Daladala Mbeya zagoma, wananchi walia nauli kupanda

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,174
Reaction score
17,635
Kupanda kwa bei ya mafuta hususani petroli, makali yameanza kung'ata jijini Mbeya baada ya usafiri wa daladala kuweka 'mgomo' kutoa huduma huku wananchi wakilia na nauli za bajaji zilizofikia Sh2,000 kutoka Sh800 za awali.

Mbali na wananchi, wapiga debe nao wamepaza kilio chao wakieleza kuwa hawaelewi hatima ya maisha yao kwa kuwa riziki zao zinategemea zaidi uwapo wa daladala wakiomba Serikali kukaa na wamiliki wa vyombo vya moto kulimaliza ili shughuli ziendelee.

Bei ya lita moja ya mafuta kwa Jiji la Mbeya Machi iliuzwa Sh2,996 na sasa imefika Sh3,952 kwa lita moja, hali ambayo imeonekana kutesa wananchi ambao leo baadhi yao wameamua kutembea kutokana na daladala kutotoa huduma na kiwango kipya cha nauli.

Kutokana na huduma ya usafiri wa daladala kukosekana, baadhi ya usafiri uliotumika ni gari dogo aina ya Noah, guta huku bajaji nazo zikitumika kutoa huduma kwa bei zaidi ya ilivyokuwa awali.

Wakizungumza leo Aprili 2,2026 baadhi ya madereva wa bajaji wamesema wamefikia hatua ya kupandisha bei ya nauli kutokana na bei ya mafuta kupanda tofauti na ilivyokuwa awali , huku madereva wa daladala wakiomba kupandisha hadi Sh1,500.

Akizungumzia changamoto hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda, amesema anaendelea na kikao cha wadau wote wa usafirishaji jijini humo, akifafanua kuwa baada ya mazungumzo ya pande zote Serikali itatoa msimamo na utaratibu kwa ujumla.

"Nipo kwenye kikao na wadau wote wa usafirishaji wakiwamo daladala, bajaji, gari kubwa na wengine wote, hivyo tukimaliza Serikali itatoa utaratibu kumaliza tatizo hili" amesema Itunda.

Kupanda kwa bei ya mafuta hususani petroli, makali yameanza kungata jijini Mbeya baada ya usafi.jpg
 
Mafuta yameongezeka 33% yaani 1000 zaidi kwa kila lita,kutoka 2900/= mpaka 3900/=.

Nauli wanaongeza 150% yaani
1200 zaidi kwa kila safari, kutoka
800/= mpaka 1200/= ?

Hizi kama sio fujo ni nini?

Acheni kuionea serikali
Hapa kwa mtazamo wangu angekuwepo kiongozi mkali kama mzilankende magufuri..

Pandisha bei ya usafiri kiholela holela mfano now Huku kwetu bajaji zilikua 500

Now wanachaji 1000 hii ni dhuluma kwa kweriiiii haikubaliki tukiendelea hivi..kipato kile kile then usafiri unaongezeka hapo tutegemee kupanda kwa mazao ya chakula na bidhaa mbali mbali maana TRANSPORTATION INDUSTRY Ina impact kubwa kwenye kupanga bei za bidhaa
 
Mabadiliko gani unadhani yatatokea kama waliodhini chama ndio hao hao wenye sheli?
 
Ilitakiwa iongezeke kama 165 na iwe angalau 700 tu
 
Mabadiliko gani unadhani yatatokea kama waliodhini chama ndio hao hao wenye sheli?
Kwenye economics kwenye law of demand & supply.

Ukiwa na stock kubwa ya mafuta kama serikali ilivyo jinadi kutokana na yanayo endelea ulimwengu vita ya Iran..

Najiuliza kwani mafuta yanatoka huko uajemi pekee mbona MAFUTA YA LIBYA NA NCHI ZA kiafrika kwanini tusiyatunie yatusaidie?

Nchi hizi za third world countries kamwe tutaendelea kutawaliwa na neo colonialism

Ogopa sana mkoloni mweusii...ugumu wa MAISHA una angukia kwa mtu maskini makodi kibao
 
Yaani kitu cha kwanza mtawala mweusi amefanya ni ku normalize incompetency, underachievement zionekane ni sehem ya maisha which is a lie

Is why tuko hapo, wana avoid sana wananchi kuujua ukweli
 
Ukiangalia sana heka heka zote hizo anazopitia binaadamu kupitia masuala ya siasa na Majanga ya asili Mwisho was siku unagundua kwamba kuzaliwa ni jambo la kipumbavu sana Kwasababu kunamfanya binaadamu aje duniani kuteseka tu nothing else
 
Ni kweli na kuusaka ukweli ni kama kumenya vitunguu.. mengi yatakutoa machozii.....

Na ndio maana watu aina ya POLEPOLE hawakupaswa kuwekwa zile nafasi wangebakia kua ma common man TU...walijua mengi mwishoo wakaenda kinyume na mfumoo.
 
Masikitiko makubwa ndugu yangu...Mimi naona kuzaliwa kwenye third world countries tena ukakosa privilage ya kuzaliwa familia Bora ni matatizo na majanga zaidi ya snura mushi
 
Ukijua too much na ukweli unakuwa threat kwa utawala ambao unatumia uwongo ili kubaki in power

And wako tayari kuua kabisa for that

Wananchi ndio waamue they dont need this peoples
 
Mwananchi maskini na mnyonge + uoga..Ina kua ngumu kwenda kinyume na SERIKALI

Yaani wengi wakienda bungeni kwa chama tawala wanageuka wananchi na kujiangalia wao na kuwaza next election
 
Masikitiko makubwa ndugu yangu...Mimi naona kuzaliwa kwenye third world countries tena ukakosa privilage ya kuzaliwa familia Bora ni matatizo na majanga zaidi ya snura mushi
Kuzaliwa popote tu ni changamoto labda tu itokee uzaliwe kwenye Royal family angalau inaweza kupunguza maumivu na mateso ya heka heka tunazo pitia binaadamu duniani maana maisha yamejaa mateso sana

Mfano mdogo umeona kama Israel ni Nchi ambayo Ina mifumo safi siasa safi za ndani ya Nchi wananchi walikuwa wanakula Bata lakini wanasiasa wameleta choko choko now Nchi inawaka moto raia wanaishi Kwa hofu huku wengine wakifikwa na umauti

Ndio maana nasema kuzaliwa duniani ni upumbavu haya unaweza kuwa unatoka kwenye Royal family lakini ukaja kukutana na kilicho mkuta manji kuzaliwa ni upumbavu pia unaweza usikutane na kilicho mkuta manji au kinacho wakuta Israel na Iran still ikatokea tetemeko la Ardhi Likakuua wewe na family Yako nzima kuzaliwa ni upumbavu mtupu
 
Back
Top Bottom