WANA-JF;
Katika pongezi zangu kwa ndugu yetu Seick Ponda na baadhi ya viongozi wenzake katika kazi nzuri wanayoifanya hasa katika kipindi hiki cha uongozi wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naomba nianze kwa kuweka nukuu hii hapa japo ni kwa kiingereza, lkn ni imani yangu itaeleweka kwa urahisi `The problems in marketing, finance, operation, personnel and distribution are essentially managerial ones. Thus, it can be argued that,whatever the problem is, be it internal or external to the firm, it could have been successfully solved and controlled if there was managerial adequacy and competency in the organization. "Most firms fail because of poor management and nothing else". The growth and survival of the business is determined by the human factor, and specifically, the managers' ability in management and motivation, largely dictate its survival and growth potential.
Ndugu zangu,
Tumekuwa na maswali mengi sana kuhusu nchi yetu pendwa ya Tanzania kuzidi kuwa katika hali mbaya sana kiuchumi, kisiasa na kijamii hasa katika kipindi hiki cha awamu ya nne.Tumeshuhudia ndani ya kipindi kifupi deni la taifa likiongezeka na kufikia Trilioni 21. Sote tu mashahidi kwamba gharama za maisha yamepanda na ya nazidi kupanda kila siku kwasababu hakuna jitihada za kupambana na hali hiyo. Sote tu mashahidi ya mahusiano kati ya ndugu wawili ambao ni waislamu na wakristo unavyozorota kila siku (rejea makanisa kuchomwa moto Zanzibar kipindi kifupi kilichopita na watuhumiwa kutopatikana mpaka leo). Mauaji dhidi ya raia hasa katika mikutano ya CHADEMA, kwamba hawakuwa na haki ya kuandamana na hivyo polisi wanaolipwa kwa kodi zetu wanaamua kuua ndugu zao watanzania wasio na hatia. Mara zote mauaji haya yanapofanyika utasikia tamko nyingi sana za kutisha kutoka kwa viongozi wa polisi hasa Paul Chagonja na IGP Mwema. Baada ya hapo, tume au kamati inaundwa na ikishaundwa hakuna matokeo yoyote ya maana kwasababu mtuhumiwa atawezaje kujichunguza? badala yake ni kodi zetu ndizo zinaliwa kwa mgongo wa tume lkn kusema ukweli hakuna lolote. Unaweza ukajiuliza swali moja tu dogo kuhusu kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, kwamba kamati 2 zilizoundwa na Waziri pamoja na IGP zinafanya kazi gani tofauti? Je, zile picha zilizovuja na sasa zinapatikana kwenye mitandao duniani kote zinaonyesha wazi kabisa wahusika ni wakina nani, je kuna haja gani ya kuwa na kamati mbili? kama siyo kula pesa zetu?
Katika yote haya na mengineyo mengi, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema kwamba kwasasa kuna ombwe la uongozi katika nchi yetu, ndiyo maana badala ya kupunguza taabu na matatizo, zinaongezeka kila kukicha. Yawezekana ikawa kweli au si kweli, lkn nikisoma hiyo nukuu ya kiingereza kwenye para ya kwanza, nashawishika kuamini kwamba kwasasa Tanzania tunakabiliwa na OMBWE KUBWA SANA LA UONGOZI katika sehemu nyeti.
Hivyo basi, nampongeza ndugu yetu Ponda kwasababu hata yeye amezidi kunifanya niamini kwamba kwa hakika tuna tatizo kubwa sana la kiuongozi katika nchi yetu na tunakoelekea sisi kama nchi ni kubaya zaidi. Harakati za ndugu Ponda zimetusaidia kujua aina ya uongozi tulionao. Katika harakati zote za ndugu Ponda na wafuasi wake, Intelejensia ya polisi na Usalama wa Taifa hawana uwezo wa kugundua na hata kuchukua hatua dhidi ya muhusika au wahusika. Hili ni tofauti kabisa na mikutano ya CHADEMA hasa wanapotaka kufanya mikutano yao halali kwa misingi ya Katiba yetu, kwani mara nyingi sana Intelejensia ya polisi inatoa taarifa mapema ili hiyo mikutano isifanyike. Intelejensia ya Jeshi letu halina kabisa uwezo katika mambo mawili, mosi ni katika harakati za Ponda na pili ni katika uhalifu unaofanyika nchini mwetu na hata kwenye taasisi za kifedha kama benki-rejea uwizi wa jana CBA.
Hivyo ndugu Ponda na wafuasi wake wanafaa kupongezwa kwasababu wametusaidia kufahamu zaidi aina ya uongozi tulionao kwasasa, ndiyo maana matatizo hayakomi wala kupungua na badala yake yanaongezeka kila kukicha. Rejea mifano miwili hapa chini;
1. Sheick Ponda alipinga hadharani na hata kusaidia kusambaza vipeperushi ya kupinga Sensa ambayo ilikuwa ni agizo la Serikali. Lkn mpaka leo hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake.
2. Pia leo wamefanya maandamano na kufanikiwa bila bugudha yoyote ile, pamoja na kwamba hii habari ya kuandamana iliandikwa hata kwenye gazeti la leo la AL-NUUR, lkn Intelejensia ya Jeshi letu halikuweza kupata taarifa hizi. Kumbuka leo bado sensa inaendelea na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali, ni kwamba maandamano hayaruhusiwi mpaka baada ya tarehe 8 septemba 2012.
Mimi nampongeza sana Ponda kwasababu ametuthibitishia kwamba serikali yetu inafanya double standard katika uendeshaji wa mambo yake. Kumbuka CHADEMA walipopigwa Iringa waliambiwa hawaruhusiwi kufanya mikutano mpaka baada ya Sensa, lkn siku hiyo hiyo kule Zanzibar Makamu wa Rais alifungua kampeni za uchaguzi. Kule Mwanza napo Clouds FM waliendelea na FIESTA 2012 pale CCM Kirumba, ambao ulikuwa na watu wengi sana na hata ulinzi wa Polisi. Kule Mvomero pia kuna mikutano imeendelea ya Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri. Pia kumekuwa na chaguzi mbalimbali za CCM katika maeneo mbalimbali hapa nchini bila bugudha yoyote ile toka Jeshi la Polisi.
Hivyo basi, nakupongeza sana ndugu yangu Ponda kwa mafanikio makubwa uliyopata hasa katika kipindi hiki, kwani tayari nimeona watu wanakutia moyo ugombee Ubunge mwaka 2015. Nakutakia kila la kheri. Na zaidi naomba nikupe siri moja, hili nakunongòneza kwa sauti ya chini na usimwambie mtu yeyote labda wafuasi wako hasa wale tu unaowaamini asilimia mia moja, `kwamba maadam tuna ombwe kubwa sana la uongozi katika nchi yetu kwasasa, basi hii ni nafasi pekee sana ya kuhakikisha kwamba madai yako yote, yaani ya miaka yote kabla ya uhuru, baada ya uhuru, kipindi cha Nyerere, kipindi cha Mwinyi, kipindi cha Mkapa, na kipindi kijacho, hakikisha kwamba yote yanapatikana sasa. Usichelewe kuyatimiza wala kuyashinikiza sasa, kwani hatuna uhakika na uongozi utakaoingia madarakani mwaka 2015. Hivyo, huu ndio muda muafaka, hasa kipindi hiki ambapo Intelejensia ya Polisi na Usalama wa Taifa haina meno na hata uongozi hauna uwezo wa kupambana na wewe`. Kila la kheri.
NB: Mods, hii mada ni haina uhusiano wowote na mada zingine, hivyo isihamishwe wala kuunganishwa na nyingine, kwani inajitegemea na inajitosheleza. Wakati mwingine tunajadili specific issues na siyo general. Nategemea ushirikiano wenu na hii mada itasimama kama ilivyo.
Nawasilisha, TELO.