Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,982
Kwanza niseme hali ya mkoa ipo salama, hali nishwari tunaendelea na shughuli zetu. Kwahiyo, hata ile operesheni ya panya buku na panya road imefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kimya kabisa! Lakini, nikuahidi kuwa ni operesheni endelevu.
…juzi tulipata matukio ya moto lakini sisi uliotupa majukumu tukuhakikishie kwamba jambo lile tumeweza kulidhibiti na wananchi wale wafanyabiashara watarudi katika nafasi zao na kuendelea na biashara zao.
LADISLAUS MWAMANGA, MKURUGENZI MTENDAJI – TASAF
Tanzania inashika nafasi ya kwanza kwa Afrika na nafasi ya pili duniani kwa kujenga uchumi junmuishi. Hili limewezekana kutokana na ushirikiano katika ngazi zote za utekelezaji.
Ahsante Rais Samia kwa kuidhinisha kuandikisha kaya mpya 498,091 kwenye mpango wa TASAF ili ziweze kushiriki katika shughuli za kukuza uchumi wa kaya na pia kutoa fedha za UVIKO-19 Shilingi bilioni 5.5 ili ziweze kuwafikia walengwa wa TASAF katika maeneo hatarishi kwa ugonjwa wa UVIKO-19.
Mh. Rais, Awamu ya Tatu ya TASAF ndiyo inatekelezwa sasa. Utekelezaji wake ulianza Februari 2020 na unatarajiwa kukamilika 2025. Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu kimetengewa shilingi trilioni 2.
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Tumeendelea kuhakikisha wananchi wanaoishi katika mazingira duni (mjini na vijijini) wanaendelea kupata mahitaji yao ya msingi kwa kupata fursa ya kujiimarisha kiuchumi kupitia programu mbalimbali, ikiwemo: kutoa mikopo isiyo na riba na kutoa ruzuku kwa kaya zinazoishi katika mazingira duni.
- Mpango unazaa matunda
Lengo la serikali kuanzisha TASAF ilikuwa ni kupunguza uasikini. Kwahivyo, tunafarijika sana kusikia na kuona kuwa lengo hilo linaendelea kufikiwa.
Taarifa zinasema kwamba hadi kufikia mwaka huu, TASAF inaonesha kuwa mpango huu unachangia kupunguza umasikini wa mahitaji ya msingi ya kaya kwa zaidi ya 10% na umasikini uliokithiri kwa zaidi ya 110%
Kutokana na mafanikio ya mpango huu, sasa ni azma ya Serikali kuendelea na utekelezaji wake ili kuwafikia wahitaji wote katika vijiji, mitaa na shehia
- Viongozi wa kisiasa wasitengwe
Niseme, katika uandiishaji wa kaya masikini, niombe Ndugu Mwamanga, kuna viongozi wa vyama vya siasa, ambao wamepewa vueo vya vyama vya siasa kule chini,… lakini ukimwangalia hali anaishi katika umasikini kwani kuwa mtu wa kuaminiwa na kuwa na busara hakuhitaji pesa. Unaweza kuwa na mazingira duni nab ado ukaaminiwa na jamii.
Kwahiyo, kama watu wamemchagua kuwahudumia katika eneo lile, kusimzuie kufaidika na mapango huu wa TASAF. Isimzuie!
Kama vigezo vinaonesha anaishi kwenye mazingira duni, basi isimzuie kunufaika na mpango huu. Viongozi wote wa vyama vya siasa.
- Elimu ya matumizi ya rasilimali
TASAF mmefanya vizuri kutoa fedha, kusomesha na kuwapa huduma za kiafya. Lakini kuna mwananchi ana uwezo mkubwa sana, anaishi kwenye mazingira yasiyoridhisha, ana ng’ombe 200, 300 lakini anaishi katika mazingira yasiyoridhisha.
Anaishi kwenye nyumba ambayo haiwezi kumkinga dhidi ya maradhi ya TB. Kinyumba hakieleweki. Watoto hawaendi shule, mambo ya bima hana. Naombeni mfanye pia kazi ya kutoa elimu kuwatoa watu kwenye umasikini wa fikira nan a waishi maisha ambayo yanaeleweka.
Lengo ni kuwatoa watu kwenye maisha duni wanayoishi.
- Wasaidiwe kibiashara
Ingawa mradi huu umeiletea sifa Tanzania, bado tukipimwa katika viwango vya umasikini bado tupo chini.
Kupitia TASAF tunakwenda kuinua watu wenye maisha duni wanyanyuke, waungane na wengine katika biashara lakini pia katika maisha. Tukifanya hivyo tutatimiza malengo endelevu SDG’s bila kumuacha mtu nyuma.
Nilipopita kwenye maonyesho, nimeona vikundi vimetengeneza vitu vizuri sana. Wanahitaji misaada midogomidogo, kwa mfano kwenye vifungashio ya vitu wanavyovizalisha. Vifungashio vitawapa soko.
Wote wamelilia masoko. Lakini masoko kwakuwa bidhaa zao hazijafikia viwango, na moja kati ya viwango ni vifungashio.
Naomba sana wasaidiwe.
- Fedha zitumiwe ipasavyo
Ndugu zangu, wanangu mnaofanya kazi TASAF, TASAF kama ilovyosemwa ina Tshs trilioni 2 ambazo fedha hizi si msaada. Fedha hizi ni mkopo. Tunachukuwa mikopo nafuu kuinua watu wetu wa chini.
Naomba mkazitumie fedha hizi ipasavyo. Nina taarifa, nina habari kwamba kwenye baadhi ya maeneo bado kuna walafi. Kuna watu wapo midomo wazi na wanafanya kila wanaloweza wale fedha hii.
Na inapotokea kuna mmoja mgumu, huyo ndiyo adui yao na huyo ndiye anapigwa vita.
Kuweni na imani. Fedha hii tunakwenda kuilipa Watanzania wote. Chukuwa kile unachopaswa kuchukuwa kutokana na kazi yako.
- Kamati ziwe Jumuishi
TASAF inalazimisha mchanganyiko wa wajumbe katika kamati zake – wanawake na wanaume. Maeneo mengine kwa idadi sawa na maeneo mengine kwa idadi ya kutosha ya Wanawake.
Sisemi mpango huu hauna mapungufu – yapo. Lakini kwa uchache sana.
Tulifanya makossa kwenye awamu ya kwanza ambapo kamati zile hazikuwa na uwiano wa uwakilishi. Kuna maeneo unaambiwa, au unakuta, tatizo la mahali hapo unaambiwa ni soko. Soko linajenngwa lakini ukienda ukitembea soko halitumiki kwasababu siyo shida ya sehemu hiyo.
Na kwenye kamati waliokuwa wakipendekeza soko walikuwa wanajitazama wao kuliko mahitaji ya jamii ile. Lakini kwenye yale maeneo ambapo jamii imeshirikishwa kweli kumejengwa mahitaji ya jamii.
- Maangalizo kuhusu magari
1. Ili kufuatilia nyendo za magari haya, magari yatafungwa mifumo ya car-tracking
2. Magari hay ani kwaajili ya shughuli zaTASAF mijini na vijijini. Yatumike kwenye shughuli za TASAF kama ilivyoainishwa katika mkataba na makubaliano baina ya TASAF na Halmashauri.
3. Utunzaji wa magari haya ni jukumu la Halmashauri. Yamenunuliwa kwa fedha nyingi hivyo ni vema yakatunzwa ili yafanye kazi kwa miaka mingi. Magari haya yasiende kuharibiwa kwa makusudi, yakapangiwa mawe ili Wakurugenzi waje kuomba kuyanunua.
Likiharibika mapema, Mkurugenzi utatuambia kwanini limeharibika mapema.
4. Service ya magari haya ifanywe na wazoefu, kutoka kampuni ya Toyota ambao ndiyo wasambazaji. Najua mtasema Toyota watawafanyia service kwa gharama, lakini kama wameweza kutuuzia kwa nusu bei, inawezekana kuzungumza nao. Zungumzeni na Toyota.
Magari ya zamani ambayo yalikabidiwa kwaajili ya utekelezaji wa TASAF na ambayo yalitolewa taarifa kuwa ni mabovu, yote yarudishwe ofisi za TASAF tawi la Dar es Salaam yakiwa na vifaa vyote muhimu. Mwamanga, usipokee magari yaliyotolewa vifaa.