kabudi alilisema ambalo hao "wanafunzi" wake walikuwa hawalijui. Kama alikuwa amekusudia kujibu hoja za Mh Lissu, pia sikusikia hoja zikijibiwa zaidi ya mipasho na majigambo tu. Ukishaona mtu ana demand aheshimiwe (kwa umri wake?), ujue tayari lipo tatizo. Ukweli na hoja zinapaswa kusimama zenyewe bila kuangalia anayezitoa.


mnaweza kukaa kwenye lecture hall watu wengi na mkahudhuria seminars pamoja ila mtihani ukitoka kuna wanaopata A, B, C.....na wengine F.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom