Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

sio ubora kama unavyotaka tuamini.
Hakuna nilipoongelea ubora wala kulinganisha na maendeleo ya Misri, nimesema hii sio Misri wala Tunisia hii ni Tanzania.. Nimeunganisha mambo mengi mpaka kusema hivyo Ila sijayataja.
 
Wananchi wenye busara wamewashauri polisi kuachana na Lisu kwakua uu uchaguzi amesha shindwa kwaiyo anatafuta pa kuangushia lawama.
Jaribu nawewe kuisumbua polis kiasi hiki alafu wananchi wenye busara washauri kuachana nawew uone km polisi watakubali ushauri huo.. LISSU hayupo peke yake, ni mtego mkubwa kwa nchi, hata baada ya uchaguzi. Labda wamuue
 
Jaribu nawewe kuisumbua polis kiasi hiki alafu wananchi wenye busara washauri kuachana nawew uone km polisi watakubali ushauri huo.. LISSU hayupo peke yake, ni mtego mkubwa kwa nchi, hata baada ya uchaguzi. Labda wamuue
Na wasithubutu kumuuwa ndio watadakwa faster na watashitakiwa na kunyongwa wooote
 
Jeshi la polisi hapo nawapongeza sana kwa kuweka busara mbele. IGP Sirro acha kumtetea Magufuli anayevunja sheria ovyo kwa kutukana na kutishia wananchi kuwa hatawaletea maendeleo wakimchagua mtu asiye wa CCM. Hivi NEC hamuoni hili kama ni kosa???? NALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA BUSARA MLIYOONYESHA. Bado huyo DPP anayefungwa watu wasio na makosa kwa sababu ya chuki aliyonayo juu ya CHADEMA.
Wameona maji yameshazidi unga .......... Mzee with underlying conditions atakuwa yuko tabaani kwa mahasira yake!!
 
sio ishu ila utaulizwa mamlaka ya kutangaza fulani ni mjinga umeyatoa wapi??

Mjinga ana jidhihirisha kwa maneno yake na vitendo vyake katika jambo lolote ,ukifanya jambo lenye kupendeza utapata Sifa njema.
 
Mjinga ana jidhihirisha kwa maneno yake na vitendo vyake katika jambo lolote ,ukifanya jambo lenye kupendeza utapata Sifa njema.

ok bado siku 26 mkuu.

mambo ya kutamka fulani mjinga nk,ni kuchagua upande wa kushindwa.
 


Mambosasa: Polisi tumesitisha kumuita Tundu Lissu, tunamtaka aendelee na Kampeni zake

Baada ya mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, kukataa kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, uliotolewa jana ukimtaka aripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro.

Lissu kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa ataendelea na ratiba zake ikiwemo kikao cha mabalozi kinachofanyika leo.

“Wito wa polisi sio barua ya kirafiki ni amri kisheria, wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama, huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria, nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho” ameandika Lissu kupitia kaunti yake ya Twitter.

Kwa mujibu ya barua iliyotumwa kwa Mwenyekiti wake wa Chama, Freeman Mbowe, Lissu alitakiwa kuripoti polisi 02/10/2020 kwa ajili ya mahojiano kufuatia kauli na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwenye mikutano yake ya kampeni dhidi ya maafisa wa polisi.
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Video ya maelezo ya kamanda wa kanda maalum Lazaro Mambosasa akithibitisha kusitisha wito wa kumtaka Tundu Lissu kuripoti kwa jeshi hilo kanda ya Dar es Salaam
Hahahahhaha, dah jamaa kawashika pabaya
 
mkuu aliambiwa akaripoti dar au hukuisoma barua ya kwanza??

ok barua iliandikwa kwa chadema,lissu alijibu kama nani??

yaani polisi hawajui sheria na lissu ana kiwewe.
Lissu hakujibu barua bali amereact kwa wito wa Sirro kwenye vyombo vya habari na barua aliyoandikiwa!!
 
Hakuna nilipoongelea ubora wala kulinganisha na maendeleo ya Misri, nimesema hii sio Misri wala Tunisia hii ni Tanzania.. Nimeunganisha mambo mengi mpaka kusema hivyo Ila sijayataja.

Mmmh.
 
Mpka sasa nina nadharia mbili:

1. Si ajabu mkaja kusikia mambosasa akiyakana maneno yake ( agizo kutoka juu) kuhusu kusitisha tamko la kumuita lissu.

2. Mambosasa akatumbuliwa within 72hrs.
 
Mkuu aliambiwa akaripoti dar au hukuisoma barua ya kwanza??

Ok barua iliandikwa kwa chadema,lissu alijibu kama nani??

Yaani polisi hawajui sheria na lissu ana kiwewe.
Ambacho hujagundua wewe ndio una kiwewe
 
Kwa siku hizi kumi tu kwa Tundu Lissu, toka tume ya uchaguzi na jeshi la polisi kuingilia kampeni zake, imenibidi nisome maandiko haya matakatifu:

Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake
27 Wakafika tena Yerusalemu. Wakati Yesu alipokuwa akitem bea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia 28 wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?

Na ni nani aliyekupa mamlaka hayo?”

29 Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali mmoja. Mkinijibu, mimi pia nitawaeleza ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 30 Niambieni, mamlaka aliyotumia Yohana kubatiza watu, yalitoka kwa Mungu au kwa watu?”

31 Wakaanza kubishana, “Tukisema, ‘Yalitoka kwa Mungu’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 32 Je, tunaweza kusema ‘Yali toka kwa watu’? - Waliogopa watu kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa nabii. 33 Kwa hiyo wakamjibu, “Hatujui.” Na Yesu akawaambia, “Mimi pia sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”
 
Back
Top Bottom