Dar es Salaam: Askari 300 waongezwa kudhibiti panya road

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mikoa mingine mbona hawa vijana wanadhibitiwa?

========

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amesema mkoa huo umeongeza askari 300 kwa ajili ya msako wa kuwakamata wahalifu maarufu 'panya road'.

Makalla ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba 15, 2022 alipokuwa akizugumza na wananchi wa Kata ya Zingiziwa mara baada ya kutembelea ujenzi wa barabara ya Chanika -Homboza.

Amesema msako wa wahalifu huo umeanza tangu jana Alhamisi na kuwaambia wazazi ambao watapotelewa na vijana wao kuanzia leo Alhamisi wakawafuate vituo vya polisi au hospitali za wilaya.

"Hawa panya road wamezaliwa na wazazi, ni watoto wetu, na kwa kuwa baadhi mmeshidwa kuongea nao sisi tutashughulika nao na tayari tumemwaga askari 300,” amesema

"Hivyo kuanzia leo naomba mzazi au mlezi ambaye hatamuona kijana wake afike vituo vya pilisi na hospitali kubwa za wilaya ikiwemo Amana Mwananyamala, Muhimbili wodi ya Mwaisela na Temeke," amesema Mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama

Hata hivyo, Makalla amesema inasikitisha ķatika matukio mawili yaliyotokea siku mbili hizo katika maeneo ya Kawe na Tabata, waliokamatwa kuhusika wengi na vijana waliotoka kutumikia vifungo vya miezi sita hadi mwaka mmoja jela.

Mwananchi
 
Naona Makalla anawaruhusu polisi kuendelea kuwapiga watuhumiwa wakiwa mikononi mwao, tujiandae kupokea taarifa zaidi za mahabusu kufia vituo vya polisi.

Hata hiyo sababu aliyoitoa Makalla, kwamba baadhi ya hao panyarodi walishafungwa miezi sita hadi mwaka mmoja, haina maana wazazi wao ndio wakawatafute vijana wao mahospitalini, hii ni kauli ya mihemko.

Kawaida, kule mahakamani, baada ya mtuhumiwa kukutwa na hatia, hakimu/jaji hutoa nafasi kwa mawakili wa pande zote mbili, waseme kwanini mtuhumiwa afungwe miaka mingi, au miaka michache.

Sasa hiyo ni nafasi nzuri kwa mawakili wa serikali kuiambia mahakama, mtuhumiwa anastahili adhabu kubwa zaidi kwasababu amerudia kosa, kwani adhabu aliyopewa mwanzo haikutosha kumbadili tabia.

Inashangaza, hawa polisi wetu waliozoea kubambikia kesi watuhumiwa, kuwaruhusu wapige watuhumiwa wakiwa mikononi mwao ni kosa kubwa sana, litakuja kuwaumiza panya rodi na wale wasio panya rodi.

Jamaa wanatatua tatizo moja kwa kutengeneza tatizo lingine, huu ni mfano halisi wa mamlaka iliyochoka akili inayostahili kupumzika kuwaongoza watanzania.
 
Yote haya yanatokana na tozo za hovyo zilizoanzishwa na hii serikali ambayo haijachaguliwa na wananchi.Tozo zimesababisha maisha kuwa magumu na kuzalisha makundi ya kihalifu kama haya ya panya road.serikali zitoeni hizi tozo za kisengelenyuma
 
Naona Makalla anawaruhusu polisi kuendelea kuwapiga watuhumiwa wakiwa mikononi mwao, tujiandae kupokea taarifa zaidi za mahabusu kufia vituo vya polisi.

Hawa jamaa wanatatua tatizo moja kwa kutengeneza tatizo lingine, huu ni mfano halisi wa mamlaka iliyochoka akili inayostahili kupumzika kuwaongoza watanzania.
Makalla hafai kuingoza Dar jamani
 
Naona Makalla anawaruhusu polisi kuendelea kuwapiga watuhumiwa wakiwa mikononi mwao, tujiandae kupokea taarifa zaidi za mahabusu kufia vituo vya polisi.

Hawa jamaa wanatatua tatizo moja kwa kutengeneza tatizo lingine, huu ni mfano halisi wa mamlaka iliyochoka akili inayostahili kupumzika kuwaongoza watanzania.
Panya road sio binadamu wanastahili kifo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana weee! Turudishe ile staili yetu ya zamani, tukiwakama ta basi tunawapeleka chocho kisha pyu pyu pyuuu. Then tunasema waliruka kutoka kwenye difenda wakati wanapelekwa kituoni.
 
Naona Makalla anawaruhusu polisi kuendelea kuwapiga watuhumiwa wakiwa mikononi mwao, tujiandae kupokea taarifa zaidi za mahabusu kufia vituo vya polisi.

Hawa jamaa wanatatua tatizo moja kwa kutengeneza tatizo lingine, huu ni mfano halisi wa mamlaka iliyochoka akili inayostahili kupumzika kuwaongoza watanzania.
Tunaomba ushauri wako wa kina kifanyike nini? kama wanakaa jela miezi sita halafu wanatoka wanarudi yaleyale what shoud we do? Umesikia binti aliekatwa mapanga kawe? imagine angekua mwanao ungesjisiakiaje? dawa ya mot ni moto, police waachwe wafanyake kazi zao tusiwangilie.
 
Watu wa dathram tunadhalilika, yaani tuna import polisi zaidi kulindwa kutokana na mashambulizi ya panya road??
 
Back
Top Bottom