tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,847
- 18,253
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Juzi niliongea na daktari bingwa anayemiliki hospitali kubwa jijini kuhusu chanzo cha uraibu unaosababishwa na kinywaji cha energy. Daktari huyu alinihakikishia kwamba kinywaji chochote kinachosababisha uraibu lazima kinakuwa na kilevi au dawa za kulevya.
Jibu hili lilinifanya nifikiri sana kuhusu kinwaji cha energy kinachotengenezwa na matajiri wakubwa wawili hapa nchini. Madhara ya kinywaji hiki yamewahi kufanyiwa utafiti na madaktari wa hospitali ya Muhimbili ambao waliwahi kumfanyia upasuaji wa mishipa ya moyo iliyoziba mgonjwa mmoja mraibu wa energy ambaye alikuwa akigida sio chini ya chupa 5 za energy kwa siku.
Napenda kuelekeza lawama zangu kwa matajiri hawa wawili wanaowaua raia kimyakimya huku serikali ikiwa imekaa kimya imejikita kwenye ukusanyaji wa kodi wakati afya za wapigakura zinadhurika. Dawa za kulevya na vilevi vinavyotiwa kwenye kinywaji cha energy zina madhara makubwa kuliko uvutaji wa bangi au sigara.
Bangi imepigwa marufuku hapa nchini. Watengenezaji wa sigara wanaandika onyo kwenye paketi ya kila sigara: uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako. Ni kwanini serikali haiwahimizi hawa matajiri wawili waandike maandishi kwenye chupa za energy:….unywaji wa energy ni hatari kwa afya yako….kama ilivyo kwenye sigara? Ina maana wameamua kuwaacha wapigakura wauawe na matajiri halafu mwaka 2025 nani atawapigia kura?
Sijawahi kuona nchi ya ajabu na isiyojali afya za wananchi wake kama hii nchi ya kusadika na kufikirika, Tanzania. Watawala wanataka wafe watu wangapi ndipo wachukue hatua? Inasikitisha na inahuzunisha sana.