Mkuu wa Mkoa Chalamila azindua usafiri wa Mwendokasi Mbagala-Gerezani

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,821
Hongera sana Serikali kazi nzuri inaonekana .
---

SAFARI za Magari yaendayo haraka (Mwendokasi) kutoka Gerezani hadi Mbagala zimezinduliwa rasmi leo kuelekea msimu wa Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 47 (Sabasaba) ambapo jumla ya magari 30 yataanza kutoa huduma.

Safari hizo zitaanza kesho na gharama ya nauli itakuwa Sh 750 kwa tiketi ambazo pia zitatolewa kwa njia ya mtandao kupitia application ya DART.

Akizungumza wakati wa kuzindua safari hiyo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Deusdecity Casmir amesema wataongeza watumiaji wa magari hayo kwa asilimia 50 ambapo pia wataanza na magari 20 kwa siku ya leo na kuendelea kuongeza.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka DART kuongeza muda wa safari za mabasi hayo kwa saa 24 ili wananchi waweze kupata huduma za usafiri kwa wakati wote.

"Mradi ulianza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza, pili na tatu na imetumia fedha nyingi na zinazotolewa na serikali na hapa ni sehemu muhimu kwani Mbagala inawatu wengi watu wamejua kuzaa na kuongezeka na vituo vimeongezeka pia," ameeleza.
 
Kwa siku ya kwanza wangeweka free kama enzi za chuma
Msipende sana free ndugu zangu, kwani hiyo Free ndio inayouwa uendeshaji wa shughuli za usafirishaji. Tulipe tu ili waongeze ufanisi. La msingi ni kuwa, na Mbagala leo tumepata MWENDO KASI! Nimesubiri sana, sikujua kama Mama ataimaliza. Mama Samia M Mungu akupe maisha marefu yenye afya njema. Mitano tena!
 
Back
Top Bottom