Dar: Msanii Nay wa Mitego amepata ajali ya bodaboda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,931
Msanii Emmanuel Eribariki Munis (Nay wa Mitego), amepata ajali ya bodaboda wakati anawahi kwenye Interview.

Kwa sasa msanii huyo yupo katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni akipatiwa matibabu na hali yake bado haiko vizuri.

Inaelezwa alipanda bodaboda ili kuwahi kipindi baada kukwama kwenye foleni akiwa na gari yake.

Hali yake haijatengamaa.
IMG_20210528_234527_593.jpg
 
Msanii mwenye msimamo na asiyeyumba Ney wa Mitego amepata ajali ya boda boda wakati akiwahi kwenye kipindi cha Friday night live cha EA TV , amelazwa hospitali ya Kairuki

Tutafanya uchunguzi huru kujua kama ni hujuma au ni ajali ya kawaida
EATV walivyo toa habari hii nikaona comment ya Veronica france akisema anamsema vibaya Mjomba ndo maana yanampata hayo
 
Msanii Emmanuel Eribariki Munis (Nay wa Mitego), amepata ajali ya bodaboda wakati anawahi kwenye Interview.

Kwa sasa msanii huyo yupo katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni akipatiwa matibabu na hali yake bado haiko vizuri.

Inaelezwa alipanda bodaboda ili kuwahi kipindi baada kukwama kwenye foleni akiwa na gari yake.
View attachment 1800835
Augue pole na apone haraka msema ukweli
 
Bahati inaoneka ahueni ipo! Hawa wenye majina makubwa, ikibidi wawe na escort tu za wajomba kuepuka boda zisizo na usalama hata punje.

Kuna bingwa mmoja alijaribu kupanda boda, hata mita 500 hakumaliza, akapigiwa simu na insurer wake kuwa, tafadhali shuka kwenye hicho ulichopanda, tuko tayari kukufata na kukupeleka popote kwa gharama zetu...jamaa ana bima ya maisha, waliogopa kulipa pesa mingi jamaa akila mkeka.

Polee Nay.
 
Msanii Nay wa Mitego amepata ajali ya bodaboda wakati anawahi kwenye Interview ya kipindi cha Friday Night Live cha East Africa TV, kwa sasa msanii huyo yupo katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni akipatiwa matibabu na hali yake bado haiko vizuri.

Taarifa iliyotolewa na EAST AFRICA RADIO inaeleza kuwa Nay alipanda bodaboda ili kuwahi kipindi baada kukwama kwenye foleni akiwa na gari yake. Tutaendelea kutoa taarifa zaidi za maendeleo ya afya yake.


.......................................................
Hivi ni kweli hadi sasa Nay anatumia bodaboda tena usiku kama usafiri? si tuliambiwa na alionesha ana magari mengi sasa imekuwaje?
 
Back
Top Bottom