Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Umepewa hoja zote za kwa sababu gani haipendezi mtu kuwa Kaimu Jaji Mkuu kwa muda wote huo na mtu kama Pascal Mayalla amekutajia hadi sababu za msingi zinazoweza kumfanya Rais kuteua Kaimu Jaji Mkuu!!

Yote hayo huyataki!!!

Now your turn: Toa sababu moja tu ya msingi yenye busara ndani yake kwanini mtu awe Kaimu Jaji Mkuu muda wote huo!!! Sababu inaweza kuwa na uhalali wa kisiasa au hata kijamii... JUST ONE!

Hili ndilo tatizo; sasa mimi nitajuaje sababu ya uhakika ya kwanini hili limefanyika. Kama unataka nikisie nitakuambia sababu moja ni kuwa Rais bado hajaona sababu ya kumthibitisha aliyepo ama hajapata mtu wa kuchukua nafasi hiyo. Ukiniuliza "kwanini" nitakuambia sijui ni Rais mwenyewe anajua. Na kwa vile hakuna sheria imevunjwa sina tatizo. Nasubiri tu amthibitisha Ibrahim au amteue mwingine. That is his prerogative. Nje ya hapo nitakuwa kwenye klabu ya wadhaniao.

Usituambaie masuala ya kuvunja au kutovunja katiba kwa sababu JPM hana moral authority linapokuja suala la ulindaji wa katiba!!!

Huna sababu ya kupayuka; naweza kusoma vizuri tu.

Isitoshe, hakuna anayesema JPM amevunja katiba kwenye hilo... sana sana watu wanailaumu katiba kutoa loophole ya Rais kuweza kukaa hata miaka 5 madarakani huku Mahakama ikiongozwa na Kaimu Jaji Mkuu kwa miaka yote hiyo!

Na hivyo, kwa sababu nilizotaja mwanzoni... Rais anaweza kubadilisha Kaimu Jaji Mkuu mara nyingi apendavyo bila kuwapo kwa legal argument kwamba Rais anavunja sheria!!!

Sasa kama havunji tatizo liko wapi; kama tatizo ni la kisheria njia ni kufix it kwa kutumia taratibu za kibunge za kushughulikia mapungufu ya kisheria au hata Kikatiba.

Or else, labda ukiri kwamba Rais anatumia ana-take advantage ya mapungufu ya katiba kufanya vile anavyotaka yeye na hivyo kuthibitisha ile kauli ya Hayati Baba wa Taifa kwamba "Katiba hii inampa rais nguvu ya kuwa dikteta!"

Hili linawezekana lakini ndio mazao ya demokrasia na sheria. Kile ambacho sheria haikatazi, sheria inaruhusu. Na mtu hawezi kuadhibiwa kwa kitu ambacho si kosa kisheria.

Btw, mwanzoni nilikutajia watu walioyakana yale waliyokuwa wanayasimamia hapo mwanzoni kwa sababu tu ya madaraka na nikahitimisha kwamba, unless huyo Ibrahim ni very exceptional lakini nae hana tofaauti yoyote na akina Polepole, Mwakyembe, Kitila Mkumbo na wengine kahaa!!!
Well, kama kila mtu yuko hivi; na kwamba hakuna tena waadilifu (unless ukimaanisha wale nje ya serikali tu ndio waadilifu) basi hakuna matumaini kwani hakuna yeytoe ambaye ana tofauti. Hii ni namna mbaya sana ya kuubariki uzembe, ufisadi na utendaji mbovu wa kazi. Kama kila mtu ni mbovu basi haijalishi kama mtu anakaimu au anathibitishwa. Wote kama wasemavyo wajomba zangu "zikongwine".

Kwavile umehoji kwanini watu waamini Ibrahimu anaweza kuwa cheap guy!! Jibu ni kwamba we make judgement basing on past experience or else, tuambie hapa ni nini kinachomfanya Profesa Ibrahimu awe so exceptional!

That's is silly; how can you make a judgement on somebody based on someone else's past experience. Unless you are saying that you know something about Prof. Ibrahim compromising incompetency and professional mediocrity. Is that what you are saying?

I hope post hii utaijibu kwa sababu una kawaida ya kuzikimbia baadhi ya post(hoja) though unaweza kuwa na sababu inayokubalika kwamba "...huwezi kujibu kila post!" hata kama utakuwa unafanya hivyo kwa kusukumwa na jambo lingine!!!

Not really, huwa najibu watu ambao najua tunaweza kujadiliana nao kwa staha na heshima. Sijibu mtu yeyote ambaye for whatever reason hawezi kufanya majadiliano bila vijembe vya kitoto au mashindano ya kisiasa. Na wakati mwingine sijibu kwa sababu bado nafikiri jibu vizuri. Sipendi kujibu out of impulse.
 
Mpewe kama nani na kwanini? Rais halazimiki kutoa maelezo yake ya maamuzi yake. Tunaweza kudai ni vizuri tuambiwe lakini kama hakuna tatizo hadi hivi sasa tunachodai tunakidai kwa ajili gani hasa? Na vipi tutaridhika tukiambiwa sababu?

Mfano mzuri kwa kiasi ndio maana nimesema kama wanafikiri kuna sheria au sehemu ya Katiba imevunjwa; kuna namna moja tu ya kuresolve that; go to court! Kwanini kina Lissu au taasisi za wanasheria hawajaenda mahakamani "kudai" waambiwe kwanini Rais hajamthibitisha Ibrahim au hajateua mtu mwingine tusikie reasoning ya Serikali? Inawezekana hawajafanya hivyo kwa sababu wanajua ni kesi ambayo ngumu kushinda.

Hili wazo la probation ni fabrication ya fikra za watu tu. Amepewa kukaimu that's it; amekula kiapo cha kukaimu ndio hilo. Kama ni probation hakuna anayejua isipokuwa watu wamejiumbia wenyewe kwenye fikra zao. Tusije kutengeneza utaratibu kuwa kila Rais anapompa mtu nafasi ya kukaimu watu wakaanza kuona ni probation na kama hatothibitishwa basi waje kusema "hafai". Tusidai hilo kwa mtu mwenye weledi na caliber ya Prof. Ibrahim. Hatumtendei haki na kwa kweli hata mahakama yenyewe hatuitendei haki.

Hatakuwa tena RAis kama atakuwa analazimishwa. Na ukitaka njia nzuri badili katiba au sheria. Na njia sahihi ni kupata wabunge wengi wanaoweza kuunga mkono hoja hiyo. Haya ni matokeo ya demokrasia. lakini kutaka Rais alazimishwe tu ilimradi watu Fulani wasikie siyo sawa hata kidogo na sidhani kama nchi yeyote inaweza kuruhusu hilo. Si umeona hapa US wanavyohangaika kupata nakala za taarifa za kodi za Trump; kaam hataki kutoa hakuna namna ya kumlazimisha atoe. Ndio demokrasia. Tunapokataa udikteta wa mtu mmoja tusitengeneze na kukubali udikteta wa wengi - tyranny of the majority.
Mkuu Mzee Mwqnakijiji, much respect. Tuendelee kusubiria hii movie ya kukaimishwa itaishaje!. Asipomthibitisha hatutakubali!, tutakiwakisha!.

Japo kwa mfumo wa katiba yetu, imempa rais wetu mamlaka ya kiumungu mtu, Mwalimu Nyerere aliwahi kuwalaumu watawala kwa kuacha mazuri na kukumbatia mambo ya kijinga.

Kwa vile Magufuli wetu sio Mungu ni binadamu, then akina sisi tutaendelea kumueleza mawazo yetu, ayasikie au asiyasikie, haijalishi kazi yetu ni kusema tuu.
Na tutaendelea kusema tuu kwa sababu that is the only thing we are capable to do, and on my part kuanzia mwezi ujao nitakwenda one step further katika utekelezaji wa hoja yangu hii
2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom Bite", Tusiishie Kubweka Tuu, Tung'ate!.

Paskali
 
How? litakuwa na madhara gani? Na kama sheria au Katiba haijaweka kikomo hilo ni tatizo la nani hasa? Kwanini LIssu asije na hoja ya dharura ya kutaka mabadiliko ya sheria au kushawishi wabunge angalau 2/3 yao wafanye mabadiliko ya Katiba?
Mazingira yaliyopo bungeni kwa sasa unayajua. Kwa hiyo wewe kushauri kuwa Lissu angefanya nini (kushawishi wabunge 2/3,) ni kukwepa ukweli wa hali halisi iliopo.
 
Hili ndilo tatizo; sasa mimi nitajuaje sababu ya uhakika ya kwanini hili limefanyika. Kama unataka nikisie nitakuambia sababu moja ni kuwa Rais bado hajaona sababu ya kumthibitisha aliyepo ama hajapata mtu wa kuchukua nafasi hiyo. Ukiniuliza "kwanini" nitakuambia sijui ni Rais mwenyewe anajua. Na kwa vile hakuna sheria imevunjwa sina tatizo. Nasubiri tu amthibitisha Ibrahim au amteue mwingine. That is his prerogative. Nje ya hapo nitakuwa kwenye klabu ya wadhaniao.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwa hili uko right, kwa tunaomjua Prof. Juma, kumkaimisha this long ni kumdhalilisha, ndio maana sisi tunaomjua Juma na kuujua uadilifu wake, asipomthibitisha hatutakubali!.
Usiniulize tutafanya nini?!.
Tutakiwakisha!.

Paskali
 
Lissu had no authority whatsoever to demand that. As a matter of fact ndio maana Kabudi alijibu kwa kuonesha kuwa ni vizuri kuheshimu hiyo mihimili; kama vile wabunge wanataka waheshimiwe kwa sababu ni "mhimili" wao vile vile wanapaswa kuheshimu mhimili bila kujali nani anashikilia au anaongoza mhimile ule. Hiyo ndio ilikuwa essence ya majibu ya Prof. Kabudi as I understood them.
Mkuu hii si issue ya Lissu kama Lissu

Lissu aliwakilisha maoni ya ya upinzani. Alieleza kwa kirefu hoja yake kabla ya kutoa maoni.
Kambi ya upinzani haihitaji 'fadhila' inahitaji kusikika.

Kama tunadhani mihimili inahitaji kuheshimiana, mbona mawakili waliambiwa 'watiwe ndani'?

Kabudi aliongea akiwa perturbed , disarrayed and irrational hakuwa na majibu ya hoja

Alijibizana na wabunge,anaondoka kwenye mada na hakukuwa na ''red meat''

Ilikuwa embarrassment badala ya kujibu hoja za upinzani ya probation akalifanya jambo la Lissu
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwa hili uko right, kwa tunaomjua Prof. Juma, kumkaimisha this long ni kumdhalilisha, ndio maana sisi tunaomjua Juma na kuujua uadilifu wake, asipomthibitisha hatutakubali!.
Usiniulize tutafanya nini?!.
Tutakiwakisha!.

Paskali

Then badala ya kumtaka Rais amthibitishe au ateue mwingine ili huyu mnayemjua uadilifu wake asidhalilike Zaidi mnachotakiwa kufanya ni kumtaka huyu mtu kuonesha uadilifu wake kwa kuomba kujiuzulu nafasi hiyo ili Rais amteue mtu mwingine kukaimu au mtu wa kudumu. Hili la kujaribukumlazimisha Rais si sahihi hata kidogo. Kama Ibrahim ni mwadilifu - na naamini ni kweli na anaona anadhalilika - basi aombe ajiuzulu aendelee na ujaji wake. SIYO lazima kwake kuwa Kaimu Jaji Mkuu.
Sidhani kama ni lazima amthibitishe na nina uhakika asipomthibitisha hakuna lolote "mnaloweza" kufanya. None.
 
Mazingira yaliyopo bungeni kwa sasa unayajua. Kwa hiyo wewe kushauri kuwa Lissu angefanya nini (kushawishi wabunge 2/3,) ni kukwepa ukweli wa hali halisi iliopo.

Usidhani sijui mazingira ya Bungeni; najua ndio maana nimependekeza hivyo ili upinzani ufikirie namna gani nzuri Zaidi ya kukabiliana na hali ilivyo Bungeni. Mwisho wa siku tunaendelea na siasa zile zile za 2005 na wakati wote wa Kikwete.
 
Inasikitisha kuona jambo rahisi kaka hili watu wanalipigapiga chenga bila sababu za msingi kwa sababu ya ushabiki wa kisiasa. Maelezo ya TL mbona yako wazi sana? Kubwa sana na la muhimu ni la mihimili yote mitatu kuwepo wakati wote. Kudhoofisha muhimili mmoja ni kuharibu mipango ya kuendesha nchi.
 
Then badala ya kumtaka Rais amthibitishe au ateue mwingine ili huyu mnayemjua uadilifu wake asidhalilike Zaidi mnachotakiwa kufanya ni kumtaka huyu mtu kuonesha uadilifu wake kwa kuomba kujiuzulu nafasi hiyo ili Rais amteue mtu mwingine kukaimu au mtu wa kudumu. Hili la kujaribukumlazimisha Rais si sahihi hata kidogo. Kama Ibrahim ni mwadilifu - na naamini ni kweli na anaona anadhalilika - basi aombe ajiuzulu aendelee na ujaji wake. SIYO lazima kwake kuwa Kaimu Jaji Mkuu.
Sidhani kama ni lazima amthibitishe na nina uhakika asipomthibitisha hakuna lolote "mnaloweza" kufanya. None.
Hili la kumshauri ajiuzulu sikubaliani nalo kwa sababu atamthibitisha. Only if ikitokea asimthibitishe ndipo usubiri moto wake!. Hiyo ya kusema there is nothing we can do, usiendelee nayo kwa sababu don't underestimate the power of social media!. Usitudharau, we have a very big impact!.

Maxence kupitia JamiiForums, ametoa mchango mkubwa sana kwa taifa hili, Hastahili kukaa mahabusu

Mbona mimi ni gwiji katika hili na nguvu yake naijua labda kuliko wengi humu.
 
Hili ndilo tatizo; sasa mimi nitajuaje sababu ya uhakika ya kwanini hili limefanyika. Kama unataka nikisie nitakuambia sababu moja ni kuwa Rais bado hajaona sababu ya kumthibitisha aliyepo ama hajapata mtu wa kuchukua nafasi hiyo. Ukiniuliza "kwanini" nitakuambia sijui ni Rais mwenyewe anajua. Na kwa vile hakuna sheria imevunjwa sina tatizo. Nasubiri tu amthibitisha Ibrahim au amteue mwingine. That is his prerogative. Nje ya hapo nitakuwa kwenye klabu ya wadhaniao.
Haikuwa lazima iwe sababu anayoona yeye; hata ile unayoona wewe kama hiyo kwamba hajaona sababu ya kumthibitisha!

Kwanini hajaona sababu ay kumthibitisha?

Sababu ni ile ile niliyoisema hapo awali kwamba ana-take advantage ya mapungufu ya kikatiba kufanya vile anavyotaka yeye ili kuimarisha mfumo wake wa kiutawala!!!!

Lisilo na shaka hadi sasa ni kwamba, JPM huwa hataki mtu atofautiane nae bila kujali sababu za kutofautiana huko zina uhalali kiasi gani!!

Miezi kadhaa nyuma JPM alinukuliwa wazi wazi akimshangaa JK alipowaachia wana-CCM waliokuwa wanampinga wazi wazi wakati wa uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015!!! Bila kupepesa macho, JPM alieleza wazi angekuwa yeye asingewaacha watu hao!!!

Na kweli, alipoukwaa tu Uenyekiti wa CCM, hiyo ikawa ndio agenda yake ya kwanza as if tatizo kubwa la CCM ni what's so called "usaliti!"

Kwa JPM; yeye hapaswi kupingwa na anayempinga anapaswa kutiwa adabu instantly!!

That's one, but second, ni wiki chache tu zilizopita tumeona akimvua madaraka Nape Nnauye simply because Nape aliunda tume ya kumchunguza Makonda; Makonda ambae siku moja kabla JPM aliuelezea umma ni namna gani anamkubali na vile asivyopaswa kutishika na "kelele za watu!"

Kwahiyo suala la Nape kuunda Tume ya kumchunguza Makonda; kwa JPM hiyo ilikuwa ni kama anapingwa na ndio maana akamfukuza kazi mara moja... I know it, you know it and I know you agree with me hata kama hutakubali hadharani but deep inside your heart unafahamu ninachosema ni ukweli mtupu!!!

Si hivyo tu; ni juzi tu hapa JPM ameueleza umma kuhusu Lecturer wa UDOM anayedai alimtukana na hivyo kuagiza kufutwa kazi! Basing on above facts, na vile ambavyo mara kadhaa ameshaonesha wazi kwamba havumilii criticism basi kuna kila dalili huyo lecturer hakumtukana JPM bali inawezekana alitoa harsh criticism.

And our Supreme Dearest Leader, The President of the United Republic of Tanzania, Honorable Ayatollah Dr. John Joseph Pombe Magufuli hayupo tayari kwa hilo na ndio maana JPM akaagiza afutwe kazi mara moja!!!!

Yote hayo yanathibitisha jambo moja tu!! JPM anataka awe na control kwa kila mtu in his/her line of work but more importantly; control ya kuweza ku-hire and fire kila anapotaka kufanya hivyo!

Kinyume chake, wakati JPM ana nguvu ya kufanya hayo kwa mawaziri, ma-lecturer na watendaji wengine wa serikali; hana ubavu huo kwa majaji na CAG!!! Kwahiyo haishangazi hata punje kuona HATAKI kumthibitisha Kaimu Jaji Mkuu kuwa Jaji Mkuu kwa sababu anafahamu akishafanya hivyo control yake over him itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa sana!

So, the best way ni kuacha kumthibitisha ili akienda kinyume na yeye; anamuondoa mara moja na kumweka mwingine!!! Na sitashangaa hata kidogo, Assad nae akimaliza muda wake; nafasi yake ikachukuliwa na Kaimu CAG!!!

Na athari ya hayo tushayaeleza sana na haina sababu ya kurudia rudia lakini itoshe tu kusema kwamba, walioweka hizo sheria sio kwamba nao hawakutaka kuwa na control na viumbe wooooooooote; la hasha lakini walifanya hayo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa na sio matakwa ya mtu mmoja hata kama yeye ndio head of stateC!

Najua unajua kwamba ninachosema ni ukweli mtupu usio na haja ya kupelekwa maabara!! Na haijalishi kama utaukubali ukweli huo hadharani au hapana but deep inside your heart; you know kwamba nasema ukweli!! Sina shaka na hilo cuz' I also know you're good in judgement!!!!

Huna sababu ya kupayuka; naweza kusoma vizuri tu.
NIlikuambia usituambie masuala ya katiba kwa sababu ndio hoja ambayo umekuwa ukijificha nayo!!
Sasa kama havunji tatizo liko wapi; kama tatizo ni la kisheria njia ni kufix it kwa kutumia taratibu za kibunge za kushughulikia mapungufu ya kisheria au hata Kikatiba.
Tatizo nimeshataja kwenye posts za nyuma na kugusia hapa...!!! Na hilo suala la ku-fix nimeshasema sio busara hata kidogo kwa kiongozi kutumia mapungufu ya kikatiba hata kama yanampa mwanya huo!!! Kwahiyo badala ya kuhangaika kwanini hayo mapungufu yasiwe fixed jambo ambalo ni mlolongo; busara (leadership wisdom) ya kwanza ni kutojaribu kutumia mapungufu hayo!!!

Hili linawezekana lakini ndio mazao ya demokrasia na sheria. Kile ambacho sheria haikatazi, sheria inaruhusu. Na mtu hawezi kuadhibiwa kwa kitu ambacho si kosa kisheria.
I know you're smart enough kufahamu nini maana ya ku-take advantage!!

Hapa tunaweza kuilezea idiom ya "end justifies the means" in other way round!!!!

Si wakati wote ku-take advantage linakuwa ni jambo jema and in most cases, inakuwa si kwa sababu ya jambo jema! But anyway, what matters is "the end" of why capitalizing a named advantage!

Kama una-take advantage kwa maslahi ya umma, then it's okay na hapo utakua una-capitalize mapungufu ya kikatiba kwa maslahi ya umma!!!

Lakini kwa hili JPM hafanyi kwa maslahi ya umma bali kwa kutaka kui-package ego yake ya kuwa na control kwa kila mtendaji... ili hata akitofautiana nae kwa mambo yasiyo na tija; basi amtimue hapo hapo!!! Matokeo yake ndo yale ambayo tumeshayasema hapo juu!!
 
Then badala ya kumtaka Rais amthibitishe au ateue mwingine ili huyu mnayemjua uadilifu wake asidhalilike Zaidi mnachotakiwa kufanya ni kumtaka huyu mtu kuonesha uadilifu wake kwa kuomba kujiuzulu nafasi hiyo ili Rais amteue mtu mwingine kukaimu au mtu wa kudumu. Hili la kujaribukumlazimisha Rais si sahihi hata kidogo. Kama Ibrahim ni mwadilifu - na naamini ni kweli na anaona anadhalilika - basi aombe ajiuzulu aendelee na ujaji wake. SIYO lazima kwake kuwa Kaimu Jaji Mkuu.
Sidhani kama ni lazima amthibitishe na nina uhakika asipomthibitisha hakuna lolote "mnaloweza" kufanya. None.
Mkubwa wenzangu , kwanza nikuulize swali nje ya mada.
Ile Binocular yako umeweka wapi au umemwazima nani?

Pili, hakuna anayemlazimisha Rais, wapo wanaoonyesha 'genuine concern' zao kwa hali iliyopo

Kujiuzulu au kutojiuzlu kwa Prof Ibrahimu hakujibu concern zilizopo, pengine kutachochoea

Rais hupelekewa Majina na miongoni huteua mmoja. Paschal sidhani kama anaweza kufanya lolote ingawa hoja yake hatuwezi kuidharau kirahisi, hata hivyo kudharau jicho la jamii lililotengenezwa na macho tofauti ni hatari sana

Afadhali wanaoonyesha concern hata kama ni wapuuzi, kuliko wenye 'reservations' tusizozijua.
 
Then badala ya kumtaka Rais amthibitishe au ateue mwingine.... Hili la kujaribu kumlazimisha Rais si sahihi hata kidogo.
Sidhani kama ni lazima amthibitishe na nina uhakika asipomthibitisha hakuna lolote "mnaloweza" kufanya. None.
Mkuu umetumia maneno kumtaka, kumlazimisha Rais mara nyingi sana katika mjadala huu. Ninaswali moja kwako, kwani katika utawalu huu Rais 'hajalamishwa au kutakiwa' na akafanya?
 
Back
Top Bottom