Polisi wadaiwa kuua vijana wawili vingunguti

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) wamefariki dunia huku vifo vyao vikigubikwa na utata kwakuwa mara ya mwisho December 27,2023 walichukuliwa kwa nguvu nyumbani kwao Vingunguti Jijini Dar es salaam na Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari na kisha kupelekwa kusikojulikana na baada ya Familia kuwatafuta bila mafanikio hatimaye December 28,2023 asubuhi miili yao ikafikishwa Amana Hospital na Watu waliojitambulisha ni Askari wakidai miili hiyo wameiokota.

Mzee Swalehe Kacheuka ambaye ni Baba Mzazi wa Shomari ameiambia @AyoTV_ kuwa “Babuu alikuwa anafanya kazi Kariakoo kampuni ya kuuza pikipiki, aliporudi kazini wakaja Wat waliojitambulisha ni Askari ila hawajavaa sare wakamsimamisha kwamba upo chini ya ulinzi akawauliza nimefanyaje wakawa wanabishana wakampiga risasi ya mguu, Kaka yake katoka wakamnyooshea bastola, akaja Rafiki yake Ismail wakati wanamkunja akasogea wakampiga risasi ya mguuni na wakawachukua wote wakaondoka nao, Ismail walimpakia kwenye IST, Bakari wakampakia kwenye Defender”

Kwa upande wake Mzazi wa Shemeji wa Bakari Ismail amesema “Tulipopata taarifa asubuhi December 28,2023 tukaamkia Polisi Buguruni tukaambiwa hawajaletwa, tukazunguka vituo vya polisi karibu sita hatukufanikiwa, tukazunguka Hospitali tukaambiwa hawajaletwa, mida ya saa 8 mchana tukaambiwa kuna miili Amana ambayo imepelekwa na Polisi wakisema wameowakota Vingunguti”

Familia hizo mbili zimesema miili ya Vijana hao imekutwa na matundu ya risasi na macho yao yametobelewa, Ayo TV imefanya jitihada za kulitafuta Jeshi la Polis Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo lakini hatujafanikiwa ingawa bado tunaendelea na jitihada za kuwatafuta youtu.be/AEIYY8IyB9w?si…
 
Sijui kwa kweli, ila kuna sababu, kutobolewa macho? Kama ni kweli, labda wamesoma ramani ya uhalifu wao usiovumilika na wakataka maelezo zaidi ili wakamate wengine.
Na mimi nshisi hilo.
Lazima walikuwa ni majambazi sugu
 
Na mimi nshisi hilo.
Lazima walikuwa ni majambazi sugu
Sidhani kama ni kweli. Polisi wabongo ni waonevu tu bila kujali wewe ni raia mwema au la.

Ukisoma maelezo ya tukio lilivyokuwa, utaona kabisa sio issue ya ujambazi, bali ukosefu wa akili kutoka kwa polisi. Inaonekana Nia yao ilikuwa ni huyo Babuu, alivyobisha wakampiga risasi. Rafiki yake (Ismail) aliposogea kwa ajili ya kujua status ya mwenzake, nae akapigwa risasi. Pengine hayo majeraha ya risasi ndio yalipelekea kifo.

Alafu kingine, sisi raia ndio tunawala kiburi maaskari kufanya uhalifu. Maana tukio lolote ambalo polisi anaua raia, huwa tunaweka hisia za ujambazi kwa aliyeuawa which is not fair. Hivi mpaka leo hatujazizoea akili za hawa mapolisi wetu?
 
Kwani hawakuwepo raia wakachukua video za tukio??....mtu anakamatwa, anapigwa risasi public na ham-record?
 
Back
Top Bottom