Waziri Kombo amuaga Balozi wa Vatican nchini

Waziri Kombo amuaga Balozi wa Vatican nchini

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
506
Reaction score
341
WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA VATICAN NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), ameishukuru Vatican kwa mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa muda mrefu na wa kirafiki na Tanzania.

Akizungumza wakati wa kumuaga Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Angelo Accattino, Waziri Kombo amempongeza kwa huduma yake nchini na kumtakia mafanikio katika majukumu yake mapya nchini Colombia.

Amesema Tanzania inathamini mchango wa Vatican na Kanisa Katoliki katika elimu, afya, kukuza amani, maridhiano na mazungumzo ya kidini, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano katika mabadiliko ya tabianchi na uhifadhi wa mazingira.

Kwa upande wake, Balozi Accattino ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano alioupata wakati wa uwakilishi wake nchini, akieleza kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, mshikamano na umoja wa kidini. Aidha, ameahidi kuendelea kuwa rafiki na balozi mwema wa Tanzania.
 

Attachments

  • WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA VATICAN NCHINIWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Ma...jpg
    WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA VATICAN NCHINIWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Ma...jpg
    109.4 KB · Views: 2
  • WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA VATICAN NCHINIWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mash.jpg
    WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA VATICAN NCHINIWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mash.jpg
    137.2 KB · Views: 2
  • WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA VATICAN NCHINIWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Ma...jpg
    WAZIRI KOMBO AMUAGA BALOZI WA VATICAN NCHINIWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Ma...jpg
    139.2 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom