Dar: Wananchi wa Mbezi waandamana kushinikiza kuwekewa vivuko vya usalama barabarani, DC aingilia kati

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462
Kufuatia maandamano ya baadhi ya wananchi wa Kata ya Msigani, Jimbo la Kibamba Wilayani ya Ubungo jijini Dar es Salaam katika eneo la Mbezi Kibanda cha Mkaa, wakiishinikiza serikali kuwajengea kivuko chenye usalama zaidi katika eneo hilo, kutokana na ajali za mara kwa mara, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba ametoa maagizo kwa TANROADS kuhakikisha wanaweka taa za kuwavusha wananchi kwenye eneo hilo, kama ambavyo imefanyika kwenye maeneo mengine.

DC Komba ametoa maelekezo hayo leo baada ya kufika kwenye eneo linalolalamikiwa na kuzungumza na wananchi, kuhusu michakato ya kutatua changamoto yao, ambapo pia amewaelekeza TANROADS kuweka matuta madogo maarufu kwa jona la 'Rasta' endapo haitoathiri matumizi ya barabara hiyo ya Morogoro Kimataifa.

Katika hatua nyingine, DC Komba amelielekeza Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, kuhakikisha linaweka Askari katika eneo hilo muda wote, watakaosaidia kuongoza magari, huku akisisitiza kuwa suala hilo ni la lazima.

Maandamano hayo yaliyofanyika jana Machi 29, 2023, yaliyopelekea wananchi hao kufunga barabara, yamesukumwa na ajali ya iliyotokea siku za hivi karibuni na kusabaisha vifo vya wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi, huku mmoja akijeruhiwa, ambapo Mkuu wa Wilaya ameliagiza Jeshi la Polisi kumchukulia hatua kali za kisheria aliyesabanisha ajali hiyo, ili haki za msingi zipatikane.
 
Back
Top Bottom