TANZIA Dar: Pacha Rehema aliyebaki baada ya kutenganishwa naye afariki dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
FWaAS9kXoActJKm.jpg

Mtoto Rehema ambaye ni pacha aliyekuwa amesalia baada ya mwenzake waliyetenganishwa kufariki dunia, naye ameaga Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana Agosti 11, 2022.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema: "Ni kweli amefariki jana saa tano asubuhi".

Watoto hao walifanyiwa upasuaji wa kutenganishwa Julai Mosi, 2022, pacha wa kwanza, Neema alifariki Julai 10, 2022.

Pia soma:
Pacha waliotenganishwa, mmoja afariki dunia
 
Pole kwa wafiwa.

Madaktari wasivunjike moyo, hata mbuyu ulianza kama mchicha, ni kweli kibinadamu inaumiza kuna watu watahisi madaktari wanachezea uhai wa watu.

Ila hakuna mafanikio bila majaribio kadhaa yaliyoshindikana, inaumiza tu kwa kuwa ni binaadamu mwenzetu, hata huko kwa wenzetu yanatokea, si kila wanalofanya wanafanikiwa.

Watanzania tujifunze kupunguza lawama, tunawavunja moyo watu wanaojaribu kutafuta namna ya kutuponya hapa hapa nchini.
 
Mloganzila university teaching hospital tuleteeni wanatalaluma kutoka EUROPE and AMERICA waje wafundishe madactari nchini.
 
Pole kwa wafiwa.

Madaktari wasivunjike moyo, hata mbuyu ulianza kama mchicha, ni kweli kibinadamu inaumiza kuna watu watahisi madaktari wanachezea uhai wa watu.

Ila hakuna mafanikio bila majaribio kadhaa yaliyoshindikana, inaumiza tu kwa kuwa ni binaadamu mwenzetu, hata huko kwa wenzetu yanatokea, si kila wanalofanya wanafanikiwa.

Watanzania tujifunze kupunguza lawama, tunawavunja moyo watu wanaojaribu kutafuta namna ya kutuponya hapa hapa nchini.
Unataka tuwatie moyo kwa uzembe wa wazi na makusudi kabisa..? Waliwafanyia operation kwajil yakutaka sifa tu, ilitakiwa wangoje watoto wakomae kidogo... Baadhi ya madaktari walihojiwa kabla ya operation, wakasema kisomi zaidi wanatakiwa wafanyiwe baada ya mwaka au miaka miwili...
 
Back
Top Bottom