MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Nimeshagombana na polisi hapa Clock tower sasa hivi eti anasema " kama huna akili huna akili tu" akimaanisha kuwatukana hawa jamaa wa daladala waliogoma nami nikamjibu" Kwa mtu asiye na akili ndiye tu atakeyeona hawa waliogoma hawana akili" basi akaondoka na bunduki yake akibwatabwata akaelekea kujificha maeneo ya TANESCO. Hapa kwa mkuu wa Mkoa kulikuwa na maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa na hawa madereva walipoonekana wanaelekea kwa mkuu wa mkoa ndo mabomu yakapigwa hapa clock tower na sasa wameelekea Meru Post na wamesema watakuwa mtaa wa Sabena kumsubiria mkuu wa wilaya.