Tabia za mwanamke ambaye ameumizwa kihisia

Tabia za mwanamke ambaye ameumizwa kihisia

george aloyce

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2017
Posts
1,302
Reaction score
2,035
ACHA KUJIWEKA KINYONGE NYONGE, TAFUTA MARAFIKI NA ACHA KUWA MTU WA HASIRA!

(1) Umejitenga kabisa na dunia kwanza mkimya, hujichanganyi na watu wengine, unajiona mtu wa Mungu sana kiasi kwamba kila kitu unadhani ni cha shetani, hata kuongea na watu wa imani tofauti na wewe unaona kama unatenda dhambi.

(2) Huna marafiki, labda wale wa kazini ambao mkishamaliza kazi huwezi hata kutoka nao, ukikutana na watu njiani unakua kama unawakimbia. Unafanya mambo yako kivyakovyako kiasi hata wanawake wenzako wanaogopa kukushirikisha mambo yao.

(3) Una hasira sana, unahisi kuwa kila mtu anakuonea, mwanaume akikusemesha unamjibu vibaya, unahisi anakudharau, kakudhalilisha, anataka kukuchezea na kukuacha, yaani kama anataka kukutia dhambi.

(4) Hujiamini kiasi kwamba unahisi kila mwanaume anayekusalimia anakutania, akikuambia ni mzuri unakasirika kwakua unaona kama anakuchora, kwa kifupi umejiwekea ukuta na watu wengine.

Mapenzi ni starehe, mapenzi si ibada wala kazi. Hivyo mtu anapenda kufanya starehe na mtu ambaye kachangamka, mtu ambaye atampa raha na mtu ambaye atafurahi kuwa na yeye.

Sasa kama wewe kila siku una mawazo, una huzuni, umetoka na marafiki lakini umekaa kimya, upo kama haupo. Kama unataka mwanaume kuja kwako kwanza kua na furaha yako mwenyewe.
 
Back
Top Bottom