Je wazijua sifa kumi (10) za mke mwema

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Mohamed mtaleban leo nakuletea sifa kumi (10) za mke mwema ,maaudhui hii ni ukumbusho kwa wanawake wote walio ndani na nje ya ndoa na hata wanaume ambao ni wasimamizi wa ndoa na wanawake kwa ujumla.

01. MKE MWEMA ANA MAHUSIANO MEMA NA MOLA WAKE.

Mke mwema ni mwenye kudumu katika kumtii na kumcha Mwenyezi Mungu anahifadhi ´ibaadah na utiifu kwa Mungu, kutilia umuhimu faradhi za Uislamu na kuacha kuyaapuza.

02. MKE MWEMA HUJAWA NA HEKIMA.

Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mwanaume anaempenda anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata mpaka marafiki wanatambua kuwa hali ni Mbaya.

03. UVIVU SIO SEHEMU YA MAISHA YAKE.

Kuna wanawake ambao ni wavivu kupita kiasi hawawezi fanya jambo lolote wenyewe lazima kumtegemea dada wa kazi. Kila kitu huwa wanakua na sababu utasikia sipigi deki sababu kiuno kina mshituko, sifui nguo kuchazangu ni laini zinakatika, Hawakosi sababu kwa kile wanachotakiwa kufanya,ili uwe mwanamke/mke mwema jifunze kujibiidisha na uache uvivu.

04. NI MSAFI, ANAYEJUA KUPANGILIA MAVAZI YAKE

Kuna wanawake ambao wanaamini wanaume wanaangalia tabia tuu. Sio kweli. Lazima avutiwe na wewe kwanza maana tabia haionekani kwa nje ni kitu cha ndani,so mwonekano wako ndio unaoweza kumfanya kutaka kujua tabia yako.

Mwanamke/mke mwema anajua avae nini kwa wakati gani na anajua namna yakupangilia rangi za mavazi yake ili kuonekana akiwa na mvuto ndani ya nyumba yake. Mwanaume anapomwangalia mwanamke anapata picha hata ya watoto wake watakavokua wanavalishwa.

Sio tu mavazi hata mwili- ni vizuri kuwa msafi wa mwili sio kijasho cha hatari au harufu isiyo kuwa ya kawaida, kumbuka Allaah ndio anaangalia moyo ila mwanadamu anaangalia nje kwanza moyo badae kwa hiyo usafi wa mazingira na mwili ni jambo muhimu.

05. HAKIKISHA UNATIMIZA MAHITAJI YA NDOA KWA MUME WAKO.

Mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku.” Kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipiza visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama anapanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa mwisho kaongeza mwingine.

Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.

06. MWANAMKE ANATAKIWA KUJUA KUPIKA CHAKULA KITAMU, AMBACHO FAMILIA ITAFURAHIA.

Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Taste”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani. Ni hatari mwanamke kuwaza ndoa wakati hata chai ukipika unaunguza

07. MWAMINI MUMEWAKO WIVU NA HISIA MBAYA NI ADUI WA NDOA YAKO.

Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Allaah (Subhanahu Wata'aala) akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza ndoa kwa uadilifu na upendo, sio unaita watu nakuanza kusimulia madhaifu ya mumemo.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wale ambao watakuwa na daraja ya chini kabisa mbele ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Siku ya Kiyama ni wale ambao anastarehe (kimwili) na mkewe, naye (mke) na mumewe, kisha akaeneza siri zake hizo” (Ahmad, Abu Dawud na al-Bazzaar).

08.MWENYE MATUMIZI MAZURI YA PESA.

Hili ni jambo la msingi sana na wanawake wengi huwa hawajui wanaume wengi huwatega katika huu mtego na kuwapima. Siku zote usitake kukomoa kwasababu anaekununulia ni mwingine na sio wewe, mtu katolewa labda chakula cha jioni ataanza kuagiza vitu alivyokua anaviona kwa tv bila hata kujua bei yake mradi halipi yeye, au kama ni shoping atahakikisha kanunua kila kitu alichokuwaga anawaza maishani bila kujali gharama kwa alie mtoa.

09. KUJISHUSHA NA KUOMBA MSAMAHA.

Ugomvi mwingi kati ya mwanaume na mwanamke au mume na mke mara nyingi hutokana na wote kutaka kua juu hakuna aliyetayari kushuka. Kumbuka mwanamke ndio mlinzi wa ndoa. Wakati mwingine kushuka kwako ndio kunaweza pelekea mume/mwanaume naye kuona makosa yake lakini kutojishusha mara nyingi huleta magomvi ambayo mwishowe huleta aibu

10. MWENYE MAWAZO YA KUENDELEZA FAMILIA.
Mwanamke mwenye upeo mpana wa kufikiri sio yule anaewaza namna ya kubadilisha ma dera, mwanamke mwema ni yule mwenye kukaa na kushauriana na mumewe juu ya mipango ya maendeleo na kumtia moyo mumewe juu ya mipango aliyonayo na sio kuwa kikwazo kwake na kumuonyesha kuwa hawezi kufikia malengo yake.

Waleykum Salam
HD-wallpaper-islamic-hijab-girl-anime-girl-hijab-girl-islamic.jpg
 
Waleykum SalamView attachment 2811371

Na hawa wanawake toleo la pili tunawaweka wapi [mention]Ritz [/mention] & [mention]CityHunter1 [/mention]
 
Back
Top Bottom