Biashara za mabasi faida utaanza kuiona kwa wastani wa muda miaka kuanzia miwili.
Kuna biashara ambazo zitakusaidia tu kutengeneza flow nzuri ya pesa , kuweka pesa kwenye mzunguko na kutengeneza discipline nzuri ya pesa lakini si biashara zitakazo kutoa au kukupa utajiri maradufu.
Naweza sema ni kama ile unaona kuliko kukaa na milioni 300 bank, kwa nini usiiweke kwenye mzunguko izae taratibu kuliko kukaa na pesa mwisho utaiharibu kwa matumizi ya ajabu au kutumia hovyo ikaisha.
Ni kama utumie milioni 50 kujenga nyumba utakayoipangisha kwa mwaka upate mil 4, itachukua miaka 12 kuanza kupata faida, lakini ni biashara ambayo unaweza kusomesha watoto wako hadi chuo kikuu wakitegemea kodi ya nyumba, lakini hio mil 50 ungekaa nayo ndani, isingetoboa mwaka.
Biashara ya mabasi ni nzuri kama huna pesa za tia maji tia maji, inapaswa uwe na mfuko wa kueleweka, mapato unaweka bank unakuja kuchungulia account baada hata ya mwaka au zaidi.
Si kila biashara ni kwa ajili ya faida kubwa. Ni baadhi, na unapoanzisha business unakuwa na malengo.
Hatuwezi sema amefilisika, ni maamuzi tu.