Dar Lux, kampuni bora ya mabasi inayoelekea kaburini

Dar Lux, kampuni bora ya mabasi inayoelekea kaburini

Naunga Hoja, kuna siku nilikua natoka Dar kuja mwanza, Safari tulianza saa nne Mchana kutokana na gari ilihitaji Maintanance. Mara ya pili nilikua natoka MWZ kwenda Dar nilitumiwa ujumbe wa simu saa nane za usiku kuwa safari haitaanza saa kumi na mbili asubuhi bali itaanza saa nne asubuhi,

Nilichogundua ni hawa jamaa sasa hivi wanamagari machache hivyo wanasubiri gari ikifika ndio hiyo hiyo inarudi, kutokana na speed limit ya kipindi cha sasa ni vigumu gari kutoboa Dar Mwanza bila kulala Morogoro, Nzega au Shinyanga.

Sasa ikilala pindi inapofika kutokana na safari ndefu lazima gari ifanyiwe usafi, na kama kuna breakdown irekebishwe.... cha msingi hawa watu waongeze magari ruti ambazo kuna uwezekano wa kulala njiani.
Wana magari mengi kuliko kampuni yoyote kuna yard yao tegeta kama sikosei yapo mengi kama sisimizi, mapya yote
 
Hamna kampuni iana magari mengi kama dar lux,mzee
Abood yuko mbali sana , mbali mno ... Hakuna trip anayoenda ambayo ina gari chini ya tatu..na hivi trip fupi kama dsm moro.. Kila baada ya dakika 30 chuma inanyuka

Safari karibu zote anazoenda dar lux hapa nyumban nao wanenda , ila abood ana maeneo mengi tu hapa hapa nyumban anaenda Dar lux haendi ....kila baada ya dk 30 chuma inang'oa na hutosikia uhaba wa gari au abiria kusubiria gari inayotoka sehem fulan ije...hutosikia kwa abood, Dar lux n case kila siku
 
Eti Dar lux hyo kampuni ishakufa kitambo, mnaopanda mnapanda kwajina bila kufanya utafiti Rudi nyumbani kumenoga. Hapy national baba lao+ tungis,
 
Mbona ipo vizuri tu acheni unafiki basi waungwana
 
Vipi kwa magari ya Dar Harare?
LATRA na TRAFIC waingilie Kati. Safari za mbali jinsi hii Mimi naona si Sawa Basi likifika ligeuze. Walipumzishe wafanye service liondoke Kesho yake. Basi zianze Safari zikiwa Fresh na wafanyakazi kama Drivers.
 
Polen watu wa mwanza, nyanda za juu kusini kumenoga na new force DPK 712 chini ya usimamizi wa Linyama, DPK 715 wanamwita Jaja brazilian mtu hatar sana, DPK 711 mtu mbaya wa kuitwa ustadh Rama mbele kama tai, hizo scania zote zilishanyoosha mikono kwa mchina. Ni mwendo wa honi tu
 
Back
Top Bottom