Dar: Maandamano makubwa katikati ya Jiji

Dar: Maandamano makubwa katikati ya Jiji

Status
Not open for further replies.
Nadhani hakuna haja ya kueleza zaidi, Watz wote leo wameona unafiki, uongo na undumila kuwili wa policcm. Maandamano ya Waisilamu leo hayakuingiliwa kabisa, hayakudhibitiwa wala hayakuwa halali kufuatana na wanachodai polisi kuwa kuna sensa inaendelea.

Lazima Nchimbi atoe maelezo.
 
serikali inaogopa raia wake kwa kuwa iko madarakani kwa wizi wa kura
 
Nadhani hakuna haja ya kueleza zaidi, Watz wote leo wameona unafiki, uongo na undumila kuwili wa policcm. Maandamano ya Waisilamu leo hayakuingiliwa kabisa, hayakudhibitiwa wala hayakuwa halali kufuatana na wanachodai polisi kuwa kuna sensa inaendelea.

Lazima Nchimbi atoe maelezo.

Nakuhurumia ndugu yangu iwapo thread hii itadumu dak 5. Jf siku hizi wamebadilika, thread zote zenye angle tofauti na ile ya mwanzo kuhusu suala hili la maandamano ya Wisilamu haitakiwi kabisa.

lakini kuhusu Mwangosi thread nyingi zimeruhusiwa na nyingi ya hizo ni negative kwa CDM.

 
Wakuu naomba kujulishwa kama haya maandamano ya leo yalikuwa na baraka zote za jeshi la polisi maana napata wakati mgumu sana nikifikiria ni nini lilikuwa lengo la maandamano haya ukitofautisha na ule mkutano wa CDM kule kijiji cha Nyololo uliosababisha mauti ya yule mwanahabari (RIP).

Kama yalikuwa na kibali cha polisi basi ni kigezo gani kinatumiwa na hili jeshi letu kutoa vibali vya maandamano au mihadhara maana (with due respect) hawa jamaa walikuwa wanainfluence uvunjifu wa sheria, kama sheria inasema mtu yeyote atakayekataa kuhesabiwa au kuvuruga sensa amefanya kosa la jinai na baadhi ya hawa ndugu zetu waislamu wamefanya hivyo basi walikuwa wanastahili adhabu kwa mujibu wa sheria. Ni mawazo yangu (ambayo nayaamini kuwa ni sahihi) kuwa kwa vile Polisi inaongozwa na hao hao ndio maana baadhi ya mambo yanayofanywa na wenzao wanayafumbia macho.,what a shame!!!

Kweli hii unaweza kuiona Tanzania tu, pale ambapo kikundi cha wananchi kinaweza kuandamana kuishinikiza serikali iachie huru wahalifu na serikali inaogopa na kuwaachia huru..,this is a very bad precedent.

Why this double standard?, wakifanya CDM ni kosa kubwa sana lakini wakifanya wengine khewallaah.


01.jpg 02.jpg 05.jpg 06.JPG
 
Leo ndugu zetu waislamu baada ya swala waliamua kuandamana hadi ofisi za wizara ya mambo ya ndani..walifanya hivyo kuhimiza wenzao waliokamatwa kwa kugomea sensa waachie tena bila masharti. maandamano hayo ya amani sidhani kama yalikua na kibali cha polisi(hata hivyo hata kama wangesema waombe kibali wasingepewa)kutokana na hii nchi tulivyoizoea yalikua ni makubwa sana na mwisho wa siku walipata haki yao waliyokua wanaitafuta..kutokana na hili kuna maswali ya kujiuliza
1.Je kwanini leo polisi hawajatumia nguvu ilihali waandamanaji walivunja sheria?
2.Je ni kwamba wameelimika au kwasababu si chadema?
3.Ukivuta sura jinsi umati ulivyokua mkubwa na ukalinganisha na siku chadema walipokua wanafungua tawi nafikiri utagundua umati wa chadema haufiki hata robo ya waandamanaji leo ila askari walikua zaidi ya ishirini.kwanini nguvu yote hii kwa chadema lakini waandamanaji wengine nguvu haitumiki?
4.Au hawajatumia nguvu maana JK anajua waandamanaji ni "ndugu zake"?
Maoni yako tafadhali
 
Leo ndugu zetu waislamu
baada ya swala waliamua kuandamana hadi ofisi za wizara ya mambo ya
ndani..walifanya hivyo kuhimiza wenzao waliokamatwa kwa kugomea sensa
waachie tena bila masharti. maandamano hayo ya amani sidhani kama
yalikua na kibali cha polisi(hata hivyo hata kama wangesema waombe
kibali wasingepewa)kutokana na hii nchi tulivyoizoea yalikua ni makubwa
sana na mwisho wa siku walipata haki yao waliyokua wanaitafuta..kutokana
na hili kuna maswali ya kujiuliza
1.Je kwanini leo polisi hawajatumia nguvu ilihali waandamanaji walivunja
sheria?
2.Je ni kwamba wameelimika au kwasababu si chadema?
3.Ukivuta sura jinsi umati ulivyokua mkubwa na ukalinganisha na siku
chadema walipokua wanafungua tawi nafikiri utagundua umati wa chadema
haufiki hata robo ya waandamanaji leo ila askari walikua zaidi ya
ishirini.kwanini nguvu yote hii kwa chadema lakini waandamanaji wengine
nguvu haitumiki?
4.Au hawajatumia nguvu maana JK anajua waandamanaji ni "ndugu zake"?
Maoni yako tafadhali

wameanza kujifunza!
 
waziri kaagiza sehemu zote walioko mahabusu waachiwe kwa dhamana baada ya shinikizo hilo la maandamano yasiyo na kibari cha polisi.
 
Leo nimekuwa nikifuatilia habari za maandamano ya ndugu zetu waislam mkoa wa Dar es Salaam.

Sababu ya maandamano hayo imeelezwa kuwa ni kuitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kuwaachia huru wananchi/waislamu waliowekwa chini ya ulinzi kwa kukwamisha shughuli ya sensa.

Baadae, vyombo vya habari ITV na Clouds FM vimetoa taarifa kuwa Waziri husika ametoa amri ya walioshikiliwa kuachiwa huru.

Kumekuwa na maoni mbalimbali juu ya tukio la maandamano na agizo la waziri. Katika kufuatia maoni hayo, nimegundua kuna sehemu jamii inaelekea kukosea. Hivyo basi nimeona kuna haja ya kuandika haya ninayoandika.

Ili kuelewa vizuri yaliyotokea, ni vyema tukatambua kuwa katika tukio au matukio ya leo kuna mambo makubwa manne (4) yanayotakiwa kuangaliwa kila moja peke yake. Mambo haya yasichanganywe na kutolewa "hukumu moja". Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. Watanzania/waislamu kuandamana
2.Sababu inayowafanya waislamu kuandamana
3. Polisi kuheshimu haki ya watanzania/waislamu kuandamana
4. Waziri kutoa agizo la madai ya waislamu kutekelezwa.

Kama nilivyoandika awali, kila moja kati ya haya mambo linahitaji kuangaliwa kivyake na linaweza kuwa na mjadala mrefu tu. Mimi nitagusia kifungu namba tatu (3) kinachohusu polisi kuheshimu haki ya raia kuandamana.

Siku zote, kilio chetu kimekuwa kwa polisi kutokuheshimu haki za raia hasahasa linapokuja swala la maandamano ya kuishinikiza serikali.

Leo polisi wameonyesha ari tofauti. Hawajatumia nguvu wala kuzuia maandamano kwa namna yoyote ile. Ikumbukwa kuwa kuna magazeti leo yalishatoa fununu kuwa waislamu wataandamana na polisi walikuwa na nafasi ya kujiandaa kuwadhibiti waandamanaji iwapo wangekuwa na nia hiyo.

Kwa mtazamo wangu, kama watanzania tunaitakia mema nchi yetu. Kitendo cha polisi kuheshimu haki za raia kilichofanywa na polisi leo ni kitendo cha kupongezwa na kuhamasishwa kiendelee kuwepo siku zote. Ni dhahiri kuwa wapo waliochukizwa na kitendo cha watu fulani kukwamisha sensa au swala la waislamu kuandamana au wamechukizwa na kitendo cha waziri kutoa agizo la kuachia huru "watuhumiwa", lakini tukumbuke kuwa hizo ni mada nyingine zinazohitaji mjadala wake na si busara hata kidogo kuruhusu mada hizo zitupe upofu wa kuona jinsi polisi walivyoheshimu haki za raia na tukaachia mwanya wa kuwapongeza na kuwahimiza kuendelea hivyo.

