Ndio ukweli unaojengewa hoja dhaifu kabisa. Hakuna sababu za nchi hii kuwa na kaimu kwa muda wote
Othaman alitoa notisi kwa muda mrefu, hakuamka asubuhi na kusema anastaafu
Vetting ilitakiwa ifanyike, Rais ana vyombo vyote ambavyo hata siku moja vingeweza kumpa habari zote anazotaka kupata Jaji mkuu
Kabudi kasema, Nyerere alitoa sababu na sote tunajua. Mwaka 1962 hatukuwa na Madaktari (MD) zaidi ya 10, wapi tungepata Jaji mkuu?
Hali si hiyo, sasa hivi wakurugenzi wengine wana PhD. Kuna majaji wenye uzoefu.
Tunaweza kuomba Kenya, Uganda n.k. Kwanini tuwe na kaimu muda wote huo?
Kinachofanyika ni kuondoa nguvu ya Jaji mkuu na kumweka kaimu katika level sawa na mkurugenzi wa TRA , Bandari au kwingine kwa kujua Jaji mkuu mchakato wa kumuondoa si rahisi na utazua maswali mengine ndani na nje ya nchi.
Sasa MM anaposema ni pres prerogative, nakubaliana naye, lakini tukubali prerogative hata pale inapotumika kinyume na inavyokusudiwa?
Turuhusu mambo yaende ende kwa kutumia neno prerogative?