Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Tundu lisu amekutana na gwiji. Hata mmutee vipi anapwaya alikuwa anapewa kiki na wasiojua sheria. Sasa kaja mwenyewe. Ila nilikuwa nasikia siku nyingi sana kuwa tundu lieu hajui sheria Bali ni mwanaharakati tu Wa sheria na mpayukaji pasipo kujua lolote ndo mana kabudi kasema mwanasheria yeyote anapaswa kuwa na busara siyo kila kitu kinatatuliwa na sheria bali jamii nabethics sake.
Too early to comment
 
Huwezi kuishi kwa kudhania tu; kwani ni kitu gani kinaweza kumzuia Jaji Mkuu kufanya mambo kwa kutaka kuridhisha mhimili wa Urais?
Hakuna suala la kudhania hapa kwa sababu, uzoefu umeonesha wazi watu katika kulinda madaraka yao wapo tayari hata kuyapinga yale ambayo waliyaamini na kuyasimamia kwa miaka kadhaa!!!

Humphrey Pole Pole wakati akiwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; alipiga kelele sana kuhusu nafasi ya Ukuu wa Wilaya to the point hakuna ambae alidhania ingetokea siku Pole pole angekuja kukubali nafasi ya u-DC kwa bashasha!!

Kitila Mkumbo, wakati akiwa Mshauri wa ACT Wazalendo na Mhadhiri wa DUCE, alimkosoa JPM kwa tabia yake ya kufanya uteuzi zake kwa Wahadhiri wa Vyuo kwa kile alichodai hatua hiyo ya JPM inapunguza nguvu kazi ya watoa taaluma vyuo vikuu!!!

Siku JPM alipomteua Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu; watu tulimtarajia angeikana nafasi hiyo kwa sababu ilikuwa inapunguza nguvu kazi ya watoa taaluma lakini kinyume chake, Mkumbo nae alifurahia kweli kweli uteuzi huo!!!

Dk. Harrison Mwakyembe kila mmoja alimshuhudia alivyokuwa anayakana maandiko yake mwenyewe wakati wa kikao cha Bunge la Katiba!!! Mwakyembe aliliazimika kuyakana maandiko yake kwa sababu tu ya kulinda uwaziri wake!!!!

Siku anateuliwa Profesa Kabudi niliwaambia watu tusubiri viroja vya msomi mwingine atakavyokuwa anayakana yake aliyokuwa anayasimia! And for real, it's just a matter of time na Kabudi nae ataingia kundi hilo hapo juu!!!

Mifano ipo mingi ambayo yote hiyo inathibitisha jambo moja tu: HAKUNA SUALA LA KUDHANIA hapa bali ndio uhalisia wenyewe unless kama huyo Kaimu Jaji Mkuu ni very exceptional!!!

Sasa, Kaimu Jaji Mkuu nae haitashangaza hata kidogo kuona anachotamani yeye sio kubakia kuwa Kaimu Jaji Mkuu bali kuwa Jaji Mkuu kabisa!! I hate to say this, lakini uzoefu umeshaonesha JPM hayupo tayari kufanya kazi na mtu anayezingua kwa sababu yoyote ile!!!! Hata pasipo na sababu za maana, atakuondoa!!!

Kama ndivyo, kwanini basi nae Kaimu Jaji Mkuu asiwe very cautious na utendaji wake ambao bila shaka anaota siku moja awe Jaji Mkuu kabissa badala ya kukaimu nafasi hiyo?!
 
How? litakuwa na madhara gani? Na kama sheria au Katiba haijaweka kikomo hilo ni tatizo la nani hasa? Kwanini LIssu asije na hoja ya dharura ya kutaka mabadiliko ya sheria au kushawishi wabunge angalau 2/3 yao wafanye mabadiliko ya Katiba?