Wanasaikolojia wanatufundisha kuwa jambo jema likifanyika likapongezwa, inaongeza uwezekano wa jambo hilo kujirudi. Likitokea jambo jema likapuuzwa, inapunguza uwezekano wa jambo hilo kujirudia. Tunataka kujenga Tanzania ambayo mambo mema yanajirudia kila siku na kwa leo, tuwapongeze polisi ili heshima yao kwa haki za raia liwe ni jambo linalojirudia na kuzoeleka kwenye jamii.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Zemarcopolo...
 
sasa hiv polis wakiua mtu, au kujeruhi inakuwa soo,

sasa hiv kila mtu anaishambulia polisi
 

Nakuhurumia ndugu yangu iwapo thread hii itadumu dak 5. Jf siku hizi wamebadilika, thread zote zenye angle tofauti na ile ya mwanzo kuhusu suala hili la maandamano ya Wisilamu haitakiwi kabisa.

lakini kuhusu Mwangosi thread nyingi zimeruhusiwa na nyingi ya hizo ni negative kwa CDM.


Mkuu nakunga mkono.Mods wanatakiwa wawe makini hasa katika kuunganisha baadhi ya thread.Wakati mwingine kuunganisha thread kuna ficha mambo fulani.
 
Bila shaka ruksa ya maandamano hayo ilitoka kwa bwana mkubwa aliyepanga magogoni by implication. Kuna wa kuleta fyoko? Nyie wa chama cha waleta fujo mlie tu.
 
Kwa picha iliyojitokeza leo katikati ya jiji la dsm kufurika maelfu ya waislam wakishinikiza wenzao walio kamatwa kwa kugomea sensa waachiwe huru ni kielelezo tosha kwamba mamia ya maelfu ya watanzania wa itikadi hiyo hawakuhesabiwa, maana yake serikali imeshindwa vbaya na malengo yake kwa ujumla.

Kwa kuwa serikali yetu kila kitu ni propaganda je tuzikubari taarifa/matokeo ya sensa ambayo sasa yatakuwa yanapikwa?? Je ghalama yote nani ameilipa kwa zoezi hili ambalo limeshndwa vibaya?? Kuhusiana na maandamano ya leo, je usalama wa taifa wanakazi gani kama walishndwa hata kung'amua njama na hatari ya uvunjifu wa amani wa waislamu hao waliondamana tena bila kibali na kuharibu taratibu za watu kwa masaa 5?

Hasala waliyosababisha kwa kuwapotezea mda italipwa na nani? Serikali babaishaji kabisa, ina maana kesho waislamu wakiandamana tena na kutaka waislamu woote waliofungwa kwa makosa tofauti itawaachia? Serikali iache woga na isimamie sheria na siyo kufanya maamuzi kwa kutishwa au mashinikizo
 
Nahofia ccm kugawanyika ndani kwa ndani muda si mrefu kwasabab alhaji kakosa hekima ya kuwaunganisha wenzie.

Mwisho umetimia, kwa haya tunayoyashuhudia ccm kimejiangamiza chenyewe kisije na kisingizio cha cdm wala mfumo katoliki.

Kama kunamtu haamini tusubiri, muda si mrefu magogoni hapatamtosha alhaji Kikwete, kwanini? kwasababu ameshindwa kukidhi kiu ya haki, upendo na usawa miongoni mwa jamii ya watanzania wote na wabaya watakaommaliza ni wale anaotawala nao madarakani.
 
Zomba, achana na Jmushi1 atakupotezea muda wako. Anaongea ili mradi tu. Bora ukacheki hata catoons than kumuelimisha kichwa kizito. Refer Al-Baqarh 2:18, Allah anasema; Viziwi, mabubu, vipofu kwahiyo hawatarejea. Ndo huyo Mushi sasa
Hakuna kitu kinachoitwa Islam supremacy wala kutaka kuisilimisha dunia, weka ushahidi kama unacho? yakiwakumba huwa mko tayari kudanganya.

Halazimishwi mtu kuingia kwenye Uislaam. Soma Uislaam uujuwe.

Qur'an 109:

Say, "O disbelievers,
I do not worship what you worship.
Nor are you worshippers of what I worship.
Nor will I be a worshipper of what you worship.
Nor will you be worshippers of what I worship.
For you is your religion, and for me is my religion."
 
kuandama ni haki waache waandamane. wakizuia kama ya chadema watapigwa na hao waislamu mpaka watashangaa
 
nashaka na sheria za nchi hii hasa ya sensa, waliokamatwa walikamatwa kwa sheria gani?na pia wanapoachiwa wanaachiwa kwa sheria gani?je kulikuwa na haja ya kuwakamata?je maandamano no chombo cha kisheria?Pia bado siku za senza hazijaisha , je amri ya kutofanya maandamano nani kaifuta?pia nani aliridhia maandamano hayo?napata taabu na jamii forum hasa moderator , na pia ccm kukumbatia hili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom