Daladala za Arusha zagoma



Mkuu niwaulize nyie wa Arusha swali, Biashara nyingi za Daladala si Askari Police wengi wanaendesha(Wamiliki) hizo biashara?? Mtu mmoja kaniambia kama zile za Ndesa Tokea Arusha last time nilishangaa ni nyingi nivyo ziona na nilipo uliza niliambiwa ni za Askari Huko USA.


Ukweli ndio huo mkuu siyo magari mengi ni ya traffic tu bali matraffic wengi wa kike ni wapenzi wa makondakta na madereva.
 
haw chadema wanachochoe vurugu soon watahamia kwa watoto wa kindergaten wagome.. Au sio magamba?
una jicho chongo wewe.!? Chadema hata hawahusiki na mgomo! Ni madereva na makondakta wa daladala. Muda wote we unawaza siihaasa tu.
 
una jicho chongo wewe.!? Chadema hata hawahusiki na mgomo! Ni madereva na makondakta wa daladala. Muda wote we unawaza siihaasa tu.
huja msoma vizuri....nilivyo msoma mimi kama ni kejeri kwa magamba
 
Nimekumbuka Mramba alivyosema tutembee kwa miguu kugomea kupanda kwa nauli za dalala
 
Nimekumbuka Mramba alivyosema tutembee kwa miguu kugomea kupanda kwa nauli za dalala

VIVIAN,

Ulilolisema ni sahihi kabisa ila sasa sisi waTZ tatizo ni kulalamika sana ndio twajua ila vitendio ni vichahche mno, hilo lingekuwa limefanyika huko nyuma leo naamini viongozi wetu wangekuwa na Adabu sana. Sasa hapo kwa Issue ya Arusha sijui ni SUMATRA na TRAFFIC ndio wanaleteana Ubabe undava kiubagaubaga tuwaeleweje sasa,

Mji wa Arusha nadhani ndio mji No;1 kwa kukithiri vitu vya kona kona vingi sana na ndio maana life expense pale huwa ni kubwa na umaskini pia ni mkubwa kuliko na ndio sijui wataishi mpaka lini. Watu wa arusha mwamke msipelekeshwe amkeni muda ndio huo sasa FREEDOM IS COMING TOMORROW
 
Huu ni mwanzo tu, inabidi yafanyike mambo ya kuwafungua macho watanzania - kwani njia rahisi imeshindikana sasa inabidi huduma muhimu wazikose ndipo watajua umuhimu wa sanduku la kura... ukiniuliza mimi kuhusu mgao nitakwambia bora ubungo ilipuke tuchukue hata miezi miwili gizani ili mpaka vikongwe watazinduka..

Wenzetu walivuka kipindi cha mageuzi kuelekea utawala bora na wa haki kwa kumwaga damu sisi hata giza linatuogopesha, bora huduma za jamii zikosekane kwa kipindi kirefu halafu tuone wale wapambe wa magambas kama watabaki na misimamo yao..
 
Hali bado ni mbaya jamani. Nipo hapa mianzini kuna kosta iliyosadikiwa kupakia abiria kuja mjini, imevamiwa na wapiga debe wakaiharibu vibaya. Dereva na konda mamechezea kichapo lakini abiria waliamriwa kushuka wakatii na wamesalimika. Abiria wanalalamika kuwa wametoka Moshi lakini jamaa wamesema wamepewa taarifa kwamba gari ilipakia abiria Sanawari. Hali sio shwari kabisa!
 
Taarifa zilizo rasmi zinathibitisha mapigano kati ya makodakta/madereva hiace maarufu kama viford dhidi ya polisi wa CcM..Hali hii inatokana na manyanyaso wanayopata madereva kutoka kwa mapolisi hao..baada ya mgomo wa magari hayo katika mji wote wa arusha wanafunzi walaanza kupigania nafas yao ya kwenda katika shule kwa miguu licha ya umbali mrefu zilipo shule zenyewe ndipo walipokutana na makonda na madereva wakiwa katika maandamano kitendo kilichopandisha jazba wanafunzi hao na kujiunga na madereva na kwenda moja kwa moja kwa mkuu wa mkoa kwa maelezo zaidi..makonda na madereva wanataka yafuatayo
(1)kuachiwa wenzao wanaofikia 40 waliopo gerezan kwa kesi za kubambikiwa.
(2)kuelezwa vituo vyao haliso vya kupandisha na kushusha abiria..


kazi kwenu!!!!!!!!!!!!!
 
Hii movie imetusaidia kutambuana sisi makabwela tusiokuwa na magari na hasa sisi tunaoishi mjini kwa jeuri ya magari ya wenzetu! Leo ni mambo hadharani maana tunakutana na wanzetu tuliokuwa tunafikiri wamehama mji!
 
comfirmation plz. na inaonekana imetokea asub au karibu na mchana. idadi yawatu vipi? wafanyakazi wa kawaida wako katika hali gani?
 
Hii movie imetusaidia kutambuana sisi makabwela tusiokuwa na magari na hasa sisi tunaoishi mjini kwa jeuri ya magari ya wenzetu! Leo ni mambo hadharani maana tunakutana na wanzetu tuliokuwa tunafikiri wamehama mji!

Mkuu usisahau kauli ya riziwani kikwete, watu wanaishi kimjini mjini!!
 
[kwa hiyo sasa hali ikoje huk]
kwa sasa kumetulia ila magari bado yamegoma na vijana wa unga limited,majengo,kijenge na hapa mjin kati bado wako katika makund
..chochote kinaweza kutokea mda wowote
 
okey! kuna thread nyingine kama hii humu. tupe taarifa pale jambo linapozuka!
 
Angalieni TV baadaye mtasikia wanasema Chama fulani cha siasa kina husika na mgomo huu maana hawana aibu hao watu .
 
huu mgomo unaweza dumu hadi week jamaa wako very organised na vikao vilianza toka last week asubuhi dereva wetu wa hiace inayoenda USA alipiga simu kuwa hatakuja ila Ngaramtoni walitest asubuhi wakaazuiwa na dereva wa hiace nyingine ya ngara alichukua gari asubuhi ila ameipaki na ameshindwa kuirudisha akihofia kupigwa mawe
madai ya maderva hiace ni kama ifuatavyo
1. Wananyanyaswa saana na matraffic na ni lazima uwatoe hata kama huna kosa na ni kawaida yao kudai na ukiwa hutoi wanakumark na wakikushika wanakuweka lock up na hii ni kweli na iko saaana na wanafahamika na madereva wako tayari kuwataja kwa majina
2. Polisi kuwashika na kuwatoza fine ya wrong parking ilihali arusha hakuna vituo maalum vya kushusha na kupakia abiria
3. miundo mbinu mibovu ya stand ya vifodi pamoja na ufinyu wake na kuwafanya abiria wasiingie stand na kukaa mabarabarani ambako wakiwapakia hutozwa fine
4. Upendeleo wa wazi kwa magari ya abiria kama kandahar, ecko, n.k na Ndessamburo ambayo wengine inabidi wasajili kwa jina la ndessa na kulipa elfu tano kila siku kwa huyu mtu alikuwa trafiic usa sasa nasikia kahamishwa
5. Sumatra kugoma kutoa route kwa njia zilizozoeleka na kulazimisha gari ziende njia wanazotaka wao kama oldonyo sambo na ngusero
ila kubwa ni ubabewa polisi na rushwa ya nguvu ambayo hulazimishwa kutozwa na askari hao hutamba kama hutaki kuwapa hela bora uache kazi ya hiace kwani watakukimbiza mjini
 
*comfirmation plz. na inaonekana imetokea asub au karibu na mchana. idadi yawatu vipi? wafanyakazi wa kawaida wako katika hali gani?*
kwa sababu tunapenda iinjii yetu,basi wafanyakaz yulitembea kwa mguu kuwahi kujenga nchi,bodaboda ndo usafiri wetu mkubwa..ilitokea asubuh/mchana na hata mda huu hamna usafiri kbsa
 
Back
Top Bottom