Mwanakijiji unanisikitisha saana kwakifupi huna jpya siku hizi bora ukae kimya tu, sjui unazeeka maana hujengi hoja za maana kama zamani hata sijui umekutana na masahibu gani. pole sana mzee kidogo uwe role model wangu ila nimekustukia upo ki maslahi zaidi.
 
Kuna mtu ka cooment kuwa kaimu jaji anaweza kuwa legevu kwa aliemteua kwa kuwa anakosa kinga za jai mkuu kamili!
Tuanzie hapa: Kazi za Kaimu Jaji ni zipi na za Jaji Mkuu ni zipi ambazo zinaingilia utendaji wa aliemteua?
 
Tundu lisu amekutana na gwiji. Hata mmutee vipi anapwaya alikuwa anapewa kiki na wasiojua sheria. Sasa kaja mwenyewe. Ila nilikuwa nasikia siku nyingi sana kuwa tundu lieu hajui sheria Bali ni mwanaharakati tu Wa sheria na mpayukaji pasipo kujua lolote ndo mana kabudi kasema mwanasheria yeyote anapaswa kuwa na busara siyo kila kitu kinatatuliwa na sheria bali jamii nabethics sake.
Kabudi hajawahi shinda kesi mahakamani, hamna kitu pale practice ni zero
 
Mwanakijiji unanisikitisha saana kwakifupi huna jpya siku hizi bora ukae kimya tu, sjui unazeeka maana hujengi hoja za maana kama zamani hata sijui umekutana na masahibu gani. pole sana mzee kidogo uwe role model wangu ila nimekustukia upo ki maslahi zaidi.
Lete hoja ya kujibu hoja yake. Mimi huwa na mchalula kwa hoja ili kumrejesha kwenye msitari. Ila kwa staili yako hii sidhani kama mtaelewana.
 
Hakuna suala la kudhania hapa kwa sababu, uzoefu umeonesha wazi watu katika kulinda madaraka yao wapo tayari hata kuyapinga yale ambayo waliyaamini kwa miaka kadhaa!!!

Humphrey Pole Pole wakati akiwa kama Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; alipiga kelele sana kuhusu nafasi ya Ukuu wa Wilaya to the point hakuna ambae alidhania ingetokea siku Pole pole angekuja kukubali nafasi ya u-DC!!

Kitila Mkumbo, wakati akiwa Mshauri wa ACT Wazalendo na Mhadhiri wa DUCE, alimkosa JPM kwa tabia yake ya kufanya uteuzi zake kwa Wahadhiri wa Vyuo kwa kile alichodai hatua hiyo ya JPM inapunguza nguvu kazi ya utoaji taaluma!!!

Siku JPM alipomteua Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu; watu tulimtarajia angeikana nafasi hiyo kwa sababu ilikuwa inapunguza nguvu kazi ya watoa taaluma lakini kinyume chake, Mkumbo alifurahia kweli kweli uteuzi huo!!!

Dk. Harrison Mwakyembe kila mmoja alimshuhudia alivyokuwa anayakana maandiko yake mwenyewe wakati wa kikao cha Bunge la Katiba!!! Mwakyembe aliliazimika kuyakana maandiko yake kwa sababu tu ya kulinda uwaziri wake!!!!

Siku anateuliwa Profesa Kabudi niliwaambia watu tusubiri viroja vya msomi mwingine atakavyokuwa anayakana yake aliyokuwa anayasimia! And for real, it's just a matter of time na Kabudi nae ataingia kundi hilo hapo juu!!!

Mifano ipo mingi ambayo yote hiyo inathibitisha jambo moja tu: HAKUNA SUALA LA KUDHANIA hapa bali ndio uhalisia wenyewe unless kama huyo Kaimu Jaji Mkuu ni very exceptional!!!

Sasa, Kaimu Jaji Mkuu nae haitashangaza hata kidogo kuona anachotamani yeye sio kubakia kuwa Kaimu Jaji Mkuu bali kuwa Jaji Mkuu kabisa!! I hate to say this, lakini uzoefu umeshaonesha JPM hayupo tayari kufanya kazi na mtu anayezingua kwa sababu yoyote ile!!!! Hata pasipo na sababu za maana, atakuondoa!!!

Kama ndivyo, kwanini basi nae Kaimu Jaji Mkuu asiwe very cautious na utendaji wake ambao bila shaka anaota siku moja awe Jaji Mkuu kabissa badala ya kukaimu nafasi hiyo?!

una hoja zenye mashiko kuliko za mzee mwanakijiji. upo sahihi comrade tumezungukwa na wasaliti wengi na kuna uwezekano hata huyu mzee tuliempenda sana kwa tafakuri zake kipindi cha JK nae anasubiri kupewa kitengo aufyate kama akina kitila na polepole.

Shame on them
 
Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la. Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Urais wakati Rais hayupo kwa mujibu wa sharia ana madara yote ambayo ameruhusiwa kuwa nayo kwa mujibu wa Katiba. Na hili ni kweli kwa mtu mwingine yeyote ambaye Rais anaweza kumpa nafasi ya kukaimu jambo lolote kwa niaba yake. Mtu yeyote professional hajali sana kama atamfurahisha mtu au la atafanya kwa mujibu wa madaraka aliyopewa. Mtu ambaye atajali kuwa akifanya jambo Fulani atamuudhi aliyemteua au chombo cha juu hafasi kushika nafasi hiyo.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwenye issue ya kukaimu, sorry you've missed the point.

Sheria yoyote inapotungwa na Bunge inanakuwa na madhumuni fulani. Lengo la kifungu cha mamlaka ya rais kuteua Kaimu Jaji kilidhamiria Kaimu Jaji Mkuu atateuliwa pale tuu Jaji Mkuu yupo lakini yuko nje ya nchi, ama ana maradhi yaliyopelekea kushindwa kutimiza majukumu yake, hivyo anateuliwa Kaimu as a temporary measures, Jaji Mkuu akirudi au akipona anaendelea na majukumu yake.

Lakini Jaji Mkuu anapomaliza muda wake wa utumishi wa umma, 6 months before notification hutumwa na rais kupelekewa majina matatu to choose from.

Huu Uteuzi wa Prof. Juma kama Kaimu Jaji Mkuu wakati nafasi ya Jaji Mkuu iko wazi permanently is not right!. It is as if Dr.Juma is not trusted hivyo yuko under probation kama atafiti ndipo ateuliwe na asipofiti anateuliwa mtu mwingine!. Hii ni very demoralising na Dr.Juma hawezi kuwa na confidence ya ku exercise all his powers kwa sababu kuna vitu Kaimu Jaji hawezi kufanya ikiwemo kukaimu nafasi ya Urais!.

Ukaimu huu sio sawa na ule Ukaimu wa mtu kukaimu nafasi fulani temporary mwenyewe akirudi unapisha. Huku ni kukaimu wakati nafasi haina mwenyewe!.

Kingine ambacho Mwanakijiji hakijui, hajui kuwa kaimu hata kaimu rais, hawezi kusaini amri yeyote ambaye inapaswa kusainiwa na rais ikiwemo kusaini sheria, kutangaza hali ya hatari, kuteua wala Kaimu rais haruhusiwi kusaini Presidential Preventative Detention Order!.

Enzi za Nyerere kuna siku Ali Hassan Mwinyi alikaimu na akasaini hati ya kizuizini, aliyetiwa kizuizini alishitaki Mahakama Kuu, amri ile ikapigwa chini kwa sababu Kaimu rais ni kaimu na sio rais, ukaimu unaishia kwenye kutoa maagizo na sio kusaini jambo lolote linalohitaji saini ya rais!.

Mfano Bunge likitaka kufanya impeachment process Kaimu Jaji Mkuu hawezi kwa sababu aliielezwa kwenye sheria ni Jaji Mkuu.

