Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Huwezi kuishi kwa kudhania tu; kwani ni kitu gani kinaweza kumzuia Jaji Mkuu kufanya mambo kwa kutaka kuridhisha mhimili wa Urais?
mkuu leo umenishangaza kidogo, unaongelea nadharia tu na si hali halisi, hata siku moja huwezi kumfananisha dereva wa gari na dereva deiwaka aliyepewa kupiga route wakati mwenye gari yake anapata lunch.
 
Hoja ya lissu mbona iko wazi kabisa...hajasema kuwa rais amekosea..anachosema lissu ni kuwa sheria zetu/katiba hazijaweka limit ya kuwa na acting chief Justice

Kitu ambacho kinaweza kuwa na madhara...hivi hebu chukulia kwa mfano rais aendelee kuwa na kaimu jaji hadi mwaka 2020.....hili jambo lin athari katika utendaji wa jaji

Kwa bahati mbaya Watu wengi huwa hamumuelewi Lisu kwa kipindi hicho anaongea...mnakuja kumuelewa baada ya miezi kadhaa au miaka kadhaa kupita
Watu wengi(hasa wanazi wa ccm) huwa hawamwelewi, na hawataki kumwelewa Lisu kwa sababu ya kasumba na mtazamo hasi waliojengewa na mfumo wa chama.. Na hata ikitokea wamemwelewa, kile alichosema watakipotosha makusudi ili uma usitilie maanani. Hizo ndiyo siasa zetu za kinafiki tunazoimarisha.
 
Huyo ndie kiboko cha yule jamaa mwanasheria/mmiliki wa lile gazeti la pale Mango,enzi hizo akiwa katibu mkuu wa vijana wa afrika alipoambiwa bwana ee hebu mpishe Kabudi jamaa alianza zengwe lakini hatimae akakubali yaishe.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Haya mambo ya bungeni mnayasikia wapi wakati malaika mkuu alikataza bunge lisiwe mubashara??? Acheni viherehere ili aangalie yeye na Bashite tu

Halafu wewe Mwanakijiji unazeeka vibaya sana, sheria unaijua au unafikiri ni kama hadithi unazotunga???


Bunge kama limerudi live tujulishwe.

Wengine tutaangalia El Classico na Manchester Derby, London Derby mpaka malaika mkuu atoweke nchi ya Tanzagiza

Hata siku 'wakifa' na kuwa live wakati wa maziko mi nitakuwa busy na EPL
 
Kwa kweli hakukuwa na darasa lolote. Binafsi sijaona jambo jipya ambalo Prof Kabudi alilisema ambalo hao "wanafunzi" wake walikuwa hawalijui. Kama alikuwa amekusudia kujibu hoja za Mh Lissu, pia sikusikia hoja zikijibiwa zaidi ya mipasho na majigambo tu. Ukishaona mtu ana demand aheshimiwe (kwa umri wake?), ujue tayari lipo tatizo. Ukweli na hoja zinapaswa kusimama zenyewe bila kuangalia anayezitoa.
Kwa fikra zako zilizofungwa na lissu usingeweza elewa na hutakaa uelewe.
 
How? litakuwa na madhara gani? Na kama sheria au Katiba haijaweka kikomo hilo ni tatizo la nani hasa? Kwanini LIssu asije na hoja ya dharura ya kutaka mabadiliko ya sheria au kushawishi wabunge angalau 2/3 yao wafanye mabadiliko ya Katiba?
Ndiyo maana ameliwasilisha kama changamoto kwa wadhifa wake. Kama linahitaji kuwasilishwa kwa hoja ya dharula anaweza kufanya yeyote si lazima Lisu, hasa baada ya kuwa limeonekana sasa kuwa changamoto
 
Unajua kitu!!!!!! ????ni kwamba hoja iliyobaki kwa wapinzani hasa chadema ni kimsingizia rais kuwa anavunja katiba ya nchi !! Only that!!! Na kwa sababu wanajua Wa Tanzania wengi siyo wasomi na wengi ni wavivu Wa kufikiri wanajua 2020 watakuja na hoja hiyo potofu kwa wananchi hasa vijana wasiyotumia akili kufikiri na waloyoshiba mahaba feki !!!Kusema kweli kwa sasa hawana hoja na siyo threat kwa Serikali au chama tawala!!! Na hii inatimiza utabili Wa Dr Slaa kuwa upinzani usipotafuta hoja nyengine utakufa!!! This is now happening slowly!!! Huwezi pata popularity kwa kimsingixia rais
Hayo ni mawazo ya mwaka 47. Dunia haikusubiri. Hoja hii ilivyojadiliwa tangu mwanzo, ni wewe pekee, labda na Barbarossa mnaleta mawazo mgando. Hapa linajadiliwa jambo la msingi kwa faida ya nchi, unakuja na uharo?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimesikiliza kwa makini kile kinachoitwa "darasa" la Prof. Kabudi jana Bungeni kuhusiana na suala la Kaimu Jaji Mkuu na hasa hoja nzima ya kukaimiwa kwa nafasi ya Jaji Mkuu. Inasikitisha kwanza kwamba kuna watu wanasifia kuwa ametoa "darasa" na kwamba watu walikuwa wanamsikiliza kama wanafunzi katika Shule ya Msingi Mtakuja!

Je, ni kweli kile alichokisema watu walikuwa hawakijui? Ni kweli wabunge na wanasheria walioko Bungeni walikuwa hawajui yale yaliyokuwa yanasemwa?

Kuna hoja ya kuuliza swali; kwamba - kwanini Rais amemteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu kwa muda wote huu. Swali ambalo halipaswi kuulizwa na tulilikataa wakati ule ni kuhusu mamlaka ya Rais kumteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu. Hili liko ndani ya mamlaka ya Rais (Presidential prerogative). Lakini pia swali hili kwa ukubwa wake halipaswi kuulizwa isipokuwa kisiasa (political question) ili watu kupata hoja za kisiasa au ujiko wa kisiasa. Kwamba, mtu anataka kuonesha kuwa Magufuli amekosa mtu wa kuwa jaji mkuu, au kwamba Magufuli ana tatizo na mahakama n.k. Hili si jambo sahihi; wabunge kama wanaona Rais anatumia muda mrefu kujaza nafasi ya jaji mkuu wana uwezo wa kubadilisha sharia na hata Katiba chini ya Ibara ya 100 ya Katiba yetu.

Kama wanataka nafasi ya Jaji Mkuu isikaimiwe indefinitely (kama hoja ya Lissu ilivyoashiria) namna pekee ni kubadilisha Katiba au sheria ili kuweka kikomo kama ilivyo katika baadhi ya nafasi za utumishi wa umma ambapo sheria inasema mtu atakaimu nafasi kwa muda fulani na baada ya hapo basi mtu wa kudumu ateuliwe au aliyekaimu athibitishwe. Wao wabunge (watunga sheria na wanaoweza kufanya mabadiliko ya Katiba) wanaweza kuweka kikomo labda kwa ajili ya mustakabali)

Kama kwa mfano Rais angejaza cheo cha Ujaji siku moja tu baada ya Jaji Othman kustaafu wapo ambao labda wangeweza kuja na hoja ya kwanini amejaza nafasi haraka bila kuonesha tafakari sana au klutumia muda kufanya utafiti wa kutosha! Lakini pia kuna swali ambalo inabidi liulizwe kwa wale wanaolalamikia - kwa Rais kuweka Kaimu Jaji Mkuu ni shughuli gani ya Mahakama Kuu ambayo haiwezi kufanyika sasa hivi kwa vile kuna kaimu Jaji Mkuu au ni kitu gani hakifanyiki katika mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambacho kinapaswa kufanywa na jaji mkuu peke yake. Hili ndilo linaweza kuwa hoja ya kwanini inahitajika Jaji Mkuu na siyo Kaimu Jaji Mkuu?

Lakini kung'ang'ania kitu ambacho wote wanajua hakipo - kwamba Rais hajavunja sheria wala Katiba, na kuwa hakuna kikomo cha muda kilichowekwa kwa hoja ya kuwa ni mazoea mapya haitoshi kuwa hoja.

Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la. Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Urais wakati Rais hayupo kwa mujibu wa sharia ana madara yote ambayo ameruhusiwa kuwa nayo kwa mujibu wa Katiba. Na hili ni kweli kwa mtu mwingine yeyote ambaye Rais anaweza kumpa nafasi ya kukaimu jambo lolote kwa niaba yake. Mtu yeyote professional hajali sana kama atamfurahisha mtu au la atafanya kwa mujibu wa madaraka aliyopewa. Mtu ambaye atajali kuwa akifanya jambo Fulani atamuudhi aliyemteua au chombo cha juu hafasi kushika nafasi hiyo.

Somo ambalo Kabudi angepaswa kulitoa na labda wengi wanalihitaji kulielewa ni hili la Presidential prerogatives..

Hii mada ina upande mwingine wa shilingi. Management ya watumishi (Jaji Mkuu ni mtumishi wa umma) ni fani ya kitaalamu yenye kanuni na taratibu zake. Mtumishi anapaswa kutimiza wajibu wake katika mazingira yatakayofanya utendaji wake uwe bora to the maximum ili kutimiza kikamilifu malengo ya nafasi yake. Mtumishi hawezi kamwe kutimisa azima hii katika mazingira ya kukaimu nafasi aliyo nayo. Hii ni kanuni na hili halina ubishi. Kuna tofauti kubwa sana kiutendaji kati ya afisa anayekaimu cheo na aliyethibitishwa kwenye hicho cheo. Hii bila shaka ilikuwa ndio concern ya Tundu Lissu kama mdau wa mfumo wa utoaji haki nchini.

Labda kitu kinachohitaji tafakuri pana hapa na ambacho kitalazimu kuingia kwenye viatu vya Rais Magufuli ili kuwa katika nafasi ya ku-hypothesize: je, ni kwa nini rais hakuteua Jaji Mkuu kamili na badala yake akateua kaimu? Hapa haitarajiwi hoja nyepesi na ya kisiasa kama, "rais alifanya hivyo kwa sababu ana mamlaka hayo"! Presidential prerogative just for the sake it?
 
Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la.[/QUOTE]
Kinadharia ni sawa lakini kiuhalisia KAIMU JAJI MKUU ni KAIMU JAJI MKUU na ndio maana haitwi JAJI MKUU. Ni wazi saa yeyote RAISI anaweza kumchagua JAJI MKUU na wewe KAIMU utang'oka. Kwa muungwana yeyote ukweli huu utamfanya afanye kazi kwa "tahadhari" hasa kama ana tegemeo la kuthibitishwa au kuchaguliwa. Mtizamo huu haumpi uhuru ambao kisheria na kinadharia anao. Kwa hiyo wasi wasi wa Lisu ni wa msingi achilia mbali ufafanuzi wa Kabudi. Na kwa kiongozi wa haiba ya JPM inabidi uwe "mwangalifu" mara mbili zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lisu anacheza na uzuzu wa watz kwamba hatujui sheria na haki zetu ila kimsingi huwezi kumwita mwanasheria bingwa kwakuwa hata sio mwepesi wa kusite vifungu wala katiba .. anatumia personal instincts to justify mambo.. plus anafanya siasa/mwanaharakati zaidi kuliko sheria.
Najua kuna wanasheria kibao TZ Lisu hawafikii ila sio watu wa kiki/media na sio politicians.. kuna vipanga wa Havard hapo TZ kibao.
Mkuu umetoa point za kipumbavu mno... Pls go back to school. Au ni chuki binafsi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Na hili la kuwa na Kaimu Jaji Mkuu limefanywa kwa makusudi kabisa ili kurahisisha upindishaji wa sheria za nchi kama ambavyo tumekwishaona kwenye matukio mbali mbali nchini. Huyu hawezi kunyanyua sauti yake kukemea ukiukwaji wa katiba nchini n.k. kwa kuhofia kutumbuliwa. Ataendelea kuangalia pembeni huku sheria mbali mbali za nchi zikiukwa ikiwemo katiba ili kitumbua chake kisiingie mchanga.

Kinadharia ni sawa lakini kiuhalisia KAIMU JAJI MKUU ni KAIMU JAJI MKUU na ndio maana haitwi JAJI MKUU. Ni wazi saa yeyote RAISI anaweza kumchagua JAJI MKUU na wewe KAIMU utang'oka. Kwa muungwana yeyote ukweli huu utamfanya afanye kazi kwa "tahadhari" hasa kama ana tegemeo la kuthibitishwa au kuchaguliwa. Mtizamo huu haumpi uhuru ambao kisheria na kinadharia anao. Kwa hiyo wasi wasi wa Lisu ni wa msingi achilia mbali ufafanuzi wa Kabudi. Na kwa kiongozi wa haiba ya JPM inabidi uwe "mwangalifu" mara mbili zaidi.
 
Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala.
Sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji, hapo umekosea sana kama alivyokosea anayedaiwa kutoa somo bungeni...sijui ni kwa sababu gani umeamua kutosema ukweli lakini yeye naamini alifanya hivyo makusudi kwani alijua uwezo na uelewa wa walio wengi huko bungeni wa kupiga makofi bila kuhoji.
Unapokaimu nafasi unakuwa na madaraka yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la.
Hapana Mzee Mwanakijiji, kuna kitu kinaitwa "security of tenure" ambayo anayekaimu ofisi kama ya Jaji Mkuu hana. Prof. Kabudi akitoa kinachoitwa somo kwa watu wenye uelewa mdogo, alijua fika jambo hili lakini akaamua kuwa mnafiki kwa ama ukaribu wake na aliyemteua au kwa kulinda maslahi binafsi.

Security of tenure: Without security of tenure, an office-holder may find his or her ability to carry out their powers, functions and duties restricted by the fear that whoever disapprove of any of their decisions may be able to easily remove them from office in revenge. Security of tenure offers protection, by ensuring that an office-holder cannot be victimised for exercising their powers, functions and duties. It enables the democratic or constitutional methodology through which an office-holder comes to office not to be overturned except in the strictest and most extreme cases.

Ni wazi Rais hajavunja sheria ila kwa ujanja ujanja hataki kujaza nafasi hiyo ama anavuta subira hadi ampate mtu wake muafaka kwake (yes man) au ana hofu ya kumpata mtu mwenye msimamo asiyeyumbishwa hovyo.

Mh. Tundu Antiphas Lissu anaona mbali na ndio maana Prof. Kabudi alikwepa kujibu hoja zake na kuishia kuzungukazunguka kwa majigambo.
 
Mkuu umetoa point za kipumbavu mno... Pls go back to school. Au ni chuki binafsi?
Tatizo la kuabudu mtu.. anayesema against Lisu ama yeyote wa chandema ni mpumbavu.. very irrational
labda sis wote ni wapumbavu ama wewe pumbavu zaidi.. sina factor ya kuku qualify you kwa chochote.. so just kiss ya own assho
 
Hivi kaimu Jaji Mkuu akisafiri nje ya nchi watateuza kaimu mwingine kukaimu nafasi ya kaimu Jaji Mkuu?

Halafu kuna nyakati huwa tunasahahu kuwa hawa kina Lissu ni wawakilishi tu. Sitashangaa kusikia kuwa hoja ya Lissu kuhusu CJ na katiba inatokana na watu wazito tu huko kwenye judiciary! Sio rahisi kwa majaji au hata wabunge wa CCM kuraise concerns zao moja kwa moja hasa kama hizo ambazo zinamuhusu bosi wao na kwa hivyo the logical and easier route ni "kuwatumia" wapinzani.

Mbona Katiba iko wazi juu ya hili? kuna hoja ya seniority ya majaji ambao inapolazmu wanaweza kuchukua nafasi kwa muda ya kuwa kaimu.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom