Dada zetu mnaboa kutuonyesha miraba ya nguo zenu za ndani

hehehe, im bad in my own good ways banaa.
kwanza mie huwa naona shida sana kumchagulia mtu zawadi ambae hatuko karibu. hata harusini sibebi zawadi unless tuko close na najua standards zako. nilikaa na mtu akiletewa zawadi anainanga afu kama isipoishia kwa dustbin basi ujue hgal kajivunia. to be honest, nilishawahi kutupa zawadi nililetewa, a very sub standard thing kwa kweli. kama sitaki kuwekeza kwako, nitakupa smiles zitakutosha ( Pasco, ndo maana mi nakupiga mzinga wa apartment. afu yule fundi naona hajaleta zile bati za migongo mbinyuko lol, tiles za italy zilifika. hizo skin tite zako za kichina mi hazinitoshi, usinletee)
King'a, wewe kwa jinsi ninavyokuimagine, hustahili bati za mgongo mbinyuko, wewe unastahili viezekeo vya tiles za decra high quality with 50-year guarantee na hizo tiles za Italy, nitakubadilishia, zimetoka za tiles za Spanish, ziko spiral!, hata kama umeishajengea nitamlipa fundi kubomoa!.

Tuachane utani, nyie dada zetu mliojaaliwa, kwa wale wanaojua kuyatumia majaaliwa yao vizuri, wanaishi peponi hapa hapa duniani!. Juzi kati a friend anaedrive Vogue sport, nimensindikiza pale LRT kuweka service booking, si nikakiona kile ki Female mini vogue pale, nikakiulizia tuu ili kujifurahisha!, nikaelezwa vinaletwa kwa order tuu, mwanzo walileta only 10 pieces to test Tanzania Market, vilikwisha hapa hapo on the spot!, "wazeiye" waliwanunulia "nanihino" hivyo nikiwaona wadada wadogo wanavuta hizo kitu mabarabarani, najiishia tuu kusema "mashallah", sisi kanda ya Ziwa, moyo ukindondoka mahali, tunaupendo mkubwa ajabu wa kutoa kila kitu kuliko hata upendo wa mshumaa, yaani siku nikukona!, naweza kabisa kupasua kifua changu, nikakupa moyo wangu ukaenao wewe, mimi hata nikibaki bila moyo!, kwani moyo wa nini ukilinganisha na kutaka ukitakacho!, bora kuishi bila moyo kuliko kukukosa!.
Pasco.
 
Kweli, kwenye sherehe na harusi, bora kumpelekea mtu gift voucher, kuna watu hawapendi vitu vibaya hata kidogo na hawezi vumilia.

mmh, pasco anataka kupambana na paw?
Kongo, sisi Kanda ya Ziwa siku hizi hatupambani kama enzi za chagulaga!, siku hizi tunapambanisha "visu" tuu!, mwenye kisu kikali, ndio anakula nyama!.
Pasco.
 
hahahaha, Pasco umenichekesha mwenzio im from a working class, nikifukuzwa kazi hapa i will go insane!
mie nna pasi kama nilipigwa na broom nikiwa mdogo. hizo vogue ntaziona kwenye top gear tu wallah. sasa mbona mie natokewa na wanaonipiga mizinga hadi ya lunch? au niende kwa babu? hahaha.
ila na wewe pia mashaallah kaka, yaani una mashosti wenye kwenda kufanya service huko kwenyewe? chini ya mti haupajui wewe. dah, kweli mjini msingi ni nanihii.

hizo misaada zenu za spiral tiles sijui nini mie hata sizitaki. misaada ina masharti na emotional baggage kama mkosi? akhuuu, mie na paw wangu tunazeeshana na nyumba yetu tumepaulia zile bati za kuezekea choo zilee. kwanza nilimuambia tuezekee majani kama wazungu akasema anaogopa vibaka.
King'a, wewe kwa jinsi ninavyokuimagine, hustahili bati za mgongo mbinyuko, wewe unastahili viezekeo vya tiles za decra high quality with 50-year guarantee na hizo tiles za Italy, nitakubadilishia, zimetoka za tiles za Spanish, ziko spiral!, hata kama umeishajengea nitamlipa fundi kubomoa!.

Tuachane utani, nyie dada zetu mliojaaliwa, kwa wale wanaojua kuyatumia majaaliwa yao vizuri, wanaishi peponi hapa hapa duniani!. Juzi kati a friend anaedrive Vogue sport, nimensindikiza pale LRT kuweka service booking, si nikakiona kile ki Female mini vogue pale, nikakiulizia tuu ili kujifurahisha!, nikaelezwa vinaletwa kwa order tuu, mwanzo walileta only 10 pieces to test Tanzania Market, vilikwisha hapa hapo on the spot!, "wazeiye" waliwanunulia "nanihino" hivyo nikiwaona wadada wadogo wanavuta hizo kitu mabarabarani, najiishia tuu kusema "mashallah", sisi kanda ya Ziwa, moyo ukindondoka mahali, tunaupendo mkubwa ajabu wa kutoa kila kitu kuliko hata upendo wa mshumaa, yaani siku nikukona!, naweza kabisa kupasua kifua changu, nikakupa moyo wangu ukaenao wewe, mimi hata nikibaki bila moyo!, kwani moyo wa nini ukilinganisha na kutaka ukitakacho!, bora kuishi bila moyo kuliko kukukosa!.
Pasco.
 
Last edited by a moderator:
hakuna mpambano hapo. namchuna tu (siri yako, yeye ananichuna hisia mie namchuna hela, mutual benefit hehehe). unajua mwanaume asipochunwa anajisikia kama sio mwanaume? mtendee haki zombie

Teh teh king'asti unaua, kumbe kweli bhana i xperinced that.hahaha mbav zangu mie
 
Imekuwa ni kawaida sana kwa dada zetu kuvaa nguo ambazo zimekuwa zinatuonyesha amevaa nguo ya ndan ambayo ina ukubwa kisi gan hasa pale uangaliapo miraba yake na mbaya zaidi nygne hata rangi zake huwa zinaonekana ! Ndo kututega au ?

Competition ni kali kwao na hivi tena kuna kaka zao wanadai haki ya kuolewa.wasipo jichanganya na kujitangaza wanaozea kwao.
 
He he he he, once in a while kutongozwa kama njia ya kumrusha mtu roho?? Bad girl!

Kuna watu wanaomba hadi outing wanawake, unabaki unashangaa tu. Na kuhusu zawadi kuna wengine hawajui watoe zawadi gani kwa mtu gani. Underwear hutolewa kwa watu walio karibu sana. Mie kuna mmama aliwahi nipa moja nikaitupa kabisa. Nikaona asije nikaanga mayai yangu bure.

Ndio maana nikasema punguzeni makusudi!, kuna some kind of dress ukivaa, kutokana na umbo na shape yako (kama ya kawaida) au shape lako (kama ni rusha roho), ukivaa unajua kabisa "watu" roho zitatutoka!, kumbe mnafanyaga makusudi mli mturushe tuu?!.

Hizo zawadi za pichu na diriasi yaani usiseme kabisa!.

Hiki ni kiss cha Pichu na Diriasi. This is a true story mimi mwenyewe yalinikuta!.

"Kuna mdada nilitokea kumdondokea, akifanya kazi front office hoteli fulani kubwa hapa mujini!, anaishi na dada yake anayemuheshimu kama mama hivyo feedom yake kujichanganya ni limited!, akanishauri the only chances ni siku anaiingia evening shift na kutoka kutoka saa 5 usiku, atamwambia dada kuwa ame double, hivyo atatarajiwa home kesho yake asubuhi!. Enzi hizo mimi ni biker, sipakizi mtu mchana!, kwa vile mida hiyo ni usiku, nani ataniona!, akanieleze nikija nisifike kwa hoteli ili watu wasijue!. Nikafanya kama nilivyoelekezwa, baada ya hapo ni kama kawa!. Kumbe Darisalaam ndogo!, nikijua usiku huonekani, kumbe kuna mabundi kibao!, binti wa watu akaonekana!, kumbe alikuwa na kakijana kake hapo hotelini!, wenyewe wamepanga kuona!, mimi sina hili wala lile!. Kijana akaambiwa "mali" zake zimeonekana sehemu sehemu na fulani!.

Sisi watu wa Kanda ya Ziwa, tukipenda, tunapenda kweli, kwenye kweli hakuna siri, nikaamua sasa lunch zangu mara moja moja nikula hoteli ile!. Siku ya siku ikafika, mtoto yuko zamu mchana, hivyo nikasingizia kwenda kula lunch, japo nimuone tuu!. Jamaa si akaonyeshwa!, akaamua leo ni leo, ama zake, ama zangu!. Akanisubiri nje ya hoteli nikitoka anikabili!. Nilipotoka, akanisimamisha kishari fulani, huku keshawaambia wenzeka hivyo wamekusanyika hapo nje wakisubiria kushuhudia ndindo!.

Kiukweli in my life, sijawahi kupigania mwanamke!, kwa kawaida nikigundua tuu tuko wawili, huwa ninajiachia zangu!, kuna watu wanataka kufanya "machani ya chai ni bidhaa adimu!", akaniuliza fulani ni nani wako?!, na mimi nakamuu kwani wewe ni nani wako?, akajibu "mchumba wangu!", nikamuomba kama ni hivyo, naomba tusizungumzie hapa na kuwapa watu faida huku mijamaa ikizidi kusogea!, washabiki maandazi wake wakasema usiende popote eti tumalizane pale pale!, hapo nje ya hoteli kulikuwa na taxi, nikamuomba naomba twende kwenye ile taxi nitailipia, tuongelee mule na sio zogo!, nikaelekea kwenye taxi wakaanza kuzomea as if nimekimbia!, nikaingia ndani nikamwambia dereva afungue mlango wa nyuma after two three minuts jamaa akaja na kutoa shurti taxi isiondoke!.

Nikamwambia dereva awashe gari, aweke AC, tukafunga vioo, mazungumzo yakafuatia, nikaanza kwa kumuambia huyo binti, nimetokea kumpenda na nimemwambia, bado hajanikubalia, ila hajaniambia kama ana mchumba!, Maadam yeye yupo na ndie mchumba mwenyewe, na huyo binti yumo hapo ofisini, na kwa vile anakaribia kutoka, tumsubirie hapa hapa, akitoka aje, anitamkie kweli wewe ndio mchumba wake, mimi nitashuka na huta kaa usikie nikimfuatilia!. Jamaa akakubali. Wato tukanyamaza kimya, gari inauguruma huku mijamaa uko nje inazubiria songombingo lianze!.

Habari pia zimeishafiki ndani kwa binti!, saa ya kutoka imefika, binti atoke, toka na wewe!, nikamshauri, mpigie basi mchumba aje!, akapiga binti akamkatalia kuwa hatoki!, ikafuatia zamu yangu, nampigia, hapokei!. Nikamtumia sms kali!, aje na rafiki anayemuamini, nikamuahidi no harm intended, anatakiwa aje aseme neno moja tuu, mimi niondoke!.
Akaja mwenywe, akaingia kwenye gari. Nje kundi la watu linazidi, wote waliotoka shifti hawaondoki wanasubiria movie live!.

Nikashauri, ili tusiwape watu faida, dereva awashe gari tukazungumzie mahali pengine!. Binti akakubali, jamaa akagoma, mimi nikamsihi kuwa tukimazana, nitawarudisha pale pale kwa sababu bike yangu iko hapo!, jamaa akakubali!. Taxi ikaondoka huku inakwenda mazungumzo yakaanza, mimi sasa ndio mwendeshaji mahojiano, nikaanza straight,

Mimi: fulani (jina la binti)"huyu unamfahamu?.
Binti: Ndio!.
Mimi: Ni nani wako?.
Binti" "ni mfanyakazi mwenzangu!"

Nikageukia kijana>

Mimi: " Naomba ueleze ulivyonieleza ili mwenyewe asikie, jee fulani"binti" ni nani wako?.
Jamaa: "Kweli ni mfanyakazi mwenzangu ila ni mpenzi wangu na ni mchumba wangu!"
Mimi: Nikamgeukia binti " mbona hukuniambi una mpenzi, tena mchumba?!".
Binti: " Huyu kaka ananitaka sana, ila mimi sijamkubali, sio mpenzi wala sio mchumba, japa anadai anataka kunioa!. mimi
simtaki!".
Jamaa amekakaa na binti nyuma hasira zikapanda akataka kumpiga binti kwa hasira
Jamaa: "Unasema mimi ni nani wako?!, wewe sio mpenzi wangu?, kama hunitaki mbona kila siku nakunulia pichu ngapi zinazofanana na dirisia zake, mbona hukatai?, mbona kila siku nakununulia vocha mbona hukatai?, kila ukiwa na shida unaniomba hela hata kama sina, nakopa, leo unanikana?!. Wakaanza kuzozana!. Nikawaambia kwa vile wanafanya kazi ofisi moja, wao watamalizana ofosini kwa wakati wao!.

Nikamwambia dreva taxi, aturudishe pale hotelini nikaichukue bike yangu!. Tulipofika mimi nikawa wakwanza kushuka, jamaa akamwambia tushuke tukazungumze, binti akagoma!, nikamlipia ile taxi imdrop kwake, jamaa akasema haondoki mtu mpaka alipwe gharama alizomgharimia!. Binti akamchamalia, kama ni chupi tuu ametumia kiasi gani, akamwambia andika ghara zote ulizotumia kwa ajili yangu, kesho nakufungashia pichu zako na dirisia zake usinifuate fuate tena!.

Nikajiondokea zangu.

Hiki ndicho kisa cha mtu kununuliwa pichu na kisha ikadaiwa!.

Pasco
 
Pasco, ulimrudia sasa yule binti?
Ila wanamme wa kisukuma wakipenda, wanakuwa kama wamerogwa, wanapendaga jumla. Tena kama na ka rangi kawepo.
 
Last edited by a moderator:
Pasco, ulimrudia sasa yule binti?
Ila wanamme wa kisukuma wakipenda, wanakuwa kama wamerogwa, wanapendaga jumla. Tena kama na ka rangi kawepo.

Teh kongosho, we utakuwa una ka experince na hao watu maana umewapatia vibaya mno. Msukuma akiona mwanamke mweupe anachanganyikiwa aisee. Kama ni laana basi hiyo imeshika
 
Last edited by a moderator:
Teh kongosho, we utakuwa una ka experince na hao watu maana umewapatia vibaya mno. Msukuma akiona mwanamke mweupe anachanganyikiwa aisee. Kama ni laana basi hiyo imeshika
Suri, tafadhali punguza makusudi!. Please tusitesane humu ku..ana majaribuni!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom