Dada uzuri wako usiulete nyumbani kwako, utaachika

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
Dada Yangu,
Ni kweli wewe ni mzuri sana wa sura, tumekubali.

Ni kweli mwonekano wako na shepu lako linaweza kumvutia kila mwanaume rijali, hili pia tumekubali.

Ni kweli umesoma sana, elimu nzuri na sasa kimtindo kama umejipata hivi!! Aisee!! tumekubali.

Ni kweli umetoka kwenye familia bora, yani baba, mama na ndugu zako wapo vizuri. Hatuna ubishi mwali wangu, tumekubali.

Ni kweli Mungu amekujalia, una kazi nzuri na biashara zako zimekuwa kubwa sana mjini, tumekubali.

Ni kweli umekuwa mcha Mungu na mfuasi mzuri wa dini, hukauki kanisani au msikitini. Hii ni sifa njema sana, tumekubali.

Ni kweli hivi vyote, vinaweza kuwavuta wanaume kutaka kuwa nawe kimapenzi na hata ndoa. Hakuna ubishi, lazima tukubali.

LAKINI, ili kudumu katika ndoa, ni lazima utambue maisha ya ndoa ni zaidi ya hivi vyote. Hapa sasa na wewe itabidi ukubali tu.

Mwanaume anapenda uzuri wako, lakini uzuri huo usiulete ndani mwako.

Mwanaume anapenda mwonekano wako, lakini mwonekano huo usiulete ndani mwako.

Mwanaume anapenda elimu yako, lakini elimu hiyo usiilete ndani mwako.

Mwanaume anapenda sana vile umetoka kwenye familia bora, lakini utajiri wao usiulete ndani mwako.

Mwanaume anapenda sana vile una kazi nzuri na biashara zako zinaenda, lakini zisikufanye ukaleta dharau nyumbani kwako.

Mwanaume anapenda sana vile umekuwa mcha Mungu, lakini kanisa au msikiti visikufanye ukashinda na kukesha huko ukasahau majukumu ya nyumbani kwako.

Neno la Mungu linasema,
"Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana."
Wakolosai 3:18

"Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno."
1 Petro 3:1

Pamoja na sifa na neema zote ulizojaliwa lakini kumbuka kuwa siku zote mwanaume anapenda kuwa mume ndani ya nyumba.

Mwanaume kuwa mume ni yeye kuwa na nguvu, ni yeye kuwa na madaraka na ni yeye kuwa na mamlaka ndani ya nyumba.

Ndio maana neno la Mungu linasisitiza wake kuwa na utii kwa waume zao.

Sifa ulizo nazo zitakufanya upendwe na hata kuolewa lakini sifa hizohizo ndizo zitakazokufanya uachike na kila mwanaume kama utakosa kuwa na utii.

#No_Learning_No_Earning
So we have to Learn.

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

IMG_20231111_210108_197.jpg
 
Uzuri wake ndio umemuweka hapo, mumewe akirudi kazini anaridhika na kufarijika kuona nyumba yake ina pambo zuri, acheni kuingilia mahusiano ya watu kila mtu anavitu avipendavyo kwa mwenzi wake,

Mfano kuna watu wameoa wanawake wanachamba lile domo la mkewe yeye ndie burudani yake.
 
Ndoa haina formula maalum, yaani ukileta formula kwenye ndoa lazima itakula kwako
Kikubwa ni kwenda na beats
Ila kweli ndoa/mapenzi hayana expert kuna muda huwa nafikiria sana na sitaki kushauri mtu yeyote kuhusu haya mambo kikubwa tu Ingia kwenye ndoa ukiwa umeamua na unajitambua itakusaidia kuwa na maamuzi sahihi katika kila changamoto mpya ambayo hukutegemea kukutana nayo.

Siyo kusalitiwa au kudharauliwa tu ndo chanzo cha migogoro kuna vyanzo vingi vya migogoro ndo hapo unapoambiwa hayana formula unatakiwa mwenyewe tu kichwan uwe timam kutatua changamoto zinazovumilika.
 
Dada Yangu,
Ni kweli wewe ni mzuri sana wa sura, tumekubali.

Ni kweli mwonekano wako na shepu lako linaweza kumvutia kila mwanaume rijali, hili pia tumekubali.

Ni kweli umesoma sana, elimu nzuri na sasa kimtindo kama umejipata hivi!! Aisee!! tumekubali.

Ni kweli umetoka kwenye familia bora, yani baba, mama na ndugu zako wapo vizuri. Hatuna ubishi mwali wangu, tumekubali.

Ni kweli Mungu amekujalia, una kazi nzuri na biashara zako zimekuwa kubwa sana mjini, tumekubali.

Ni kweli umekuwa mcha Mungu na mfuasi mzuri wa dini, hukauki kanisani au msikitini. Hii ni sifa njema sana, tumekubali.

Ni kweli hivi vyote, vinaweza kuwavuta wanaume kutaka kuwa nawe kimapenzi na hata ndoa. Hakuna ubishi, lazima tukubali.

LAKINI, ili kudumu katika ndoa, ni lazima utambue maisha ya ndoa ni zaidi ya hivi vyote. Hapa sasa na wewe itabidi ukubali tu.

Mwanaume anapenda uzuri wako, lakini uzuri huo usiulete ndani mwako.

Mwanaume anapenda mwonekano wako, lakini mwonekano huo usiulete ndani mwako.

Mwanaume anapenda elimu yako, lakini elimu hiyo usiilete ndani mwako.

Mwanaume anapenda sana vile umetoka kwenye familia bora, lakini utajiri wao usiulete ndani mwako.

Mwanaume anapenda sana vile una kazi nzuri na biashara zako zinaenda, lakini zisikufanye ukaleta dharau nyumbani kwako.

Mwanaume anapenda sana vile umekuwa mcha Mungu, lakini kanisa au msikiti visikufanye ukashinda na kukesha huko ukasahau majukumu ya nyumbani kwako.

Neno la Mungu linasema,
"Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana."
Wakolosai 3:18

"Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno."
1 Petro 3:1

Pamoja na sifa na neema zote ulizojaliwa lakini kumbuka kuwa siku zote mwanaume anapenda kuwa mume ndani ya nyumba.

Mwanaume kuwa mume ni yeye kuwa na nguvu, ni yeye kuwa na madaraka na ni yeye kuwa na mamlaka ndani ya nyumba.

Ndio maana neno la Mungu linasisitiza wake kuwa na utii kwa waume zao.

Sifa ulizo nazo zitakufanya upendwe na hata kuolewa lakini sifa hizohizo ndizo zitakazokufanya uachike na kila mwanaume kama utakosa kuwa na utii.

#No_Learning_No_Earning
So we have to Learn.

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

View attachment 2811107
Kweli kabisa. Umesema kweli
 
Ila kweli ndoa/mapenzi hayana expert kuna muda huwa nafikiria sana na sitaki kushauri mtu yeyote kuhusu haya mambo kikubwa tu Ingia kwenye ndoa ukiwa umeamua na unajitambua itakusaidia kuwa na maamuzi sahihi katika kila changamoto mpya ambayo hukutegemea kukutana nayo.

Siyo kusalitiwa au kudharauliwa tu ndo chanzo cha migogoro kuna vyanzo vingi vya migogoro ndo hapo unapoambiwa hayana formula unatakiwa mwenyewe tu kichwan uwe timam kutatua changamoto zinazovumilika.
Basi, ndoa inahitaji uwe commited kwa ndoa unaweza ukafanya usaliti mwenzako akakuvumilia tu au ukamdharau mwenzako akakuvumilia tu ila ukaja fanya kitu kidogo tu ukaharibu kila kitu
 
Mwanamume akiwa kama kichwa cha familia lazima aweke MISINGI na MIONGOZO ya jinsi ndoa na familia yake inapaswa kwenda

Hiyo kwenda na beats ndoa itakushinda mapema sana.

Ndoa ni taasisi lazima iendeshwe kwa kanuni na misingi
Mkuu labda hujaelewa nilipomaanisha kwenda na beats
Soma vzr uelewe
 
Naomba unieleweshe mkuu huenda hatujaelewana
Kwenda na beats ni kwenda na mazingira yaliyopo mfano
Kuna mume/mke mwingine kwa maumbile yake tu alivyoumbwa sio watu wakujali wengine,na wala haoni shida,sasa hapa mke ukitaka kujaliwa lazima ndoa ibume tu maana mwenzako anaona sawa, na sio kwamba hakupendi no, anakupenda sana tu ila ndo alivyo wale watu wakuchukulia pao mambo, so kwenda na beat ni kumsoma mwenzako na kujua namna ya kwenda nae
 
Sio kweli... formula ipo nayo ni mke kumtii mume, hayo mengine ndo yatajipanga badae
Shida itakuja wewe unae tiiwa (mwee kiswahili hiki) are you willing kurudisha unachopokea

Ntabaki na msimamo wangu hakuna formula
 
Kwenda na beats ni kwenda na mazingira yaliyopo mfano
Kuna mume/mke mwingine kwa maumbile yake tu alivyoumbwa sio watu wakujali wengine,na wala haoni shida,sasa hapa mke ukitaka kujaliwa lazima ndoa ibume tu maana mwenzako anaona sawa, na sio kwamba hakupendi no, anakupenda sana tu ila ndo alivyo wale watu wakuchukulia pao mambo, so kwenda na beat ni kumsoma mwenzako na kujua namna ya kwenda nae
Umesema vyema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom