Dar Lux, kampuni bora ya mabasi inayoelekea kaburini

Dar Lux, kampuni bora ya mabasi inayoelekea kaburini

Ha dar express ana basi Mpya sasa hivi, Scania 95 kama sikosei bodi ya Kenya,
Kama sikosei pia dar express ni kampuni kongwe Sana kwa sasa kwenye usafirishaji wa abiria

ni kweli but hayuko serious au amebweteka naona kama hana mafundi na washauri wazuri haingii akilini zile G7 kuna moja ilitoka kioo cha nyuma akaweka cha plastic yani ile low quality kabisaa, unakuta gari imeumiza taa mathali kile kioo anaenda kuziba na plastics na malami!! ile kampuni kubwa na reputable sana ila kuna mambo hayaendi sawa hasa gari gani zinazoenda kurekebishwa board haziji na mvuto kabisaa

kwa sasa kwa kaskazini Kilimanjaro Express hana mpinzani!!

mimi ni mdau wa Dar Express kitambo ila kampuni haiko sawa kulinganisha na Kilimanjraro
 
Ukiwa mshabiki wa mpira utamtukana mchezaji aliyekosa penati au goli. Kama ni bondia utamcheka anthony joshua kwa kurukaruka bila kupigana unavyotaka.
Biashara zina season huwezihkuwa juu siku zote. Kashachukua chake na huyo unayemsema anaenda chini kanunua malori howo 100. Yanasubiri matrela aende transit atakuwa analaza bill moja na ushehe kila mwezi.
So kama ana future na mabasi sawa kama akiamua kuachana nayo ni yeye mwenyewe na ela zake wpi patamlipa zaidi
 
Hii gari hiii hii hii hiii [emoji112] asee nasikia ni mashine moja balaaa mwezi uliopita saa12 inapita mbezi imetoka mbeya eti[emoji1][emoji1]
Itakuwa haina vts ama,Hapo nahisi abiria njiani roho ilikuwa mkononi
 
Kabisa zipo hoi kama njia ya Dar - Songea kupitia Iringa kuna vilima sana aisee basi zimechoka,akaamua kuleta mpya..angalia Majinja anavyotesa Dar - Sumbawanga yeye ana volvo na Scania lakini mashine zinakimbiza miaka tele
Mkuu
Ishu kuu iliyofanya tujadili huu uzi ni malalamiko kuhusu safari za dar lux , ambaye kwa sasa anasua sua mno na kimsingi anafanya kaz na gari za kichina!!

Kwanza tuelewane, mpaka sasa hakuna ubishi kuwa scania bus ni far superior kuliko basi yoyote ya kichina ,

Kinachotutofautisha mimi na wewe ni kuwa , kweli kuna baadhi ya matajiri wanaonekana kutosumbuliwa na basi hizo za kichina , ambazo we unazi narrow down kwenye good maintainace ya basi hizo kutokana na matajiri hao,

Hapo mimi ndo natofautiana nawe , matajiri wote waliofanya vizuri na basi za kichina wanabebwa na geographical location ya centre za biashara zao , mfano abood, na shabibby, to the best of my knowledge abood hana safari inayozid km 300 ambayo anapeleka youtong, ukiacha moro arusha!, Ndo mana basi zake zinadumu , hali kadhalika shabiby

Mkuu katika watu wajanja wa biashara ya mabasi huyo abood hana mpinzani , route ngumu zote hafanyi, na ndomana akinunua basi zinakaa muda , hata hiyo moro arusha ukiangalia ni route nyepesi sana ndo mana kaweka youtong, iringa pafupi ila sababu ya mlima kitonga anapeleka scania

Zile youtong za terias nadhan abood ndonalikuwa wa kwanza kabisa kuzileta , bado zipo hadi leo , super feo rungwe n.k walifata baadaye lkn bas zao zipo hoi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kaka nafikiri nimejisahau hapo kwa New force ni kweli,,,mfano mpaka leo ana Zonghtong DKX na bado ziko poa ila Superfeo ameshabidili mara Mbili mabasi yake.

Na hiyo njia ndugu ina vilima sana si rahisi gari istahimili sana Newforce amewini gemu maana kama uoivyosema gari iliyoenda leo hairudi kesho wataipaki msamala pale sheli inasubiri siku nyingine irudi.
Hii nilikuwa sijaisoma
Songea kweli gari zote ni za kichina , gari zenye uhakika kule ni new force tu , naoo kwa kuwa ye ana back up ya basi mbili kila siku songea , yaan basi ikiingia songea leo , kesho haiondoki , inaondoka iliyokuja juz yake , New force kiuhalisia sio mfanya biashara ya usafiri , ye anauza mabasi , ndo mana hakuna mtu anafata nyayo zake , na hakai na basi muda mrefu anauza au kubadili kuja route ya dar moro

Super feo zinakufa sana tu njiani, ila tu kwa kuwa huzioni , kinamchomsaidia ye route hiyo ni kama ameiteka , hana mpinzani ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar Lux ameruhusu uswahili. Labda kwenye routes ambazo hazina competition kama Dar-Mwanza, Mbeya na BK lakini Dar-Arusha-Nairobi hakunaga hizo
 
Ukiwa mshabiki wa mpira utamtukana mchezaji aliyekosa penati au goli. Kama ni bondia utamcheka anthony joshua kwa kurukaruka bila kupigana unavyotaka.
Biashara zina season huwezihkuwa juu siku zote. Kashachukua chake na huyo unayemsema anaenda chini kanunua malori howo 100. Yanasubiri matrela aende transit atakuwa analaza bill moja na ushehe kila mwezi.
So kama ana future na mabasi sawa kama akiamua kuachana nayo ni yeye mwenyewe na ela zake wpi patamlipa zaidi
Sasa aachane na Mabasi kabla hajatoa Roho za watu Kwa Bus zake Mbovu. Ndiye anayemiliki Malory ya NUNU? Zina rangi ya Blue kama Buses
 
Princess Muro pamoja na ubovu wa mabasi yake,ila kafanikiwa kuyauza yote....Bongo hakuna kitu kibaya wala kibovu.
Dar Lux akiamua kuyaweka sokoni hayo mabasi atayauza....within a short time.
Hofu yangu ni kwamba mabasi ya long route huenda huwa hayafanyiwi service hasa yanapofika usiku....
Ndugu wanajamvi leo asubuhi ya tarehe 5 nikiwa nimesindikiza abiria wangu anaesafiri kwenda Dar kwa kutumia basi la Dar Lux toka Mwanza nimeshuhudia mabasi yote mawili yakiwa na kasoro ambazo zimesababisha mabasi yote kuchelewa kuondoka katika muda muafaka!!

Basi namba moja ambalo ni Higer lilikuwa na tatizo la betri mbovu na basi namba mbili ambalo ni Marcopolo limeshindwa kupanda kilima cha kutokea Stendi ya mabasi ya Nyegezi kiasi cha kufikia kushusha abiria wote!!
Dar Lux wajipange upya la sivyo yatakuwa yale yale kama ya PRINCESS MURO!!View attachment 1282151

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom