Sabaya ni jambazi au Mkuu wa Wilaya (DC)?

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
166
593
Mama ametupa zawadi nzuri ya Eid. Huu ni ushahidi kuwa Sabaya ameumiza watu wengi ndio maana maamuzi ya kumfurusha yamepokelewa kwa furaha kubwa na nchi nzima.

Jambo la muhimu zaidi mama hajaishia kumfurusha tu bali ameagiza ufanyike uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ili afikishwe mahakamani. Kwahiyo sasa hivi Sabaya ni mtuhumiwa. Muda wowote tutamuona nyuma ya karandinga.

Sabaya ana tuhuma mbalimbali (lukuki) kama taarifa ya Ikulu ilivyoeleza. Anatuhumiwa kupora, kunyanyasa na kutumia madaraka yake vibaya. Tuhuma hizi zimekuwepo tangu enzi za mwendazake lakini amekua akilindwa.

Yeye mwenyewe amewahi kujitapa kuwa hakuna anayeweza kumpa order isipokua mwendazake pekee. Alimdharau hadi RC wake. Ndio maana mama Mghwira alipomwambia aache kutumia mabavu alimcheka kwa dharau. Mwaka 2019 PM alifanya ziara K'njaro wafanyabiashara wakamueleza jinsi Sabaya anavyowanyanyasa, lakini hakuchukua hatua yoyote. Akasema atayafikisha kwa mamlaka yake ya uteuzi.

Lakini hakuna chochote Sabaya alichofanywa. Badala yake alizidi kuwa kiburi kuliko mwanzo. Wale wafanyabiashara "waliomchongea" kwa PM walipata joto ya jiwe. Na PM hakuwa na chochote cha kumfanya. Hatimaye leo mama amevunja kisiki kilichowashinda maksai.

Sabaya anatuhumiwa kutumia mabavu kupora fedha kwa wafanyabiashara mbalimbali. Mmoja wao ni Cuthbert Swai mmiliki wa Asante Tours na Hoteli ya kitalii ya Weruweru.

Cuthbert anadai mwaka 2018 Sabaya alitaka ampe 10M otherwise atampa kesi ya uhujumu uchumi. Kwa kuhofia jela akampa. Baadae akataka tena 10M, akamwambia hana. Baada ya vitisho vya mara kwa mara, wafanyabiashara wenzake wakamwambia mpe tu, usicheze na mjinga atakutoboa jicho. Akampa kishingo upande.

Baada ya miezi michache Sabaya akamwambia kuna "special mission" amepewa hivyo inatakiwa pesa nyingi kuitekeleza. Kwahiyo wafanyabiashara wanatakiwa wachangie. Akamtaka Cathbert atoe 15M. Cuthbert akamwambia biashara ya utalii imeyumba hivyo hawezi kupata fedha hizo.

Na hapo akatangaza uhasama na Cathbert. Akaenda kwenye mashamba yake huko Rundugai akasema alidhulumu wanakijiji. Akatengeneza wazee feki waliojifanya wamedhulumiwa, halafu akatangaza kuyataifisha.

Hakuishia hapo akavamia hoteli ya kitalii ya Weruweru inayomilikiwa na Cathbert. Siku hiyo Nandy alikua na show Arusha, akalala Weruweru. Usiku saa 9 Sabaya akavamia akiwa na kikosi cha watu 6 wenye silaha. Akalazimisha aoneshwe chumba cha Nandy, mhudumu aliyekua mapokezi akakataa. Sabaya akampiga sana. Walinzi walipotoka nao wakapigwa na mabaunsa wa Sabaya.

Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV camera but who cares? Pamoja na video hiyo kusambaa lakini hakupewa hata onyo. Utamwambia nini mtoto pendwa wa mwendazake? Aliwahi kujitapa kuwa yeye ndiye DC pekee anayeweza kumpigia simu mwendazake usiku wa manane na akapokea.

