Dar es Salaam: Kituo cha mwendokasi Mbagala chageuzwa danguro

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Kama ulidhani kutokukamilika kwa mradi wa mwendokasi awamu ya pili kutoka Gerezani hadi Mbagala Rangi Tatu kunawakera wakazi wanaohangaika na usafiri kila linapokucha au kukuchwa unajidanganya. Ipo adha nyingine ya vituo vyake kugeuzwa madanguro, walalamikiwa wakubwa wakiwa baadhi ya askari polisi wanaodaiwa ‘kutengeneza fedha’ kupitia biashara hiyo ya ngono.

Japokuwa polisi na viongozi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) wanasema hawana taarifa ya kinachoendelea katika vituo vya mabasi hayo, Mwananchi Digital imefanya utafiti na kujiridhisha kwamba biashara hiyo imeshamiri na inafahamika miongoni mwa wakazi wa maeneo husika wakiwamo viongozi wa serikali za mitaa.

Sio Kamanda Muliro tu, Ofisa Habari wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) inayosimamia miundombinu hiyo, William Gatambi alisema hana taarifa kuhusu kinachoendelea katika vituo hivyo.

Wakati Polisi na Dart wakitoa maelezo hayo, katika kituo cha mabasi hayo Mbagala Rangi Tatu biashara hiyo inaelezwa kushamiri na wanaoifanya wanasema wanalazimika kutoa fedha takribani Sh 10,000 kwa waliopewa dhamana ya kulinda raia na mali zao.

Inaelezwa kwamba, magari ya doria yanayopita kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku hayakamati watu, lakini yanayopita kuanzia saa sita hadi saa saba usiku ndiyo yanakamata watu. Wakishakamatwa, wanapandishwa katika gari kisha wanachukuliwa fedha na kuachiwa waendelee na biashara yao.


CHANZO: MWANANCHI
 
Soma maneno haya hapa ,huko bungeni Dodoma wabunge walipewa siku 15 kujadili bajeti halafu Jana wote Kwa maneno wakasema ndiyoooo,swali hivi kulikuwa na maana gani kupeleka hiyo bajeti kujadiliwa huku posho zikiangamia mithili ya tembo ,Kwa hiyo mtoa mada hizo ndio akili na mfumo wa CCM rushwa na ufisadi uliotamalaki
 
Soma maneno haya hapa ,huko bungeni Dodoma wabunge walipewa siku 15 kujadili bajeti halafu Jana wote Kwa maneno wakasema ndiyoooo,swali hivi kulikuwa na maana gani kupeleka hiyo bajeti kujadiliwa huku posho zikiangamia mithili ya tembo ,Kwa hiyo mtoa mada hizo ndio akili na mfumo wa CCM rushwa na ufisadi uliotamalaki

Pesa wanakula wenzako we unasema zinaangamia.!
 
Toa Bei elekezi ya huduma, ubora wa bidhaa ikiwezekana na picha, wateja tunashindwa kufanya maamuzi sahihi, Hawa wa kuwatumia nauli binafsi nimesha wachoka.
 
Kwa hiyo polisi ndio wanaendesha hiyo biashara? Vichwa vya habari kama hivi vinapoteza maana ya uandishi wa habari
 
Hela za hawa madada poa,kuitumia tu, inatia ukakasi. Maana kwa jinsi inavyopatikana?

Yaani binti anasindiliwa kitu anavumilia maumivu, halafu kidume unachukua hiyo hela una relax kabisa?

Unaagiza mishikaki na bia unakunywa uko fresh kabisa.

Watu wana roho ngumu....

Sisi wengine tuna kinyaaa....!!!
 
Back
Top Bottom