TANZIA Dar: Pacha Rehema aliyebaki baada ya kutenganishwa naye afariki dunia

Duu! Pole nyingi kwa wafiwa, Pia Shukurani nyingi kwa mola wetu na madaktari wote waliojaribu kupambania maisha ya viumbe hao!
Tuliwapenda na tukapenda kuwa nao lakini Mungu kawapenda zaidi!
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe!
Mola wetu azihifadhi roho zao pahala peponi . Amina!
 
mi nilijua tu k'bongo bongo mission impossible.

innalillahi wa inna ilayh rajiun 🙏
 
Huwaga sishabikiagi ujinga lakini hili la kuwalaumu madaktari wa MNH ni upuuzi, wamejitahidi sana kwa kiwango chao na wanahitajika kupongezwa the operation was very deadly lakini wameonyesha wanawweza despite kutokuwa na maslahi makubwa kama wanasiasa NK. wapewe kongole na sio kulaumiwa.
 
Unataka tuwatie moyo kwa uzembe wa wazi na makusudi kabisa..? Waliwafanyia operation kwajil yakutaka sifa tu, ilitakiwa wangoje watoto wakomae kidogo... Baadhi ya madaktari walihojiwa kabla ya operation, wakasema kisomi zaidi wanatakiwa wafanyiwe baada ya mwaka au miaka miwili...
Mponyaji ni Mungu pekee ila Madaktari ni watekelezaji tu kuisaidia afya yako.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Tangu mwanzo nilikuwa nasita kusema, ila kwa ma Dr wetu hawa wa Tz. naapa nilijua hakutakuwa na usalama kabisa!
 
View attachment 2321684
Mtoto Rehema ambaye ni pacha aliyekuwa amesalia baada ya mwenzake waliyetenganishwa kufariki dunia, naye ameaga Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana Agosti 11, 2022.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema: "Ni kweli amefariki jana saa tano asubuhi".

Watoto hao walifanyiwa upasuaji wa kutenganishwa Julai Mosi, 2022, pacha wa kwanza, Neema alifariki Julai 10, 2022.

Pia soma:
Pacha waliotenganishwa, mmoja afariki dunia
Hv hapo gharama zilikuwa za serikali ama wazazi?
 
Pole kwa wafiwa.

Madaktari wasivunjike moyo, hata mbuyu ulianza kama mchicha, ni kweli kibinadamu inaumiza kuna watu watahisi madaktari wanachezea uhai wa watu.

Ila hakuna mafanikio bila majaribio kadhaa yaliyoshindikana, inaumiza tu kwa kuwa ni binaadamu mwenzetu, hata huko kwa wenzetu yanatokea, si kila wanalofanya wanafanikiwa.

Watanzania tujifunze kupunguza lawama, tunawavunja moyo watu wanaojaribu kutafuta namna ya kutuponya hapa hapa nchini.
Majaribio unafanyia kwa binadamu?
Hujawahi kujiuliza kwanini wenzetu wanajaribia kwa nyani?Ok R.I.P
 
Pole kwa wafiwa.

Madaktari wasivunjike moyo, hata mbuyu ulianza kama mchicha, ni kweli kibinadamu inaumiza kuna watu watahisi madaktari wanachezea uhai wa watu.

Ila hakuna mafanikio bila majaribio kadhaa yaliyoshindikana, inaumiza tu kwa kuwa ni binaadamu mwenzetu, hata huko kwa wenzetu yanatokea, si kila wanalofanya wanafanikiwa.

Watanzania tujifunze kupunguza lawama, tunawavunja moyo watu wanaojaribu kutafuta namna ya kutuponya hapa hapa nchini.
Ndo wafanyie majaribio Kwa wnadamu? Kwanini wasiwe wanajaribubkwanza Kwa wanyama Ili waone athari ni zipi? Bila shaka Kuna BAADHI ya pacha hua hawatenganishwi. Kuna mabinti wapo ulaya na vijana wapo hapo India ni wakubwa wameungana na wanapendelea vizuri
 
Back
Top Bottom