Akaendelea kuvuruga biashara mbalimbali za Cathbert na kuagiza TRA wafreeze baadhi ya akaunti zake. Hali ikawa ngumu hadi mali za kampuni ya Asante Tours zikapigwa mnada. Akavuruga shamba la wanyama (zoo) la Cuthbert maeneo ya Maili sita. Akaharibu mizinga 200 ya nyuki kwenye shamba la Cathbert kwa madai hana kibali cha maliasili cha kufuga nyuki.

Baada ya hapo Cuthbert anadai Sabaya alitishia kumuua. Ikamlazimu kukimbilia ziwa Jipe mpakani mwa Kenya akaishi huko. Zaidi ya watu 300 waliokua wameajiriwa kwenye biashara zake mbalimbali wakapoteza ajira kwa sababu ya Sabaya. Just imagine.

Lakini hakuishia kwa Cuthbert, akaendelea kufanya ukatili kwa watu wengine. September 2020 alivamia hoteli ya Protea Aishi iliyopo Machame, inayomilikiwa na Freeman Mbowe. Hotelini hapo kulikua na wageni kutoka nje ya nchi wanaopanda mlima Kilimanjaro.

Sabaya akawakamata na kudai wamekuja kusaidia Chadema kwenye uchaguzi. Wakatolewa hotelini usiku wa manane na night dress kupelekwa kituo cha Polisi Bomang'ombe. Wakahojiwa na kuachiwa, lakini wamesababishiwa usumbufu, na wameweka doa kwenye sekta yetu ya utalii. Kumbuka tunatumia fedha nyingi kutangaza utalii, halafu mtu mmoja anawadhalilisha kwa mihemko tu.

Siku ya uchaguzi (October 25) alivamia tena Aishi hotel akiwa na magari yenye namba za UN. Wakawapiga walinzi na kukamata baadhi ya mawakala wa Chadema waliokua hapo. Wakawatia matambara mdomoni na kuwapiga sana kabla ya kwenda kuwatelekeza maeneo ya Sanya stesheni usiku huo.

Mmoja wa vijana hao Simon Mwacha alivunjwa mkono karibu na joint. Hadi sasa amefanyiwa upasuaji mara 3 lakini hajapona. Wiki iliyopita viongozi wa BAVICHA walimtembelea na kumkuta amewekewa POP jingine. Huu ni mwezi wa 7 tangu avunjwe na Sabaya na bado hajapona.

Kutumia number za UN kufanya uhalifu ni doa katika diplomasia ya nchi, lakini hakujali hilo. Yeye ni mtoto pendwa wa mwendazake, mtamfanya nini? Kama PM alishindwa kumfanya lolote, aliamini wengine hawamuwezi.

Aliwekeza nguvu na akili zake zote kwa mwendazake. Alimtumainia, alimuabudu na kumsujudu. Lema aliwahi kumwambia huyo unayemtegemea si Mungu. Ipo siku hatakuwepo na utakosa mtetezi. Sabaya akacheka kwa dharau. Leo yametimia yale aliyosema Lema miaka mitatu iliyopita.

Sabaya anatuhumiwa kumteka na kumpiga mtia nia wa udiwani huko Machame. Anatuhumiwa kunyanyasa wananchi mbalimbali kwa sababu za kisiasa. Anatuhumiwa kumpiga ngumi na kumpasua uso mfanyabiashara (Shoo) wa Bomang'ombe baada ya kumkuta akiuza vileo kwenye duka la bidhaa za rejareja.

Sabaya alitengeneza kikundi cha "mabaunsa" ambacho kilikua kinatembea nae popote. Hawakua walinzi rasmi wa serikali. Ni "wahuni" tu aliowaokota mtaani na kuwapa silaha, kama alivyofanya(ga) Bashite.

Kikundi hiki kilikua hakina tofauti na "Mungiki" maana kilitii kila order ya boss wao, hata ambazo ni unlawful. Kiliteka, kilijeruhi na kiliharibu mali kwa order ya Sabaya. Kikundi hiki kiliwahi kuteka moja ya magari ya Freeman Mbowe (likiwa imepaki Arusha) na kutia chumvi kwenye engine. Pamoja na Mbowe kuripoti polisi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Kitendo cha Sabaya kuokota vijana mtaani wasio na mafunzo yoyote ya kijeshi na kuwapa silaha wamlinde ni kosa kisheria. Lakini nani wa kuhoji kama mwendazake alibariki hilo?

Kikundi hiki kimewahi kumpiga mfanyabiashara mmoja (Molel) pub moja maeneo ya Kijenge. Vijana wa Sabaya walimzingira na kumtuhumu kumshika "makalio" mpenzi wa mmoja wao. Wakampiga na kumlazimishwa kutoa kiasi cha pesa ili wamwachie. Kitendo hicho kiliharibu biashara ya eneo hilo, hadi sasa pamepoa licha ya kwamba ni eneo zuri la starehe.

February 09, 2021 Sabaya na genge lake walienda Arusha kumvamia Ally Asaad Ajirin, anayemiliki duka la mapazia la Shaahidi Stores lililopo Barabara ya Nyamwezi jirani na Soko Kuu. Wakamwambia "tuna taarifa unafanya biashara ya kubadili pesa za kigeni kinyume cha sheria" Asaad akakataa.

Anadai Sabaya alimtaka atoe 100M ili asipewe kesi ya uhujumu uchumi. Lakini akamwambia wewe ni DC wa Hai unapata wapi mamlaka ya kuja kunihoji Arusha? Sabaya kusikia hivyo akaagiza milango ifungwe, wakampiga na kumtaka aoneshe pesa zilipo. Wananchi kusikia kilio wakampigia simu Diwani wa Sombetini Bakari Msangi. Alipofika na kuhoji akaunganishwa kwenye kipigo.

Kwa kifupi Sabaya alimiliki kikundi cha kigaidi. Na alikua anaenda nacho popote, iwe ofisini au night club. Hata juzi Dar alikua nacho, akizunguka nacho sehemu mbalimbali.

Mimi ni "survivor" wa kikundi hicho. November mwaka jana nilisema kitendo cha Sabaya kutumia plate number za UN kufanya uhalifu ni doa kubwa kidiplomasia. Akanipigia simu, sikupokea. Akaniandikia 'sms' ya vitisho. Akaniambia akinikamata nitajuta kuongelea vitu nisivyovijua. Sikumjibu lakini nikascreenshot na kumtumia rafiki yangu mmoja ambaye ni kiongozi serikalini just for reference likitokea lolote.

December 26 nikiwa na Don J Mbowe mahali flani Moshi, tukifurahia sikukuu za mwisho wa mwaka, tukaondoka saa 7 usiku. Kesho yake Meneja wa eneo hilo akanipigia simu akasema tulipoondoka tulimuachia balaa kubwa. Sabaya alifika na kikundi chake na kutuulizia. Alipoambiwa tumeondoka, hakuamini.

Akachomoa bastola na kufyatua hewani. Akaleta taharuki, watu wakatawanyika. Hakujali kuharibu biashara, alichojali ni kutimiza matakwa yake. Mabaunsa wakapekua counter hadi vyooni. Hatukuwepo.

Sijui wangetukuta ingekuaje. Pengine tungepigwa na kuwekewa dawa za kulevya mfukoni. Halafu kesho yake dunia ingetangaziwa kuwa tumekutwa na dawa za kulevya. Tungeshtakiwa na kunyimwa dhamana. Huenda hadi leo tungekua tunasota gerezani.

Lakini Mungu wa rehema akakumbuka watanzania tunaowarudishia(ga) tabasamu kwa njia mbalimbali, akaamua kutuokoa. Tuliondoka tukidhani tunaenda kupumzika, kumbe ilikua njia ya Mungu kutuepusha na mkono wa yule mwovu.

Huyu ndiye Lengai Ole Sabaya Jambazi aliyejificha kwenye kivuli cha ukuu wa wilaya na kulindwa na mamlaka za nchi. Mtu aliyewahi kughushi kitambulisho cha idara ya usalama wa taifa, na kushtakiwa mahakamani lakini bado akapewa ukuu wa wilaya. Unampaje uongozi mtu mwenye 'jinai' ya kughushi?

Ajabu ni kwamba kila alipoulizwa kuhusu tuhuma zake alikimbilia kumtaja Mbowe. Nikajiuliza je Mbowe ndiye alimtuma kuteka watu? Mbowe ndiye alimtuma kumvamia Nandy hotelini? Mbowe ndiye alimtuma aweke namba za UN kwenye magari yake ya kufanyia ujambazi? Mbowe ndiye alimtuma ampige diwani wa Sombetini? Kwanini kila anapoulizwa anamtaja Mbowe?

Nikagundua hii ndio njia aliyokua akiitumia kumhadaa mwendazake. Alikua akifanya ukatili anajificha kwenye kivuli cha Mbowe na upinzani. Na mwendazake alimuelewa maana upinzani ulikua adui yake mkubwa. Ukiteka, ukijeruhi, ukiharibu mali ya mtu we sema unafanya hivyo ili kuumaliza upinzani, mwendazake atakuelewa.

Kwahiyo Sabaya alisahau kwamba zama zimebadilika. Ndio maana juzi alipokua CMG alimtaja Mbowe mara nyingi zaidi kuliko tuhuma zinazomkabili. Alidhani kwa kusema amemng'oa Mbowe itamsaidia kujustify maovu yake, kumbe mama ana hofu ya Mungu na hapendezwi na huo uzandiki.

Suala hili la Sabaya lisaidie media kuzingatia profesionalism. Ni aibu media kubwa kama CMG kutumika kumsafisha "jambazi" Sabaya. Ile interview ya juzi ilikua "biased" na ilikosa impartiality and objectivity. Hata Sabaya alivyokua ana-behave sio kama interviewee, bali kama bepari aliyenunua kipindi, akajiandalia maswali na hivyo anajibu anavyojisikia.

Kaka mkubwa Edo Kumwembe aliwahi kusema "Heshimu watu, sponsor hufariki" nadhani hili ndio somo ambalo kila kiongozi anapaswa kujifunza kwa Sabaya. Ukipewa madaraka watendee haki watu wote. Usinyanyase watu kwa sababu una sponsor. Ipo siku sponsor hatakuwepo na utapata tabu sana.

Asante mama kwa kuirudisha nchi kwenye mstari wa haki. Hakika wewe ni zawadi tuliyopewa na Mungu. Tunakuombea ili Mungu mwenyewe awe taa ya njia zako na mwanga wa miguu yako, usiteleze wala kuanguka (Zab 119:105).!

Na
Malisa GJ
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
7,893
8,816
Mkuu hii ni tuhuma nzito sana, ungeileta mapema Jf muda wa tukio tungeijadili kwa mapana na kumtathimini muhusika bila ya kumumunya maneno.

Kuileta leo haitakuwa na ladha maridhawa itakiwayo na great thinkers.

Inakuwa kama tunamjadili mfu asiyeweza kujitetea.

Ujue nini, ule ukali wa andiko lile la jana la Msigwa kumsuspend, hatakuwa na raha na amekesha akiiota ofisi usiku kucha.

Hata angeliletewa huyo Nandy aliyetaka kumhujumu kingono, angelionekana yeye 'mtoto si ridhiki' na kulala naye 'mzungu wa nne'.

amevurugwa kisaikolojia kiasi kwamba, hawezi kujenga hoja za kibabe na kujimwambafy kama pale clouds alivyofanya juzi.

Binafsi nilikuwa nikimfurahia sana anavyokaba wale aliowamulika wakati akiwachukulia hatua.

Kila alipomulikwa 'akitenda',mimi nilimpa heko kwa utendaji uliotukuka kutokana na wale aliowabana wengi wao kama si wote, walionekana kuwa ni wakosaji dhahiri kwa kuungama kwao hadharani, kutepeta na kutela!

Ndiyo nikasema ingawa tunaijadili habari hii kwa sasa, imekuja 'too late', pole kwa misuko suko yote uliyoipata bwashee!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

20 Reactions
Reply
Top Bottom