Hakuna suala la kudhania hapa kwa sababu, uzoefu umeonesha wazi watu katika kulinda madaraka yao wapo tayari hata kuyapinga yale ambayo waliyaamini na kuyasimamia kwa miaka kadhaa!!!
Humphrey Pole Pole wakati akiwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; alipiga kelele sana kuhusu nafasi ya Ukuu wa Wilaya to the point hakuna ambae alidhania ingetokea siku Pole pole angekuja kukubali nafasi ya u-DC kwa bashasha!!
Kitila Mkumbo, wakati akiwa Mshauri wa ACT Wazalendo na Mhadhiri wa DUCE, alimkosoa JPM kwa tabia yake ya kufanya uteuzi zake kwa Wahadhiri wa Vyuo kwa kile alichodai hatua hiyo ya JPM inapunguza nguvu kazi ya watoa taaluma vyuo vikuu!!!
Siku JPM alipomteua Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu; watu tulimtarajia angeikana nafasi hiyo kwa sababu ilikuwa inapunguza nguvu kazi ya watoa taaluma lakini kinyume chake, Mkumbo nae alifurahia kweli kweli uteuzi huo!!!
Dk. Harrison Mwakyembe kila mmoja alimshuhudia alivyokuwa anayakana maandiko yake mwenyewe wakati wa kikao cha Bunge la Katiba!!! Mwakyembe aliliazimika kuyakana maandiko yake kwa sababu tu ya kulinda uwaziri wake!!!!
Siku anateuliwa Profesa Kabudi niliwaambia watu tusubiri viroja vya msomi mwingine atakavyokuwa anayakana yake aliyokuwa anayasimia! And for real, it's just a matter of time na Kabudi nae ataingia kundi hilo hapo juu!!!
Mifano ipo mingi ambayo yote hiyo inathibitisha jambo moja tu: HAKUNA SUALA LA KUDHANIA hapa bali ndio uhalisia wenyewe unless kama huyo Kaimu Jaji Mkuu ni very exceptional!!!
Sasa, Kaimu Jaji Mkuu nae haitashangaza hata kidogo kuona anachotamani yeye sio kubakia kuwa Kaimu Jaji Mkuu bali kuwa Jaji Mkuu kabisa!! I hate to say this, lakini uzoefu umeshaonesha JPM hayupo tayari kufanya kazi na mtu anayezingua kwa sababu yoyote ile!!!! Hata pasipo na sababu za maana, atakuondoa!!!
Kama ndivyo, kwanini basi nae Kaimu Jaji Mkuu asiwe very cautious na utendaji wake ambao bila shaka anaota siku moja awe Jaji Mkuu kabissa badala ya kukaimu nafasi hiyo?!