Dar: Wabunge 19 wa Viti Maalum waliovuliwa uwanachama na CHADEMA, Kuongea na Wanahabari

Status
Not open for further replies.
Tumeshaelezwa utaratibu na mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum CHADEMA. Utararatibu upo kiprinciple zaidi. Lazima kamati kuu ya chama ikae na kuthibitisha hayo majina kabla ya kupeleka tume. Hayo hayo hayakufanyika. Sasa wanataka kutuaminisha nini tena. Its now over. Hakuna kipindi cha mmomonyoko wa maadili kisiasa ambapo mambo yanaendeshwa ovyo as if hatujawahi kuwa sheria , katiba na kanuni kama kipindi hiki. Taifa limepoteza maadili kabisa. Wote tuliowaamini kama Icon wa nchi kukemea, kulaani, kuonya, kukosoa na namna mambo yalivyo ovyo hawasemi chochote. Vijana na wanasiasa wa kuijenga Tanzania ya kesho wanajifunza nini?. Tunatengeneza taifa gani baada ya haya yote?. Its a terrible moment!!!.
Kama Ni suala la maadili mabovu basi lianze na Mbowe..ni kwanini alikuwa anawapa kibali kila hatua...na barua ikapelekwa NEC..Sasa hapa imekuwa shida
 
Dada Halima, mtoto akijinyea, kama anaufahamu kidogo, atabaki bila kugaragara mpaka hausigeli aje kumnasua na kumtakasa. Kwa kadiri anavyokukulika kitandani ndivyo anavyozidi kujipaka mavi. Mimi nakushauri kwa sasa usingeongea chochote na yeyote. Tulia kwanza upime upepo unavyokwenda na upate hekima ya nini cha kuongea kwa wakati huu na jinsi ya kukiongea huku ukijua audience yako. Ukimuuliza mzee Jemsi atakueleza hivyohivyo!
 
Kwa afya ya Nchi mwenyekiti wangu wa CCM akutane na hawa vyama rafiki ili maisha yaendelee. Tunachafuka sana sana.
Kama ilivyotokea kwa wale viti maalumu wa CUF CHADEMA watateua sasa wabunge halali wa viti maalumu na kuwasilisha majina yao.

CCM na Rais tutambue kwamba hivi vyama vingine ni muhimu kwa uhai wa Taifa lazma tuvijenge na pia.

Tuheshimu Viongozi wa vyama vyote kuna vitakataka ndani ya CCM eti vinamdharau Mbowe au Lissu au Maalim Seif. Hii ni laana.
CCM tumeiba tukashindishwa Sasa tutazame taifa linaenda wapi?!

Mkuu hii inaitwa maji kuzidi unga. Hapo ni mwendo wa uji tu. Ugali hausongeki tena!
 
Mdee utambana na cdm lkn kamwe hutashinda. Mungu atakuadhibu tu, cdm wewe Ni Kama mzazi wako maana imekulea. Amin laana itakuja kukuangukia tu. Amin hata ccm wewe hawakuamini Sana wanajua we Ni mtoto halali wa cdm. Sio wa kuasili Kama bulaya.
 
MODS NAOMBA MSIUUNGANISHE HUU UZI. Huu uzi ni wa kipekee kabisa wenye mapenzi mema kwa Mdee na wenzake 18 na CHADEMA. Binafsi mimi naipenda sana chadema japo sio mwanachama. Halima Mdee na wenzake waliamua kubeti na bahati mbaya mkeka umechanika. Hivyo nawaomba wajishushe, waombe radhi na chedema pamoja na wapenzi wake tutawasamehe. Hela tamu jamani, hata mimi ningekuwa kwenye nafasi yake ningesaliti tu. Bahati mbaya amesaliti na ameshindwa kuyapata matunda ya usaliti, hivyo ni bora atubu na atasamehewa. Halima umelala jela kwa sababu ya chadema, umepigwa, umeumizwa na kudhalilishwa kwa ajili ya chadema, hivyo kosa lako moja haliwezi kuyafuta mema yote uliyokifanyia chama. Hakuna aliye mkamilifu chini ya jua. Hata Yuda alimsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha sembuse wewe! Halima tumekuelewa shida sio kwamba huna mapenzi na chadema, shida ni tamaa ya fedha hivyo tafadhali dada angu omba msamaha na hakika utasamehewa. Ni hayo tu dada angu.
 
waliobaki chadema wenyewe wanatamani asubuhi na usiku zali la kina mdee

lingewaangukia wao,watu wanajikaza tu pale ila mioyo ina tamani mengi sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom