masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,621
- 14,577
- Thread starter
- #61
Mawazo mazuri sana haya mkuu.Target kubwa ya Kenya si Rwanda wala Uganda, target kubwa ni kuichukua DRC kibiashara hivyo Kenya anajitahidi kuweka Bandari ya nchi kavu Rwanda na Uganda kuikamata East Congo, lakini Kigeographia Tanzania ndio ana advantage kubwa kaktika hili. Ni kweli miji iliyokuwa far North ya East Congo kama Goma iko karibu sana na Uganda na Rwanda na hata Tanzania kuifikia miji hiyo ni lazima tupite Rwanda,
lakini Tanzania ina advantage ya kufanya biashara na sehemu kubwa ya East Congo na mpaka Katanga province.
Tukitoa Kivu ya Kaskazini ambayo iko mbali na Tanzaia, Kivu ya Kusini na Maniema (Manyema) Pronvice inaweza kuwa target kubwa ya kibiashara, Reli inayotoka Kalemie (Katanga province) kabla ya kufika Lubumbashi (Katanga Province) inapitia Kasongo (Maniema Province), hivyo kunakuwa na Link ya Ziwa Tanganyika kuzifikia pronvice tofauti za DRC na hiyo ni root nzuri sana ya kusafirisha Shaba kutoka copper belt (Katanga Province) kwenda Asia na Europe
Kuna Advantage nyingine ambayo bado hatujaiona vizuri Watanzania ile ya kutumia Ziwa Tanganyika, Kuna link kubwa sana kati ya Tanzania na Zambia na labda Zimbabwe, kwa maana sasa (Wazimbabwe) wanaingia kwa wingi sana Tanzania kufanya manunuzi. kama Rail ya kati ikifanyiwa marekebisho makubwa na Kigoma ikawa Bandari ya nchi kavu na soko kubwa la bidhaa mfano wa Kariakoo (au Dubai ya JK), kinachotakiwa ni kuwekwa Boti za abiria za kisasa ndani ya Ziwa Tanganyika zitakazo unganisha Zambia (Mpulungu port), DRC-Kalemie Port (Katanga province) na DRC-Uvira port (South Kivu), Hilo likiwezekana Tanzania haitatingishika na Coalition inayotengezwa ya Kenya, Uganda, Rwanda
CC: Tuko, Sikonge
Watanzania tungane katika hili na kujitengenezea uhalali wa kiuchumi kwa vizazi na vizazi vijavyo.
Last edited by a moderator: