"Mzee Mwanakijiji, post: 20873879, member: 118"]Nimesikiliza kwa makini kile kinachoitwa "darasa" la Prof. Kabudi. Inasikitisha kuna watu wanasifia ametoa "darasa"
Ni kweli inasikitisha kwasababu darasa alilotoa halikujibu hoja mezani
Kuna hoja ya kuuliza swali; kwamba - kwanini Rais amemteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu kwa muda wote huu.
Swali ni kwamba, kwanini nafasi imekaimiwa kwa muda mrefu kiasi hicho? Jaji Othman alitoa notisi akijua uzito wa nafasi hiyo na vetting inayotakiwa. Hakuamka asubuhi na kufikisha 24hrs notice!!!Swali lina mantiki na lijibiwe kwa mantiki.
Swali ambalo halipaswi kuulizwa na tulilikataa wakati ule ni kuhusu mamlaka ya Rais kumteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu. Hili liko ndani ya mamlaka ya Rais (Presidential prerogative).
Sidhani kama kuna aliyehoji hili. Hapa tuwe wakweli
Wabunge kama wanaona Rais anatumia muda mrefu kjujaza nafasi ya Urais wana uwezo wa kubadilisha sharia na hata Katiba chini ya Ibara ya 100 ya Katiba yetu.
Mfumo mbaya umetufikisha hapa, hatuhitaji katiba viraka.Unaposema Wabunge na wa CCM ambao kila jambo ni sawa wapo katika kundi unaloongelea? Angalia 'odds' ya hoja yako kuwa ya kweli
Kama wanataka nafasi ya Jaji Mkuu isikaimiwe indefinitely (kama hoja ya Lissu ilivyoashiria) namna pekee ni kubadilisha Katiba au sheria ili kuweka kikomo kama ilivyo katika baadhi ya nafasi za utumishi wa umma
Hatuwezi kuweka viraka kila siku , kwanini tusikubali kuandika upya katiba ili mfumo uendane na wakati tukishirikisha mawazo kama ya hili. Hapa unaunga mkono hoja ya mfumo
Kama kwa mfano Rais angejaza cheo cha Ujaji siku moja tu baada ya Jaji Othman kustaafu wapo ambao labda wangeweza kuja na hoja ya kwanini amejaza nafasi haraka bila kuonesha tafakari sana au klutumia muda kufanya utafiti wa kutosha!
Hapana, angehoji mjinga tu. Urais ni taasisi, uteuzi una vetting, kulikuwa na notisi ya kustaafu ambayo kwa muda mrefu. Nani angehoji hilo? Mbona hawahoji teuzi za nafasi nyingine nyeti?
Jibu,Rais ana vyombo vya kazi si lazima public ijue. Asingehoji mtu timamu
Lakini pia kuna swali ambalo inabidi liulizwe kwa wale wanaolalamikia - kwa Rais kuweka Kaimu Jaji Mkuu ni shughuli gani ya Mahakama Kuu ambayo haiwezi kufanyika sasa hivi kwa vile kuna kaimu Jaji Mkuu au ni kitu gani hakifanyiki katika mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambacho kinapaswa kufanywa na jaji mkuu peke yake. Hili ndilo linaweza kuwa hoja ya kwanini inahitajika Jaji Mkuu na siyo Kaimu Jaji Mkuu?
Hapa unafanya 'adulteration' ya nafasi ya Jaji mkuu
Prof Kabudi kasema hakuna hata dakika nchi inaweza kukaa bila Jaji mkuu. Hakumaanisha anafanya kazi za mhakama zote, alimaniisha ni sehemu muhimu ya maamuzi ya mahakama
Pili, unajichanganya kihoja. Kama hakuna kinachosimama, wapo wanaouliza kwanini Rais asimteue tu mtu bila kukaimu ikiwa hana impact unayosema?
Jaji mkuu anahitajika kwasababu alizosema Kabudi
Kumbuka huu ni mhimili mkubwa, hauwezi kuendeshwa kama TRA au Bandari
Lakini kung'ang'ania kitu ambacho wote wanajua hakipo - kwamba Rais hajavunja sheria wala Katiba, na kuwa hakuna kikomo cha muda kilichowekwa kwa hoja ya kuwa ni mazoea mapya haitoshi kuwa hoja.
Sawa kabisa, hakuna sheria iliyovunjwa.
Kimaadili hilo linatia shaka sana. Rais ana public trust, anaweza kuamuru nchi iingie vitani kisha kulitaarifu Bunge, anaweza kuvunja idara, mamlaka za umma n.k. bila kuhojiwa.
Ana nguvu za kisheria 'Exec order' na inakuwa sheria wakati huo.
Katika kufanya hivyo haipaswi kufanya kitu kinachoweza kuleta hisia za ' abuse of power''
Abuse of power si lazima iwe kuvunja sheria, ni misconduct kwa kutumia nafasi hiyo
Kabudi alieleza kwanini Nyerere alichukua muda kupata Jaji mkuu.
Tungeelewa Kabudi angeeleza kwanini Rais anachukua muda kupata Jaji mkuu.
Hakuna anayehoji kwanini hajamthibitisha, wanahoji sababu.
Hizi zipo katika uwezo wao kwasababu katiba inasema 'mamlaka yanatoka kwa wananchi'
Wananchi wanasababu za kuhoji ili kumnusuru Rais na 'abuse of Power' Si lazima Rais afanye wanavyotaka, ni muhimu kwake kuhakikisha anachokifanya kina public trust
Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako.
Je, hii si genuine concern! Hili linaonyesha tayari kuwana mistrust, kazi ya Kabudi ilikuwa kuondoa mistrust inayojengekea si kutueleza ukubwa wa mamlaka yake.
Yes tunajua anayo, lakini je, yanatumika bila kuwa na shaka za 'abuse'.
Mkuu, kama hakuna sababu za kwanini Jaji mkuu awe kaimu, hoja ya kwamba amewekwa 'njia panda' haiwezi kupingika kwa hoja. Umejaribu lakini hukufanikiwa kunishawishi.
Mfano uliotoa haulingani na hali ilivyo.
Kumpa ukaimu ni kumuondolea kinga ya 'kutoondelewa' kiholela.
Kwa maana kuwa ameshikizwa na si kishikizo halisi.
Hili ndilo Kabudi alipaswa kulitolea ufafanuzi. Hakufanya kama ambavyo hujafanya.
Presidential prerogatives..
Hili litumike kiholela. Prerogative ina misingi yake na sababu za kueleweka. Nyerere hakuwa na wasomi, tunasababu gani wakati huu?