Mwaka 1992 nikiwa kambi ya jeshi pale nyumbani Mafinga kuna kuruta mwenzangu alipata matatizo ya tumbo ikabidi aende katika hospital ya jeshi, akaambiwa na daktari inambidi apimwe wacheki anatatizo gani, sisi wenzake tulikuwa katika kazi za kilimo pale Dubliganga kwa wale wanaokufahamu jioni tuliporudi tulipata taarifa za kusikitisha toka kwa yule rafiki yetu, alitueleza kwamba alibakwa na daktari na kwakuwa hapakuwa na sheria kali kuhakikisha vitendo hivi vinakoma kabisa na zilivyo adha za JKT kama wengi mnavyofahamu haikuwezekana kufanya chochote hadi leo. Kwa hiyo si jambo geni kwa hawa Madaktari kufanya hivyo yatubidi kukemea mambo haya.