Taratibu ni kama sheria. Kama hutajawahi kuwa na Kaimu Jaji Mkuu muda wote huu, why now?!.

Paskali
 
Lete hoja ya kujibu hoja yake. Mimi huwa na mchalula kwa hoja ili kumrejesha kwenye msitari. Ila kwa staili yako hii sidhani kama mtaelewana.

Huyu mzee kaishapotea haina haja ya kujibishana nae namhurumia busara zote sijui kazitupa wapi? sijui kakumbwa na nini, yaani kila nikitafakari maandishi yake naona kuna ka unafiki fulani hivi kamejificha
 
Hoja ya lissu mbona iko wazi kabisa...hajasema kuwa rais amekosea..anachosema lissu ni kuwa sheria zetu/katiba hazijaweka limit ya kuwa na acting chief Justice

Kitu ambacho kinaweza kuwa na madhara...hivi hebu chukulia kwa mfano rais aendelee kuwa na kaimu jaji hadi mwaka 2020.....hili jambo lin athari katika utendaji wa jaji

Kwa bahati mbaya Watu wengi huwa hamumuelewi Lisu kwa kipindi hicho anaongea...mnakuja kumuelewa baada ya miezi kadhaa au miaka kadhaa kupita
Lisu haelewekagi bwana kwanza anajifanya anajua kuliko wote alafu anaboa
 
Hoja ya lissu mbona iko wazi kabisa...hajasema kuwa rais amekosea..anachosema lissu ni kuwa sheria zetu/katiba hazijaweka limit ya kuwa na acting chief Justice

Kitu ambacho kinaweza kuwa na madhara...hivi hebu chukulia kwa mfano rais aendelee kuwa na kaimu jaji hadi mwaka 2020.....hili jambo lin athari katika utendaji wa jaji

Kwa bahati mbaya Watu wengi huwa hamumuelewi Lisu kwa kipindi hicho anaongea...mnakuja kumuelewa baada ya miezi kadhaa au miaka kadhaa kupita
mkuu umemsoma Lissu au umeandika tu?

YA KAIMU JAJI MKUU

Mheshimiwa Spika,
Mahakama ya Tanzania haina kiongozi wake kamili, yaani Jaji Mkuu. Hii ni kwa sababu, tangu Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman astaafu tarehe Mosi Januari ya mwaka huu, Rais John Pombe Magufuli hajateua Jaji Mkuu mpya kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu Chande Othman. Badala yake, Rais Magufuli amemteua Jaji wa Rufaa Prof. Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu.

Mheshimiwa Spika,
Ibara ya 118(4) ya Katiba yetu, Rais anaruhusiwa kuteua Kaimu JAji Mkuu iwapo itatokea kiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi; au Jaji Mkuu hayupo Tanzania; na au Jaji Mkuu atashindwa kutekeleza kazi yake kwa sababu yoyote, na Rais ataona kuwa kwa muda wa tukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua Kaimu Jaji Mkuu. Kaimu Jaji Mkuu aliyeteuliwa kwa utaratibu huu “... atatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpaka atakapoteuliwa Jaji Mkuu mwingine....”

Mheshimiwa Spika,
Pamoja na kuwapo kwa ibara ya 118(4), Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inaamini kwamba Rais Magufuli anavunja Katiba ya nchi yetu kwa kushindwa kuteua Jaji Mkuu kamili takriban miezi mitano tangu kustaafu kwa Jaji Mkuu Chande Othman. Hii ni kwa sababu, ibara ya 118(4) haikutungwa kwa lengo la kumwezesha Rais kuteua Kaimu Jaji Mkuu bila kikomo cha muda.

Kama ilivyo kwa sheria zote, ibara ya 118(4) ina sababu yake maalum. Ibara hiyo imewekwa kwa makusudi ya kuhakikisha kwamba kwa muda wote kunakuwa na kiongozi wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania pamoja na kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, wakati Jaji Mkuu kamili anasubiriwa kuteuliwa. Kaimu Jaji Mkuu ni sawa ni kile kinachoitwa na wanasheria ‘interlocutory position.’ Kaimu Jaji Mkuu ni nafasi ya muda inayoshikiliwa na mtu mwenye sifa za kuwa Jaji Mkuu kabla nafasi hiyo haijajazwa na Jaji Mkuu kamili.

Swali halali linahitaji majibu ni, je, Kaimu Jaji Mkuu anastahili kuwapo madarakani kwa muda gani? Hili ni suala la tafsiri ya Katiba linalohitaji kujibiwa na Mahakama. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, miezi mitano ni muda mrefu mno wa kuwa na Kaimu Jaji Mkuu.

Mheshimiwa Spika,
Bunge lako tukufu, kama mmojawapo wa mihimili mikuu ya dola ya Tanzania, lina kiongozi wake mkuu muda wote: Spika au Naibu Spika. Serikali, kama mhimili mwingine mkuu, ina kiongozi wake mkuu muda wote: Rais au Makamu wa Rais. Kwa Mahakama ya Tanzania, mhimili mkuu wa tatu wa dola ya Tanzania, kutokuwa na kiongozi wake kamili miezi mitano baada ya kustaafu kwa Jaji Mkuu Chande Othman, kunatoa taswira potofu kwamba Mahakama ina hadhi hafifu au ya chini ikilinganishwa na mihimili mingine mikuu ya dola ya Tanzania.

Kitendo hiki vile vile kinatoa taswira potofu kwamba pengine Kaimu Jaji Mkuu wa sasa hatoshelezi nafasi hiyo; au kwamba miongoni mwa Majaji wote wa Rufaa au wa Mahakama Kuu ya Tanzania au mawakili na wanasheria wengine wa nchi hii pamoja na wale wa nchi za Jumuia ya Madola hakuna hata mmoja wao mwenye uwezo au sifa za kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inamtaka Mheshimiwa Waziri amshauri Rais Magufuli, kwa heshima zote anazostahili, amthibitishe Kaimu Jaji Mkuu Prof. Juma katika nafasi hiyo au, vinginevyo, ateue mwanasheria mwingine anayemwona ana sifa za kuwa Jaji Mkuu kamili wa Tanzania. Hali ilivyo hivi sasa inawatia aibu wanasheria wote wa Tanzania na inaitia aibu nchi yetu katika jumuia ya kimataifa.
CC : Mzee Mwanakijiji
 
Tundu lisu amekutana na gwiji. Hata mmutee vipi anapwaya alikuwa anapewa kiki na wasiojua sheria. Sasa kaja mwenyewe. Ila nilikuwa nasikia siku nyingi sana kuwa tundu lieu hajui sheria Bali ni mwanaharakati tu Wa sheria na mpayukaji pasipo kujua lolote ndo mana kabudi kasema mwanasheria yeyote anapaswa kuwa na busara siyo kila kitu kinatatuliwa na sheria bali jamii nabethics sake.
Mie mpaka keshokutwa nitaendelea kumdharau Tundu lissu, na kumuona mwanasheria tapeli, Alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza na akaomba muongozo wa spika eti bunge lihairishwe kwa kuwa TUNDU LISSU anatakiwa mahakamani Dar es salaam. Akasimamie kesi ya mteja wake. Huyo ndio mwanasheria wa chadema.
Tafuteni ansard za bunge la 2011 mwezi wa 3.
 
Mkuu Mwanakijiji mimi nimetulia kwenye hoja yako kwamba unataka uambiwe ni nini ambacho kimepungua kwa kuwepo kaimu Jaji Mkuu.

Mwanakijiji upungufu ni kwamba muhimili wa mahakama kwa sasa upo mikononi mwa Rais Magufuli kwa maana kwamba hakuna uhuru wa Mahakama hata kama unaweza kusema mbona kesi zinaendelea kuamriwa.

Wasomi wa sheria watakubaliana na mimi kuwa moja ya principle muhimu ya uhuru wa Mahakama ni security of tenure of Judges, nashindwa kupata kiswahili chake ila ninaweza kutafsiri kama kinga ya ajira, Jaji inatakiwa afanye shughuli zake bila kuhofia kutumbuliwa au kuondolewa kwenye ujaji kutokana na maamuzi yake anayoyafanya. Katiba yetu imetoa security of tenure kwa Majaji wote kwamba hawataondolewa kwenye ujaji kirahisi kirahisi na hii mpaka pale taratibu kadhaa zikifuatwa ikiwemo kuundwa kwa tume maalumu ya kumchunguza jaji anayehisiwa kuwa anaenenda kinyume na maadili na tume hiyo itakuwa ya majaji kutoka nchi za jumuiya ya madola ambao watachunguza kujiridhisha dhidi ya tuhuma za jaji anayetuhumiwa na kuja na mapendekezo ambayo Rais atalazimika kuyafuata.

Hivyohivyo Utaratibu wa kumtoa ofisini Jaji Mkuu siyo rahisi tofauti na utaratibu wa kurevoke uteuzi wa acting chief justice ambao ni rahisi na inategemeana na uamuzi wa Rais hivyo Acting chief justice anakuwa hajiamini kwani wakati wowote anaweza akaondolewa ofisini.

Ninakubaliana na wewe kwamba Rais hajavunja Sheria ila si kweli kwamba hakuna athari ya kutokuwa na Jaji Mkuu kamili athari zipo tena kubwa tu kumbuka Chief justice ni kiongozi wa Jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani ambayo ina jumla ya majaji watano tu na kesi moja ya CA haisikilizwi na chini ya Justices watatu hivyo ni mara nyingi CJ anashiriki kwenye maamuzi ya kesi hivyo kutokuwa kwake huru kwa kukosa security ya ajira yake anaweza akafanya baadhi ya maamuzi ya kuifurahisha serikali take example serikali inakata rufaa kesi ya ndoa za utotoni na imeshasema haipo tayari kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa huko CA unakutana na Majaji watatu akiwemo acting CJ asipogeuka dissenting justice ili tu kuipendeza serikali basi serikali itashinda.
 
Mie mpaka keshokutwa nitaendelea kumdharau Tundu lissu, na kumuona mwanasheria tapeli, Alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza na akaomba muongozo wa spika eti bunge lihairishwe kwa kuwa TUNDU LISSU anatakiwa mahakamani Dar es salaam. Akasimamie kesi ya mteja wake. Huyo ndio mwanasheria wa chadema.
Tafuteni ansard za bunge la 2011 mwezi wa 3.

Huna akili ya kumwelewa Lissu. Na hiyo 'ansard' unayotaka watu wakasome haipo duniani.

Na Lissu hakuingia bungeni mara ya kwanza 2011
 
Mwana Kijiji kakuuliza ni shughuli gani iliyokwama kutekelezeka kwa sababu kwa sasa hatuna Jaji Mkuu!? Ni ipi hiyo shughuli inayomshinda Kaimu Jaji mkuu wetu wa sasa kuitekeleza, kisa tu, si jaji mkuu!?
Hebu jiulize pia ni kitu gani kinazuia kuteuliwa Jaji mkuu hadi sasa? Ktk maelezo ya Kabudi alisema baada ya Jaji wa mwisho wa kiingereza, hapakupatikana kirahisi wa kujaza nafasi hadi alipopatikana wa kutoa Trinidad.Unataka kuuaminisha umma wa Tz kuwa hakuna wa kujaza nafasi hiyo hapa ndani,Tutegemee "mgeni tena" karne hii?
Tuwe wa kweli :this is an affront to the judiciary!
 
Back
Top Bottom